Meremeta & TANGOLD Revealed!

Unayosema ni kweli kabisa!!!!! Wengi ni matajiri na hatujui walipata wapi mali hawa. Kila walichonacho ni siri kwa sababu ndivyo mwana usalama Pinda alivyosema.
 
Labda anataka kufikisha post 30,000 kisha tumtumie pongezi

Usiidharau RESOLVE YANGU KWA MANENO YAKO YA KIPUUZI!
NCHI IMEUZWA!
Maswali ni mengi!
Na kama wewe uko comfortable..Well i dont know how!
Unless unajua kitakachofanyika!
TAIFA LIMEOZA!
 

imagine na wewe ungekuwa mbunge, halafu ukawaback up kina Zitto kusharpen hoja zao, mambo yangenyooka in a little while. Kagombee ubunge (jimbo la chenge,lowassa au karamagi) 2010. Tunahitaji michango yenu vijana (excluding vijana mafisadi maana nick names nazo zinafcha mengi).
 

Sikubaliani na wewe..
Madini na nishati ni rasilimali za TAIFA!
Na kama nchi ikivamiwa leo...Watakaovamia watayachukua hayo madini na pamoja na kulipua vyanzo vya umeme ili kutupa giza watuvamie vizuri...Sasa unasema si usalama wa Taifa huo?
 
Kama ni kweli wanasema Mkapa alichukua maamuzi hayo ili kulilinda TAIFA...BASI WATUWEKEE WAZI NI KIVIPI MIKATABA HIYO YA MEREMETA ILIKUWA IKILINDA TAIFA LISIVAMIWE KAMA WANAVYOTAKA KU IMPLY.
 

Kuhani,

Mara nyingi tuna confuse that which is with that which it ought to be.Sheria zenyewe nyingi ziko vague.Si zetu tu, bali hata za hao tunaowaita walioendelea. Nilikuwa nasoma kuhusu an awkward comma in the wording of the US Constitution's second amendment making big stories now, kuna sehemu wamesema wamarekani wote wanahaki ya kuwa na silaha halafu kuna sehemu nyingine wanasema wanatakiwa kuwa kwenye militia, halafu kuna vi comma viwili vitatu vimekaa katikati hapo vinaleta ambiguity kwamba wenye haki ya kuwa na silaha ni wamarekani wote au wamarekani wote walio katika militia?

Pengine muheshimiwa ndiyo anatunga au anapalilia kutungwa kwa sheria mpya zitakazokuwa sharper zaidi.

Kwani sheria yetu inasemaje na/ au inaweza kutafsiriwaje kuhusu masuala ya usalama wa taifa?
 
Sikubaliani na wewe..
Madini na nishati ni rasilimali za TAIFA!
Na kama nchi ikivamiwa leo...Watakaovamia watayachukua hayo madini na pamoja na kulipua vyanzo vya umeme ili kutupa giza watuvamie vizuri...Sasa unasema si usalama wa Taifa huo?

Angalau sasa hivi hauongelei mambo ya Mwinyi kuruhusu watanzania kula vyura na kitimoto, baba una mambo wewe yaani sikuwezi kabisa.

Na hao wanaotaka kuvamia nchi na kuzima umeme ili kuleta giza ni kina nani?
 

Safi sana zito. Nashauri kila njia ifanyike tukurudishe 2010. Mbona umesema yote kweli? Wajifanye hawasikii lakini masikioni mwao limegusa na ukweli wameujua.
 
 
Mhhhhhhhhhh jm hivi wewe ndiye mwenye uchungu kuliko wana jf wote kweli kiasi kwamba wengine si tunaonekana wapuuzi?.
Sorry mie sina ubavu wa kubishana na wewe kama mwanamke mwafirika.
Naheshimu kauli zako mkuu na kuzikubali hata kama zina kaarufu ka matusi🙁
 
Safi sana zito. Nashauri kila njia ifanyike tukurudishe 2010. Mbona umesema yote kweli? Wajifanye hawasikii lakini masikioni mwao limegusa na ukweli wameujua.

Mkuu samahani sana kwani ndiyo maana hata OLE alisema kitu!
Ila HII HOTUBA YA ZITTO HAPO JUU NDIYO IMENIPAGAWISHA!
HUYU JAMAA ATAKUWA SHUJAA KWA AWAMU NYINGINE!
MARK MA WORDS!
Kama kweli akisimamia hapo!
Basi ukombozi ni lazima!
 
Good job Bw.Zitto lakini experience inaonyesha speech hizi zinaishia hewani tuu na hakuna chochote kitakacho badilika,sasa kuna bill yeyote mezani umetayarisha unayotaka kuweka bungeni ili kubadilisha hayo mambo uliyozungumzia? action plseee!

Hapo ndipo anapopatikana mtu ,maana kuna kila aina ya upingaji hapo Bungeni ,lakini woote utawasikia wakitema eti cheche lakini hatuoni action yeyote ,hakuna cha kuweka shilingi wala kuweka bili ni makelele na wananchi kupewa tamaa kuwa sasa bungeni kuna waka moto ,lakini kikao kikimaliza palipounguwa hapaonekaniki .hapo ndipo wengi wetu tunapoachwa kwenye mshangao.
Sasa kuna wengine wamezuka hawa wamikuja na neno ...tusubiri...!
 

Halafu wakuu...Rejea hiyo quote hapo juu...

Naomba kama kuna anayejuwa anijibu hili.
Rais huchagua mkurugenzi wa Idara ya Usalama ambaye ndiye mwajiri wa wanausalama.
Je...Mkurugenzi wa usalama wa MKAPA NA KIKWETE NI MMOJA AMA TOFAUTI?
NA KAMA NI TOFAUTI...BASI LAZIMA MMOJAWAPO NDIO WA KUSIKILIZWA
 
Waulize hao waliodai kuwa mikataba ya KIWIRA,RICHMOND NA MEREMETA NI YA USALAMA WA TAIFA!
NB:USALAMA GANI WA TAIFA HUO AMBAO AUHUSIANI NA KULINDA TUSIVAMIWE?

Mambo ya kuvamiwa yanahusiana vipi na mikataba? Au ndio yale yale ya kuandika chochote ili uonekane umechangia. Nani anavamia nchi ya Tanzania?

Hata hivyo sikushangai sana maana muda mfupi uliopita ulianza kumlaumu Raisi mstaafu kuwa aliruhusu watu kula vyura na kitimoto kwenye hii thread wakati ukijua kabisa hayo yote hayana uhusiano wowote na hii thread.
 
Mara nyingi tuna confuse that which is with that which it ought to be.

Hiyo confusion hiyo, unayoisema ndio Mushi anaifanya hapa:

Sikubaliani na wewe..
Madini na nishati ni rasilimali za TAIFA!
Na kama nchi ikivamiwa leo...Watakaovamia watayachukua hayo madini na pamoja na kulipua vyanzo vya umeme ili kutupa giza watuvamie vizuri...Sasa unasema si usalama wa Taifa huo?

Ulichokisema hapo, Mushi, ni kile wewe unadhani kina make sense kiwe ni sheria. Lakini sio existing law.

Kwa hiyo, reformers lazima kwanza mkubali kwamba under existing law, Rashid Othman sio mzuia wezi. Wa mikufu ya dhahabu au migodi ya dhahabu.

Halafu ndio uanze ku argue kwamba hiyo hai make sense. Lakini mnachokisema sasa hivi, Mushi, pamoja na Zitto (Mh.) na reformers wengine, ni kwamba Usalama umeshindwa kufanya kazi yao. Sasa hilo, kama ni kweli, halihitaji mabadiko ya sheria. Kwa maneno mengine mnasema utendaji ndio mbaya. Ndio maana nikasema watetea ufisadi Bungeni wangeweza kuwazimilia mbali na hizo hoja ambazo hazija pikwa vizuri. Bahati nzuri kwa reformers, CCM ya kina Pinda na Waziri Marmo nao sio wazuri sana katika ku cover mafisadi, as hard as they appear to try.

