Memento Mori

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,457
154,323
Memento Mori,

Katika kilele cha Himaya ya Warumi, kulikuwa hakuna tukio kubwa na la kifani kama la mapokezi ya Mkuu wa Majeshi wakati akitoka vitani alikoenda kuongeza himaya.

Watu wote walitoka barabarani kushangilia. Wote wakiimba jina la Jenerali huyo na makamanda wake. Nyimbo zote nzuri. Akipewa fedha, mifugo, wanawake na pongezi kutoka makundi yote.

Warumi wale wenye akili wakaja kubaini baadaye kwamba sifa zile zilikuja kuleta athari hasi kwa wapiganaji hao. Manake ilifka mahali askari wale wakajiona kama Miungu Watu.

Basi ukatengenezwa mfumo. Ikaja kuwa kwamba siku ambayo Jenerali alikuwa anarejea kutoka vitani, kuna mtu alipewa kazi ya kuwa jirani naye na kutamka maneno yafuatayo; Memento Mori, Memento Mori, Memento Mori.... Mpaka mwisho,

Nini maana ya Memento Mori? Maana yake ni kuwa ipo siku nawe utakufa. Utaingia kaburini. Utaoza. Ni kama kusema wewe si Mungu. Wewe ni mwanadamu tu.

Lengo lao lilikuwa nini? Lengo lilikuwa ni kuwakumbusha kwamba wanatakiwa wawe na utu. Wasijione kama wao ni daraja tofauti na wengine. Kwamba wao nao wataondoka hapa duniani. Na wakifa wataoza na kubaki mifupa kama watu wengine wote.

Neno langu jioni hii ni moja tu kwenu nyote; Memento Mori.

Ezekiel Kimwaga
 
Mkuu umeielezea vizuri Lakini naona kama kuna kitu naweza kuongeza. Memento Mori ni phrase maarufu sana Duniani.

Ilitokea arround 70AD, ambapo Roma ya kale ilikuwa na nguvu kubwa sana kijeshi Duniani na iliteka makoloni na nchi nyingi sana kutokana na mbinu za General wake anaitwa Cesar. Jamaa alijiita Mungu wa miungu, Mungu wa Jupiter na Mars. Na kila baada ya kuteka nchi yoyote kubwa kulikuwa na utaratibu wa kurudi nyumbani na kufanya sherehe kubwa sana kwenye triumphantly square na huku general akipita kabebwa na gari la kuvutwa na farasi huku nyimbo, mapambio, na maua yakipamba ardhi kwenye sherehe hiyo kubwa kuliko zote kwenye ancient Rome.

Siku hiyo kuna mtumwa (Slave) mmoja alichoka na kujikweza, kujiona,kiburi na ujinga wa General akauvaa ujasiri kwa sauti ya kunong'ona akamwambia general aliekuwa anapita pembeni yake Maneno haya : Memento mori.“Remember that you too will die,” Respice post te. Hominem te memento. “Look after you [to the time after your death] and remember you’re [only] a man and you must die too.” na baadae General alikufa kweli.

Msemo huu mdogo wa memento Mori ukabadilisha jamii nzima ya ulaya na Dunia kuanzia sanaa, Dini, michezo, uchumi e.t.c watu wakaukumbatia kwa lengo la kuishi kama binadamu wanaopendana bila chuki, kuuana na kuteka himaya nyingine kibabe wakiamini kuna siku watakufa na kuiacha Dunia na Yote ya udhalimu waliyofanya ni ubatili tu wa Duniani.

Memento Mori.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Quote:

Magufuli: "Memento mori.“Remember that you too will die,” Respice post te. Hominem te memento. “Look after you [to the time after your death] and remember you’re [only] a man and you must die too.” na baadae General alikufa kweli." johnthebaptist
 
JF katika ubora wake...

Very rare these days.

Kumejaa maujinga ya misisiem tu.
 
Memento Mori.
images%20(1).jpeg
images%20(2).jpeg
images%20(3).jpeg
the-look-and-learn-version-of-events1.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo mnampa za uso mungu wa Tanzania .Watetezi wake hawaonekani hapa msamiati mgumu kwao ,ndio wanausikia Leo ?
 
Umeeleweka vizuri na hongera. Ila sidhani kama kuna mtu yoyote aliyepata kudhani kuwa yeye hatakufa. Ukiona binadamu anajiendekeza hivyo ujue mtu huyo anayo matatizo makubwa sana. Ni mtu wa kumhurumia na KUMUOMBEA.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom