Men Use A Little Brain Mnapoomba Demu Hela. It is a pity!

Men Use A Little Brain Mnapoomba Demu Hela. It is a pity!

Kuazimana hela sioni shida ila ikizidi 1M lazima mtu aweke bond kwakuwa wabongo warushi sana,kina dada mtuelewe kuna wakati tunafulia ila masharti ya matumizi ya hela utakayonikopa yapunguzwe.
 
hahaaaaaaa hawakawiii kuhamisha huku kwenda kule kwanza ukizoea kumpa hela mapenzi yanapungua anajiona dhaifu na yeye anatafuta dhaifu wake mtazamo tu
 
bora nife na shida zangu ila sio kumuomba hela mwanamke,mwisho wa siku lazma usimangwe tuu hasa mkishaachana au ukimkosea kitu chochote.
 
aisee kwangu hakuna rule inayoingia hapo, nimegoma kupigika kizinga hata cha vocha, yaani mwanaume anipige kizinga!! uwii nitatoka mbio hatari.
 
Yuuuu, Cha! bora uwe maskini jeuriii, Kila MTU abaki na visenti vyake kuliko kupelekeshana ivooo. Mimi hua sipendi kuombwa hela na sipendi kuomba in short nikikupa roho itaniuma,
 
1. akipanda daladala kakosa siti nimpishe siti.
2. akifika bar nimuwahie siti.
3. akimaliza kula nimtole sahani hata kama alitaka kutoa mwenyewe.
as a man nasema siwezi kabisa kumuomba hela mwanamke labda awe mama yangu au dada tena kwa kuwakopa. mama yangu huwa nakuwa huru kumuomba hela maana naweza sema nikipata mshahara pale home ninahemea kila kitu hadi gunia la mkaa, hivyo siku nikiyumba namkopa hadi mwisho wa mwezi namrudishia hiyo ananipa tena anaweza hata akakataa nisimrudishie kwa maana natoa mchango mkubwa ktk mambo ya familia.
ila kumuomba hela mpenzi wangu kwa jinsi wadada hasa wa sasa wasivyo na ufikiri wa kutunza utu wa mwenzake si ntatangazwa kwa mashemeji zangu wote. kwa principal zangu itabaki cha kwangu ni cha mwanamke pia ila cha mwanamke ni chake peke yake. nikiyumba ninao washkaji najua wana huwa hatutupani never.
 
Safi sana lala umejuaje apa nimeazimwa laki apa lakini izo amri zake balaa, mafumbo kibao katika stori but bingwa wa kupuliza alipouma utasikia 'usidhani nakusema wew' lakin msj senti
 
It is simply a condition of life that nature doesnt lose its way!!...men are born to take care of their women and show them some love in a satisfactory manner!!..naturally women desires love while men like much respect!
..contrary to that-relationships face challenges like those of men to beg for financial support!!!...it is shameful and im not scared to say this at all!!
 
It is simply a condition of life that nature doesnt lose its way!!...men are born to take care of their women and show them some love in a satisfactory manner!!..naturally women desires love while men like much respect!
..contrary to that-relationships face challenges like those of men to beg for financial support!!!...it is shameful and im not scared to say this at all!!
 
KWAKWELI sijawahi na sintaweza kimwomba Mwanamke hela.

Anaweza kukusaidia ila baadaye kila mtu atajua
 
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!

Sijui maisha magumu au nini ila wimbi la wanaume kuwaomba mademu hela limeongezeka sanaa. Sote binadamu haina ubaya, kuna kupanda na kushuka. I dont have a problem with a man asking me for money. Ila nisichopenda ni me kushindwa kucheza kwa kanuni zenu mlizotuweke tuwaombapo hela. Kanuni muweke nyie, afu ikifika zamu yenu kuomba ziwashinde kutii. Alaaaaaaa!

Kaka zangu mda mwingine mnajivua nguo kabisaa na mizinga yenu. Mnakosea totally kupiga hio mizinga mpaka anaepigwa mzinga anahamaki. Leo ngoja niwape pointers za kutokukimbiwa na mademu kwa mizinga yako.

Rule no 1: She is not stupid
Unapomuomba demu hela kaa ukijua kuwa demu ana akili zote na ni mtu mzima, sasa kutumia uongo usiokuwa na akili sio issue. Tena akijua unamdanganya ndo hela sikupiii kabisaaa, yani sikupiii. Hata ukidanganya tumia uongo wenye akili na kutia moyo. Kuna kajitu kalitaka kunipiga mzinga wa 1m, eti oooh niazime ada ya mdogo wangu. Mnaumwaa kweli kweli wewe na mdogo wako tena mnaumwa kichocho sugu. Sasa ada ya mdogo wako kwenye ukoo hamna ndugu wengine maana jambo serious hilo mpaka nitoe mie hio hela? Hahahahaa! Au nina matatizo kweli niazime 300,000 hahahaaaaa ili na mimi 300,000 zangu zipotelee kwenye matatizo yako? Aaaaaa wapi. Usichukulie ni rahisi mtu kuachana na mbesa yake. Akili inahitajika tena si ndogo

Mpige mtu mzinga kwa habari njema mbeleni wala hachomoi, mfano Baby nimeagiza gari, nataka nibadilishe hii au kama huna ndo umeagiza sasa, nimekwama kama 1 m hivi fanya ado ado likitoka nikitulia tu nalipa. Hapo sawa kama umeweza kunua kitu cha 15m kulipa hio 1 m hushindwi. Niazime laki kadhaa site kidogo hakujakaa fresh. Nakupaa. Kama unajenga labda na mimi nitaishi humo huwezi jua. Hii hata mwanaume ukimpiga mwanaume kizinga kwa postiive news anakupa hela faster. Ni sawa na kukopa bank, hata kumkopa mpenzi wako tumia formular zile zile za CAMPARI mbona utafaidi mizinga mpaka basi. Afu tumia NIKOPESHE kuliko NAOMBA utapewa haraka, kama mjuavyo akishakukopesha kiendacho kwa Bae hakirudi.

Rule no 2 KUWA FLEXIBLE MSAADA HAUNA RISITI
Unapomuomba mtu kitu sio lazima akupe kile kile ulichoomba as if unamdai, rigidity ya request ndo mwanzo wa kunyimwa. Mfano naomba laki moja. Unajipangia kabisaaa unajuaje kama ninayo? Tarehe Mwisho wa mwezi nisaidie pesa flani, yaani unajipangia kabisaa mda wa mie kukupa hio hela na kiasi. Umebanwa kweli haja kubwa. Heheheeee! Yaani unakuwa specific na ombi lako hamna mfano. Haitakiwi

Ukiomba kamzinga unatakiwa uwe flexible na ombi lako liache flexible. Hata ukitaja kiwango kwa sababu zako maalumu ila still mpe mtoa msaada flexibility. Mfano nimebanwa na ishu ya kununua dispencer pale kwangu, dispencer zenywe wanauza laki 3 siku hizi, nifanyie basi maarifa yoyote tu katika hilo. Vovote utavoweza nitashukuru kweli utakuwa umenifaa sio kidogo. Hapo unampa uwanja kama hana hio laki 3 basi atoe hata kukaribiana.


Rule no 3 Cha Mtu Mavi. Ujiandae kumlamba Miguu kabla na Baada ya Kizinga.
Vizinga vya mara moja moja sio vigumu sana, challange iko kwenye vizinga endelevu. Yaani mtu huo huyo uwe unampiga vizinga endelevu huo mtihani. Watua wanashindwa hili kwa kukosa kujishusha na kujikomba. Ili mtu akusaidie tena na tena inabidi uwe unajikomba haswaa, usimchukulie tena ordinary. Unatakiwa at all times uwe unaenda extra miles.

Sio mtu katoka kukupa laki zake 3 hata meseji asubuhi na jioni zinakushinda. Siku zingine hakupi hata 10. Inatakiwaakishaonesha nia ya kukupa na akishakupa sasa akome na wewe. Sio meseji za kumsalimu kila saa umuanze wewe. Kumsifia kwa watu ni mtu mzur, mpaka sifa zirudi. Kama kwenye haice kakosa siti unampishaa, Bar unamuwahia siti ya kona, game sio lazima akuombe yeye unajiongeza. Kama sahani anajitolea unatoa wewe. You work for the moeny. Ionekane tofauti kabla na baada ya hela kubadili mifuko. Dont make it look as if kupewa ile hela ni haki yako sababu sio.

Rule No 4 Be Patient. Mtu akikugea hela yake utu unaishaa, anaanza kuona kama anakununua flani vile. Ule utu wake wa kila siku unakuwa umeshuka sanaa sasa wewe mpewa hela kaka angu unatakiwa uwe patient ukiendekeza jazabajazba utajikuta umekinukishaa. Kitu kidogo tu anaweza ingizia hiko kizinga alichokupa shavu. Yani na hela zangu nilizokupa ndo unanijibu hivo? Hahahaaaaaaa! Au katika malavida unamuuliza kimazoea tu baby unanipenda? Unasiki nisingekupenda ningekupa hio hela unadhaniii? Hahahaaaa sikati mie.

Ukiwa na roho nyepesi unaweza rudisha pesa yote siku hiio hio. Ila la maana ni kuwa na uvumilivu tu, na kuelewa hela inaumaaa jamaniii. Mwenzio anagugumia maumivu ya hlea zake so ni kumuelwa tu na kumpuuzia.
Kwel Pesa ndio kila k2. Zaman walisema Pesa n Sabun ya Roho sasa Pesa ni nn...........................?
 
Mwanaume wakupiga mizinga Kila Leo sio kabisa..nachukia sana
 
Back
Top Bottom