Meremeta & TANGOLD Revealed!

Mbona ni mengi yamesemwa humu jamvini lakini hakuna kilichofanya na Serikali juu ya Meremeata,Tangold na Deep Green Finance.Nafikiri umefika wakati muafaka wa kuchukua hatua ili serikali ijue watanzania sasa wamenuia kuiadibisha kwa sababu wabunge tuliowatuma wamekwenda likizo.

Natumai tukijiunga na asasi zisizo za kiserikali na kuandamana nchi nzima kushinikiza waziri mkuu ajiuzuilu,mafisadi wa meremeta,tangold,deep green,mwananchi,kagoda wachukuliwe harua za kufikishwa mahakamani na pia kutaka mabadiliko ya msingi serikalini,hatua zitachukuliwa.Hivi tutaendelea kuongea mpaka lini si wataendelea kudharau kama vile Sumari alivyoonyesha dharau kwa Dr.Slaa.

Hima hatua zichukuliwe ili kuiadibisha serikali,vinginevyo ule msemo kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi zitakuwa za kweli.
 
ukiona hivi jua hakuna ushahidi wowote ndo mana serikali hawezi kusema lolote
 
Hiima hatua zichukuliwe hilo nalo neno maana tumechoshwa na kulindana uchafu wa mafisadi hata ikiwezekana hawa mafisadi pindi wanapo onekana ni kupigwa mawe tu jamii yote iwakatae.
 
Ufisadi wa Meremeta hauna kinga, uchunguzwe
Monday, 08 August 2011 20:59
Mwananchi

KWA miaka kadhaa sasa wabunge wa Bunge la Bunge la Jamhuri ya Muungano wamekuwa wakipaza sauti zao juu kuhusiana na ufisadi wa zaidi ya Sh205.9 bilioni unaodaiwa kufanywa kupitia Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Meremeta iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kilio hichi cha wabunge wenye uzalendo wa dhati katika kusimamia rasilimali za Taifa hili, bila kuchoka walisimama kidete kutaka ufisadi wa aina yake uchunguzwe, lakini baadhi ya viongozi wa Serikali, akiwamo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda waliamua kwa dhati kabisa kuziba masikio na kufumba macho yao kwa kutoa visingizio luluki vyenye lengo la kuficha ukweli.

Pamoja na vizingiti vyote hivi, wabunge walivyokumbana navyo, bado waliendelea kusimama kwenye uzalendo na kuendelea kuibana Serikali kwa lengo la kutaka tuhuma hizi za ufisadi wa Meremeta zichunguzwe na ukweli ujulikane kwa maslahi ya taifa.

Ndio maana taarifa za kwamba Bunge kupitia Kamati yake ya Nishati na Madini litachunguza ufisadi huo zinapoza kilo cha wengi kuwa taasisi hili muhimu kwa mustakabli wan chi imesikia kilio cha wabunge wake na Watanzania kwa ujumla.Ndio maana tunaamini kwamba uchunguzi huu utaisaidia kubaini wahusika wa ufisadi huu ili sheria ichukue mkondo wake.

Tunaambiwa kwamba Kamati ndogo ya Madini itafanya uchunguzi wa uhalali wa malipo ya dola milioni 132 (sawa na Sh205.9 bilioni kwa viwango cha sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Tsh1560 dhidi ya dola) ambazo zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenda Ned Bank ya Afrika Kusini, kama malipo ya mkopo wa dola milioni 10, uliokuwa umechukuliwa na kampuni ya Meremeta Ltd.

Kwa hiyo, uchunguzi huu ni mwanzo mzuri wa kupima hoja za viongozi wa Serikali ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kwamba suala la Meremeta lisingeweza kufanyiwa uchunguzi kutokana na “sababu za kiusalama”.

Ndio maana sisi tunasema kwamba uchunguzi wa kina wa sakata la Meremeta ni muhimu kwa kuwa hakuna usalama ambao unalea ufisadi mahali popote duniani.Tunaamini kwamba wanasiasa ambao walikuwa wakitumia mwavuli wa usalama au vyombo vyetu vya ulinzi kuficha uovu watatoa ushirikiano kwa Kamati ya Bunge.

Hata hivyo, wajumbe wa Kamati hiyo ndogo tunawaasa kwamba endapo watakutana na vizingiti kama vya huko nyuma basi wasisite kupaza sauti zao juu kuuhabarisha umma wa Watanzania ambao ndio wadau wakuu wa rasilimali za nchi.

Hatupendi kuamini na wala kushawishika kwamba Jeshi letu ambao lina kazi muhimu ya kulinda mipaka ya nchi yetu na watu wake limejiingiza kwenye biashara ya madini. Ndio maana tunasema kwamwe hatupendi JWTZ ipakwe matope kwa ufisadi wa watu wa chache ambao hawalitakii mema Taifa hili.

Kama walivyo Watanzania wote, tunatambua kazi nzuri ambayo Jeshi letu limefanya ndani na nje ya mipaka yetu, hivyo tusingependa baadhi ya viongozi wa Serikali walitumie kama kichaka cha kuficha uozo wa wachache.

Ni kweli tunambua unyeti wa kazi za jeshi letu, lakini kwa hili la ufisadi wa Meremeta, JWTZ wasibebeshwe mzigo; hivyo tunataka wenye mzigo wajulikane na wafikishwe kwenye vyombo vya dola.

Kila wakati msimamo wa gazeti ni kwamba ufisadi wowote wa fedha za umma hauwezi kuvumilika kwa visingizio vya namna yoyote ile, ndio maana tuaamini kwamba uchunguzi utasaidia kuwekla wazi kila kitu.

Uchunguzi ufisadi wa Meremeta wayeyuka
Friday, 11 November 2011 21:21

Neville Meena, Dodoma
Mwananchi

KUNA kila dalili kwamba uchunguzi uliokuwa ukikusudiwa na Bunge kuchimbua ufisadi wa zaidi ya Sh205.9 bilioni unaodaiwa kufanywa kupitia Kampuni ya Meremeta iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) hautafanyika, Mwananchi limebaini.

Matumaini ya kuchunguzwa kwa kashfa hiyo yalitokana na hatua ya Spika wa Bunge Anne Makinda kuamua kupeleka jambo hilo katika kamati za Bunge zilizopo, badala ya kuunda kamati teule kama ilivyokuwa imependekezwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

Zitto wakati wa mkutano wa nne wa Bunge la bajeti mwaka huu, aliwasilisha kwa Spika Makinda hoja binafsi akitaka bunge liunde kamati teule kuchunguza suala hilo ambalo Serikali imekuwa ikitaka lisiguswe kwa maelezo kwamba ni linagusa mambo ya ulinzi na usalama wa nchi.

Mtizamo huo wa Serikali ndiyo unaoonekana kukwaza uchunguzi ambao ulikuwa umekaribia kuanza pale Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah alipoliambia Mwananchi mjini Dodoma kuwa: "Ninavyokumbuka ni kwamba suala hili lilishafungwa tangu bunge la tisa, Serikali ilishaweka wazi suala hili wakati wa Bunge la tisa".

Dk Kashillilah alisema katika mazingira hayo haoni ni kwa jinsi gani jambo hilo linaweza kurejeshwa tena bungeni na kwamba hata hoja hiyo ikilazimishwa, itafika wakati itakwama na kutotoa matokeo yanayokusudiwa.

"Labda walazimishe tu na wanaweza kufanya hivyo lakini kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zetu limekwisha. Kama tunavyojua sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa taratibu zilizopo, kwa hiyo tukisimama hapo sidhani kama jambo hili litakuwa na tija," alisema Dk Kashillilah ambaye wakati hoja hiyo ilipoibuliwa tena alikuwa kwenye likizo ya ugonjwa.

Kwa kauli ya Katibu huyo wa Bunge, ni dhahiri hoja ya Zitto itakuwa imekwaa kisiki hivyo suala la kilichojiri ndani ya Meremeta kubaki siri kubwa.

Msimamo wa Serikali

Maelezo ya Dk Kashillilah yanarejea msimamo uliowahi kutolewa bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Juni 27, 2008 kwamba yuko tayari kusulubishwa lakini si kueleza undani wa Meremeta.

Akihitimisha Makadirio ya Bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka 2008/09, Pinda alisema: "Meremeta haukuwa mradi wa uraiani ambako tungeweza tukasema jambo lolote tunalotaka kulisema, 'this is a unique situation' (haya ni mazingira ya kipekee)."

"Nilitaka tu niseme, mimi kusimama hapa nianze kusema 'this is what it was and this is what' (hiki ni kitu gani na ilikuwaje)…, hapana. Napata taabu, sitaweza. Sitaweza for a simple reason (kwa sababu nyepesi), tu kwamba ni jambo ambalo lina uhusiano wa karibu sana na masuala ya ulinzi na usalama wa nchi yetu," alisema Pinda na kuongeza:

"Mengine yote niko radhi, ila kwa hili na kwa sababu nalijua na mimi, kwa kweli inafika mahali nasema hapana, nadhani iwe protected na tui-protect Serikali na tu-protect jambo hili ambalo linahusiana na ulinzi na usalama. Sasa kama mtaona hiyo inatosha, vyema. Mkiona mnisulubishe kwa sababu sijasema yote, well and good (ni vyema) vilevile."

Mchakato wa uchunguzi

Mara ya mwisho, Spika alikuwa ameamua kupeleka suala hilo kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, lakini uchunguzi umebaini kwamba suala hilo bado halijawasilishwa rasmi mbele ya kamati hiyo.

Mkurugenzi wa Huduma za Bunge, John Joel ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya Dk Kashillilah wakati akiwa likizo alithibitisha kwamba ofisi yake haikuwahi kuiarifu Kamati ya Lowassa kuhusu suala hilo.

Awali, baada ya Spika kupokea taarifa ya kusudio la Zitto la kutaka kuundwa kwa kamati teule, aliamua suala hilo lifanyiwe kazi katika Kamati ya Nishati na Madini. Hata hivyo, baadaye Spika Makinda alibatilisha uamuzi wake wa awali, hivyo kuamua kupeleka suala hilo katika Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Zitto akiwa chanzo cha hoja hiyo aliwahi kupongeza uamuzi wa Spika kupeleka suala la Meremeta chini ya Kamati ya Nishati na Madini lakini suala hilo lilipohamishiwa Kamati ya Mambo ya Nje, alieleza wasiwasi kwamba ulikuwa ni mwanzo wa kuua hoja yake.

Zitto alianzisha hoja ya kuchunguzwa kwa Meremeta alipowasilisha barua kwa Katibu wa Bunge akitoa taarifa ya hoja ya kuunda Kamati Teule kwa ajili ya kuchunguza tuhuma za ufisadi kupitia kampuni hiyo ya uchimbaji wa dhahabu.

Barua hiyo ilitanguliwa na taarifa yake ya mdomo aliyoitoa bungeni Julai 13, mwaka huu kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge Namba 117 (2)-(a) inayomruhusu kutoa taarifa ya kusudio lake la kuwasilisha hoja ya kutaka Bunge liunde Kamati Teule.

Mbunge huyo alimwandikia Spika Makinda barua kutoa taarifa ya hoja husika Julai 15, mwaka huu akisema: "Kuna haja ya kujua uhalali wa ongezeko la Dola 122milioni zilizoongezeka katika malipo yaliyofanywa."

Historia ya Meremeta

Meremeta Ltd ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na JWTZ kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Mkoa wa Pwani huku taarifa za usajili zilizotolewa na Msajili wa Kampuni wa Uingereza na Wales zikisema kuwa kampuni hiyo iliandikishwa nchini humo mwaka 1997 na kabla ya kufilisiwa hukohuko mwaka 2006.

Taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ya Mei 31, 2005 inabainisha kwamba Meremeta Ltd ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania, Oktoba 3, 1997 na kwamba hisa 50 za kampuni hiyo zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini, wakati hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania.

Utata kuhusu umiliki wa Meremeta Ltd unatokana na taarifa ya Brela ambayo pia inazitambua kampuni mbili za Kiingereza, London Law Services Ltd na London Law Secretarial Ltd kuwa wamiliki wa hisa moja kila moja ndani ya Meremeta.

Licha ya Serikali kutokuwa mmiliki pekee wa kampuni hiyo, BoT inadaiwa kuwa ililipa madeni yote ya Meremeta badala ya kusaidiana na washirika wake ambao kisheria wanaonekana kuwa walikuwa wakimiliki hisa katika kampuni hiyo.

Serikali Tanzania ilikuwa ikimiliki asilimia 50 ya hisa na kwa mujibu wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uhalali wa malipo hayo ulikuwa na walakini kwani kiutaratibu Nedbank Ltd ilitakiwa iachwe idai fedha zake kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo sawa na wadeni wengine.

Hatua ya kurejeshwa kwa mkopo huo pamoja na faida ya zaidi ya asilimia 1,000 ndilo chimbuko la kutaka kufanywa kwa uchunguzi huo.

Wakuu vipi za leo?

Katika pita pita zangu mitandaoni,nikasema ngoja nijifanyie kiji research kuhusu madini yetu,niliyokutana nayo ni mengi na nikipata nafasi nitabandika hapa.

Hata nimekutana na something interesting.Ni hili la MEREMETA.

Kwanza kuna taarifa kwamba ilikuwa liquidated na pia wali file for bankruptcy.

At the same time kuna confusing information kwamba bado iko na inamilikiwa na serikali na yenye pia inamiliki migodi kadhaa ikiwemo Buhemba,North Mara na huko Geita.

Dhumuni la kujiuliza kama serikali yetu ni kampuni binafsi lilitokana na mimi kukumbana na hii...Ninataiweka habari kwenye quote,ni kutoka This Day...Kwanza ni kipengele kuwa Kampuni hiyo sasa iko in dissolved status...

THE involvement of the Tanzania People’s Defence Forces (TPDF) in the controversial Meremeta Limited formally ceased in 2005/06 after the joint venture company between the government and South African investors was officially dissolved, impeccable sources have revealed to THISDAY.

Lakini ebu tujikumbushie....Uanzishwaji wake...

Going by official government records, Meremeta was registered as a 50-50 joint venture project between the Tanzanian government and Triennex (PTY) Limited of South Africa.
However, other strong evidence indicates the presence in Meremeta’s affairs from the outset of at least two British legal firms, London Law Services Ltd and London Law Secretarial Ltd, both described as ’nominal shareholders.’
In October 1997, the company was given certificate of compliance number 32755 by the Business Registration Licensing Authority (BRELA), allowing it to formally operate in Tanzania.

Halafu tena nikakutana na habari hii inayoonyesha kuwa kampuni hiyo imefutwa ama dissolved..Lakini wamiliki wake ni wa tofauti na wale waliotajwa na both na serikali na This Day.

MEREMETALIMITED
Company update is from 25/02/2011. Do you want to update company now?

Company Number
03424504
Registered Office
69 SOUTHAMPTON ROW
LONDON
WC1B 4ET

Company Origin
United Kingdom
ountry
England
County
Greater London
Borough
Camden
Postcode
London - WC1B 4
Company GPS

Company Status
Dissolved
Company Type
Private Limited Company
Incorporation Date
19/08/1997
Dissolution Date
10/01/2006

lat: 51.520288, long: -0.1227
accuracy: address level

However ilianza kazi ya uzalishaji ama uchimbaji wa madini...Mwaka mmoja kabla haijatangaza kufilisika...

In 2005, the Meremeta company announced it had produced 2,075kilogrammes of gold at a cash cost of $384 per troy ounce of gold.

Apart from the Buhemba gold mine, Meremeta also held the Kilamongo and Mwizideposits, both located south of Buhemba, and the Nyasanero deposit.
Baada ya huo mwaka wa uzalishaji kuanza...Ikafilisika!

But then in 2006 – only a year after officially beginning goldproduction the company declared bankruptcy, and was formally dissolved.

Jeshi nalo likajitoa in the proccess....

’’With the dissolution of Meremeta, both the TPDF and the SouthAfrican company (Triennex) formally pulled out of gold mining activities atBuhemba,’’ said one of our well-informed sources, adding: ’’So officially,any military involvement in the Meremeta project ended in 2006 when the companywas declared bankrupt.’’

Insiders further say the initial involvement of the TPDF in the Buhemba goldmining operations was aimed at raising funds to finance its cash-strappedvehicle manufacturing division – Tanzania Automotive Technology Centre, betterknown as the Nyumbu project.
It is understood that Meremeta was also set up to assist in developing thecountry’s informal gold mining sector.

Lakini kuna maswali ya kujiuliza.Kwanza kampuni hii ina historia na walipakodi,hivyo ndiyo maana sikushangazwa kufile for bankruptcy kwasababu walipakodi bado wanaumizwa na si hao wamiliki wa serikali kampuni, halafu at the same time wanaolipwa ni hao walio dissolve(kampuni serikali)

Kama mwanzoni walisema MEREMETA ilikuwa inamilikiwa na serikali,baada ya utata na kufile bankruptcy one year after production began,bado serikali ilitoa tamko kuwa assets hizo zilizokuwa zikimilikiwa na "serikali kampuni" ya MEREMETA,sasa zitamilikiwa na "serikali kampuni" ya TANGOLD,yani vituko tu!

Pia katika proccess ya kuwa dissolved ama kuacha production,bado kampuni serikali hiyo ilijichotea zaidi ya $ milini 118 kutoka BOT kama pesa za walipa kodi...

Working in collaboration with the TPDF at the Buhemba open pit gold mine inMara Region, Meremeta officially began gold mining operations in February 2003,with its operations being heavily financed by Tanzanian taxpayers through theBank of Tanzania (BoT).

Official government records show that as Meremeta Ltd was winding up itsoperations, the BoT paid more than $118m (approx. 150bn/-) to Nedcor TradeServices Limited after having guaranteed a loan from the South African firm toMeremeta.
The BoT raised the funds to pay off the loan to Meremeta through acontroversial 155bn/- Treasury bond, in a transaction that raised seriousqueries from auditors.

Haya,sasa hapa ndiyo mwanzo wa mtiririko uliopelekea nijiulize si tu kama serikali ni kampuni binafsi,bali kama wanaamini kuwa watanzania wana akilitimamu ama la...

Walirudi bungeni kuanza upya...Wakajifungulia TANGOLD...

Kwamba sasa assets zote za MEREMETA ambazo zilikuwa ni za serikali,sasa ni za serikali tena kwa mara nyingine kwa kupitia kampuni ya serikali ambayo ni serikali yenyewe yenye limited shares kwa wamiliki hao wa serikali, kwenda kwa jina la TANGOLD...

Following the liquidation of Meremeta Ltd, the Ministry of Energy andMinerals announced in Parliament that a wholly-owned government company,TANGOLD Limited, had been formed and assumed all Meremeta company assets,including the Buhemba gold mine.

Hivyo wakawa wameshaji rekebishia njia kiu halali kuendeleza ufisadi kwaku endelea kula pesa za walipa kodi kupitia BOT once again...

Investigations by THISDAY have already established that the BoT paidanother $13.34m (approx. 17bn/-) to TANGOLD through an account at the NationalBank of Commerce Limited’s Corporate Branch in Dar es Salaam.

Haya ebu tuiangalie hiyo TANGOLD iliyo assume majukumu ya serikali nakuichukuwa MEREMETA...Hiyo nayo ambayo ni kampuni serikali, inamilikiwa na kina Chenge,Mgonja na wenzake. Hao ndo serikali!

Serikali ikatoa tamko kupitia wizari ya nishati na madini kuwa kampuni hiyo inamilikiwa na serikali kwa asilimia 100!

Hata hivyo maajabu ni kwamba inamilikiwa na serikali kama a foreign company ambayo ikasajiliwa Tanzania ili iweze ku OPERATE locallyTanzania...Na serikali hiyo ni kina Chnege na Balali.
Sasa kampuni zinazomilikiwa na serikali kwa asilimia 100 zinamilikiwa na hao kina Chnege kwa asilimia hizo hizo?Hapo imekaaje hii?

TANGOLD was initially registered as an offshore company in Mauritiusin April 2005, with its address listed as Suite 520, Barkly Whart, Le CaudanWaterfront, Port Louis.

In February 2006, the company was registered in Tanzania, with its localshareholders including former BoT governor Daudi Ballali (now deceased); the thenMinister for Infrastructure Development, Andrew Chenge; and the PermanentSecretary in the Ministry of Finance, Gray Mgonja.

Other TANGOLD shareholders are the current PS in the Ministry of Water andIrrigation, Patrick Rutabanzibwa; and the then permanent secretary in theMinistry of Livestock Development, Vincent Mrisho.

Although the Ministry of Energy and Minerals claimed that TANGOLD was 100%owned by the government, it has failed to explain why the company wasregistered in Mauritius and not Tanzania, and why its articles ofassociation give the listed shareholders permission to transfer all or part oftheir shares to their next of kin.

TANGOLD is also not listed at the Treasury Registry among companies partlyor wholly-owned by the government, and has thus not been subjected tostatutory auditing by the Controller and Auditor General (CAG).

When addressing the National Assembly in Dodoma last Friday, premier Pindaappeared evasive to the point of fumbling in his attempts to answer queriesfrom opposition members of parliament regarding Meremeta, TANGOLD and DeepGreen Finance Limited.

Hata hivyo kwa mujibu wa Raw Materials Data (http://www.rmg.se/RMDEntities/M2/Meremeta_Ltd_MEREME.htm)MEREMETA pia bado ipo na data zinaonyesha hivyo kwenye webiste yaokuwa walikuwa kwenye production 2008/2009...

Meremeta Ltd, Tanzania

Meremeta Ltd is a company in Tanzania. It is controlled/owned by
State of Tanzania

Meremeta Ltd is just one of 26 000 entities to be found in Raw MaterialsData, the mining industry's most extensive database. Below is an example ofwhat can be pulled out of Raw Materials Data.

For the past 20 years, Raw Materials Group has been mining and refining data,to bring you the world's most extensive mining data "Raw MaterialsData", unsurpassed within the industry.

Raw Materials Data contains 26,000 entities (mines, smelters, refineries,projects, companies, associations, etc), a wealth of mine details (type (openpit - underground), metals, metal grades, ore production and reserves, presentand past metal production, cash costs for gold mines, project cost forgreenfield and brownfield projects and more...), and covers 25 commodities.Company, mine and country data can be displayed quickly on exportable maps,documents and spreadsheets.

The database contains unique information on ownership and control, providing anexcellent picture of each metal industry's structure and its evolution. As anatural extension, we have compiled mergers and acquisitions details from 1994to present. We also have a "What if?" function that allows users tomodel company mergers and show their impact on production and industrystructure and ownership. Our gold cost curve product "Raw MaterialsGold" is updated with the most recent quarterly cost and productioninformation.
A partial
list of entities in RawMaterials Data

(c) Copyright 2011 Raw Materials Group

Mods please musiifute ama kuiunga hii,na mkifanya tafadhali mnipe sababu.

Hapa ningependa tujadili ni kwa jinsi gani serikali yetu inavyoweza kutuchezea akili kwa namna inayosikitisha sana.Yani this ni "on your face"attitude kutoka kwa viongozi wetu...

Kampuni inayomilikiwa na serikali na inayokuwa financed na walipa kodi ni lazima iwajibike kwa walipa kodi na maswali yajibiwe kwa walipa kodi na maelezo hayoni fair game ndani ya bunge.

Kinyume cha hapo ni unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za msingi za watanzania na demokrasia kwa ujumla, na hilo peke yake linaweza kupelekea wananchi waitake serikali ijiuzulu mara moja!

Hizo kampuni ni za serikali lakini inaonekana zina share holders ama kumilikiwa na watu ambao hawatajwi na kama wao ndo wamiliki wa serikali,na ambao umiliki wao hauna manufaa kwa wananchi ama kuwa na maslahi kwa Taifa na wananchi.

Pia tupewe sababu ni kwanini ili file for bankruptcy mwaka tu baada ya kuanza uzalishaji?

kama wananchi wali i bail out kampuni hiyo again and again kwa jasho lao, ni yapi hayo manufaa yake kwao?

Hata mara baada ya kubadili badili majina,basi n
i lazima wananchi wapewe taarifa kuhusiana na kufilisika huko na sababu zake...Na pia hao next of kin waserikali yetu ambayo sasa ni kama kampuni?

Na pia ni kina nani hao behind hayo makampuni ambao wanajiita serikali?
 
Ni maajabu kuwa kampuni inayoendeshwa kwa kutumia pesa za walipa kodi kuwa tata na kutokujulikana kwa uhakika wamiliki wake.
Utata uliopo ni so extensive,na ni maajabu,only in Tanzania this is possible na mambo yakawa sawa tu.
 
hili lishajulikana ila tatizo ni sisi mitanzania kwa kutowauliza hao (ambao ni watu dhaifu sana) waliotubinafsisha wakatupa maelezo ya kina juu ya mstakabali wetu huko tuendako!

Ina maana issue hii ni ya kawaida sasa?
Duh!Naanza kuogopa kuitwa mtanzania.
 
Mods ile thread yangu ya MEREMETA inaosema serikali a Tanzania ni kampuni iungwe na hii.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mods ile thread yangu ya MEREMETA inaosema serikali a Tanzania ni kampuni iungwe na hii.

Sidhani nchini kama kuna archive kubwa ya ufisadi mbali mbali uliofanywa nchini katika awamu ya tatu na ya nne kama hili jamvi, lakini wahusika wote wa ufisadi huo bado wanapeta tu na huku usanii wa Kikwete ukiendelea na msamiati wao wa "kujivua gamba" kwa siku 90 na sasa ni zaidi ya miezi sita na hakuna dalili zozote za kujivua gamba.
 
mihangwa.jpg

Nasaha za Mihangwa

MEREMETA: Kashfa ya ufisadi kabambe isiyoweza kumeremeta

Joseph Mihangwa

Toleo la 112
16 Dec 2009

SI siri tena kwamba Tanzania imegubikwa na ufisadi wa kutisha, mkubwa na wa aina yake Afrika Mashariki, kama si bara zima la Afrika.Ufisadi huu, ulioanzia awamu zilizopita zilizobinafsisha kila kitu kilichokuwa cha Umma, kwa usiri mkubwa, mizengwe na kwa bei ya kutupa, umeongeza kasi jinsi siku zilivyopita.

Kipindi hicho, tumeshuhudia kashfa kubwa kubwa za ufisadi zenye kuatamiwa kwa machukizo ya Umma, kama ile ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL/TANESCO), ambapo nchi imeporwa mabilioni ya fedha kwa mkataba tata wa umeme wa miaka 20 kuanzia mwaka 1999.

Chini ya mkataba huu, nchi imetupwa gizani kwa kukosa umeme, lakini inaendelea kuilipa IPTL zaidi ya 5bn/= kwa mwezi bila kujali, umeme uwepo au usiwepo; tutumie au tusitumie, kwa sababu mkataba wa mwaka 1995 unaelekeza hivyo. Walioliingiza Taifa katika mkenge huu wanafahamika kwa vyeo na kwa majina; lakini wapo huru, wanapeta.

Kashfa nyingine zenye kuangamiza ustawi wa Taifa ni pamoja na zile za EPA, ununuzi wa rada na ndege ya Rais; ubinafsishaji wa NBC na uuzaji wa nyumba za Serikali; mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, Richmond/Dowans, mikataba mibovu ya madini; Loliondo, na ufujaji wa zaidi ya bilioni 150/= za mfuko wa kuwezesha uagizaji bidhaa (CIS), kwa kutaja chache tu.

Na kama tusingeshituka, manyang'au hawa walikuwa wamepania pia kuhujumu mifuko ya Akiba ya wafanyakazi kwa kujichotoa mabilioni ya fedha kwa njia ya ushiriki katika vitega uchumi vya mifuko hiyo. Na ingawa ufisadi huu unafahamika vizuri, na wahusika wanajulikana kwa Serikali (ikiwamo Serikali ya awamu ya nne), juhudi zimeendelea kufanywa kuatamia uchafu huo, na wahusika kuoshwa kwa sabuni kali ili, kwa hadaa kubwa, waweze kumeremeta machoni mwa Umma.

Hizo ndizo zilikuwa enzi za mwanzo kabisa za utamaduni wa kukwapua mali ya umma miongoni mwa wanasiasa na watawala, kwa kushirikiana na kada ya wafanyabiashara, kuota mizizi.

Utafiti makini umeonesha kwamba, katika juhudi za kujiponya, wahujumu hao ama wamekimbilia kunyakua (kupora) nafasi za kisiasa ili wapate kinga ya kisiasa, au wamegeuka kuwa wafadhili wakubwa wa Chama Tawala na kampeni za uchaguzi ili walindwe na kusafishwa.

Lakini pamoja na hayo, licha ya chama tawala na Serikali kujitahidi kuzisafisha kashfa mbalimbali za ufisadi ziweze kumeremeta, kashfa moja kabambe nchini, ya mradi wa Mgodi wa Meremeta, imeshindwa kumeremeta. Kushindwa kwa juhudi za Serikali hivi karibuni za kuisafisha Meremeta ili imeremete zimepelekea Bunge kuitaka Serikali iwasilishe hesabu za Kampuni hiyo kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zikaguliwe ili kukata mzizi wa fitina.

Hata hivyo, pamoja na Agizo hili la chombo hicho cha kutunga Sheria, chenye jukumu pia la Kikatiba la kusimamia utendaji kazi wa Serikali, hesabu za Kampuni hiyo hazijakaguliwa wala kuwasilishwa kwa CAG. "Nitakagua nini wakati sijapata hesabu zenyenyewe kutoka Serikalini ….. siwezi kufanya ukaguzi wowote", alinukuliwa akisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG), Ludovick Utouh, akilalama hivi karibuni, juu ya Serikali kukataa kutii Agizo la Bunge, kwa hofu inayofahamika.

Serikali kwa upande wake, inaonekana kuiatamia kashfa hii kwa madai kwamba siri za Meremeta hazizungumziki, na hesabu zake hazikaguliki kwa sababu zinahusu mambo ya usalama wa Taifa. Kuna ukweli gani juu ya madai haya? Je, Meremeta ni mradi wa Serikali? Kwa misingi ipi; na kwa kiwango gani?. Hebu tuchimbue kidogo kuusaka ukweli.

Kampuni ya Meremeta, ambayo inadaiwa haijasajiliwa chini ya Ofisi ya Hazina kama kampuni au shirika, tayari imechota malipo tata zaidi ya 155 bn/= zilizolipwa na Benki Kuu (BOT) kwa Kampuni ya Nedcor Trade Service, baada ya udhamini wa Kampuni yenye hisa ya Triennex (PTY) limited ya Afrika Kusini. Malipo haya na mengine, kama tutakavyoona badaye, ndiyo yaliyozua utata na Bunge kuagiza mahesabu yakaguliwa.

Katika makala haya, tutaona na kufahamu kama ni kweli kampuni ya Meremeta ni ubia wa Serikali na Kampuni ya Triennex, unaohusisha Jeshi la Ulinzi, kama inavyodaiwa, na pia kuhusisha Usalama wa Taifa. Tutaona ni kwa vipi, makampuni mengine kama Deep Green Finance na Tangold (yanavyoguswa na kashfa hii) yalivyoingia; na kwa nini Serikali inajiuma mdomo na kukunja mikono yanapotajwa.

Inaelekea kwamba Serikali ya Awamu ya Nne, haihusiki sana na sakata hili, japo inalijua fika; lakini imejitahidi kuliatamia bila mafanikio kwa njia ya "kufunika kombe mwanaharamu apite".

Lakini ifahamike kwa misingi ya sheria kwamba, kitendo cha mtu kufunika kombe au kuatamia kosa lililotendwa na mtu mwingine, kwa lengo la kumwepusha mtu huyo mwingine sheria isichukue mkondo wake dhidi ya mtu huyo; au kosa alilotenda lisijulikane, kinamfanya mtu huyo mwenye kutaka kumwokoa huyo mtu mwingine na yeye kuwa mshiriki wa kosa hilo kwa kiwango sawa na cha mtuhumiwa halisi wa kosa. Kwa hiyo, viongozi wanaowalinda au kuwasafisha mafisadi wana hatia ya ufisadi ule ule wa wale wanaojaribu kuwaokoa.

Huu ndio utamaduni wa kulindana kwa maovu, unaoshika kasi nchini kwa machukizo ya Umma; kana kwamba viongozi na washirika wao wana kinga ya kimsahafu (Luka 12:32) kwamba, "Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa baba yenu (mfumo wa kifisadi) ameona vema kuwapa ule ufalme - (wa ulaji?)"
Hebu tuziangalie sasa Meremeta, Deep Green na Tangold, Kampuni zinazolindwa na mfumo wa utawala wa nchi kwa maumivu na chukizo kubwa kwa wananchi; tuone kama kweli shughuli zake zina chembe ya Usalama wa Taifa.

Kampuni ya Meremeta iliandikishwa na kusajiliwa nchini Uingereza Agosti 9, 1999 (kisiwa cha Isle of Man) na kupewa namba ya Usajili 3424504; lakini Serikali yetu inadai ni ubia kati ya Serikali ya Tanzania yenye asilimia 50 ya hisa, na Kampuni ya Triennex ya Afrika Kusini, inayomiliki hisa asilimia 50 pia.
Utata unaongezeka pale inapodaiwa kuwa, Makampuni ya London Law Serivices Ltd, na London Law Secretarial Ltd, nayo ni wanahisa wa Meremeta.

Madhumuni ya Kampuni hiyo yanaelezwa kuwa ni kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo nchini, pamoja na kuwasaidia zana za kufanyia kazi. Swali linalojitokeza hima hapa ni kwa vipi kampuni inayomilikiwa na Serikali, na ambayo shughuli zake zinafanyika hapa hapa nchini na kwa misingi ya Usalama wa Taifa, iandikishwe na kusajiliwa katika nchi ya kigeni?

Kati ya mwaka 2003 na 2005, Kampuni hii ilitelekeza wajibu na madhumuni ya kuanzishwa kwake na kuanza kuchimba dhahabu yenyewe huko Buhemba, Musoma. Hapo ndipo hadithi ya Meremeta kuhusisha Usalama wa Taifa ilipoanza; hapo ndipo hadithi ya Meremeta kujihusisha kusaidia kiwanda cha magari cha Jeshi cha Nyumbu (Kibaha ) ilipoanza kupikwa na kusikika.

Ikumbukwe kuwa, katika kipindi hicho (2003 – 2005), kiwanda cha Nyumbu kilipangiwa fedha kutoka serikalini jumla ya Sh. 950 milioni, kwa ajili ya kutengeneza magari 21 ya kijeshi, kwa wastani wa 45.2m/= kwa kila gari, na hakukuwa na fedha zaidi zilizoingia kutoka vyanzo vingine kipindi hicho.

Ukweli juu ya kwamba Mradi wa Meremeta haukuhusika kwa namna yoyote ile na Jeshi la Wananchi, unathibitishwa pia na Waziri wa Ulinzi, Philemon Sarungi, katika hotuba yake ya Bajeti ya 2004/2005, aliposema: "Mradi wa Buhemba umejengwa katika eneo lililokuwa Kambi ya Jeshi, na shughuli za uchimbaji na uzalishaji zinasimamiwa na Idara ya Madini".

Kile tu kwamba mradi huo ulijengwa mahali ambapo zamani ilikuwa Kambi ya Jeshi, hakufanyi uwe Mradi wa Jeshi wenye kuhusishwa na Usalama wa Taifa. Ukweli ni kwamba, Mgodi mpya wa Buhemba ulijengwa kwa rand milioni 240 (dola 56m) na Kampuni ya WBHO (Pty) Ltd ya Afrika Kusini, na ulikamilika mwaka 2000.

Ujenzi huo ulifanywa kwa niaba ya Meremeta na Triennex (Kampuni zote tata), na si kwa niaba ya Serikali ya Tanzania. Ulizihusisha pia kampuni za kigeni za Jefferies and Green na Time Mining, zote za Afrika Kusini.

Niharakishe kusema hapa kwamba, mmoja wa wanahisa wakubwa wa Kampuni ya Time Mining (TM), alikuwa mama mmoja Mtanzania mke wa mmoja wa vigogo nchini ambaye ndiye pia aliyeileta kampuni hiyo nchini kuja kusimamia na kuendesha Mgodi wa Meremeta, eti kwa niaba ya Serikali ya Tanzania.

Cha kushangaza hapa pia ni kwamba, wengi wa watumishi wa nje (expatriates) wa Kampuni ya Ukaguzi ya Alex Stewarts ya mjini Washington, iliyoletwa Tanzania kukagua mauzo ya nchi za nje ya dhahabu kwa makampuni ya madini nchini, ndio hao hao waliokuwa watumishi pia wa Kampuni ya Time Mining.

Kama kweli serikali ilikuwa na maslahi katika Meremeta, kwa nini iliruhusu mtu binafsi kusajili kampuni binafsi ya kigeni kusimamia mradi huu? Hatutazungumzia sana suala la Alex Stewarts hapa, kwa sababu liko mahakamani, likiwahusisha mawaziri wa zamani na katibu mkuu msitaafu.

Baada ya kukomba dhahabu yote huko Buhemba na Buhemba Kusini, Nyamongo na Magunga, mwaka 2006, Meremeta ilitangazwa kuwa ilikuwa inafanya kazi kwa hasara, na ikaundwa Tume ya Serikali ya watu watano, kuchunguza matatizo ya Kampuni hiyo.

Wazito na Waheshimiwa sana waliokuwa katika Tume hiyo, ni Daudi Balali – Gavana wa BOT na Mwenyekiti wa Tume; Gray Mgonja, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, na Patrick Rutabanzibwa, wakati huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Wengine walikuwa ni Vincent Mrisho, Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Andrew Chenge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na Michael G. Garner, kama Mshauri huru wa Tume, ambaye alikuwa pia ndiye Mshauri wa Benki ya Nedbank, yenye uhusiano na Kampuni ya Nedcor Trade Service, iliyochota bilioni 155/- kutoka Benki Kuu katika mazingira ya kutatanisha.

Tume hiyo ilipendekeza kusitishwa kwa shughuli za Kampuni ya Meremeta za kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo, jukumu ambalo tayari ilikwishalitelekeza tangu mwaka 2003, na kujiingiza katika uchimbaji na umiliki wa migodi.

Tume ilipendekeza pia kuanzishwa kwa Kampuni mpya yenye jukumu la kusimamia na kuendesha Mgodi wa Buhemba yenye kumilikiwa na Serikali asilimia kwa mia. Kwa lugha nyingine ni kwamba, baada ya kung'atuka kwa Meremeta, Serikali iliamua kusimamia yenyewe Mradi huo wa dhahabu kupitia chombo au taasisi teule.

Na kwa uzito wa mapendekezo ya Tume hiyo ya Balali, Meremeta ilifilisiwa, ambapo mali na madeni yake yalichukuliwa na Kampuni mpya ya "Tangold," inayodaiwa kumilikiwa na Serikali kwa asilimia mia. Na ingawa Meremeta (halisi) ilifungwa rasmi mwaka 2006 nchini Uingereza, shughuli zake hazikukoma nchini Tanzania wakati huo, kama tutakavyoona baadaye katika makala haya.

Hapa kuna utata mwingine, kwamba kumbukumbu zinaonyesha kuwa, Kampuni ya Tangold ilianzishwa katika Visiwa vya Mauritius, Aprili 4, 2005; na kupewa Leseni ya Biashara Aprili 8, 2005 kama kampuni binafsi. Lakini kumbukumbu nyingine zinaonyesha kuwa, Tangold ilifungua Akaunti ya Benki Namba 011103024852, Tawi la Corporate Drive la NBC, Dar es Salaam, Januari 1, 2003; kabla hata Tume ya Balali na wenzake haijaundwa kutatua tatizo la Meremeta.

Taarifa nyingine zimeonyesha zaidi kuwa, kampuni hiyo ni ya kigeni iliyosajiliwa nchini Mauritius na kupewa leseni nchini Tanzania, Februari 20, 2005 kama tawi la kampuni ya kigeni; na ilianza kupatiwa fedha na BOT Agosti 1, 2005 kwa kazi isiyojulikana.

Je, ina maana kwamba Tangold ilikuwapo nchini Tanzania kabla ya kuanzishwa nchini Mauritius mwaka 2005, au ni aina fulani tu ya usanii? Hata kama ilikuwapo, iliwezaje kufungua akaunti benki, Januari 1, 2003 ambayo ilikuwa Sikukuu ya Kitaifa ya Mwaka mpya?. Kama ilikuwapo, kwa nini Tume ilipendekeza kuundwa kwa kampuni ambayo tayari ilikuwapo? Nini tofauti kati ya Tangold iliyofungua akaunti Januari 2003, na Tangold iliyosajiliwa Mauritius April 4, 2005 kurithi Meremeta?

Ingawa mapendekezo ya Tume na tamko la Serikali yalikuwa kwamba, kampuni hiyo mpya (Tangold) imilikiwe kwa asilimia mia na Serikali, utekelezaji wake ulikuwa ni kinyume chake; ambapo inaelekea wajumbe wa Tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya Meremeta, ndio waliogeuzwa kuwa Wakurugenzi wa Kampuni hiyo mpya.

Hao wanatajwa (kwa baadhi majina yao kuongezwa herufi moja ya katikati), kuwa ni Daudi Balali, Gray S. Mgonja, Andrew Chenge, Patrick J. W. Rutabanzibwa na Vicent F. Mrisho.

Inawezekana, kwa mtazamo wa enzi hizo na kwa kusudi hilo, kwamba hao watano ndio walikuwa Serikali yenyewe; lakini kifungu cha saba (7) cha Katiba ya Kampuni ya Tangold kinatibua dhana yote hiyo, kinaposema, "Wenye hisa ya Kampuni wanaweza kurithisha hisa zao kwa ndugu zao".

Je, ni kweli Tangold ilikuwa inamilikiwa na Serikali asilimia mia kama ilivyopendekeza Tume ya Balali, na pia kwa mujibu wa tamko la Serikali? Ni ndugu wapi hao wa Serikali (kama kweli Serikali ina ndugu!) waliostahili kurithishwa hisa za Serikali?

Haya ni maswali magumu, na tunashawishika kuamini kwamba, Tangold haikumilikiwa na Serikali asilimia mia; bali ilikuwa kampuni binafsi iliyorithishwa mali za kampuni ya Meremeta.

Wakati matatizo ya Meremeta yakiendelea, na wakati huo huo tayari mapendekezo ya Tume ya Balali ya watu watano yakiwa yameanza kufanyiwa kazi, Machi 18, 2004, iliundwa Kampuni nyingine iitwayo "Deep Green Finance" (DGF) ambayo madhumuni na shughuli zake hazijafahamika vizuri mpaka sasa. Wakurugenzi wa DGF walikuwa ni Mark Ross Weston wa New Zealand; Antón Taljaard wa Afrika Kusini, na Rudolf Van Schalkwyk, pia wa Afrika Kusini.

Wanahisa wa DGF walitajwa kuwa ni Protase R. G. Ishengoma, Stella Ndikimi wa kampuni ya uwakili ya IMMA, ya jijini Dar es Salaam; Benki ya Nedbank Africa Investment Ltd ya Afrika Kusini (ambayo mshauri wake, Michael G. Garner, ndiye pia aliyekuwa Mshauri huru wa Tume ya watu watano, iliyochunguza matatizo ya Meremeta na kupendekeza kuundwa kwa Tangold), na Kampuni ya SBM Nedcor Holdings, ambayo haijafahamika bado, kama ina uhusiano wowote na Kampuni ya Nedcor Trade Service, iliyolipwa na BOT malipo tata ya zaidi ya Sh. 155 bn/= kwa niaba ya Meremeta.

Wakurugenzi hao watatu wa Deep Green Finance, ndio waliokuwa maofisa pia wa NedBank; na jina la Deep Green limetumiwa mara nyingi na NedBank katika miradi yake ya kijamii.

Haifahamiki pia ni kwa vipi na kwa njia ipi, Watanzania pekee wawili, Protase Ishengoma na Stella Ndikimi, walitembelewa na ngekewa ya kununua hisa za kampuni yenye kumilikiwa na wageni kama hii (DGF); na kama ni kweli inavyodaiwa, kwamba hatimaye walichukua hisa (kwa njia ya kuhamishia au kununua) katika Nedbank Ltd na Nedbank Africa Investments, Aprili 15, 2004.

Kama ilivyokuwa kwa kampuni ya Tangold, iliyofungua akaunti siku ya Sikukuu ya mwaka mpya; ndivyo ilivyokuwa pia kwa kampuni ya Deep Green Finance, iliyofungua akaunti Benki ya NBC, Na. 011103024840, tawi hilo hilo la Corporate Drive; safari hii ilikuwa Sikukuu (ya mapunziko) ya Mei Mosi, 2004.

Kuna utata kuhusu utoaji wa namba za akaunti za benki hiyo, kwamba akaunti ya Tangold, namba 011103024852, iliyofunguliwa Januari 1, 2003, ni kubwa (kwa akaunti 12 zaidi), ikilinganishwa na Akaunti Namba 01110302840 ya Deep Green Finance, iliyofunguliwa zaidi ya mwaka mmoja baadaye, Mei 1, 2004.

Je, ni utaratibu wa NBC kutoa namba za akaunti kuanzia na namba za juu, kushuka chini? Kama sivyo, basi kuna uwalakini unaotufanya tuamini kwamba kulikuwa na hitilafu ikizingatiwa pia kwamba akaunti zote mbili zilifunguliwa siku za mapumziko ya Sikukuu za kitaifa.

Toka Mei 1, 2004 akaunti ya Tangold ilipofunguliwa, hadi Julai 31, 2005 (zaidi ya mwaka mmoja), hapakuwa na shughuli za DGF zilizoingiza fedha katika akaunti hiyo, hadi Agosti 1, 2005 ilipoanza kupokea mabilioni ya fedha kutoka ama Benki Kuu, Deep Green Finance au Tangold, kwenda ama Deep Green Finance, Tangold, Meremeta, IMMA Advocates au kusikojulikana.

Wakati tunaelezwa kwamba Tangold ilianzishwa Aprili 5, 2005 na kupewa leseni ya biashara Aprili 8, 2005 kuchukua nafasi ya Meremeta, na mali na madeni ya Meremeta kuhamishiwa au kuchukuliwa na kampuni mpya, kwa maana kwamba Meremeta ilikuwa imefilisiwa na kufungwa; lakini kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Oktoba 12, 2005, jumla ya 1,690,500,000/= zilihamishwa kutoka Tangold kwenda kampuni (mfu?) ya Meremeta; na vivyo hivyo Novemba 23, (555,300,048/=) na Deseaba 12 (551,060,000/=).

Iliwezekanaje Meremeta kulipwa fedha hizo wakati ilikwishafilisiwa? Nani aliifufua?
Kwa kifupi, kati ya Agosti 1, 2005 na Desemba 21, 2006, jumla ya 32bn/= zilihamishwa kutoka Benki Kuu kwenda Deep Green Finance na Tangold; mbali na zile zilizopelekwa kusikojulikana.

Tunashawishika kuamini kwamba, Deep Green Finance iliundwa kurahisisha na kuhakikisha utoroshaji wa fedha za Meremeta na Tangold kwenda nje ya nchi na si kwa sababu nyingine yoyote ile.

Baada ya mahesabu hayo, na kuonekana kwamba Mradi wa Tangold hauwezi kuendelea, Serikali iliuza haki za Mgodi huo kwa Kampuni ya "Rand Gold" ya Afrika Kusini, kwa bei ya chini ya soko, na kusababisha hasara ya dola za Kimarekani milioni 100; na pia kulipa dola milioni 132 pamoja na adhabu na riba, kutokana na Serikali (BOT) kudhamini wakopaji/wawekezaji waliofilisika na kutupa mzigo kwa Serikali kuyalipa.

Tangu kuundwa kwa Kampuni ya Meremeta, hadi kuundwa na kufilisika kwa Kampuni ya Tangold, licha ya kuruhusu uporaji mkubwa wa mabilioni ya fedha na rasilimali, ilisababisha pia hasara ya jumla ya dola za Kimarekani milioni 232, sawa na 232bn/= wakati huo, kwa njia ya kifisadi. Malipo hayo yalifanyika Oktoba 2005, mwezi mmoja tu kabla ya Rais Benjamín Mkapa kumaliza awamu yake.

Kwa hiyo wanaodai kwamba kashfa ya Meremeta haizungumziki, eti kwa sababu inagusa mambo ya Usalama wa Taifa, wajichunguze kwanza kabla hawajanena; kisha watueleze hayo wanayatoa wapi; vinginevyo tutawahesabu Wasaliti wa Taifa hili.

Na kwa nini tusalimu amri kwa taarifa za uongo, wakati nchi yetu inageuzwa "Shamba la Bibi" kwa ulafi wa wachache wa ndani, wakishirikiana na wahujumu uchumi wa kimataifa?
King'aracho ni dhahabu, lakini si kila king'aracho au kimeremetacho ni dhahabu.

Kashfa ya Mradi wa dhahabu wa Meremeta ni mfano wa ufisadi uliokithiri nchini, kiasi kwamba hata upambwe kwa lugha ya vito na kufukiziwa ubani, hauwezi kumeremeta wala kunukia. Wale makuwadi wa ufisadi nchini, wanaodhani kwamba wanaweza kutudanganya tukadanganyika, wajue kwamba wanajaribu kutemea mate mbingu, na hivyo hawawezi kukwepa kuchafua nyuso za
O.
 
Mhhh ngumu kumeza ila ndo hivyo maana mpaka Premier wetu anasema ukiitaja Meremeta taifa litatikisika
 
Sio Mchezo hii.Daud Balali =Marehemu, Mgonja =Mtuhumiwa. Chenge=Vijisenti.

Nasikia nae Rutabanzibwa kashasitaafishwa kwa Manufaa ya Umma.
 
Inatia huzuni na hasira wanaposema meremeta haizungumziki na nchi itazizima nchi ni wananchi ikizizima mm mwananchi sitzizima ila nitajifunza kufanya makosa tena viongozi wachache ndo watazizima na ni haki yao wazizime maana waliyataka kweupe, tuungane kupiga kelele juu ya jambo hili popote.
 
SI siri tena kwamba Tanzania imegubikwa na ufisadi wa kutisha, mkubwa na wa aina yake Afrika Mashariki, kama si bara zima la Afrika.

Ufisadi huu, ulioanzia awamu zilizopita zilizobinafsisha kila kitu kilichokuwa cha Umma, kwa usiri mkubwa, mizengwe na kwa bei ya kutupa, umeongeza kasi jinsi siku zilivyopita.

Kipindi hicho, tumeshuhudia kashfa kubwa kubwa za ufisadi zenye kuatamiwa kwa machukizo ya Umma, kama ile ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL/TANESCO), ambapo nchi imeporwa mabilioni ya fedha kwa mkataba tata wa umeme wa miaka 20 kuanzia mwaka 1999. Chini ya mkataba huu, nchi imetupwa gizani kwa kukosa umeme, lakini inaendelea kuilipa IPTL zaidi ya 5bn/= kwa mwezi bila kujali, umeme uwepo au usiwepo; tutumie au tusitumie, kwa sababu mkataba wa mwaka 1995 unaelekeza hivyo. Walioliingiza Taifa katika mkenge huu wanafahamika kwa vyeo na kwa majina; lakini wapo huru, wanapeta.

Kashfa nyingine zenye kuangamiza ustawi wa Taifa ni pamoja na zile za EPA, ununuzi wa rada na ndege ya Rais; ubinafsishaji wa NBC na uuzaji wa nyumba za Serikali; mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, Richmond/Dowans, mikataba mibovu ya madini; Loliondo, na ufujaji wa zaidi ya bilioni 150/= za mfuko wa kuwezesha uagizaji bidhaa (CIS), kwa kutaja chache tu.

Na kama tusingeshituka, manyang'au hawa walikuwa wamepania pia kuhujumu mifuko ya Akiba ya wafanyakazi kwa kujichotoa mabilioni ya fedha kwa njia ya ushiriki katika vitega uchumi vya mifuko hiyo. Na ingawa ufisadi huu unafahamika vizuri, na wahusika wanajulikana kwa Serikali (ikiwamo Serikali ya awamu ya nne), juhudi zimeendelea kufanywa kuatamia uchafu huo, na wahusika kuoshwa kwa sabuni kali ili, kwa hadaa kubwa, waweze kumeremeta machoni mwa Umma.

Hizo ndizo zilikuwa enzi za mwanzo kabisa za utamaduni wa kukwapua mali ya umma miongoni mwa wanasiasa na watawala, kwa kushirikiana na kada ya wafanyabiashara, kuota mizizi.

Utafiti makini umeonesha kwamba, katika juhudi za kujiponya, wahujumu hao ama wamekimbilia kunyakua (kupora) nafasi za kisiasa ili wapate kinga ya kisiasa, au wamegeuka kuwa wafadhili wakubwa wa Chama Tawala na kampeni za uchaguzi ili walindwe na kusafishwa.

Lakini pamoja na hayo, licha ya chama tawala na Serikali kujitahidi kuzisafisha kashfa mbalimbali za ufisadi ziweze kumeremeta, kashfa moja kabambe nchini, ya mradi wa Mgodi wa Meremeta, imeshindwa kumeremeta. Kushindwa kwa juhudi za Serikali hivi karibuni za kuisafisha Meremeta ili imeremete zimepelekea Bunge kuitaka Serikali iwasilishe hesabu za Kampuni hiyo kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zikaguliwe ili kukata mzizi wa fitina.

Hata hivyo, pamoja na Agizo hili la chombo hicho cha kutunga Sheria, chenye jukumu pia la Kikatiba la kusimamia utendaji kazi wa Serikali, hesabu za Kampuni hiyo hazijakaguliwa wala kuwasilishwa kwa CAG. "Nitakagua nini wakati sijapata hesabu zenyenyewe kutoka Serikalini ….. siwezi kufanya ukaguzi wowote", alinukuliwa akisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG), Ludovick Utouh, akilalama hivi karibuni, juu ya Serikali kukataa kutii Agizo la Bunge, kwa hofu inayofahamika.

Serikali kwa upande wake, inaonekana kuiatamia kashfa hii kwa madai kwamba siri za Meremeta hazizungumziki, na hesabu zake hazikaguliki kwa sababu zinahusu mambo ya usalama wa Taifa. Kuna ukweli gani juu ya madai haya? Je, Meremeta ni mradi wa Serikali? Kwa misingi ipi; na kwa kiwango gani?. Hebu tuchimbue kidogo kuusaka ukweli.

Kampuni ya Meremeta, ambayo inadaiwa haijasajiliwa chini ya Ofisi ya Hazina kama kampuni au shirika, tayari imechota malipo tata zaidi ya 155 bn/= zilizolipwa na Benki Kuu (BOT) kwa Kampuni ya Nedcor Trade Service, baada ya udhamini wa Kampuni yenye hisa ya Triennex (PTY) limited ya Afrika Kusini. Malipo haya na mengine, kama tutakavyoona badaye, ndiyo yaliyozua utata na Bunge kuagiza mahesabu yakaguliwa.

Katika makala haya, tutaona na kufahamu kama ni kweli kampuni ya Meremeta ni ubia wa Serikali na Kampuni ya Triennex, unaohusisha Jeshi la Ulinzi, kama inavyodaiwa, na pia kuhusisha Usalama wa Taifa. Tutaona ni kwa vipi, makampuni mengine kama Deep Green Finance na Tangold (yanavyoguswa na kashfa hii) yalivyoingia; na kwa nini Serikali inajiuma mdomo na kukunja mikono yanapotajwa.

