Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Meta, kampuni inayomiliki Facebook na Instagram, imekubali kulipa hadi $17.1B (Tsh. Trilioni 45.1/=) kumaliza kesi iliyohusisha madai kwamba mitandao hiyo iliundwa kwa namna inayoweza kuwafanya watoto na vijana kuwa na utegemezi wa matumizi ya mitandao.
Kesi hiyo, iliyohusisha majimbo 29 nchini Marekani, imeibua mjadala kuhusu usalama wa watoto kwenye mitandao ya kijamii.
Kama sehemu ya makubaliano hayo, Meta inatarajiwa kuweka hatua mpya za kuwalinda watumiaji wadogo, ikiwemo kuweka kikomo cha muda wa matumizi kwa siku, kuzuia matumizi wakati wa usiku, kupunguza notifications wakati wa masomo na kuongeza udhibiti kwa wazazi.
Hata hivyo, Meta imekanusha kufanya makosa, ikisema kulinda vijana ni jambo la muhimu sana.
Makubaliano hayo pia yanamaanisha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Meta, Mark Zuckerberg, hatalazimika kutoa ushahidi katika kesi hiyo.