Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amjibu Shigongo

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
26,580
48,733
Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya. Baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako.

Siku zote nimekuheshimu na sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wwengine na watu mbalimbali.... tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu.

Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond ila sie tumekaa kimya na kujifanya unazunga eti unatushauri. Kweli mtu unasema unampenda unamshauria instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?

Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini? Na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya @Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi kupost tumepost ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa.

Hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na mashabiki zao hii ndio kuwaeka karibu wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula Madawa yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kum'bomoa msanii kupitia magazeti yako.

Tafadhali heshimu heshima yetu kwako. "Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao.
 
Shingongo bana akiwa na bifu anataka kila mtu ajue. Kuna kipindi alikuwa na bifu na uwoya kisa wanakijua wao,jamaa akapiga stop kuandika habari za uwoya kwenye magazeti yake huku akijitapa alimpandisha umaarufu na atamshusha. Saiv zamu ya dai na team yake jaman
 
duh hakuna m'babe wa wababe hata Osama enzi zake zilipita na hapa naona kuna m'babe enzi zake zinataka kupita hivi
 
Huwa nachukia sana kauli za "Tulisema, nilisema" ila kwa leo ngoja na mimi niseme kuwa jana nilisema hili ni suala la biashara, Tanzania kuna watu wanapenda sana Kuwatumikisha wengine kama watumwa bila kujali una jina umelitengeneza kwa shilingi na gharama gani na muda. Harmonize was nobody and no body gave a https://jamii.app/JFUserGuide abt him leo ametengenezwa amepata jina mtu anajipa MAMLAKA YA UTABIRI kwa kutaka kukutumia BURE tu

- Aiyola (Video + Audio 35M )

- Bado ( Video + Audio 40 )

- Matatizo ( 8M )

Bado kuna gharama za muda, utunzi, kukesha muda na ubunifu, LEO MTU ANATAKA KUKUTUMIA BURE TU Ka kisingizio eti anakuweka karibu na MASHABIKI na watu wanaoongoza kufanya haya ni SHIGONGO na CLOUDS, Ukibuma ndo WANAKUCHEKA NA HAKUNA ATAKAYEKUJALI
 
Shigongo biashara zimedunda ameamua kulazimisha apate kiki na mdomo uingie kinywani
Mambo yamebadirika sana UMBEYA WOTE EXCUSIVE unapatikana INSTAGRAM na BLOGS za UDAKU, Hardcopy HAZIUZI KABISA Yale yale ya NOKIA na BLACKBERRY Kama hakuwekeza upande mwingine ajiandae KURUDI BUSEGA Maana nasikia kawekeza pia kwenye HOTEL ambazo kwa sasa zinapitia MTIKISIKO MKUBWA
 
Nina muda mrefu sana sijasoma magazeti maana taarifa zote na kila kinachojiri nakipata mtandaoni Jamiiforumz,Twitter, Instagram, Facebook, WhatsApp na telegram, habari zote nazipata kwa wakati mpaka wengine huwa wananiuliza napata wapi habari, sisomi magazeti wala sipati muda wa kusikiliza redio, nikiamka tu naingia mtandaoni kidogo baadaye naendelea na mambo mengine nikipata time natupia tena jicho mtandaoni, sasa akina shigongo wana njaa mambo yamebadilika
 
angemkaushia tu maana awezi kubadili chochote amuige mzee wa msoga watu kama hao uwa anawacheka tu yule ana stres biashara imeenda kombo anajaribu kuirudisha kwenye mstari anavyomjibu ndo anampa nafasi zaidi
 
Back
Top Bottom