Inaelekea kwamba Serikali ya Awamu ya Nne, haihusiki sana na sakata hili, japo inalijua fika; lakini imejitahidi kuliatamia bila mafanikio kwa njia ya "kufunika kombe mwanaharamu apite".

Lakini ifahamike kwa misingi ya sheria kwamba, kitendo cha mtu kufunika kombe au kuatamia kosa lililotendwa na mtu mwingine, kwa lengo la kumwepusha mtu huyo mwingine sheria isichukue mkondo wake dhidi ya mtu huyo; au kosa alilotenda lisijulikane, kinamfanya mtu huyo mwenye kutaka kumwokoa huyo mtu mwingine na yeye kuwa mshiriki wa kosa hilo kwa kiwango sawa na cha mtuhumiwa halisi wa kosa. Kwa hiyo, viongozi wanaowalinda au kuwasafisha mafisadi wana hatia ya ufisadi ule ule wa wale wanaojaribu kuwaokoa.

Huu ndio utamaduni wa kulindana kwa maovu, unaoshika kasi nchini kwa machukizo ya Umma; kana kwamba viongozi na washirika wao wana kinga ya kimsahafu (Luka 12:32) kwamba, "Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa baba yenu (mfumo wa kifisadi) ameona vema kuwapa ule ufalme - (wa ulaji?)"

Hebu tuziangalie sasa Meremeta, Deep Green na Tangold, Kampuni zinazolindwa na mfumo wa utawala wa nchi kwa maumivu na chukizo kubwa kwa wananchi; tuone kama kweli shughuli zake zina chembe ya Usalama wa Taifa.

Kampuni ya Meremeta iliandikishwa na kusajiliwa nchini Uingereza Agosti 9, 1999 (kisiwa cha Isle of Man) na kupewa namba ya Usajili 3424504; lakini Serikali yetu inadai ni ubia kati ya Serikali ya Tanzania yenye asilimia 50 ya hisa, na Kampuni ya Triennex ya Afrika Kusini, inayomiliki hisa asilimia 50 pia.

Utata unaongezeka pale inapodaiwa kuwa, Makampuni ya London Law Serivices Ltd, na London Law Secretarial Ltd, nayo ni wanahisa wa Meremeta.

Madhumuni ya Kampuni hiyo yanaelezwa kuwa ni kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo nchini, pamoja na kuwasaidia zana za kufanyia kazi. Swali linalojitokeza hima hapa ni kwa vipi kampuni inayomilikiwa na Serikali, na ambayo shughuli zake zinafanyika hapa hapa nchini na kwa misingi ya Usalama wa Taifa, iandikishwe na kusajiliwa katika nchi ya kigeni?

Kati ya mwaka 2003 na 2005, Kampuni hii ilitelekeza wajibu na madhumuni ya kuanzishwa kwake na kuanza kuchimba dhahabu yenyewe huko Buhemba, Musoma. Hapo ndipo hadithi ya Meremeta kuhusisha Usalama wa Taifa ilipoanza; hapo ndipo hadithi ya Meremeta kujihusisha kusaidia kiwanda cha magari cha Jeshi cha Nyumbu (Kibaha ) ilipoanza kupikwa na kusikika.

Ikumbukwe kuwa, katika kipindi hicho (2003 – 2005), kiwanda cha Nyumbu kilipangiwa fedha kutoka serikalini jumla ya Sh. 950 milioni, kwa ajili ya kutengeneza magari 21 ya kijeshi, kwa wastani wa 45.2m/= kwa kila gari, na hakukuwa na fedha zaidi zilizoingia kutoka vyanzo vingine kipindi hicho.

Ukweli juu ya kwamba Mradi wa Meremeta haukuhusika kwa namna yoyote ile na Jeshi la Wananchi, unathibitishwa pia na Waziri wa Ulinzi, Philemon Sarungi, katika hotuba yake ya Bajeti ya 2004/2005, aliposema: "Mradi wa Buhemba umejengwa katika eneo lililokuwa Kambi ya Jeshi, na shughuli za uchimbaji na uzalishaji zinasimamiwa na Idara ya Madini".

Kile tu kwamba mradi huo ulijengwa mahali ambapo zamani ilikuwa Kambi ya Jeshi, hakufanyi uwe Mradi wa Jeshi wenye kuhusishwa na Usalama wa Taifa. Ukweli ni kwamba, Mgodi mpya wa Buhemba ulijengwa kwa rand milioni 240 (dola 56m) na Kampuni ya WBHO (Pty) Ltd ya Afrika Kusini, na ulikamilika mwaka 2000. Ujenzi huo ulifanywa kwa niaba ya Meremeta na Triennex (Kampuni zote tata), na si kwa niaba ya Serikali ya Tanzania. Ulizihusisha pia kampuni za kigeni za Jefferies and Green na Time Mining, zote za Afrika Kusini.

Niharakishe kusema hapa kwamba, mmoja wa wanahisa wakubwa wa Kampuni ya Time Mining (TM), alikuwa mama mmoja Mtanzania mke wa mmoja wa vigogo nchini ambaye ndiye pia aliyeileta kampuni hiyo nchini kuja kusimamia na kuendesha Mgodi wa Meremeta, eti kwa niaba ya Serikali ya Tanzania.

Cha kushangaza hapa pia ni kwamba, wengi wa watumishi wa nje (expatriates) wa Kampuni ya Ukaguzi ya Alex Stewarts ya mjini Washington, iliyoletwa Tanzania kukagua mauzo ya nchi za nje ya dhahabu kwa makampuni ya madini nchini, ndio hao hao waliokuwa watumishi pia wa Kampuni ya Time Mining.

Kama kweli serikali ilikuwa na maslahi katika Meremeta, kwa nini iliruhusu mtu binafsi kusajili kampuni binafsi ya kigeni kusimamia mradi huu? Hatutazungumzia sana suala la Alex Stewarts hapa, kwa sababu liko mahakamani, likiwahusisha mawaziri wa zamani na katibu mkuu msitaafu.

Baada ya kukomba dhahabu yote huko Buhemba na Buhemba Kusini, Nyamongo na Magunga, mwaka 2006, Meremeta ilitangazwa kuwa ilikuwa inafanya kazi kwa hasara, na ikaundwa Tume ya Serikali ya watu watano, kuchunguza matatizo ya Kampuni hiyo. Wazito na Waheshimiwa sana waliokuwa katika Tume hiyo, ni Daudi Balali – Gavana wa BOT na Mwenyekiti wa Tume; Gray Mgonja, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, na Patrick Rutabanzibwa, wakati huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Wengine walikuwa ni Vincent Mrisho, Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Andrew Chenge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na Michael G. Garner, kama Mshauri huru wa Tume, ambaye alikuwa pia ndiye Mshauri wa Benki ya Nedbank, yenye uhusiano na Kampuni ya Nedcor Trade Service, iliyochota bilioni 155/- kutoka Benki Kuu katika mazingira ya kutatanisha.

Tume hiyo ilipendekeza kusitishwa kwa shughuli za Kampuni ya Meremeta za kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo, jukumu ambalo tayari ilikwishalitelekeza tangu mwaka 2003, na kujiingiza katika uchimbaji na umiliki wa migodi.

Tume ilipendekeza pia kuanzishwa kwa Kampuni mpya yenye jukumu la kusimamia na kuendesha Mgodi wa Buhemba yenye kumilikiwa na Serikali asilimia kwa mia. Kwa lugha nyingine ni kwamba, baada ya kung'atuka kwa Meremeta, Serikali iliamua kusimamia yenyewe Mradi huo wa dhahabu kupitia chombo au taasisi teule.

Na kwa uzito wa mapendekezo ya Tume hiyo ya Balali, Meremeta ilifilisiwa, ambapo mali na madeni yake yalichukuliwa na Kampuni mpya ya "Tangold," inayodaiwa kumilikiwa na Serikali kwa asilimia mia. Na ingawa Meremeta (halisi) ilifungwa rasmi mwaka 2006 nchini Uingereza, shughuli zake hazikukoma nchini Tanzania wakati huo, kama tutakavyoona baadaye katika makala haya.

Hapa kuna utata mwingine, kwamba kumbukumbu zinaonyesha kuwa, Kampuni ya Tangold ilianzishwa katika Visiwa vya Mauritius, Aprili 4, 2005; na kupewa Leseni ya Biashara Aprili 8, 2005 kama kampuni binafsi. Lakini kumbukumbu nyingine zinaonyesha kuwa, Tangold ilifungua Akaunti ya Benki Namba 011103024852, Tawi la Corporate Drive la NBC, Dar es Salaam, Januari 1, 2003; kabla hata Tume ya Balali na wenzake haijaundwa kutatua tatizo la Meremeta.

Taarifa nyingine zimeonyesha zaidi kuwa, kampuni hiyo ni ya kigeni iliyosajiliwa nchini Mauritius na kupewa leseni nchini Tanzania, Februari 20, 2005 kama tawi la kampuni ya kigeni; na ilianza kupatiwa fedha na BOT Agosti 1, 2005 kwa kazi isiyojulikana.

