Kwa hiyo unapingana na THE BIG SHOW!? anasema hiyo ni shirki... Kuna mtu kauliza hapo juu ingekuwa ni virahisi namna hiyo, Basi Obama na Netanyau wangekuwa tayari wamekwisha somewa...Unataka Ufafanuzi wa Nini?
Umeskia Mi Mganga wa Loliondo?
Muulizenu Yule mchaga Kwanini kala cha Mtu?
Na kama kala Jasho la Mtu basi Akisomewa hio Utashangaa mwenyewe.
Caliber ya Sheikh Basaleh hawezi kuongea upuuzi, source hakuna katika hiyo habari, sehemu inayoonekana kunukuliwa Sheikh Basaleh ni moja tu, nayo ni hii "Nilimtumia Wakili Profesa Saffari, nikafungua madai, tukashinda kesi, chombo hicho na mmiliki wake wametakiwa kunilipa fidia ya shilingi Milioni 49, ameeleza Sheikh.
Katika andiko zima sijaona sehemu nyingine yenye nukuu ya Basaleh, kwa hiyo ni wazi kabisa ni porojo za mleta mada.
albadil huwa haitangazwi kama unasoma na kama umedharirishwa usingeshitaki ungesoma moja kwa moja.
na ipo siku na muda wa kusoma.
Hata mimi sijaamini, Sheikh Basaleh si mtu wa vitisho kama ninavyoviona katika taarifa hii isiyo na chanzo chochote.
Na vipi kuhusu hili suala la Al Badir, ni kweli liko kwenye dini, au ni shirki tu kama nyingine? Shukrani sana.
Ova
Fungulia nyuzi yake tutakuja kukupa darsa.
Shukrani kwa nia yako, ila tatizo la humu masuala ya dini hujadiliwa kwa jazba sana hadi unaweza juta kuanzisha nyuzi.
Yaani tunahamishia vurugu za siasa kwenye mijadala ya dini ambayo naamini tunapaswa kuheshimiana kwanza kisha tupeane darsa.
Ova
SHEIKH Maarufu jijini Dar es Salaam na nchini, Ali Bassaleh ametishia kusoma kisomo (albadiri) dhidi ya mfanyibiashara maarufu nchini Reginald Mengi iwapo hatalipwa fidia anayodai.
Sheikh Bassaleh amemfahamisha Mwandishi wiki hii kwamba, amefanya subira ya muda mrefu hivyo ameona wakati umefika kwa yeye kumlilia Mwenyezi Mungu (SW) dhidi ya dhuluma aliyodai kuwa imefanywa na mfanyabishara huyo.
Amesema anakusudia kusoma kisomo hicho muda wowote na atatangaza siku maalum kwa waumini wa dini ya kiislamu na watanzania kwa ujumla.
Amesema, madai ya fedha dhidi ya Reginald Mengi yanafuatia kumalizika kwa kesi ya kashfa dhidi ya chombo cha habari kinachomilikiwa na moja ya makampuni ambayo Mengi ana hisa.
Amesema, kufuatia kukashifiwa na chombo hicho cha habari, aliwasilisha malalamiko yake Baraza la habari ambako alishinda na kupewa ruhusa ya kwenda mahakamani.
Nilimtumia Wakili Profesa Saffari, nikafungua madai, tukashinda kesi, chombo hicho na mmiliki wake wametakiwa kunilipa fidia ya shilingi Milioni 49, ameeleza Sheikh
Amesema, tangu wakati huo amekuwa akisumbuliwa, hali inayoashiria mwenye fedha ndiye mwenye haki ambaye hata vyombo vya sheria vinaashiria kutokuwa tayari kukunjua makucha dhidi yake.
Akizungumzia kisomo cha Albadiri Sheikh Bassaleh amesema, ni dua maalum, yenye utekelezaji maalum wa maombi ya mdhulumiwa ambayo huelekezwa kwa Muumba wa Mbingu na Ardhi, Mmiliki wa vyote, ambaye ndiye Mmiliki wa uhai wa Mwanadaamu, huweza kuuchukua wakati wowote atakapo.
Amesema katika mafunzo ya dini ya kiislamu, Dua ya mdhulumiwa inapoombwa kinyenyekevu haina pazia, hupokelewa moja kwa moja na kwa haraka na Mwenyezi Mungu dhidi ya aliyedhulumu na kwamba zipo aina tofauti za kujibiwa.
Miongoni mwa majibu ya Mwenyezi Mungu kwa dua hiyo ni pamoja na kuondosha uhai wa aliyedhulumu ili asiendelee kukera waja wema wanyonge au kumpa maradhi yasiyotibika kwa dawa za Hospitali wala mitishamba ili iwe ujumbe wa wazi kwa wengine.
Majibu mengine ni pamoja na kumpa aliyedhulumiwa nafasi ya juu ili kumfedhehesha aliyedhulumu au mbadala mwingine ulio bora zaidi kuchukua nafasi ya alichodhulumiwa kama mali, wasifu au heshima katika jamii.
Katika madai yake dhidi ya taarifa iliyochapishwa na chombo kinachosemekana kumilikiwa na Mengi ni kwamba, ilichapishwa taarifa yenye kumkashifu na kumshushia hadhi na heshima yake kama kiongozi wa Dini na jamii kwa ujumla.
Hata hivyo, baadhi ya watu wameendelea kumsihi Sheikh Bassaleh asichukue hatua hiyo kwa haraka kutokana na madhara yake kuto komea kwa mtu mmoja bali huusisha mlolongo wa watu wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine.
Mimi sio mwizi, Kwanini Salman Rushdie hakusomewa!? au mpaka uibe...