Mengi: Prof. Muhongo ni muongo

Mengi: Prof. Muhongo ni muongo

Bigirita ,
Ardhi ya Madini haiuzwi, unapewa kwa muda maalum kulingana na ukubwa wa eneo. Siyo ya milele.
Ok, kwahiyo wamempa wenyewe. Sasa kwanini wanasema oooh...anamiliki sijui nini!!

Mimi hizi siasa za kipuuzi sizielewi kabisa. Muhongo anatumia muda wake mwingi kupambana na Mengi, ili iweje?
Anasema wachimbaji wa madini Mererani hawalipi kodi, sasa sisi tufanyeje kama Serikali inashindwa kusimamia hiyo sector na inashindwa kukusanya kodi?

This is ridiculous indeed.....
 
Haya malumbano ya mengi na muhongo haya tusaidii kabisa.

Tumechoshwa na haya malumbano.

Na kama wote wana nia ya dhati kulijenga taifa sidhani kama haya malumbano yange kuwepo.

Ifike wakati wakati wakae chini wamalize tofaiti zao na waelekeze nguvu nyingi kulijenga taifa kuliko haya malumbano.
 
Kweli Dr Mengi anaweweseka facts and figures za last week zilikua siyo Mchezo .... I wish pangekua na video ya alichosema Prof : Muhongo hakusema kampuni ya madini mengi anayomiliki imaukubwa wa dar Es salaam Tatu Bali alisema viwanda anavyomiliki Dr Mengi in total vinaukubwa sawa na dar Es salaam Tatu .... Dr Mengi asipindishe maneno ajibu hoja aseme ukubwa wa viwanda vyake vyote anavyomiliki plus aridhi anavyomiliki wewe kwa shuguli binafsi in total ni ukubwa gani.

Huyu Mzee, kazoea kuishi kwa fitina na uongo.
 
mimi nilishangaa yale ma sqr kms yangeenea wapi ktk ramani ya Tanzania.Hilo swali liliuliza sana humu ,ila watu hawakunotice.
 
Chelsea MZEE wa fact and data shule zenu za kuunga unga Mna ifananisha na Mimi angalie Mimi ni nani
 
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, amesema madai yaliyotolewa dhidi yake na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, hayana ukweli wowote.

Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na wahariri kufafanua kauli mbalimbali, ambazo zimekuwa zikitolewa na waziri huyo dhidi yake.

Dk. Mengi alisema Septemba, mwaka huu, Profesa Muhongo alinukuliwa akisema kwamba, Mengi hana uzawa, bali ana ubinafsi na anataka kufanya udalali wa vitalu vya rasilimali za Watanzania.

“Profesa Muhongo alisema hivi namnukuu: “Mengi hana uzawa, bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu,”
Alisema yeye siyo mbinafsi na pia hajawahi kuomba upendeleo wa kupewa kitalu cha gesi, bali anapigania Watanzania kwa jumla.

Aidha, Dk. Mengi alisema Desemba 8, mwaka huu, alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Waziri Muhongo alitoa takwimu zinazomhusu, ambazo siyo sahihi.

“Ukweli ni kwamba, mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita moja ya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema,” alisema Dk. Mengi.

Aliongeza: “Naomba nisisitize kwamba, mimi binafsi nimeshapata nafasi kubwa ya kujiendeleza kibiashara. Ukweli ni kwamba, ninachopigania leo ni juhudi ya kupanua wigo ili Watanzania wengi waweze kushiriki kama ilivyo kwenye Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004, ambayo inatoa upendeleo maalumu kwa Watanzania katika rasilimali zao.”

Alisema sekta binafsi itapata nafasi ya kipekee leo ya kuwa na mkutano, ambao mwenyekiti wake atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

Alisema yeye binafsi atapata heshima ya kushiriki kama kiongozi wa sekta binafsi chini ya TPSF, hivyo aliona kuna haja ya kufafanua madai yaliyotolewa na Waziri Muhongo kumhusu ili asiende kwenye kikao cha leo zikiwapo fikra kwamba, mambo hayo ni ya kweli.

“Nina matumaini makubwa kwamba, katika mkutano wa kesho (leo), ambao utatoa fursa kwa sekta binafsi kuzungumza na uongozi wa Taifa chini ya uenyekiti wa rais utatuwezesha kupata muafaka wa jinsi gani tutashirikiana katika juhudi za kuwawezesha Watanzania kwenye nyanja mbalimbali za uchumi wetu,” alisema Dk. Mengi.

CHANZO: NIPASHE
 
conflict of interest between the two.😛lane:
 
Mzee Mengi naona kazi kulia lia tu kila siku!!
 
Kazi kwao hapo tutasikia mafisadi nyangumi na papapa hata makambale,sato nk.
 
Ngoja uletwe ushahidi wa hati ndio atajulikana muongo
Kuwa na Tv then ukayumbisha watu pia ni uongo na uzandiki ulokubuhu
 
mengi anachosema ni kweli mtupu, nchi hii tumebakia kukaribisha ukoloni mamboleo kwa njia ya uwekezaji.
Napata tabu kama huyu jamaa ni prof, huwezi kuwa na mawazo ya kutoweza.
 
Nilikuwepo kwenye mjadala Nkurumah hall. Mengi ni mkweli na kongamano halikutoa fursa kwa washiriki kuuliza ama kuhoji data aliyokuja nayo waziri mwenye dhamana. Ninashangaa sana watz. tunashnilia nini ktk hoja za Muhongo.
 
Hallow mimi nilikubali speech za prof. Ni kweli tanzania inaumizwa na watanzania kwani mengi katika speech yote ya prof. Ameona la kujibia ni hili la dar es salaam tatu?vipi kuhusu zile gharama za uwekezaji anazimudu?watu wampatie?mimi naona mengi ni walewale tu kulilia maslahi yake,kwani akipewa nafasi katika gesi ni maisha yake au ya watanzania?na hilo eneo analomliki ni maisha yake na watoto wake na klyn au ya watanzania.
Mkuu juzi juzi Wizara ilikuwa inanadi Vitalu kwa watu wenye uwezo wa kuvinunua - sina shaka Ndugu Mengi alinunua idadi ya kutosha, binafsi sitegemie kama atatumia vyombo vyake vya habari tena kuhitisha midahalo ambayo mwisho wa siku anabaki amehumbuka tu.
 
Mengi ameshindwa mjadala anakuja kuseeck public sympathy, ni wajinga wasiopenda kuumiza kichwa wataacha kumsikiliza geologist prof sos mhongo na kumsikiliza mengi na porojo zake.

wewe ndio uwezo wako wa kufikiri ni mdogo ingekuwa kweli muhongo angeshindwa toa document za hatimiliki??? document za hatimiliki ziko wapi? penda ushahidi ktkt hoja kuliko utamu wa maneno!!!
 
Back
Top Bottom