Men Use A Little Brain Mnapoomba Demu Hela. It is a pity!

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,161
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!

Sijui maisha magumu au nini ila wimbi la wanaume kuwaomba mademu hela limeongezeka sanaa. Sote binadamu haina ubaya, kuna kupanda na kushuka. I dont have a problem with a man asking me for money. Ila nisichopenda ni me kushindwa kucheza kwa kanuni zenu mlizotuweke tuwaombapo hela. Kanuni muweke nyie, afu ikifika zamu yenu kuomba ziwashinde kutii. Alaaaaaaa!

Kaka zangu mda mwingine mnajivua nguo kabisaa na mizinga yenu. Mnakosea totally kupiga hio mizinga mpaka anaepigwa mzinga anahamaki. Leo ngoja niwape pointers za kutokukimbiwa na mademu kwa mizinga yako.

Rule no 1: She is not stupid
Unapomuomba demu hela kaa ukijua kuwa demu ana akili zote na ni mtu mzima, sasa kutumia uongo usiokuwa na akili sio issue. Tena akijua unamdanganya ndo hela sikupiii kabisaaa, yani sikupiii. Hata ukidanganya tumia uongo wenye akili na kutia moyo. Kuna kajitu kalitaka kunipiga mzinga wa 1m, eti oooh niazime ada ya mdogo wangu. Mnaumwaa kweli kweli wewe na mdogo wako tena mnaumwa kichocho sugu. Sasa ada ya mdogo wako kwenye ukoo hamna ndugu wengine maana jambo serious hilo mpaka nitoe mie hio hela? Hahahahaa! Au nina matatizo kweli niazime 300,000 hahahaaaaa ili na mimi 300,000 zangu zipotelee kwenye matatizo yako? Aaaaaa wapi. Usichukulie ni rahisi mtu kuachana na mbesa yake. Akili inahitajika tena si ndogo

Mpige mtu mzinga kwa habari njema mbeleni wala hachomoi, mfano Baby nimeagiza gari, nataka nibadilishe hii au kama huna ndo umeagiza sasa, nimekwama kama 1 m hivi fanya ado ado likitoka nikitulia tu nalipa. Hapo sawa kama umeweza kunua kitu cha 15m kulipa hio 1 m hushindwi. Niazime laki kadhaa site kidogo hakujakaa fresh. Nakupaa. Kama unajenga labda na mimi nitaishi humo huwezi jua. Hii hata mwanaume ukimpiga mwanaume kizinga kwa postiive news anakupa hela faster. Ni sawa na kukopa bank, hata kumkopa mpenzi wako tumia formular zile zile za CAMPARI mbona utafaidi mizinga mpaka basi. Afu tumia NIKOPESHE kuliko NAOMBA utapewa haraka, kama mjuavyo akishakukopesha kiendacho kwa Bae hakirudi.

Rule no 2 KUWA FLEXIBLE MSAADA HAUNA RISITI
Unapomuomba mtu kitu sio lazima akupe kile kile ulichoomba as if unamdai, rigidity ya request ndo mwanzo wa kunyimwa. Mfano naomba laki moja. Unajipangia kabisaaa unajuaje kama ninayo? Tarehe Mwisho wa mwezi nisaidie pesa flani, yaani unajipangia kabisaa mda wa mie kukupa hio hela na kiasi. Umebanwa kweli haja kubwa. Heheheeee! Yaani unakuwa specific na ombi lako hamna mfano. Haitakiwi

Ukiomba kamzinga unatakiwa uwe flexible na ombi lako liache flexible. Hata ukitaja kiwango kwa sababu zako maalumu ila still mpe mtoa msaada flexibility. Mfano nimebanwa na ishu ya kununua dispencer pale kwangu, dispencer zenywe wanauza laki 3 siku hizi, nifanyie basi maarifa yoyote tu katika hilo. Vovote utavoweza nitashukuru kweli utakuwa umenifaa sio kidogo. Hapo unampa uwanja kama hana hio laki 3 basi atoe hata kukaribiana.


Rule no 3 Cha Mtu Mavi. Ujiandae kumlamba Miguu kabla na Baada ya Kizinga.
Vizinga vya mara moja moja sio vigumu sana, challange iko kwenye vizinga endelevu. Yaani mtu huo huyo uwe unampiga vizinga endelevu huo mtihani. Watua wanashindwa hili kwa kukosa kujishusha na kujikomba. Ili mtu akusaidie tena na tena inabidi uwe unajikomba haswaa, usimchukulie tena ordinary. Unatakiwa at all times uwe unaenda extra miles.

Sio mtu katoka kukupa laki zake 3 hata meseji asubuhi na jioni zinakushinda. Siku zingine hakupi hata 10. Inatakiwaakishaonesha nia ya kukupa na akishakupa sasa akome na wewe. Sio meseji za kumsalimu kila saa umuanze wewe. Kumsifia kwa watu ni mtu mzur, mpaka sifa zirudi. Kama kwenye haice kakosa siti unampishaa, Bar unamuwahia siti ya kona, game sio lazima akuombe yeye unajiongeza. Kama sahani anajitolea unatoa wewe. You work for the moeny. Ionekane tofauti kabla na baada ya hela kubadili mifuko. Dont make it look as if kupewa ile hela ni haki yako sababu sio.

Rule No 4 Be Patient. Mtu akikugea hela yake utu unaishaa, anaanza kuona kama anakununua flani vile. Ule utu wake wa kila siku unakuwa umeshuka sanaa sasa wewe mpewa hela kaka angu unatakiwa uwe patient ukiendekeza jazabajazba utajikuta umekinukishaa. Kitu kidogo tu anaweza ingizia hiko kizinga alichokupa shavu. Yani na hela zangu nilizokupa ndo unanijibu hivo? Hahahaaaaaaa! Au katika malavida unamuuliza kimazoea tu baby unanipenda? Unasiki nisingekupenda ningekupa hio hela unadhaniii? Hahahaaaa sikati mie.

Ukiwa na roho nyepesi unaweza rudisha pesa yote siku hiio hio. Ila la maana ni kuwa na uvumilivu tu, na kuelewa hela inaumaaa jamaniii. Mwenzio anagugumia maumivu ya hlea zake so ni kumuelwa tu na kumpuuzia.
 
So mbaya kumsaidia mpenzi wako ambae kweli mnamalengo kimaisha sio kwa wale wa one night stand napia usimfanye mpenzi wako tegemezi yaani kila ukiongea nae we wakumuomba hela tu inafikia hatua mtu unachoka unaamua kuuvunja uhusianoo hivihivi
 
Rule namba moja unaangalia unayempiga hicho kizinga kama anastahili kupigika na anapigika wengine hela wanazo ila ni wabahili by nature

mkate mgumu mbele za chai hakuna labda uopoe jiwe
 
Umegonga kwenyewe. Kuna mtu nampaga sana hela zangu halafu hana hivyo ulivyoviandika. Mi ndo najikuta namnyenyekea yeye. Leo nimejifunza kudadadadadeki zake
 
lara 1 una akili sana,hiyo point ya 4 ni kweli kabisaaaaa.
Na namba 3 mimi huitumia vyema.
Nikipewa pesa nakuwaje humble sasa?
Lazima uoneshe shukrani,na hata aliyekupa anapata moyo wa kukupa tena na tena.
 
women are most selfish creatures on earth ***** yani its fair wao kuomba hela hata kwa most absurd and stupid reasons ila sio kwa mwanaume kuomba wtf
Wewe toa milion hata kama ni ya kununua wigi tu,ukimnyima utasikia"hah we mwanaume bahili,je ukiombwa gari si utakimbia" sasa wewe muombe laki tu mda si mrefu atakuita mwanaume suruali,yaan ni kama walilaaniwa vile
 
Pia uelewa unahitajika jamani....akunyimae hakwambii hapana....ukiona ni mwisho wa mwezi na bado unaniomba hela nakupa viexcuse wewe elewa kuwa nishakunyima....mtu unamwambia "aisee mi mwenyewe hela iko tight ila kuna mtu namdai ngoja nimkumbushe anilipe"..anaulizia kila dakika, "vipi amelipa?"...kulipa huko vepeee?...ndo nishakataa....halafu unasema una emergency lakini wiki nzima uko kuulizia mkopo. Emergency gani hiyo...
 
Back
Top Bottom