Unaona how that reform effort is being stymied by being vague in the conception and presentation of existing law?
 

HIVI UKIIWEKA MIGODI MIKONONI MWA WATU BINAFSI BILA KUHAKIKISHA MKATABA NI WA MANUFAA kwa MWANANCHI MNYONGE
JE HUJAUZA UHURU?

Kama mtu anamiliki mgodi kuna tofauti gani na mtu anayeitwa RHODESIA alivyokuwa akiimiliki ZIMBABWE kwa msaada wa MALIKIA na hata kukufuru na kuliita TAIFA kwa jina lake?

KAMA MIGODI YETU NI MOJAWAPO YA RASILIMALI ZETU ZA KUTULISHA NA KUTULETEA MAENDELEO...THEN SI USALAMA WA MWANANCHI NA KIZAZI KIJACHO?

Wamarekani wenyewe walipovamia IRAQ walilinda visima vya mafuta.

Ni lazima hiyo mikataba ipitiwe na usalama wa TAIFA ili kutathmini kama bado inaruhusu UHURU WETU KUWA VALID!

Kwamba uamuzi wa mwisho kuhusu mikataba hiyo uzingatie sheria mpya zitakazo preserve UHURU WETU! Na kunufaika na MALI ZETU.

Sasa hiyo mikataba yenu ni sawa na kumwuzia MKABURU UHURU halafu unasema tuko huru?
 

kuhani.. umeshindwa kuona jambo moja dhahiri katika hoja ya zitto, TISS wameshindwa kufanya kazi zao si kwa sababu ya utendaji bali kutokana na sheria iliyopo. Sheria iliyopo na sera ya usalama wa Taifa (ambayo sijui nani anayo) inafanya vigumu sana kwa usalama wa Taifa kufanya kazi ambayo tunaamini inapaswa kuwepo katika ajenda yao.

Ukiangalia sheria ya Usalama wa Taifa utaona majukumu ya Idara hiyo, majukumu ambayo kimsingi hayasimamii usalama wa Taifa bali kukusanya habari tu.

Hivyo suala la kubadili sheria ni msingi mkubwa wa kuleta mabadiliko katika utendaji.
 
Hivyo suala la kubadili sheria ni msingi mkubwa wa kuleta mabadiliko katika utendaji.

Mkulu Heshima mbele,

Haya ndio maneno tunatakiwa wananchi wote wa Tanzania na wabunge kuwa tunayaimba kila siku, kwa sababu hawa wezi wetu wa bongo siku zote wanazitumia sheria zetu mbovu kutuibia kwenye taifa, the name of the game ni mabadiliko ya katiba kwanza!

Hapa tupo ukurasa mmoja!
 
Jiwe na Hollo, madhabahuni ni mahali patakatifu, mafisadi wa CCM hawasitahili kukanyaga hapo. Wao wanasatahili kupelekwa msalabani kusulubishwa kwa sababu ya ufisadi wao.
 

Tena na tena, mnajichanganya.

"Tunaamini Inapaswa," inapaswa kwa mujibu wa nini, sheria au busara?

"Kukusanya habari," habari zipi, za wezi? Na majambazi wa kuvunja benki pia? Na wapokonya pochi?

"Kuleta mabadiliko katika utendaji," kwani umeshawapa majukumu ya huo utendaji?

Hicho kitu "tunaamini inapaswa iwe ajenda yao" ni kuotea otea kuliko vague. Kama inapaswa kwa kujibu wa mawazo yenu, ina maana mnapendekeza iwe kazi yao. Kama "inapaswa" kwa mujibu wa sheria, tuonyeshe!

Sio kazi yao. Sheria haijipingi na haijawahi kuwapa Usalama kazi ya kuzui au kukusanya habari za wezi wa migodo au wa pochi. Hakuna hicho kitu. Wewe ndio "unaamini" inapaswa iwe kazi yao.

Sema kwanza, "hewala, sio kazi yao." Halafu hatua ya pili ndio sema "sasa tunataka iwe kazi yao."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…