Menu yangu ya leo. Karibuni

uuwwwwiiiiii.....
matembele yako wapi sasa? au hata bamia hakuna?
ila hii imetulia mno.....nakuja sasa hivi

hayo hapo nimeongeza, hapa ndo penyewe mboga draft full kujisevia, sema kingine.

images
 
Mama Mdogo mapishi yako vipi? Mimi huwa naona wamama wa kisambaa wanaondoa vichwa kwenye hao wadudu

Hayo ni mapishi ya mwambao wa Ziwa Tanganyika, ambako dagaa ni asili yake, kuanzia kule kwa Wabemba, Wamanyema, Wafipa, Wakonongo, Wanyamwanga hadi kwa Wabemba!!!
 
Acha banaa raha ya ugali (unga wa mahindi uchanganywe na wa muhogo weee!!!) na mboga hio halafu pembeni kuna dagaa wakavu/wabichi au steak ya kuchoma kwenye mkaa au kuku wa kienyeji wa kuchoma na pilipili mbuzi/kichaa. Halafu kuna watu wana dhana kwamba kula ugali kunasababisha kitambi kitu ambacho si kweli miye ni mpenzi mkubwa wa ugali na kitambi kimenipiga chenga na pia kuna watu chungu nzima ambao ni wapenzi wa ugali lakini hawana vitambi.

Kumbe na wewe mpenzi wa Ugali kama mie ..mboga gani unapendelea ili siku ukinitembelea nisibakia kushangaa
Dagaa ,Matembele,Mchicha ,Kisamvu ,Kuku Choma or Majani ya kunde?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom