Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,883
- 155,856
Memento Mori,
Katika kilele cha Himaya ya Warumi, kulikuwa hakuna tukio kubwa na la kifani kama la mapokezi ya Mkuu wa Majeshi wakati akitoka vitani alikoenda kuongeza himaya.
Watu wote walitoka barabarani kushangilia. Wote wakiimba jina la Jenerali huyo na makamanda wake. Nyimbo zote nzuri. Akipewa fedha, mifugo, wanawake na pongezi kutoka makundi yote.
Warumi wale wenye akili wakaja kubaini baadaye kwamba sifa zile zilikuja kuleta athari hasi kwa wapiganaji hao. Manake ilifka mahali askari wale wakajiona kama Miungu Watu.
Basi ukatengenezwa mfumo. Ikaja kuwa kwamba siku ambayo Jenerali alikuwa anarejea kutoka vitani, kuna mtu alipewa kazi ya kuwa jirani naye na kutamka maneno yafuatayo; Memento Mori, Memento Mori, Memento Mori.... Mpaka mwisho,
Nini maana ya Memento Mori? Maana yake ni kuwa ipo siku nawe utakufa. Utaingia kaburini. Utaoza. Ni kama kusema wewe si Mungu. Wewe ni mwanadamu tu.
Lengo lao lilikuwa nini? Lengo lilikuwa ni kuwakumbusha kwamba wanatakiwa wawe na utu. Wasijione kama wao ni daraja tofauti na wengine. Kwamba wao nao wataondoka hapa duniani. Na wakifa wataoza na kubaki mifupa kama watu wengine wote.
Neno langu jioni hii ni moja tu kwenu nyote; Memento Mori.
Ezekiel Kimwaga