Mengi: Prof. Muhongo ni muongo

Mengi: Prof. Muhongo ni muongo

Mnasahau kitu kimoja, Mengi alipewa udaktari mezani ila waziri yeye ni Profesa cheo cha taaluma ( academic title). siku ile Prof hakupepesa macho alitanguliza sayansi mbele. Mengi yeye ataka kutumia thesis yake ya masters kumdaganya Profesa, Data zote zipo Mengi aache kuwadanganya wa tz atahaibika akiendelea na ubishi wake.
 
Kweli Dr Mengi anaweweseka
facts and figures za last week zilikua siyo Mchezo .... I wish pangekua
na video ya alichosema Prof : Muhongo hakusema kampuni ya madini mengi
anayomiliki imaukubwa wa dar Es salaam Tatu Bali alisema viwanda
anavyomiliki Dr Mengi in total vinaukubwa sawa na dar Es salaam Tatu
.... Dr Mengi asipindishe maneno ajibu hoja aseme ukubwa wa viwanda
vyake vyote anavyomiliki plus aridhi anavyomiliki wewe kwa shuguli
binafsi in total ni ukubwa gani.

Ndugu hii inaingia akilini? viko wapi? mara tatu ya dar! wapi?
 
Mengi ameshindwa mjadala anakuja kuseeck public sympathy, ni wajinga wasiopenda kuumiza kichwa wataacha kumsikiliza geologist prof sos mhongo na kumsikiliza mengi na porojo zake.

Kila mtu anasikilizwa kwa wakati wake...Muhongo alisema na tukamsikia,why Mengi tusimsikilize!? Hofu yako ni Nini?
 
Mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa nchi hii ina wananchi wanaopenda na kushabikia uongo na uzushi bila hata kujipa muda wa kufanya uchunguzi kidogo wa mambo wanayoelezwa na kiongozi ama wa serikali au wa siasa, na hasa mtu huyo akiitwa Profesa au Dokta, au akisema ana elimu ya chuo kikuu ya shahada au shahada ya uzamili (masters). Watanzania wanadanganyika na makaratasi ya chuo yanayoitwa shahada. wanaamini mtu mwenye shahada basi anajua kila kitu na msema ukweli, kumbe wapi, hao ndiyo wezi wakubwa wa rasilimali za nchi yetu. Huyu waziri anayeitwa muhogo sijui muhongo ni kibaraka mkubwa wa wazungu, ni mtumwa wa wazungu ambaye hatamani hata uhuru, yeye anamwamini mzungu kuliko hata baba na mama yake, anatamani angezaliwa na baba na mama wazungu, shame on him! Huyu waziri tangu ateuliwe kushika wizara hiyo kazi yake ni moja tu, kuwapiga vita wafanyabiashara wazawa, kuwapiga vita watanzania wanaojishughulisha kukuza uchumi wao na wa nchi, kazi yake kuwashambulia na kuwazuia wazawa kushiriki katika kujenga uchumi wa nchi yao, anawazuia watanzania kunufaika na rasilimali za nchi yao, anataka kila kitu wamiliki wageni, mabwana zake wazungu, huyu si adui wa Reginald Mengi pekee bali ni adui wa wafanyabiashara wote wazawa, ni adui wa watanzania wote wazawa, na anapaswa kupigwa vita na kila mtanzania mzawa mpaka atakapobadili mtazamo wako dhidi ya watanzania wenzake au mpaka atakapoondolewa katika utumishi wa umma. Mimi kwa upande wangu kama mwandishi wa habari, mwaka huu niliandika makala ya kumsema huyu waziri ikiwa ni mchango wangu wa kuhakikisha hili joka tunalitimua katika nyumba yetu, nimeamua kuiweka makala hii ndani ya JF ili watanzania wenzangu wenye mapenzi mema na nchi yetu wachangie. ............................................................................................................................................................................. WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametutukana na kutudhalilisha Watanzania. Amesema eti sisi hatuna haki wala hatustahili kushirikishwa katika kujua na kuamua sera na hata kupatiwa fursa ya kumiliki miradi ya gesi yetu kwa kile alichodai kuwa hatuna uwezo wa kuivuna. Amesema eti sisi ni hohehahe ambao uwezo wetu hauruhusu kupewa fursa ya kufanya biashara ya kuwekeza katika gesi, bali tunaweza kujihusisha na biashara za soda, juisi, machungwa, maembe, mapeasi na uchuuzi mwingine usiohitaji mitaji mikubwa. Matusi hayo ya Profesa Muhongo dhidi ya Watanzania ameyatoa kupitia kwa mfanyabiashara mzalendo Reginald Mengi. Matusi na udhalilishaji huo dhidi ya Mengi vilikuja baada ya mfanyabiashara huyo mwenye mapenzi ya dhati kwa Watanzania na taifa kwa ujumla kuitaka serikali kusitisha zoezi la kugawa vitalu vya gesi hadi pale sera ya taifa ya gesi itakapokuwa tayari imeandaliwa. Mengi alikuwa akitoa rai hiyo kwa serikali kwa niaba ya Taasisi ya sekta binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation – TPSF) ambayo yeye ni mwenyekiti wake. Katika maoni yake, TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Watanzania katika uchumi wa gesi na kuishauri serikali kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi hadi sera ya gesi itakapokuwa tayari na taasisi hiyo iliomba kukutana na Waziri Muhongo kwa mashauriano zaidi. Katika kumdhalilisha zaidi Mengi, Waziri Muhongo amediriki kumuita kuwa si mzawa wa kweli bali ni mbinafsi, dalali, na mlanguzi wa rasilimali za Watanzania. Waziri Muhongo amedai kuwa Mengi na kundi lake wanataka vitalu ili wafanye ulanguzi wa gesi na mafuta ya Watanzania. Kama nilivyotangulia kusema hapo juu, kwamba matusi na dharau za Waziri Muhongo havikumlenga Mengi tu, bali Watanzania wote. Kwamba, mtazamo wa Waziri Muhongo ni juu ya Watanzania wote, ndiyo maana akasema: “Watanzania uwezo wao ni biashara za soda, juisi na maembe, siyo gesi wala mafuta.” Hebu jiulize Mtanzania mwenye akili sawa sawa, hivi kama Mengi katukanwa na kudharauliwa kwa kiwango hicho, nani kabakizwa? Hivi kama waziri hawezi kumheshimu Mengi, ataweza kweli kumheshimu babu na bibi zangu wanaolima kule kijijini kwetu kwa kutumia jembe la mkono? Hivi Waziri Muhongo atawaheshimu kweli wamachinga wanaoshinda kutwa nzima wakitembea jiji lote la Dar es Salaam wakitembeza mashati mawili? Waziri Muhongo anawaheshimu, kuwanyenyekea, kuwaabudu wageni wanaokuja hapa nchini kwa koti la “wawekezaji”, huku wakiwa hawana chochote, lakini hutajirika ghafla kwa kutumia rasilimali zetu. Mtazamo wa Waziri Muhongo ni kwamba uwekezaji mkubwa ukiwemo ule wa sekta ya gesi, mafuta, dhahabu, almasi na vingine hauwezi kufanywa na Watanzania wazawa. Kwamba hiyo ni biashara ya Wazungu, Wachina au Wahindi. Waziri Muhongo hawaamini waswahili wenzake, anawaona wababaishaji, madalali na walanguzi! Waziri Muhongo hayuko pekee yake katika mtazamo huu. Baadhi ya viongozi katika serikali, katika chama tawala na hata katika chombo cha kutunga sheria, yaani Bunge, wamekuwa watetezi wakubwa wa wafanyabiashara wageni. Kibaya zaidi, baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya wafanyabiashara wa kigeni kuwakwamisha wafanyabiashara wazawa. Wamo watu ndani ya serikali yetu, Bunge na chama tawala (CCM) ambao ni mawakala wa wageni hawa. Wanawapa kandarasi mbalimbali za mabilioni ya fedha na kuwanyima Watanzania wazawa. Wakati mwingine baadhi ya wabunge wanatumwa kwenda bungeni kuwashambulia wafanyabiashara wazawa kwa lengo la kuwakwamisha. Nimeambiwa hata baadhi ya taasisi za fedha nchini kama benki nazo zimekuwa zikitumiwa na wafanyabiashara wageni kuwakwamisha wazawa kwa kuwanyima mikopo au kuwawekea mazingira magumu ya kuipata. Ikumbukwe kuwa hakuna benki hata moja nchini inayomilikiwa na wazawa, nyingi ni za wageni. Waziri Muhongo na viongozi wengine wa serikali wenye mtazamo hasi dhidi ya Watanzania wazawa wanapaswa kujua kuwa hao wafanyabiashara wa kigeni siyo matajiri kiasi hicho, bali huwezeshwa na serikali zao kuja kuwekeza hapa kwetu kwa kupewa dhamana ya mikopo katika mabenki ya kwao. Makampuni yote yaliyowekeza leo katika sekta ya madini nchini yamekopa mabilioni ya dola katika mabenki ya kwao kwa dhamana ya serikali zao. Hata hayo makampuni yanayoomba vitalu vya gesi na mafuta pia yamekopa huko kwao. Hakuna kampuni inayoweza kuja hapa kuwekeza bila kukopa, haiwezekani. Na hapa ndipo hoja ya waziri wa zamani wa viwanda na biashara, Idd Simba ya kutaka uanzishwe utaratibu wa kisera na kisheria wa kuwawezesha Watanzania wazawa kibiashara inapopata nguvu. Simba alianzisha hoja hiyo kutokana na ukweli usiopingika, kwamba mfumo wa kiuchumi wa kikoloni uliwapendelea Wazungu, Wahindi na Waarabu kwa kuwapa fursa za kufanya biashara zote kubwa na kuwaacha pembezoni wenye nchi. Hata hivyo, hoja ya Simba ilipata upinzani kutoka kwa wafanyabiashara wenye asili ya kigeni pamoja na mawakala wao, hususan wanasiasa watawala wenye mtazamo kama wa Waziri Muhongo, ambao kwa kiasi kikubwa wananufaika na mfumo wa sasa. Hoja iliyokuwa ikitolewa na wapinzani wa mtazamo wa Simba ni kwamba kuanzisha upendeleo maalumu wa kiuchumi kwa jamii fulani ya watu katika nchi kwa kuzingatia rangi au tofauti nyingine yoyote, ni tangazo la wazi la sera ya ubaguzi, jambo walilosema ni kinyume cha katiba na sera ya nchi yetu. Hata hivyo, naamini kuwa Simba alikuwa na hoja nzito iliyopaswa kufanyiwa kazi, si hoja ya kubishaniwa kwamba umaskini unaowakabili Watanzania wengi wazawa si wa bahati mbaya, bali ni wa kutengenezwa. Mfumo wa kiuchumi wa watawala wa kikoloni uliwabagua Waswahili na kuwapendelea Wazungu, Wahindi na Waarabu. Wakati wa ukoloni, biashara zote kubwa zilimilikiwa na Wazungu na zile za kati zilikuwa mikononi mwa Wahindi na Waarabu. Kwa mfano, viwanda na mashamba makubwa vyote vilikuwa vikimilikiwa na wafanyabiashara wa Kizungu na serikali ya kikoloni iliwapa kila aina ya msaada ikiwamo ruzuku ili kuwawezesha kupata mafanikio ya kiuchumi, hivyo kuwasaidia kututawala. Wahindi na Waarabu nao walipewa fursa ya kufanya biashara zote za kati na kupata mafanikio ya kiuchumi kwa sababu wakoloni hawakuwa na hofu yoyote ya kuhatarisha utawala wao kwani walijua wazi kuwa hawakuwa wenyeji wa Tanganyika, hivyo wasingejihusisha na harakati zozote za kupinga utawala wao. Wakoloni waliwatenga wazee wetu na mfumo wa kiuchumi kwa hofu kuwa kama wangepata nguvu za kiuchumi wangeanzisha harakati za kisiasa za kupinga kutawaliwa na wageni, hivyo kuhatarisha mamlaka yao ya kuendelea kuwatawala na kuwanyonya Watanganyika. Matokeo yake, leo hii uchumi wa nchi unadhibitiwa na wageni. Biashara zote kubwa hapa nchini zinamilikiwa na wageni. Angalia orodha ya matajiri zaidi ya 10 nchini iliyotolewa hivi karibuni ambayo Waswahili ni wawili tu. Kwahiyo, ni hoja yenye mashiko leo kutaka kuanzishwa kwa mfumo wa kisera na kisheria wa kutoa upendeleo maalumu wa kiuchumi kwa wazalendo, kwa lengo la kurekebisha dhambi ya ubaguzi waliyotendewa wazee wetu wakati wa ukoloni, ambayo madhara yake yanaendelea hadi sasa. Kukataa hoja hii ni kujifanya vipofu wa ukweli, huko ni sawa na kuendeleza ubaguzi wa wakati wa ukoloni, ni mwendelezo wa kuwazuia na kuwatenga na mfumo wa kiuchumi Watanzania weusi ambao ndio wengi nchini, jambo ambalo ni hatari kwa amani ya taifa. Mwaka 1994, serikali ya kizalendo ya Chama cha African National Congress (ANC) ilichagua kutekeleza sheria ya ‘affirmative action’ kwa lengo la kurekebisha ubaguzi wa zamani. mwisho.

Halafu uanze kusema maisha magumu muda wa kuandika mane no yote hay a umeutoa wapi vinginevyo unalipwa kwa kazi yako nzuri uliyotumwa kuifanya
 
mjadala umefanywa tarehe 8 unajibu tarehe 15 ulikuwa wapi kukanusha siku iliyofuata afu kama sijasahau professor hakusema mengi eneo la kitalu cha gesi kama sijasahau alisema mengi ana eneo lenye leseni ya uchimbaji wa madini na sio gesi mengi anatafuta huruma ya wananchi afu simple logic 1 sq km si ni 1000 sq metres hivi mengi na pesa alizonazo ni wakutudanganya hivyo. hayo maeneo si ndo tunayoyasikia yanauzwa kwa million 800 hadi bil 1.hata kama hatumpendi muhongo lakini kuna vitu tunapaswa ku reason with simple logic. Mengi si wakumiliki mita 1000 pekee viwanda vyake tu vinazidi sasa kwenye madini je. na ujue kadri unavyopewa eneo kubwa ndivyo probability ya kutengeneza faida inaongezeka acheni majungu hebu tuache story za vijiweni sio muda wa busara na hekima. Tuheshimu taaluma hizi siasa zimeshatugharimu vya kutosha

Huwezi Kula na Kunya kwa mda ule ule... Lazima chakula kiyeyuke ndipo Unye...
 
Mnasahau kitu kimoja, Mengi alipewa udaktari mezani ila waziri yeye ni Profesa cheo cha taaluma ( academic title). siku ile Prof hakupepesa macho alitanguliza sayansi mbele. Mengi yeye ataka kutumia thesis yake ya masters kumdaganya Profesa, Data zote zipo Mengi aache kuwadanganya wa tz atahaibika akiendelea na ubishi wake.

TCU walishakanusha doctorate ya Mengi kutambuliwa Tanzania. Mengi ni Dr only kwenye ITV na wanaomuabudu tu.
 
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP,bwana Reginald Mengi,ameseme kauli iliyotolewa na Prof.Muhongo hivi karibuni katika kongomano linalohusu uwekezaji si ya kweli.Katika kongamano hilo,Prof.Muhongo alidai kuwa Mengi anamiliki eneo la mgodi ambalo ukubwa wake ni sawa na mara tatu ya eneo zima la mkoa wa Dar-es-salaam.

Hata hivyo,bwana Mengi amekanusha taarifa hiyo na kudai yeye anamilki eneo la takribani 1 square km tu.Mh.Mengi ametoa maelezo hayo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Binafsi niliona kongamano hilo ambalo hata Mengi nae alihudhuria.Katika kongamano hilo, Prof Muhongo alikuwa anajisifu,tena kwa kurudiarudia, kuwa yeye kama mwanasayansi anaongea kwa "facts na data" alafu kumbe data zenyewe ni za kupika!Katika kongamano lile Muhongo alitamka bila aibu kwa kusema "Mengi anamiliki Dar-es-salaam tatu".

Mimi naona huyu waziri si mzigo tu bali ni kizingiti cha maendeleo.

CHANZO:ITV

Ukweli siyo unamiliki neo kubwa kiasi gani bali eneo hilo lina wingi kiasi gani ya madini. Satasi ya kifisadi
 
major mwendwa said:
...afu simple logic 1 sq km si ni 1000 sq metres hivi mengi na pesa alizonazo ni wakutudanganya hivyo. ...
Duh! Kaazi kweli kweli
 
mawaziri wa jk wote majanga kama raisi ni dhaifu unategemea waliopo chini yake chini yake watakuwa ccm chama chakavu kama mawaziri wake
 
Huyu mengi tamaa imemzidi kila kitu anataka mkono wake yeye tu uwepo? Hana biashara yoyote kwenye msururu wa biashara-tamaa zake ambayo ina mfano wa biashara ya kufua gesi. Unafikiri mradi wa gesi ni sawa na kutengeneza penseli na visima vya maji ya kunywa? Halafu hapo hapo kelele apige kwenye TV na radio stations zake lukuki na magazeti yake yasiyohesabika! Tamaa imekuzidi mzee wewe! Huna hata aibu! Mtu unawauzia watu hata maji ya kunywa mamilioni ya lita kila siku, hutosheki? Jenga basi hata hospitali moja yenye hadhi ya Muhimbili au University kubwa angalau urudishe kwa wananchi
 
Pofessor Muhongo's point ni kwamba Mengi ana tamaa. Hata kama atakuwa ame-exaggerate ukubwa wa maeneno anayomiliki Mengi, lakini he succeeded in making in his point.
 
nahic hata hyo muhongo alkuw hana cha kuwaambia audience kw wakat ule..thus why aka2mia uongo!!
 
alitakiwa saa 3 asb tar10 aende akapatiwe kitalu kwa vigezo stahiki je alikwenda???
 
Back
Top Bottom