Mengi: Prof. Muhongo ni muongo

Mengi: Prof. Muhongo ni muongo

Kweli Dr Mengi anaweweseka facts and figures za last week zilikua siyo Mchezo .... I wish pangekua na video ya alichosema Prof : Muhongo hakusema kampuni ya madini mengi anayomiliki imaukubwa wa dar Es salaam Tatu Bali alisema viwanda anavyomiliki Dr Mengi in total vinaukubwa sawa na dar Es salaam Tatu .... Dr Mengi asipindishe maneno ajibu hoja aseme ukubwa wa viwanda vyake vyote anavyomiliki plus aridhi anavyomiliki wewe kwa shuguli binafsi in total ni ukubwa gani.

Kwa hili ulilosemA si kweli ndugu. Prof alionyesha vitalu anavyomilik Mengi kuwa ni eneo linalozidi mara tatu ya eneo mkoa wa Dar es Salaam. Tafuta ile presentation(slide show) ya prof utaona ni ardhi ya madini(vitalu) na siyo viwanda na vitalu. Kwa ufafanuzi mkoa wa Dar es Salaam(siyo jiji la Dar es Salaam) una eneo la kilometa za mraba 1800. Hii inahusisha eneo hadi kule pwani ya Kigamboni kama Pemba mnazi ambalo halijaendelezwa kabisa! Kuna kitongoji kimoja huko Kigamboni umbali wake ni km64 kutoka ferry, ni mashambani kabisa. Umbali huo ni sawa na kutoka Dar City Centre hadi Mlandizi(km65) au Bagamoyo(km65 pia)!
 
Mengi kazidi bana..tumekuchoka huna lolote unalosaidia maendeleo ya watanzania
 
Ushahidi uko wa kutosha kuthibitisha uongo wa huyu jamaa, kama hutaki kuuona ushahidi huo basi hilo si tatizo langu. Siku za nyuma nimeshajadili kwa kina kuonyesha uongo wa huyu jamaa. Tuliambiwa Madini na Nishati sasa itaongozwa na kichwa lakini hakuna tofauti yoyote na Ngeleja. Shukrani kwa heshima zako kwangu Mkuu nami nakuheshimu sana.

mkuu BAK nakuheshimu sana lakini nahisi una negative attitude kwa professor kaa na ufikilie chini hii imekaa kimipasho na pengine nachelea kusema umeteleza baba angu sababu kuna tofauti kubwa kati ya muongo na muhongo. Hebu weka pembeni majina na jadili hoja za hao wote wawili professor na doctor.:smile-big:
 
Mimi mwenyewe nimemuona kwenye taarifa ya habari anasema ana mgodi mmoja wa TANZANITE mdogo tu.
 
mjadala umefanywa tarehe 8 unajibu tarehe 15 ulikuwa wapi kukanusha siku iliyofuata afu kama sijasahau professor hakusema mengi eneo la kitalu cha gesi kama sijasahau alisema mengi ana eneo lenye leseni ya uchimbaji wa madini na sio gesi mengi anatafuta huruma ya wananchi afu simple logic 1 sq km si ni 1000 sq metres hivi mengi na pesa alizonazo ni wakutudanganya hivyo. hayo maeneo si ndo tunayoyasikia yanauzwa kwa million 800 hadi bil 1.hata kama hatumpendi muhongo lakini kuna vitu tunapaswa ku reason with simple logic. Mengi si wakumiliki mita 1000 pekee viwanda vyake tu vinazidi sasa kwenye madini je. na ujue kadri unavyopewa eneo kubwa ndivyo probability ya kutengeneza faida inaongezeka acheni majungu hebu tuache story za vijiweni sio muda wa busara na hekima. Tuheshimu taaluma hizi siasa zimeshatugharimu vya kutosha

Tatizo la pale kwenye mjadala hewa au sijui niseme presentation Muhongo ndiyo alikuwa wa mwisho kuhitimisha from there hakukuwa na mtu wa kuuliza/ kuhoji/kusema chochote.
Kwahiyo alichosema Muhongo ndiyo umebaki nacho.
Nadhani pale ilitakiwa HARD Debate ya facts kutoka kila upande ili wananchi turidhike na ukweli from each side
 
Kuna watu walikuwa wanapendekeza Zitto apewe wizara ya Nishati na Madini.
Zitto angekuwa naibu wake sijui hii wizara ingekuwaje tena!!
 
Mengi kazidi bana..tumekuchoka huna lolote unalosaidia maendeleo ya watanzania

huyu mr. mengi anachojua ni kuzaa na vbinti vidpgo vya bongo fleva tu kina kylne badala ya kuachia vijana ...mengi mnafki sjawahi kumkubali anaiba bilion 1 anagawa milioni 60 kujsafsha nyangumi tu hana jpya...mwsho mengi hana phd kumuita dr. ni kosa ksheria
 
Mimi mwenyewe nimemuona kwenye taarifa ya habari anasema ana mgodi mmoja wa TANZANITE mdogo tu.

Kuja Ar Mererani tukuonyeshe kitu Afgerm(chinja matata, kaburu ) anapakua hapo chini, wacha utani nchi imeuzwa hii.
Ukiona Mengi anaongea yeye yupo ndani ya ngoma anaicheza anajua kila kitu kinachoendelea,wewe umekaa Bagamoyo unacheza bao baba'ako ana-sign mikataba tu.
Nchi inaliwa haswa, wanahakikisha wanaicha mashimo TU
 
Kuna watu walikuwa wanapendekeza Zitto apewe wizara ya Nishati na Madini.
Zitto angekuwa naibu wake sijui hii wizara ingekuwaje tena!!

zito kwan ana tatzo gan au kisa sababu anywi vroba vya ufpa chadema na kutembea na sumu kama vjana wa redbrgade
 
Mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa nchi hii ina wananchi wanaopenda na kushabikia uongo na uzushi bila hata kujipa muda wa kufanya uchunguzi kidogo wa mambo wanayoelezwa na kiongozi ama wa serikali au wa siasa, na hasa mtu huyo akiitwa Profesa au Dokta, au akisema ana elimu ya chuo kikuu ya shahada au shahada ya uzamili (masters). Watanzania wanadanganyika na makaratasi ya chuo yanayoitwa shahada. wanaamini mtu mwenye shahada basi anajua kila kitu na msema ukweli, kumbe wapi, hao ndiyo wezi wakubwa wa rasilimali za nchi yetu. Huyu waziri anayeitwa muhogo sijui muhongo ni kibaraka mkubwa wa wazungu, ni mtumwa wa wazungu ambaye hatamani hata uhuru, yeye anamwamini mzungu kuliko hata baba na mama yake, anatamani angezaliwa na baba na mama wazungu, shame on him! Huyu waziri tangu ateuliwe kushika wizara hiyo kazi yake ni moja tu, kuwapiga vita wafanyabiashara wazawa, kuwapiga vita watanzania wanaojishughulisha kukuza uchumi wao na wa nchi, kazi yake kuwashambulia na kuwazuia wazawa kushiriki katika kujenga uchumi wa nchi yao, anawazuia watanzania kunufaika na rasilimali za nchi yao, anataka kila kitu wamiliki wageni, mabwana zake wazungu, huyu si adui wa Reginald Mengi pekee bali ni adui wa wafanyabiashara wote wazawa, ni adui wa watanzania wote wazawa, na anapaswa kupigwa vita na kila mtanzania mzawa mpaka atakapobadili mtazamo wako dhidi ya watanzania wenzake au mpaka atakapoondolewa katika utumishi wa umma. Mimi kwa upande wangu kama mwandishi wa habari, mwaka huu niliandika makala ya kumsema huyu waziri ikiwa ni mchango wangu wa kuhakikisha hili joka tunalitimua katika nyumba yetu, nimeamua kuiweka makala hii ndani ya JF ili watanzania wenzangu wenye mapenzi mema na nchi yetu wachangie. ............................................................................................................................................................................. WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametutukana na kutudhalilisha Watanzania. Amesema eti sisi hatuna haki wala hatustahili kushirikishwa katika kujua na kuamua sera na hata kupatiwa fursa ya kumiliki miradi ya gesi yetu kwa kile alichodai kuwa hatuna uwezo wa kuivuna. Amesema eti sisi ni hohehahe ambao uwezo wetu hauruhusu kupewa fursa ya kufanya biashara ya kuwekeza katika gesi, bali tunaweza kujihusisha na biashara za soda, juisi, machungwa, maembe, mapeasi na uchuuzi mwingine usiohitaji mitaji mikubwa. Matusi hayo ya Profesa Muhongo dhidi ya Watanzania ameyatoa kupitia kwa mfanyabiashara mzalendo Reginald Mengi. Matusi na udhalilishaji huo dhidi ya Mengi vilikuja baada ya mfanyabiashara huyo mwenye mapenzi ya dhati kwa Watanzania na taifa kwa ujumla kuitaka serikali kusitisha zoezi la kugawa vitalu vya gesi hadi pale sera ya taifa ya gesi itakapokuwa tayari imeandaliwa. Mengi alikuwa akitoa rai hiyo kwa serikali kwa niaba ya Taasisi ya sekta binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation – TPSF) ambayo yeye ni mwenyekiti wake. Katika maoni yake, TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Watanzania katika uchumi wa gesi na kuishauri serikali kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi hadi sera ya gesi itakapokuwa tayari na taasisi hiyo iliomba kukutana na Waziri Muhongo kwa mashauriano zaidi. Katika kumdhalilisha zaidi Mengi, Waziri Muhongo amediriki kumuita kuwa si mzawa wa kweli bali ni mbinafsi, dalali, na mlanguzi wa rasilimali za Watanzania. Waziri Muhongo amedai kuwa Mengi na kundi lake wanataka vitalu ili wafanye ulanguzi wa gesi na mafuta ya Watanzania. Kama nilivyotangulia kusema hapo juu, kwamba matusi na dharau za Waziri Muhongo havikumlenga Mengi tu, bali Watanzania wote. Kwamba, mtazamo wa Waziri Muhongo ni juu ya Watanzania wote, ndiyo maana akasema: “Watanzania uwezo wao ni biashara za soda, juisi na maembe, siyo gesi wala mafuta.” Hebu jiulize Mtanzania mwenye akili sawa sawa, hivi kama Mengi katukanwa na kudharauliwa kwa kiwango hicho, nani kabakizwa? Hivi kama waziri hawezi kumheshimu Mengi, ataweza kweli kumheshimu babu na bibi zangu wanaolima kule kijijini kwetu kwa kutumia jembe la mkono? Hivi Waziri Muhongo atawaheshimu kweli wamachinga wanaoshinda kutwa nzima wakitembea jiji lote la Dar es Salaam wakitembeza mashati mawili? Waziri Muhongo anawaheshimu, kuwanyenyekea, kuwaabudu wageni wanaokuja hapa nchini kwa koti la “wawekezaji”, huku wakiwa hawana chochote, lakini hutajirika ghafla kwa kutumia rasilimali zetu. Mtazamo wa Waziri Muhongo ni kwamba uwekezaji mkubwa ukiwemo ule wa sekta ya gesi, mafuta, dhahabu, almasi na vingine hauwezi kufanywa na Watanzania wazawa. Kwamba hiyo ni biashara ya Wazungu, Wachina au Wahindi. Waziri Muhongo hawaamini waswahili wenzake, anawaona wababaishaji, madalali na walanguzi! Waziri Muhongo hayuko pekee yake katika mtazamo huu. Baadhi ya viongozi katika serikali, katika chama tawala na hata katika chombo cha kutunga sheria, yaani Bunge, wamekuwa watetezi wakubwa wa wafanyabiashara wageni. Kibaya zaidi, baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya wafanyabiashara wa kigeni kuwakwamisha wafanyabiashara wazawa. Wamo watu ndani ya serikali yetu, Bunge na chama tawala (CCM) ambao ni mawakala wa wageni hawa. Wanawapa kandarasi mbalimbali za mabilioni ya fedha na kuwanyima Watanzania wazawa. Wakati mwingine baadhi ya wabunge wanatumwa kwenda bungeni kuwashambulia wafanyabiashara wazawa kwa lengo la kuwakwamisha. Nimeambiwa hata baadhi ya taasisi za fedha nchini kama benki nazo zimekuwa zikitumiwa na wafanyabiashara wageni kuwakwamisha wazawa kwa kuwanyima mikopo au kuwawekea mazingira magumu ya kuipata. Ikumbukwe kuwa hakuna benki hata moja nchini inayomilikiwa na wazawa, nyingi ni za wageni. Waziri Muhongo na viongozi wengine wa serikali wenye mtazamo hasi dhidi ya Watanzania wazawa wanapaswa kujua kuwa hao wafanyabiashara wa kigeni siyo matajiri kiasi hicho, bali huwezeshwa na serikali zao kuja kuwekeza hapa kwetu kwa kupewa dhamana ya mikopo katika mabenki ya kwao. Makampuni yote yaliyowekeza leo katika sekta ya madini nchini yamekopa mabilioni ya dola katika mabenki ya kwao kwa dhamana ya serikali zao. Hata hayo makampuni yanayoomba vitalu vya gesi na mafuta pia yamekopa huko kwao. Hakuna kampuni inayoweza kuja hapa kuwekeza bila kukopa, haiwezekani. Na hapa ndipo hoja ya waziri wa zamani wa viwanda na biashara, Idd Simba ya kutaka uanzishwe utaratibu wa kisera na kisheria wa kuwawezesha Watanzania wazawa kibiashara inapopata nguvu. Simba alianzisha hoja hiyo kutokana na ukweli usiopingika, kwamba mfumo wa kiuchumi wa kikoloni uliwapendelea Wazungu, Wahindi na Waarabu kwa kuwapa fursa za kufanya biashara zote kubwa na kuwaacha pembezoni wenye nchi. Hata hivyo, hoja ya Simba ilipata upinzani kutoka kwa wafanyabiashara wenye asili ya kigeni pamoja na mawakala wao, hususan wanasiasa watawala wenye mtazamo kama wa Waziri Muhongo, ambao kwa kiasi kikubwa wananufaika na mfumo wa sasa. Hoja iliyokuwa ikitolewa na wapinzani wa mtazamo wa Simba ni kwamba kuanzisha upendeleo maalumu wa kiuchumi kwa jamii fulani ya watu katika nchi kwa kuzingatia rangi au tofauti nyingine yoyote, ni tangazo la wazi la sera ya ubaguzi, jambo walilosema ni kinyume cha katiba na sera ya nchi yetu. Hata hivyo, naamini kuwa Simba alikuwa na hoja nzito iliyopaswa kufanyiwa kazi, si hoja ya kubishaniwa kwamba umaskini unaowakabili Watanzania wengi wazawa si wa bahati mbaya, bali ni wa kutengenezwa. Mfumo wa kiuchumi wa watawala wa kikoloni uliwabagua Waswahili na kuwapendelea Wazungu, Wahindi na Waarabu. Wakati wa ukoloni, biashara zote kubwa zilimilikiwa na Wazungu na zile za kati zilikuwa mikononi mwa Wahindi na Waarabu. Kwa mfano, viwanda na mashamba makubwa vyote vilikuwa vikimilikiwa na wafanyabiashara wa Kizungu na serikali ya kikoloni iliwapa kila aina ya msaada ikiwamo ruzuku ili kuwawezesha kupata mafanikio ya kiuchumi, hivyo kuwasaidia kututawala. Wahindi na Waarabu nao walipewa fursa ya kufanya biashara zote za kati na kupata mafanikio ya kiuchumi kwa sababu wakoloni hawakuwa na hofu yoyote ya kuhatarisha utawala wao kwani walijua wazi kuwa hawakuwa wenyeji wa Tanganyika, hivyo wasingejihusisha na harakati zozote za kupinga utawala wao. Wakoloni waliwatenga wazee wetu na mfumo wa kiuchumi kwa hofu kuwa kama wangepata nguvu za kiuchumi wangeanzisha harakati za kisiasa za kupinga kutawaliwa na wageni, hivyo kuhatarisha mamlaka yao ya kuendelea kuwatawala na kuwanyonya Watanganyika. Matokeo yake, leo hii uchumi wa nchi unadhibitiwa na wageni. Biashara zote kubwa hapa nchini zinamilikiwa na wageni. Angalia orodha ya matajiri zaidi ya 10 nchini iliyotolewa hivi karibuni ambayo Waswahili ni wawili tu. Kwahiyo, ni hoja yenye mashiko leo kutaka kuanzishwa kwa mfumo wa kisera na kisheria wa kutoa upendeleo maalumu wa kiuchumi kwa wazalendo, kwa lengo la kurekebisha dhambi ya ubaguzi waliyotendewa wazee wetu wakati wa ukoloni, ambayo madhara yake yanaendelea hadi sasa. Kukataa hoja hii ni kujifanya vipofu wa ukweli, huko ni sawa na kuendeleza ubaguzi wa wakati wa ukoloni, ni mwendelezo wa kuwazuia na kuwatenga na mfumo wa kiuchumi Watanzania weusi ambao ndio wengi nchini, jambo ambalo ni hatari kwa amani ya taifa. Mwaka 1994, serikali ya kizalendo ya Chama cha African National Congress (ANC) ilichagua kutekeleza sheria ya ‘affirmative action’ kwa lengo la kurekebisha ubaguzi wa zamani. mwisho.
 
fsad nyangumi mengi kakulpa tsh ngap kwa kuandka huu upuuuz..mengi mwzi tu astafute huruma ta watanzania aendelee na honey moon na kylne na madam rta.
 
Kwenye kongamano alishindwa kuongea leo anaita vyombo vyake vya habari na kumshambulia Muhongo, nikimuita mburula au kanjanja si dhani kama nitakuwa nimekosea!
 
kiukweli mengi ni mlalamIshi hilo hakuna anayebisha ,ila ishu ya kumiliki mara tatu ya dar es salaam hapo bado hainiingii mukichwa yaani kuanzia bagamoyo hadi mvuti mpaka chanika hadi mbezi kwa msuguri tena mara tatu,UONGO MTUPU
 
Mengi ni mlafi wa kupindukia,he is next to Rostam for his worthness but still exploiting his employees and not paying their salaries at regular and right time !....analilia uzawa?....nashangaa hata CCM bado hawajamfukuza uanachama coz jamaa anafitina balaa,aligombana na Adam Malima sasa kahamia kwa Professor kuna nini kwenye madini?
me.ngi pia amehodhi freequncy nyingi sana za radio na tv ambazo hazitumii
 
Mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa nchi hii ina wananchi wanaopenda na kushabikia uongo na uzushi bila hata kujipa muda wa kufanya uchunguzi kidogo wa mambo wanayoelezwa na kiongozi ama wa serikali au wa siasa, na hasa mtu huyo akiitwa Profesa au Dokta, au akisema ana elimu ya chuo kikuu ya shahada au shahada ya uzamili (masters). Watanzania wanadanganyika na makaratasi ya chuo yanayoitwa shahada. wanaamini mtu mwenye shahada basi anajua kila kitu na msema ukweli, kumbe wapi, hao ndiyo wezi wakubwa wa rasilimali za nchi yetu. Huyu waziri anayeitwa muhogo sijui muhongo ni kibaraka mkubwa wa wazungu, ni mtumwa wa wazungu ambaye hatamani hata uhuru, yeye anamwamini mzungu kuliko hata baba na mama yake, anatamani angezaliwa na baba na mama wazungu, shame on him! Huyu waziri tangu ateuliwe kushika wizara hiyo kazi yake ni moja tu, kuwapiga vita wafanyabiashara wazawa, kuwapiga vita watanzania wanaojishughulisha kukuza uchumi wao na wa nchi, kazi yake kuwashambulia na kuwazuia wazawa kushiriki katika kujenga uchumi wa nchi yao, anawazuia watanzania kunufaika na rasilimali za nchi yao, anataka kila kitu wamiliki wageni, mabwana zake wazungu, huyu si adui wa Reginald Mengi pekee bali ni adui wa wafanyabiashara wote wazawa, ni adui wa watanzania wote wazawa, na anapaswa kupigwa vita na kila mtanzania mzawa mpaka atakapobadili mtazamo wako dhidi ya watanzania wenzake au mpaka atakapoondolewa katika utumishi wa umma. Mimi kwa upande wangu kama mwandishi wa habari, mwaka huu niliandika makala ya kumsema huyu waziri ikiwa ni mchango wangu wa kuhakikisha hili joka tunalitimua katika nyumba yetu, nimeamua kuiweka makala hii ndani ya JF ili watanzania wenzangu wenye mapenzi mema na nchi yetu wachangie. ............................................................................................................................................................................. WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametutukana na kutudhalilisha Watanzania. Amesema eti sisi hatuna haki wala hatustahili kushirikishwa katika kujua na kuamua sera na hata kupatiwa fursa ya kumiliki miradi ya gesi yetu kwa kile alichodai kuwa hatuna uwezo wa kuivuna. Amesema eti sisi ni hohehahe ambao uwezo wetu hauruhusu kupewa fursa ya kufanya biashara ya kuwekeza katika gesi, bali tunaweza kujihusisha na biashara za soda, juisi, machungwa, maembe, mapeasi na uchuuzi mwingine usiohitaji mitaji mikubwa. Matusi hayo ya Profesa Muhongo dhidi ya Watanzania ameyatoa kupitia kwa mfanyabiashara mzalendo Reginald Mengi. Matusi na udhalilishaji huo dhidi ya Mengi vilikuja baada ya mfanyabiashara huyo mwenye mapenzi ya dhati kwa Watanzania na taifa kwa ujumla kuitaka serikali kusitisha zoezi la kugawa vitalu vya gesi hadi pale sera ya taifa ya gesi itakapokuwa tayari imeandaliwa. Mengi alikuwa akitoa rai hiyo kwa serikali kwa niaba ya Taasisi ya sekta binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation – TPSF) ambayo yeye ni mwenyekiti wake. Katika maoni yake, TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Watanzania katika uchumi wa gesi na kuishauri serikali kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi hadi sera ya gesi itakapokuwa tayari na taasisi hiyo iliomba kukutana na Waziri Muhongo kwa mashauriano zaidi. Katika kumdhalilisha zaidi Mengi, Waziri Muhongo amediriki kumuita kuwa si mzawa wa kweli bali ni mbinafsi, dalali, na mlanguzi wa rasilimali za Watanzania. Waziri Muhongo amedai kuwa Mengi na kundi lake wanataka vitalu ili wafanye ulanguzi wa gesi na mafuta ya Watanzania. Kama nilivyotangulia kusema hapo juu, kwamba matusi na dharau za Waziri Muhongo havikumlenga Mengi tu, bali Watanzania wote. Kwamba, mtazamo wa Waziri Muhongo ni juu ya Watanzania wote, ndiyo maana akasema: "Watanzania uwezo wao ni biashara za soda, juisi na maembe, siyo gesi wala mafuta." Hebu jiulize Mtanzania mwenye akili sawa sawa, hivi kama Mengi katukanwa na kudharauliwa kwa kiwango hicho, nani kabakizwa? Hivi kama waziri hawezi kumheshimu Mengi, ataweza kweli kumheshimu babu na bibi zangu wanaolima kule kijijini kwetu kwa kutumia jembe la mkono? Hivi Waziri Muhongo atawaheshimu kweli wamachinga wanaoshinda kutwa nzima wakitembea jiji lote la Dar es Salaam wakitembeza mashati mawili? Waziri Muhongo anawaheshimu, kuwanyenyekea, kuwaabudu wageni wanaokuja hapa nchini kwa koti la "wawekezaji", huku wakiwa hawana chochote, lakini hutajirika ghafla kwa kutumia rasilimali zetu. Mtazamo wa Waziri Muhongo ni kwamba uwekezaji mkubwa ukiwemo ule wa sekta ya gesi, mafuta, dhahabu, almasi na vingine hauwezi kufanywa na Watanzania wazawa. Kwamba hiyo ni biashara ya Wazungu, Wachina au Wahindi. Waziri Muhongo hawaamini waswahili wenzake, anawaona wababaishaji, madalali na walanguzi! Waziri Muhongo hayuko pekee yake katika mtazamo huu. Baadhi ya viongozi katika serikali, katika chama tawala na hata katika chombo cha kutunga sheria, yaani Bunge, wamekuwa watetezi wakubwa wa wafanyabiashara wageni. Kibaya zaidi, baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya wafanyabiashara wa kigeni kuwakwamisha wafanyabiashara wazawa. Wamo watu ndani ya serikali yetu, Bunge na chama tawala (CCM) ambao ni mawakala wa wageni hawa. Wanawapa kandarasi mbalimbali za mabilioni ya fedha na kuwanyima Watanzania wazawa. Wakati mwingine baadhi ya wabunge wanatumwa kwenda bungeni kuwashambulia wafanyabiashara wazawa kwa lengo la kuwakwamisha. Nimeambiwa hata baadhi ya taasisi za fedha nchini kama benki nazo zimekuwa zikitumiwa na wafanyabiashara wageni kuwakwamisha wazawa kwa kuwanyima mikopo au kuwawekea mazingira magumu ya kuipata. Ikumbukwe kuwa hakuna benki hata moja nchini inayomilikiwa na wazawa, nyingi ni za wageni. Waziri Muhongo na viongozi wengine wa serikali wenye mtazamo hasi dhidi ya Watanzania wazawa wanapaswa kujua kuwa hao wafanyabiashara wa kigeni siyo matajiri kiasi hicho, bali huwezeshwa na serikali zao kuja kuwekeza hapa kwetu kwa kupewa dhamana ya mikopo katika mabenki ya kwao. Makampuni yote yaliyowekeza leo katika sekta ya madini nchini yamekopa mabilioni ya dola katika mabenki ya kwao kwa dhamana ya serikali zao. Hata hayo makampuni yanayoomba vitalu vya gesi na mafuta pia yamekopa huko kwao. Hakuna kampuni inayoweza kuja hapa kuwekeza bila kukopa, haiwezekani. Na hapa ndipo hoja ya waziri wa zamani wa viwanda na biashara, Idd Simba ya kutaka uanzishwe utaratibu wa kisera na kisheria wa kuwawezesha Watanzania wazawa kibiashara inapopata nguvu. Simba alianzisha hoja hiyo kutokana na ukweli usiopingika, kwamba mfumo wa kiuchumi wa kikoloni uliwapendelea Wazungu, Wahindi na Waarabu kwa kuwapa fursa za kufanya biashara zote kubwa na kuwaacha pembezoni wenye nchi. Hata hivyo, hoja ya Simba ilipata upinzani kutoka kwa wafanyabiashara wenye asili ya kigeni pamoja na mawakala wao, hususan wanasiasa watawala wenye mtazamo kama wa Waziri Muhongo, ambao kwa kiasi kikubwa wananufaika na mfumo wa sasa. Hoja iliyokuwa ikitolewa na wapinzani wa mtazamo wa Simba ni kwamba kuanzisha upendeleo maalumu wa kiuchumi kwa jamii fulani ya watu katika nchi kwa kuzingatia rangi au tofauti nyingine yoyote, ni tangazo la wazi la sera ya ubaguzi, jambo walilosema ni kinyume cha katiba na sera ya nchi yetu. Hata hivyo, naamini kuwa Simba alikuwa na hoja nzito iliyopaswa kufanyiwa kazi, si hoja ya kubishaniwa kwamba umaskini unaowakabili Watanzania wengi wazawa si wa bahati mbaya, bali ni wa kutengenezwa. Mfumo wa kiuchumi wa watawala wa kikoloni uliwabagua Waswahili na kuwapendelea Wazungu, Wahindi na Waarabu. Wakati wa ukoloni, biashara zote kubwa zilimilikiwa na Wazungu na zile za kati zilikuwa mikononi mwa Wahindi na Waarabu. Kwa mfano, viwanda na mashamba makubwa vyote vilikuwa vikimilikiwa na wafanyabiashara wa Kizungu na serikali ya kikoloni iliwapa kila aina ya msaada ikiwamo ruzuku ili kuwawezesha kupata mafanikio ya kiuchumi, hivyo kuwasaidia kututawala. Wahindi na Waarabu nao walipewa fursa ya kufanya biashara zote za kati na kupata mafanikio ya kiuchumi kwa sababu wakoloni hawakuwa na hofu yoyote ya kuhatarisha utawala wao kwani walijua wazi kuwa hawakuwa wenyeji wa Tanganyika, hivyo wasingejihusisha na harakati zozote za kupinga utawala wao. Wakoloni waliwatenga wazee wetu na mfumo wa kiuchumi kwa hofu kuwa kama wangepata nguvu za kiuchumi wangeanzisha harakati za kisiasa za kupinga kutawaliwa na wageni, hivyo kuhatarisha mamlaka yao ya kuendelea kuwatawala na kuwanyonya Watanganyika. Matokeo yake, leo hii uchumi wa nchi unadhibitiwa na wageni. Biashara zote kubwa hapa nchini zinamilikiwa na wageni. Angalia orodha ya matajiri zaidi ya 10 nchini iliyotolewa hivi karibuni ambayo Waswahili ni wawili tu. Kwahiyo, ni hoja yenye mashiko leo kutaka kuanzishwa kwa mfumo wa kisera na kisheria wa kutoa upendeleo maalumu wa kiuchumi kwa wazalendo, kwa lengo la kurekebisha dhambi ya ubaguzi waliyotendewa wazee wetu wakati wa ukoloni, ambayo madhara yake yanaendelea hadi sasa. Kukataa hoja hii ni kujifanya vipofu wa ukweli, huko ni sawa na kuendeleza ubaguzi wa wakati wa ukoloni, ni mwendelezo wa kuwazuia na kuwatenga na mfumo wa kiuchumi Watanzania weusi ambao ndio wengi nchini, jambo ambalo ni hatari kwa amani ya taifa. Mwaka 1994, serikali ya kizalendo ya Chama cha African National Congress (ANC) ilichagua kutekeleza sheria ya ‘affirmative action' kwa lengo la kurekebisha ubaguzi wa zamani. mwisho.
uandishi wa kidiv 5, hebu weka paragraphs basi tusome
 
Mengi ni mwizi tu halafu anatumia vibaya media zake kuficha wizi wake na kupotosha umma

Labda nikuulize swali Dogo tu! Nia za kutoa facts and figures aliyofanya Muhongo zilikenga nini? Hoja ilikuwa waltz hawana uwezo wa kugawiwa vitalu. Nilitegemea Muhongo angetufafanulia sasa hiv Hawa wazalendo walivyo navyowamevifanyia nini na serikali Ina mipango gain! Lakini Prof alifanya mipasho tu, yakaishia hapo. Na Kumbuka yeye Ndiye Alikuwa Msemaji wa mwisho na alihitimisha hoja. Wasomi hawakosoi tu Bali husahihisha pia, ha kufanya hivyo Muhongo, Kwa sababu ni mwongo, Alikuwa na majigsmbo tu.
 
mjadala umefanywa tarehe 8 unajibu tarehe 15 ulikuwa wapi kukanusha siku iliyofuata afu kama sijasahau professor hakusema mengi eneo la kitalu cha gesi kama sijasahau alisema mengi ana eneo lenye leseni ya uchimbaji wa madini na sio gesi mengi anatafuta huruma ya wananchi afu simple logic 1 sq km si ni 1000 sq metres hivi mengi na pesa alizonazo ni wakutudanganya hivyo. hayo maeneo si ndo tunayoyasikia yanauzwa kwa million 800 hadi bil 1.hata kama hatumpendi muhongo lakini kuna vitu tunapaswa ku reason with simple logic. Mengi si wakumiliki mita 1000 pekee viwanda vyake tu vinazidi sasa kwenye madini je. na ujue kadri unavyopewa eneo kubwa ndivyo probability ya kutengeneza faida inaongezeka acheni majungu hebu tuache story za vijiweni sio muda wa busara na hekima. Tuheshimu taaluma hizi siasa zimeshatugharimu vya kutosha
Naomba nikurekebishe ni 1000000 sq metres
 
Acha uongo na uzushi!Alisema anamiliki vitalu vya gesi vyenye ukubwa sawa na mara tatu ya ukubwa wa mkoa wa Dar-es-salaam.

Kama kuna mtu mwingine ambae aliona kipindi kile tunaomba nae atoe maelezo bila kuchakachua ukweli.[/QUOT

Kaka ww ulikuwepo nkurumah uliangalia tv au ulisimuliwa maana nashindwa hata namna ya kukusaidia
 
Back
Top Bottom