Menu yangu ya leo. Karibuni

Acha banaa raha ya ugali (unga wa mahindi uchanganywe na wa muhogo weee!!!) na mboga hio halafu pembeni kuna dagaa wakavu/wabichi au steak ya kuchoma kwenye mkaa au kuku wa kienyeji wa kuchoma na pilipili mbuzi/kichaa. Halafu kuna watu wana dhana kwamba kula ugali kunasababisha kitambi kitu ambacho si kweli miye ni mpenzi mkubwa wa ugali na kitambi kimenipiga chenga na pia kuna watu chungu nzima ambao ni wapenzi wa ugali lakini hawana vitambi.

hahaha Pilipili kichaa tena ...Kupika ugali wa mahindi uchanganye na muhogo ni shughuli pevu
Ukiotea ugali kuiva hahaha ..usiseme sijui kupiga

Ugali + maziwa ya mgando?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Jaribu uone utamu wake kama hukuunga tela lol!, lakini kweli shughuli ni pevu.

hahaha Pilipili kichaa tena ...Kupika ugali wa mahindi uchanganye na muhogo ni shughuli pevu
Ukiotea ugali kuiva hahaha ..usiseme sijui kupiga

Ugali + maziwa ya mgando?
 
ha ha haaaa, asante sana, nakuja. ila nikiwa njiani ongezea na dagaa; wawe wamekaangwa na mawese, please.... thank you
Watu wa Kigoma utawajua tu sombe bila mawese halipikwi, dagaa bila maweze hawaivi lol!
 
Kweli leo naona tunakula juisi ya maembe na mapapai na mboga mseto, ukitoka hapo si kuhara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom