Mengi yamefanyika chini ya Mwaka Mmoja. Nayakumbuka haya machache ya Mwaka mmoja wa Rais Samia ongeza yako

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Mengi yamefanyika chini ya Mwaka Mmoja. Nayakumbuka haya machache ya Mwaka mmoja wa Rais Samia ongeza yako…

1. Amepunguza gharama za matibabu ya figo kwa asilimia 66.

2. Amejenga madarasa 1500 nchi nzima.

3. Amevifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa.

4. Amemalizia Ujenzi wa Daraja la Tanzanite.

5. Amepandisha mishahara kwa Wafanyakazi kwa asilimia 23.3

6. Amefuta stakabadhi ghalani kwa mazao ya Pamba,dengu Choroko, mbaazi na Ufuta.

7. Amepandisha bei ya mbaazi kutoka shilingi mia 300 kwa kilo hadi shilingi 3000.

8. Miezi sita ya kwanza ya Rais Samia uwekezaji ulikua kwa 400% Ukafikia US$3BL toka US$510M | Nikaribu mara sita zaidi ya ule wa mtangulizi wake katika kipindi kama hicho.

9. Amepandisha Bajeti ya barabara,madaraja na viwanja vya ndege inaweza kujenga mara mbili ya barabara zote za lami zilizojengwa kwa miaka mitano iliyopita. Barabara zinaendelea kujengwa.

10. Ameongeza bajeti kwa 230% kutoka TZS 1.01T FY2020|21 hadi TZS 2.34T FY2021|22 katika Mradi wa bwawa la Umeme la JNHP.

11. Ametoa zaidi ya TZS 12.6BL kujenga kilometa 12.6 za Lami kuzunguka eneo la Viwanda la Yaani "Ummy Mwalimu Industral Park -Kahama Shinyanga.

12.Amerejesha haki za Binadamu na utawala bora.

13. Siku zote husisitiza wazi kwa wasaidizi wake kufanya kazi kwa kuangalia haki za watu na bila kumuonea mtu.

14. Amerejesha ushirikiano na kati ya Sekta Binafsi na Serikali

15. Amepunguza utegemezi wa misaada na mikopo nafuu toka kwa wahisani ( donor country ) kutoka 8.2% ya bajeti ya FY2020|21 hadi 8.1% FY 2021|22 kwa Serikali ya awamu ya sita imepunguza asilimia za misaada kutoka nje katika bajeti ya maendeleo.

16. Amelipa madeni yenye thamani ya Jumla ya zaidi ya TZS11.17623Trilioni. Yaliyoachwa na mtangulizi wake.

17. Ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 2.17BL ili kuwalipa watoa huduma mbalimbali waliokuwa wanaidai Serikali kutoka katika Wizara mbalimbali.

18. Ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 70.49BL kwaajili ya kuwalipa Wazabuni mbalimbali waliotoa bidhaa na huduma kwa Serikali yetu.

19. Ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 264.23BL kwaajili ya kuwalipa wakandarasi wetu mbalimbali wa nje na ndani waliokuwa wanaidai Serikali.

20. Ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 111.41BL ili kuwalipa watumishi wa Serikali wanaoidai Serikali. Malimbikizo pamoja na viinua mgongo kwa watumishi mbalimbali.

21. Serikali imenunua Jumla ya ambulance mpya 395 na magari mapya 214 kwa ajili ya chanjo kwa mpigo kitu ambacho hakijawahi kufanyika tangu tuwe huru kama Taifa.

22.Akiba ya Fedha zetu za kigeni Imeongezeka kwa TZS 2.3T sasa imefikia $5.8b toka $4.8b mwezi March 2021 | Pesa hii inaweza kulisha Watanzania wote kwa miezi mitatu mfululizo yaani Wale walale tu.

23. Ameruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kurejea shuleni.

25. Ametoa ametoa TZS 520BL za maji Arusha ikiwa ni zaidi ya 80% ya bajeti nzima ya maji ya Taifa ya mwaka. mradi mkubwa wa maji kwa kanda ya Kaskazini.

26. Ameidhinisha Mradi wa Gesi asilia. Mradi huu utatoa ajira za moja kwa moja zaidi ya elfu 15 na ajira ya muda elfu 5 na kuzalisha jumla ya tani 10M za LNG kwa mwaka, utaifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa nne Africa wa Gesi asilia na kuingizia nchi fedha za kigeni zaidi ya $5.5BL au Tshs 13trilion kwa mwaka kwa kuuza hiyo tani 10 kwa bei ya $11 kwa mmbtu, Pesa hii ni sawa na 100% ya bajeti nzima ya "Maendeleo" ya nchi kwa mwaka mmoja wa Fedha.

27. Amerejesha Imani kwenye Utalii kwa kimombo The effects of H. E. Samia Suluhu Hassan Royal Tour has started rapidly showing an extraordinary impacts on tourism sector and tourists attractions all over the country.

28. Ametoa TZS 35BL kujenga uwanja wa ndege wa Musoma Airport.

29. Ameweka historia kwa kujenga madarasa mapya manne ( 4 ) katika kila ilipo shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima | haijawahi kutoka Watoto wote 1M wa kidato cha kwanza nchi nzima kuanza shule siku moja.

30. Ametoa ruzuku ya bilioni 100 kunusuru kupanda kwa bei ya mafuta. Kutokana na mgogoro wa Urusi na Ukraine.

31. Ametengeneza mfuko maalum wa ruzuku kwa ajili ya mbolea kurahisisha bei ya mbole kuwa chini na nafuu kwa wakulima wote.

Yapo mengiiii ongeza…..!!!

IMG-20220518-WA0832.jpg
 
Hii itaifanya Chadema kupotea maana wanaccm mwisho wa siku wanakuwa wamoja kupambana na upinzani

USSR
 
Amekopa sana sana kuliko watangulizi wake, Mwaka mmoja tu ila mikopo kama yote ila yote heri pongezi nyingi kwake kwa ubunifu wa kutafuta vyanzo vya ziada ya mapato kama Tozo na kodi ya jengo kupitia luku, cha msingi kazi iendelee na turejee uchumi wa kati
 
Mama anaupiga mwingi, kila la heri katika kumuombea Mh Rais wetu atusogeze kwenye nchi ya asali na maziwa
 
Mwana mahesabu mmoja atusaidie kujumlisha hizo namba tajwa kisha tuone ukweli na uhalisia.

Nasikia kamalizia Tanzanite, mara barabara huko Kigoma, mara kaongeza bajeti ya bwawa(lililokwama), mara kalipa wakandarasi n.k

Hii haina maana hizo pesa wanalipwa majizi na mafisadi? Madarasa manne kila shule ya sekondari sijaona! Chanjo imenunuliwa magari, mbona dawa nyingi tu zinafika zinakotakiwa kwenda, magari ya kifahari yale ya nini?

Ambulance 395 * 300m = 118.5bn
Magari mapya 214 * 70m = 14.98bn

Karibu tsh 135bn ni magari. Jumlisha na hizo zilizobaki ili tujue hili linchi ni litajiri aje!
 
Mengi yamefanyika chini ya Mwaka Mmoja. Nayakumbuka haya machache ya Mwaka mmoja wa Rais Samia ongeza yako…

1. Amepunguza gharama za matibabu ya figo kwa asilimia 66.

2. Amejenga madarasa 1500 nchi nzima.

3. Amevifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa.

4. Amemalizia Ujenzi wa Daraja la Tanzanite.

5. Amepandisha mishahara kwa Wafanyakazi kwa asilimia 23.3

6. Amefuta stakabadhi ghalani kwa mazao ya Pamba,dengu Choroko, mbaazi na Ufuta.

7. Amepandisha bei ya mbaazi kutoka shilingi mia 300 kwa kilo hadi shilingi 3000.

8. Miezi sita ya kwanza ya Rais Samia uwekezaji ulikua kwa 400% Ukafikia US$3BL toka US$510M | Nikaribu mara sita zaidi ya ule wa mtangulizi wake katika kipindi kama hicho.

9. Amepandisha Bajeti ya barabara,madaraja na viwanja vya ndege inaweza kujenga mara mbili ya barabara zote za lami zilizojengwa kwa miaka mitano iliyopita. Barabara zinaendelea kujengwa.

10. Ameongeza bajeti kwa 230% kutoka TZS 1.01T FY2020|21 hadi TZS 2.34T FY2021|22 katika Mradi wa bwawa la Umeme la JNHP.

11. Ametoa zaidi ya TZS 12.6BL kujenga kilometa 12.6 za Lami kuzunguka eneo la Viwanda la Yaani "Ummy Mwalimu Industral Park -Kahama Shinyanga.

12.Amerejesha haki za Binadamu na utawala bora.

13. Siku zote husisitiza wazi kwa wasaidizi wake kufanya kazi kwa kuangalia haki za watu na bila kumuonea mtu.

14. Amerejesha ushirikiano na kati ya Sekta Binafsi na Serikali

15. Amepunguza utegemezi wa misaada na mikopo nafuu toka kwa wahisani ( donor country ) kutoka 8.2% ya bajeti ya FY2020|21 hadi 8.1% FY 2021|22 kwa Serikali ya awamu ya sita imepunguza asilimia za misaada kutoka nje katika bajeti ya maendeleo.

16. Amelipa madeni yenye thamani ya Jumla ya zaidi ya TZS11.17623Trilioni. Yaliyoachwa na mtangulizi wake.

17. Ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 2.17BL ili kuwalipa watoa huduma mbalimbali waliokuwa wanaidai Serikali kutoka katika Wizara mbalimbali.

18. Ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 70.49BL kwaajili ya kuwalipa Wazabuni mbalimbali waliotoa bidhaa na huduma kwa Serikali yetu.

19. Ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 264.23BL kwaajili ya kuwalipa wakandarasi wetu mbalimbali wa nje na ndani waliokuwa wanaidai Serikali.

20. Ametoa Jumla ya fedha kiasi cha TZS 111.41BL ili kuwalipa watumishi wa Serikali wanaoidai Serikali. Malimbikizo pamoja na viinua mgongo kwa watumishi mbalimbali.

21. Serikali imenunua Jumla ya ambulance mpya 395 na magari mapya 214 kwa ajili ya chanjo kwa mpigo kitu ambacho hakijawahi kufanyika tangu tuwe huru kama Taifa.

22.Akiba ya Fedha zetu za kigeni Imeongezeka kwa TZS 2.3T sasa imefikia $5.8b toka $4.8b mwezi March 2021 | Pesa hii inaweza kulisha Watanzania wote kwa miezi mitatu mfululizo yaani Wale walale tu.

23. Ameruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kurejea shuleni.

25. Ametoa ametoa TZS 520BL za maji Arusha ikiwa ni zaidi ya 80% ya bajeti nzima ya maji ya Taifa ya mwaka. mradi mkubwa wa maji kwa kanda ya Kaskazini.

26. Ameidhinisha Mradi wa Gesi asilia. Mradi huu utatoa ajira za moja kwa moja zaidi ya elfu 15 na ajira ya muda elfu 5 na kuzalisha jumla ya tani 10M za LNG kwa mwaka, utaifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa nne Africa wa Gesi asilia na kuingizia nchi fedha za kigeni zaidi ya $5.5BL au Tshs 13trilion kwa mwaka kwa kuuza hiyo tani 10 kwa bei ya $11 kwa mmbtu, Pesa hii ni sawa na 100% ya bajeti nzima ya "Maendeleo" ya nchi kwa mwaka mmoja wa Fedha.

27. Amerejesha Imani kwenye Utalii kwa kimombo The effects of H. E. Samia Suluhu Hassan Royal Tour has started rapidly showing an extraordinary impacts on tourism sector and tourists attractions all over the country.

28. Ametoa TZS 35BL kujenga uwanja wa ndege wa Musoma Airport.

29. Ameweka historia kwa kujenga madarasa mapya manne ( 4 ) katika kila ilipo shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima | haijawahi kutoka Watoto wote 1M wa kidato cha kwanza nchi nzima kuanza shule siku moja.

30. Ametoa ruzuku ya bilioni 100 kunusuru kupanda kwa bei ya mafuta. Kutokana na mgogoro wa Urusi na Ukraine.

31. Ametengeneza mfuko maalum wa ruzuku kwa ajili ya mbolea kurahisisha bei ya mbole kuwa chini na nafuu kwa wakulima wote.

Yapo mengiiii ongeza…..!!!

View attachment 2229848
Mimi nakapendaga tu hako ka Kanali ka body guard kake! Ila kwenye mafuta na mbolea siyo kwamba amefeli?
 
Hili neno ametoa ni la kis*nge sana.ametoa,ametoa,ametoa kwani ni pesa za mshahara wake?
 
Back
Top Bottom