Mengi kusomewa albadiri Dar es Salaam

Mengi kusomewa albadiri Dar es Salaam

Hapo yalipopelekwa mashtaka wameona mengi kashindwa ila wewe pangu pakavu unahukumu mengi kasingiziwa..wabongo bwana...acheni ushabiki makopo.

Mengi ni mwanahabari kwani ??
Kwahiyo mtu akizulumiwa na mfanya kazi wa bahresa utasema bahresa kamdhulumu ??
Huyo kachafuliwa na gazeti la Mengi ila Mengi sio mwandishi wala mhariri.

Hebu fikiri kwanza
 
mmh...kama albadiri ina nguvu kweli,kwa nini wasingemsomea bush kipindi kaivamia iraq??au kwa nini wasimsomee waziri mkuu wa israel wanavyomlalamikia kuwanyanyasa wapalestina..??
 
Mbulula wewe, ujinga wenu ndio umaskini wenu, mlidanganywa kuhusu al badili mkaaminishwa ujinga na kwa sababu mnaogopa sana kufa mmekuwa watumwa wa al badili, katika uislam hakuna kitu kinaitwa al badiri, neno al badiri katika uislam limekuja katika vita vitakatifu vya Badr ndipo lilipatikana neno al badir, Sasa kwa akili yako mtu atafanya nini akudhuru kwa hiyo al badir? Hii kitu haipo kabisa huo unaitwa ushirikina kama ushirikina mwingine

ndio mnanifungua macho kunasiku shee mmoja alisema kutokana na kutokuwa na uelewa kuhusu imani ya dini ya kiislam asilimia 98 ya hii jumuia inaamini ushirikina ndio nguzo yao ya kutatua matatizo
 
Caliber ya Sheikh Basaleh hawezi kuongea upuuzi, source hakuna katika hiyo habari, sehemu inayoonekana kunukuliwa Sheikh Basaleh ni moja tu, nayo ni hii "Nilimtumia Wakili Profesa Saffari, nikafungua madai, tukashinda kesi, chombo hicho na mmiliki wake wametakiwa kunilipa fidia ya shilingi Milioni 49”, ameeleza Sheikh.

Katika andiko zima sijaona sehemu nyingine yenye nukuu ya Basaleh, kwa hiyo ni wazi kabisa ni porojo za mleta mada.

nunua gazeti la al-muud kama sijakosea spelling faizfox la jtatu kama sikosei ipo kwenye front page
 
kumbe viongozi wa dini nao ni wazee wa fursa eeh!!..hivi mitume nao walikuwa akidai fidia kwa kukashifiwa? ama kweli mjini shule, kaka mimi ni mengi ningemwambia asome hiko kisomo tuishane deni, au akisoma ataendelea kunidai tena?
 
Hii kitu kumbe haipo ....huwa nashangaa sana huku mitaani utasikia nitakusomea Albadiri kumbe janja ya kuficha ushirikina
 
Chanzo cha habari yako ni kipi??

Hata hivyo kwenye uislam HAKUNA KITU KINACHOITWA ALBADILI AU DUA YA ALBADILI

ETI UMSOMEEE MTU AGEUKE CHIZI AU AFE,,HUO NI UHUNI NA USHIRIKINA KAMA ULIVYO USHIRIKINA MWINGINE TUH

UISLAM NI DINI SAFI ISIYOAMIN NGUVU YA UCHAWI WALA MASHETANI

Mbona unaanza kutukana dini yako? nakumbuka Kikwete kwenye hotuba yake alisema kasomewa ITKAF na Waislam ili afe


Soma hii


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-es-salaam-ilinisomea-itikafu-ili-nife-4.html
 
Mimi namshauri Mengi ampe angalau milioni 10, inawezekana ni njaa tu
 
kwani kikwete ni nani kwenye uislam? wanachofanya wakina kakobe ni sahihi? dini ya kiislam haimfati mtu kasema nini sisi muongozo wetu ni qur an na sunnah tu,

Okay, kumbe wale mashehe wa misikiti mitatu waliomuombea Kikwete Kifo hawajui Quran
 
Okay, kumbe wale mashehe wa misikiti mitatu waliomuombea Kikwete Kifo hawajui Quran

We Bwana Kakende bin Kapumbu unajua Itkafu maana yake nn? Na je inauhusiano wowote na hyo albadri? Au umeamua kujitoa ufahamu tu?
 
SHEIKH Maarufu jijini Dar es Salaam na nchini, Ali Bassaleh ametishia kusoma kisomo (albadiri) dhidi ya mfanyibiashara maarufu nchini Reginald Mengi iwapo hatalipwa fidia anayodai.

Sheikh Bassaleh amemfahamisha Mwandishi wiki hii kwamba, amefanya subira ya muda mrefu hivyo ameona wakati umefika kwa yeye kumlilia Mwenyezi Mungu (SW) dhidi ya dhuluma aliyodai kuwa imefanywa na mfanyabishara huyo.


Amesema anakusudia kusoma kisomo hicho muda wowote na atatangaza siku maalum kwa waumini wa dini ya kiislamu na watanzania kwa ujumla.


Amesema, madai ya fedha dhidi ya Reginald Mengi yanafuatia kumalizika kwa kesi ya kashfa dhidi ya chombo cha habari kinachomilikiwa na moja ya makampuni ambayo Mengi ana hisa.

Amesema, kufuatia kukashifiwa na chombo hicho cha habari, aliwasilisha malalamiko yake Baraza la habari ambako alishinda na kupewa ruhusa ya kwenda mahakamani.

“Nilimtumia Wakili Profesa Saffari, nikafungua madai, tukashinda kesi, chombo hicho na mmiliki wake wametakiwa kunilipa fidia ya shilingi Milioni 49”, ameeleza Sheikh

Amesema, tangu wakati huo amekuwa akisumbuliwa, hali inayoashiria mwenye fedha ndiye mwenye haki ambaye hata vyombo vya sheria vinaashiria kutokuwa tayari kukunjua makucha dhidi yake.

Akizungumzia kisomo cha Albadiri Sheikh Bassaleh amesema, ni dua maalum, yenye utekelezaji maalum wa maombi ya mdhulumiwa ambayo huelekezwa kwa Muumba wa Mbingu na Ardhi, Mmiliki wa vyote, ambaye ndiye Mmiliki wa uhai wa Mwanadaamu, huweza kuuchukua wakati wowote atakapo.

Amesema katika mafunzo ya dini ya kiislamu, Dua ya mdhulumiwa inapoombwa kinyenyekevu haina pazia, hupokelewa moja kwa moja na kwa haraka na Mwenyezi Mungu dhidi ya aliyedhulumu na kwamba zipo aina tofauti za kujibiwa.


Miongoni mwa majibu ya Mwenyezi Mungu kwa dua hiyo ni pamoja na kuondosha uhai wa aliyedhulumu ili asiendelee kukera waja wema wanyonge au kumpa maradhi yasiyotibika kwa dawa za Hospitali wala mitishamba ili iwe ujumbe wa wazi kwa wengine.

Majibu mengine ni pamoja na kumpa aliyedhulumiwa nafasi ya juu ili kumfedhehesha aliyedhulumu au mbadala mwingine ulio bora zaidi kuchukua nafasi ya alichodhulumiwa kama mali, wasifu au heshima katika jamii.

Katika madai yake dhidi ya taarifa iliyochapishwa na chombo kinachosemekana kumilikiwa na Mengi ni kwamba, ilichapishwa taarifa yenye kumkashifu na kumshushia hadhi na heshima yake kama kiongozi wa Dini na jamii kwa ujumla.

Hata hivyo, baadhi ya watu wameendelea kumsihi Sheikh Bassaleh asichukue hatua hiyo kwa haraka kutokana na madhara yake kuto komea kwa mtu mmoja bali huusisha mlolongo wa watu wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine.

Mungu gani huyo aliekwambia uende mahakamani? Soma miaka kumi na Mengi atasoma zaburi 35 kitabu cha Mungu kweli kisha Mengi atakushinda.Eti M40? Acha tamaa na pesa za wanaume wenzio fanya kazi wewe.
 
Back
Top Bottom