Nasikia raha ya roho,maana Bunge linachemka utadhani tuko Ulaya.Siku hizi wabunge wa CCM wanafoka kwelikweli....na wao...heheheheh...ati hapatoshi hapa.
Ukiona wanapaaza sauti zao bila woga ujue hayo ni mabadiliko makubwa maana wakati wa lile dude liitwalo Mkapa walikuwa kama watoto wa shule ya msingi.
Wakati wa Nyerere Bunge la Chama kimoja wabunge walikuwa ni waumini na Nyerere alikuwa Mungu mtu.mambo serious kama haya yangeweza kumtoa mtu roho wakati huo.Nafurahi kuona mahojiano yakiwaka moto wakati wa awamu ya nne si kwa wabunge tu bali hata wananchi wengine kwenye forums mbalimbali.
Kama hapa naona Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anapewa mkong'oto wa hoja za msingi.hakuna kuambiwa ukakubali na kutiii bali unapewa hoja za wazi.namshukuru mwenyezi Mungu kuwa awamu ya Nne imekuwa ni ya wanamchi kuwaandama mafisadi Bungeni hadi barabarani.This is a step forward in the awakening the peoples minds.
Hapa unakuta watu wanamwita Nyerere fisadi..na wanakupa points...like JMushi.Wengine tunafurahia mijadala ya watu wenye hasira na jinsi mambo yasivyokwenda chap chap kama wanavyotaka wao.
yote haya ni dalili kuwa kunaanza kucha.Akili zinachemka.
Mimi hapa sitajadili mada..ila ndani ya mada naona raha ya mwamko wa watu.Ipo siku watu wote wataamka na kuchukua hatua za kutupatia utawala bora.