Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,293
- 6,897
Asante kwa kunisaidia mkuu. Na pole kwa kula ban, tutaonana wiki ijayo.albadir ni shirki kama shirki nyingine tu, uislam hauna kitu kinachoitwa albadir
Ova

SHEIKH Maarufu jijini Dar es Salaam na nchini, Ali Bassaleh ametishia kusoma kisomo (albadiri) dhidi ya mfanyibiashara maarufu nchini Reginald Mengi iwapo hatalipwa fidia anayodai.
Sheikh Bassaleh amemfahamisha Mwandishi wiki hii kwamba, amefanya subira ya muda mrefu hivyo ameona wakati umefika kwa yeye kumlilia Mwenyezi Mungu (SW) dhidi ya dhuluma aliyodai kuwa imefanywa na mfanyabishara huyo.
Amesema anakusudia kusoma kisomo hicho muda wowote na atatangaza siku maalum kwa waumini wa dini ya kiislamu na watanzania kwa ujumla.
Amesema, madai ya fedha dhidi ya Reginald Mengi yanafuatia kumalizika kwa kesi ya kashfa dhidi ya chombo cha habari kinachomilikiwa na moja ya makampuni ambayo Mengi ana hisa.
Amesema, kufuatia kukashifiwa na chombo hicho cha habari, aliwasilisha malalamiko yake Baraza la habari ambako alishinda na kupewa ruhusa ya kwenda mahakamani.
Nilimtumia Wakili Profesa Saffari, nikafungua madai, tukashinda kesi, chombo hicho na mmiliki wake wametakiwa kunilipa fidia ya shilingi Milioni 49, ameeleza Sheikh
Amesema, tangu wakati huo amekuwa akisumbuliwa, hali inayoashiria mwenye fedha ndiye mwenye haki ambaye hata vyombo vya sheria vinaashiria kutokuwa tayari kukunjua makucha dhidi yake.
Akizungumzia kisomo cha Albadiri Sheikh Bassaleh amesema, ni dua maalum, yenye utekelezaji maalum wa maombi ya mdhulumiwa ambayo huelekezwa kwa Muumba wa Mbingu na Ardhi, Mmiliki wa vyote, ambaye ndiye Mmiliki wa uhai wa Mwanadaamu, huweza kuuchukua wakati wowote atakapo.
Amesema katika mafunzo ya dini ya kiislamu, Dua ya mdhulumiwa inapoombwa kinyenyekevu haina pazia, hupokelewa moja kwa moja na kwa haraka na Mwenyezi Mungu dhidi ya aliyedhulumu na kwamba zipo aina tofauti za kujibiwa.
Miongoni mwa majibu ya Mwenyezi Mungu kwa dua hiyo ni pamoja na kuondosha uhai wa aliyedhulumu ili asiendelee kukera waja wema wanyonge au kumpa maradhi yasiyotibika kwa dawa za Hospitali wala mitishamba ili iwe ujumbe wa wazi kwa wengine.
Majibu mengine ni pamoja na kumpa aliyedhulumiwa nafasi ya juu ili kumfedhehesha aliyedhulumu au mbadala mwingine ulio bora zaidi kuchukua nafasi ya alichodhulumiwa kama mali, wasifu au heshima katika jamii.
Katika madai yake dhidi ya taarifa iliyochapishwa na chombo kinachosemekana kumilikiwa na Mengi ni kwamba, ilichapishwa taarifa yenye kumkashifu na kumshushia hadhi na heshima yake kama kiongozi wa Dini na jamii kwa ujumla.
Hata hivyo, baadhi ya watu wameendelea kumsihi Sheikh Bassaleh asichukue hatua hiyo kwa haraka kutokana na madhara yake kuto komea kwa mtu mmoja bali huusisha mlolongo wa watu wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine.
Kama unataka kuelimika na unataka kuelewa na kufahamu usilolijuwa fungulia nyuzi na wenye jazba wawache na jazba zao. Hakugusi mtu humu.
Zinatakiwa nukuu ngapi ndo habari iwe real?Caliber ya Sheikh Basaleh hawezi kuongea upuuzi, source hakuna katika hiyo habari, sehemu inayoonekana kunukuliwa Sheikh Basaleh ni moja tu, nayo ni hii "Nilimtumia Wakili Profesa Saffari, nikafungua madai, tukashinda kesi, chombo hicho na mmiliki wake wametakiwa kunilipa fidia ya shilingi Milioni 49, ameeleza Sheikh.
Katika andiko zima sijaona sehemu nyingine yenye nukuu ya Basaleh, kwa hiyo ni wazi kabisa ni porojo za mleta mada.
ha ha ha ha ha ha
ha ha ha ha ha ha
Mengi kaaga kwao moshi
halafu kusema Mengi amemchafua ni kutafuta kick kupitia kwa Mengi kwani Mengi si mwandishi wa habari na sijui huo ulozi anamfanyia nani
all in all kwanini utumie ushirikina kudai chako ??
Mil 49 ni nyingi labda hana
SHEIKH Maarufu jijini Dar es Salaam na nchini, Ali Bassaleh ametishia kusoma kisomo (albadiri) dhidi ya mfanyibiashara maarufu nchini Reginald Mengi iwapo hatalipwa fidia anayodai.
Sheikh Bassaleh amemfahamisha Mwandishi wiki hii kwamba, amefanya subira ya muda mrefu hivyo ameona wakati umefika kwa yeye kumlilia Mwenyezi Mungu (SW) dhidi ya dhuluma aliyodai kuwa imefanywa na mfanyabishara huyo.
Amesema anakusudia kusoma kisomo hicho muda wowote na atatangaza siku maalum kwa waumini wa dini ya kiislamu na watanzania kwa ujumla.
Amesema, madai ya fedha dhidi ya Reginald Mengi yanafuatia kumalizika kwa kesi ya kashfa dhidi ya chombo cha habari kinachomilikiwa na moja ya makampuni ambayo Mengi ana hisa.
Amesema, kufuatia kukashifiwa na chombo hicho cha habari, aliwasilisha malalamiko yake Baraza la habari ambako alishinda na kupewa ruhusa ya kwenda mahakamani.
Nilimtumia Wakili Profesa Saffari, nikafungua madai, tukashinda kesi, chombo hicho na mmiliki wake wametakiwa kunilipa fidia ya shilingi Milioni 49, ameeleza Sheikh
Amesema, tangu wakati huo amekuwa akisumbuliwa, hali inayoashiria mwenye fedha ndiye mwenye haki ambaye hata vyombo vya sheria vinaashiria kutokuwa tayari kukunjua makucha dhidi yake.
Akizungumzia kisomo cha Albadiri Sheikh Bassaleh amesema, ni dua maalum, yenye utekelezaji maalum wa maombi ya mdhulumiwa ambayo huelekezwa kwa Muumba wa Mbingu na Ardhi, Mmiliki wa vyote, ambaye ndiye Mmiliki wa uhai wa Mwanadaamu, huweza kuuchukua wakati wowote atakapo.
Amesema katika mafunzo ya dini ya kiislamu, Dua ya mdhulumiwa inapoombwa kinyenyekevu haina pazia, hupokelewa moja kwa moja na kwa haraka na Mwenyezi Mungu dhidi ya aliyedhulumu na kwamba zipo aina tofauti za kujibiwa.
Miongoni mwa majibu ya Mwenyezi Mungu kwa dua hiyo ni pamoja na kuondosha uhai wa aliyedhulumu ili asiendelee kukera waja wema wanyonge au kumpa maradhi yasiyotibika kwa dawa za Hospitali wala mitishamba ili iwe ujumbe wa wazi kwa wengine.
Majibu mengine ni pamoja na kumpa aliyedhulumiwa nafasi ya juu ili kumfedhehesha aliyedhulumu au mbadala mwingine ulio bora zaidi kuchukua nafasi ya alichodhulumiwa kama mali, wasifu au heshima katika jamii.
Katika madai yake dhidi ya taarifa iliyochapishwa na chombo kinachosemekana kumilikiwa na Mengi ni kwamba, ilichapishwa taarifa yenye kumkashifu na kumshushia hadhi na heshima yake kama kiongozi wa Dini na jamii kwa ujumla.
Hata hivyo, baadhi ya watu wameendelea kumsihi Sheikh Bassaleh asichukue hatua hiyo kwa haraka kutokana na madhara yake kuto komea kwa mtu mmoja bali huusisha mlolongo wa watu wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine.
albadili na hiyo dini vyote ni ushirikina tu!
Aende akasome tu kama anaamn aende wala asizuiliwe. Ila ajue kuna walidhulumiwa zaid yake, kuna walio asi dini, kuna wachawi walisome na bado wanadunda tena wamefanikiwa sana. Asiuchafue Uislam kwa matakwa yake binafs. Akumbuke kuna wez waliwah kuiba makanisan na misikitn wakaombewa xaana madua lakn badala ya kufa au kuwa makn au machz, ndyo kwaanza wananeemeka. InaJamaa kama anadaiwa alipe, siyo kuchenga chenga tu.
Ninachojua mimi, ni kweli Mengi anamiliki vyombo vingi vya habari. Ukweli huu unakwenda sambamba na ukweli kuwa Mengi sio mwandishi wa habari wala sio mhariri wa chombo chochote cha habari kati ya anavyomiliki. Vyombo vyote vina watendaji kulingana na taaluma zao. Huyu Mengi anaingiaje hapa kusomewa ilibadiri ana ni njia ya vitisho kutafuta mshiko. Wewe Shekh unatakiwa ukikomalie chombo husika wala sio Mengi. Unaweza ukakaza hukumu kama kweli ulishinda kesi ya msingi na mali za chombo husika zikakamatwa kwa amri ya mahakama, zikapigwa mnada ili kulipia kiasi unachodai. Bili hivyo wewe ni mbabaishaji.