Je, ina maana kwamba Tangold ilikuwapo nchini Tanzania kabla ya kuanzishwa nchini Mauritius mwaka 2005, au ni aina fulani tu ya usanii? Hata kama ilikuwapo, iliwezaje kufungua akaunti benki, Januari 1, 2003 ambayo ilikuwa Sikukuu ya Kitaifa ya Mwaka mpya?. Kama ilikuwapo, kwa nini Tume ilipendekeza kuundwa kwa kampuni ambayo tayari ilikuwapo? Nini tofauti kati ya Tangold iliyofungua akaunti Januari 2003, na Tangold iliyosajiliwa Mauritius April 4, 2005 kurithi Meremeta?

Ingawa mapendekezo ya Tume na tamko la Serikali yalikuwa kwamba, kampuni hiyo mpya (Tangold) imilikiwe kwa asilimia mia na Serikali, utekelezaji wake ulikuwa ni kinyume chake; ambapo inaelekea wajumbe wa Tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya Meremeta, ndio waliogeuzwa kuwa Wakurugenzi wa Kampuni hiyo mpya. Hao wanatajwa (kwa baadhi majina yao kuongezwa herufi moja ya katikati), kuwa ni Daudi Balali, Gray S. Mgonja, Andrew Chenge, Patrick J. W. Rutabanzibwa na Vicent F. Mrisho.

Inawezekana, kwa mtazamo wa enzi hizo na kwa kusudi hilo, kwamba hao watano ndio walikuwa Serikali yenyewe; lakini kifungu cha saba (7) cha Katiba ya Kampuni ya Tangold kinatibua dhana yote hiyo, kinaposema, "Wenye hisa ya Kampuni wanaweza kurithisha hisa zao kwa ndugu zao".

Je, ni kweli Tangold ilikuwa inamilikiwa na Serikali asilimia mia kama ilivyopendekeza Tume ya Balali, na pia kwa mujibu wa tamko la Serikali? Ni ndugu wapi hao wa Serikali (kama kweli Serikali ina ndugu!) waliostahili kurithishwa hisa za Serikali?

Haya ni maswali magumu, na tunashawishika kuamini kwamba, Tangold haikumilikiwa na Serikali asilimia mia; bali ilikuwa kampuni binafsi iliyorithishwa mali za kampuni ya Meremeta.

Wakati matatizo ya Meremeta yakiendelea, na wakati huo huo tayari mapendekezo ya Tume ya Balali ya watu watano yakiwa yameanza kufanyiwa kazi, Machi 18, 2004, iliundwa Kampuni nyingine iitwayo "Deep Green Finance" (DGF) ambayo madhumuni na shughuli zake hazijafahamika vizuri mpaka sasa. Wakurugenzi wa DGF walikuwa ni Mark Ross Weston wa New Zealand; Antón Taljaard wa Afrika Kusini, na Rudolf Van Schalkwyk, pia wa Afrika Kusini.

Wanahisa wa DGF walitajwa kuwa ni Protase R. G. Ishengoma, Stella Ndikimi wa kampuni ya uwakili ya IMMA, ya jijini Dar es Salaam; Benki ya Nedbank Africa Investment Ltd ya Afrika Kusini (ambayo mshauri wake, Michael G. Garner, ndiye pia aliyekuwa Mshauri huru wa Tume ya watu watano, iliyochunguza matatizo ya Meremeta na kupendekeza kuundwa kwa Tangold), na Kampuni ya SBM Nedcor Holdings, ambayo haijafahamika bado, kama ina uhusiano wowote na Kampuni ya Nedcor Trade Service, iliyolipwa na BOT malipo tata ya zaidi ya Sh. 155 bn/= kwa niaba ya Meremeta.

Wakurugenzi hao watatu wa Deep Green Finance, ndio waliokuwa maofisa pia wa NedBank; na jina la Deep Green limetumiwa mara nyingi na NedBank katika miradi yake ya kijamii.

Haifahamiki pia ni kwa vipi na kwa njia ipi, Watanzania pekee wawili, Protase Ishengoma na Stella Ndikimi, walitembelewa na ngekewa ya kununua hisa za kampuni yenye kumilikiwa na wageni kama hii (DGF); na kama ni kweli inavyodaiwa, kwamba hatimaye walichukua hisa (kwa njia ya kuhamishia au kununua) katika Nedbank Ltd na Nedbank Africa Investments, Aprili 15, 2004.

Kama ilivyokuwa kwa kampuni ya Tangold, iliyofungua akaunti siku ya Sikukuu ya mwaka mpya; ndivyo ilivyokuwa pia kwa kampuni ya Deep Green Finance, iliyofungua akaunti Benki ya NBC, Na. 011103024840, tawi hilo hilo la Corporate Drive; safari hii ilikuwa Sikukuu (ya mapunziko) ya Mei Mosi, 2004.

Kuna utata kuhusu utoaji wa namba za akaunti za benki hiyo, kwamba akaunti ya Tangold, namba 011103024852, iliyofunguliwa Januari 1, 2003, ni kubwa (kwa akaunti 12 zaidi), ikilinganishwa na Akaunti Namba 01110302840 ya Deep Green Finance, iliyofunguliwa zaidi ya mwaka mmoja baadaye, Mei 1, 2004. Je, ni utaratibu wa NBC kutoa namba za akaunti kuanzia na namba za juu, kushuka chini? Kama sivyo, basi kuna uwalakini unaotufanya tuamini kwamba kulikuwa na hitilafu ikizingatiwa pia kwamba akaunti zote mbili zilifunguliwa siku za mapumziko ya Sikukuu za kitaifa.

Toka Mei 1, 2004 akaunti ya Tangold ilipofunguliwa, hadi Julai 31, 2005 (zaidi ya mwaka mmoja), hapakuwa na shughuli za DGF zilizoingiza fedha katika akaunti hiyo, hadi Agosti 1, 2005 ilipoanza kupokea mabilioni ya fedha kutoka ama Benki Kuu, Deep Green Finance au Tangold, kwenda ama Deep Green Finance, Tangold, Meremeta, IMMA Advocates au kusikojulikana.

Wakati tunaelezwa kwamba Tangold ilianzishwa Aprili 5, 2005 na kupewa leseni ya biashara Aprili 8, 2005 kuchukua nafasi ya Meremeta, na mali na madeni ya Meremeta kuhamishiwa au kuchukuliwa na kampuni mpya, kwa maana kwamba Meremeta ilikuwa imefilisiwa na kufungwa; lakini kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Oktoba 12, 2005, jumla ya 1,690,500,000/= zilihamishwa kutoka Tangold kwenda kampuni (mfu?) ya Meremeta; na vivyo hivyo Novemba 23, (555,300,048/=) na Deseaba 12 (551,060,000/=). Iliwezekanaje Meremeta kulipwa fedha hizo wakati ilikwishafilisiwa? Nani aliifufua?

Kwa kifupi, kati ya Agosti 1, 2005 na Desemba 21, 2006, jumla ya 32bn/= zilihamishwa kutoka Benki Kuu kwenda Deep Green Finance na Tangold; mbali na zile zilizopelekwa kusikojulikana.

Tunashawishika kuamini kwamba, Deep Green Finance iliundwa kurahisisha na kuhakikisha utoroshaji wa fedha za Meremeta na Tangold kwenda nje ya nchi na si kwa sababu nyingine yoyote ile.

Baada ya mahesabu hayo, na kuonekana kwamba Mradi wa Tangold hauwezi kuendelea, Serikali iliuza haki za Mgodi huo kwa Kampuni ya "Rand Gold" ya Afrika Kusini, kwa bei ya chini ya soko, na kusababisha hasara ya dola za Kimarekani milioni 100; na pia kulipa dola milioni 132 pamoja na adhabu na riba, kutokana na Serikali (BOT) kudhamini wakopaji/wawekezaji waliofilisika na kutupa mzigo kwa Serikali kuyalipa.

Tangu kuundwa kwa Kampuni ya Meremeta, hadi kuundwa na kufilisika kwa Kampuni ya Tangold, licha ya kuruhusu uporaji mkubwa wa mabilioni ya fedha na rasilimali, ilisababisha pia hasara ya jumla ya dola za Kimarekani milioni 232, sawa na 232bn/= wakati huo, kwa njia ya kifisadi. Malipo hayo yalifanyika Oktoba 2005, mwezi mmoja tu kabla ya Rais Benjamín Mkapa kumaliza awamu yake.

Kwa hiyo wanaodai kwamba kashfa ya Meremeta haizungumziki, eti kwa sababu inagusa mambo ya Usalama wa Taifa, wajichunguze kwanza kabla hawajanena; kisha watueleze hayo wanayatoa wapi; vinginevyo tutawahesabu Wasaliti wa Taifa hili.

Na kwa nini tusalimu amri kwa taarifa za uongo, wakati nchi yetu inageuzwa "Shamba la Bibi" kwa ulafi wa wachache wa ndani, wakishirikiana na wahujumu uchumi wa kimataifa?.

King'aracho ni dhahabu, lakini si kila king'aracho au kimeremetacho ni dhahabu. Kashfa ya Mradi wa dhahabu wa Meremeta ni mfano wa ufisadi uliokithiri nchini, kiasi kwamba hata upambwe kwa lugha ya vito na kufukiziwa ubani, hauwezi kumeremeta wala kunukia. Wale makuwadi wa ufisadi nchini, wanaodhani kwamba wanaweza kutudanganya tukadanganyika, wajue kwamba wanajaribu kutemea mate mbingu, na hivyo hawawezi kukwepa kuchafua nyuso zao.

Chanzo: Raia Mwema
 
Back
Top Bottom