Member mwenzetu YO YO yuko matatani

Asante kwa taarifa mkuu.
Kwa maelezo yako ni kwamba mwenzetu kavunja sheria, badala ya kusimama na 'kuongea' na walidna sheria yeye kakimbia, sasa huenda wamemuhisi ni jambazi. Angemalizana nao pale pale yangeisha. Anyway, tutafuatilia.
 
Tulishamwambia hapa bangi na pombe za kwenye visadolini bila msosi zitampeleka pabaya... ona sasa anaendesha gari utafikiri Kajima walimjengea barabara yeye... anaanza kusumbuana na wanausalama wetu!! Hope atapata mdhamana... mkulu Nguli wahi ukamsaidie huyu ndugu yetu tafadhali... mpe pole zake. Lakini mambo ya kutoa kitu kidogo usithubutu...tusijesikia nawe umesweka ndani kwa mlungula, maana jamaa sikuhizi wana vimobitel vyenye kamera pale.
una roho mbaya kama Rostam......nipo shega sina kesi ya kujibu.....
thanks Nguli
 
una roho mbaya kama Rostam......nipo shega sina kesi ya kujibu.....
thanks Nguli

Pole buddy! I had the same problem mwaka jana nilimalizana na jamaa kwa 30,000 Tshs. Yeah JF kuna magubeli wengi take easy
 
Typical you.

But that is very true Birigita. Ni sheria zimewekwa na lazima zifuatwe. Umewahi kuona waenda kwa miguu wanavyoteseka na hawa wanaotanua? Nilishuhudia mdada akigongwa maeneo ya Ubungo Tanesco sababu ya kutanua. Kwa kweli ni kutokuwa na uvumilivu sababu wote tunaelewa tatizo la foleni katika barabara zetu. Tukiwa wavumilivu foleni zitakuwa zinaenda kwa mpangilio. Utakuta mtu anatanua anaenda kuchomekea kwa mbele, kwamba hawa wengine waliofuata foleni hawana haraka au? Nachukiaga.
Watanzania tujifunze kama tuna haraka sana tuwe tunatoka nyumbani mapema kuepuka bughudha.
By the way, napma pole sana YO YO kwa kukumbwa na mkono wa sheria.
 
Nilikuwa sijaonhea na Yo Yo ndio kaachiwa tunapiga story kumbe alikimbia hadi ofisini akajifungia kwa bahati mbaya ofisi yake haiko city center iko mitaa ya kati. Basi wamemchukua mbele ya boss wake kwa sasa anarudi ofisini kumalizana na kesi ya pili ya kuchukuliwa na polisi ndani ya ofisi.

Police mwenye njaa kaimaliza kesi vizuri saana.

Naona kama tunachakachuliwa.....ninahisi kama ni hadithi ya abunuwasi
 
pole jaman
we mwambie akitoka anitafute nimpe POLE YA MAHABUSU..manake kule nako kuna mambo..lolote laweza kutokea ni segerea nusu..akitoka anione pls nimfanyie welcome hm beb
PM please Rose.....hawajanifilisi kihivyo.....
 
Ushauri kwa yoyo na wengine wanaopenda kuvunja sheria kwa kujua ama pasipo kutarajia, usiwakimbie polisi hata siku moja. Muhimu ni kuwa na ujasiri wa kusema nao tu, huwa hawashindwi kuelewa somo hata kama una kima cha chini kiasi gani.
mkuu ukifata sheria barabara za huu mji utalia kila siku.....hat hizi fine za kila siku sometimes zinakera gari uazime,uibiwe power window ulipe,ulipe parking,wese bado kimeo......na trafiki utanue umpe mkwanja??? hell noo
 
mkuu ukifata sheria barabara za huu mji utalia kila siku.....hat hizi fine za kila siku sometimes zinakera gari uazime,uibiwe power window ulipe,ulipe parking,wese bado kimeo......na trafiki utanue umpe mkwanja??? hell noo

Usitanue sasa kama hutaki kuwalipa....

Pole lakini Mkuu!!
 
Pole mkuu yoyoyo

usiwe na shaka mafisadi wako wengi jf si lazima wawe na rangi ya ra
 
But that is very true Birigita. Ni sheria zimewekwa na lazima zifuatwe. Umewahi kuona waenda kwa miguu wanavyoteseka na hawa wanaotanua? Nilishuhudia mdada akigongwa maeneo ya Ubungo Tanesco sababu ya kutanua. Kwa kweli ni kutokuwa na uvumilivu sababu wote tunaelewa tatizo la foleni katika barabara zetu. Tukiwa wavumilivu foleni zitakuwa zinaenda kwa mpangilio. Utakuta mtu anatanua anaenda kuchomekea kwa mbele, kwamba hawa wengine waliofuata foleni hawana haraka au? Nachukiaga.
Watanzania tujifunze kama tuna haraka sana tuwe tunatoka nyumbani mapema kuepuka bughudha.
By the way, napma pole sana YO YO kwa kukumbwa na mkono wa sheria.
Mkuu, issue ni moja tu, ndio kavunja sheria, kwa hiyo asisaidiwe? mleta topic ametoa taarifa na kusema **** kuna mtu anaweza kumsaidia afanye hivyo, sio kwa maana ya kushabikia au kuhalalisha kutanua. mm mwenyewe nikiona watanuaji natamani nipasue vichwa kama alivyofanya marehemu mzuzuri.
Kwa jinsi sheria zetu zilivyo, pale alikuwa anaweza kubambikwa kesi mbaya sana kama hakuna mtu around kuhakiki kuwa polisi hawachakachui.
 
kwanini hakusimama in the first place sasa unataka asaidiwe nini
 
Nilikaribia kupata mshtuko wa moyo kuona wapiganaji wanasisiza polisi wapewe rushwa ili kumnusuru mvunja sheria.

Huyo huyo mpiganaji anamlalamikia Chenge kwa rushwa kwenye dili la rada.

Shame on you.
 
Wandugu,

Nimewasiliana na ndugu wa karibu wa member mwenzetu YO YO na ameniarifu kuwa amekamatwa na amefungwa lupango/rumande leo asubuhi. Kwa kosa la kutanua barabarani kutokea maeneo ya mbezi beach akielekea kutafuta mkate wa kila siku. Inasemekana alisimamishwa na trafic lakini hakusimama. Basi traffic police wakawasilina na wenzao kwa redio call ndio wakamtia nguvuni. Kwa hiyo yuko kituo cha O'bay police na juhudi za kumfikisha mahakamani ndio zinafanywa na wanausalama wetu.

Nilikutana nae mara ya mwisho last wk end akiwa na gari yake mpya aliopata baada y Mwenyezi Mungu kumjalia ajira kijana mwenzetu. Nimesikitishwa na kustushwa na habari za ndg yetu huyu.

Tunaomba kama una ndg pale utusaidie kwa kesi hii, YO YO anaweza kunyea SIMTANK na sio NDOO kutokana na kuwa dodge wanausalama. Au kama unaweza kutoa msaada wa kisheria pia tutashukuru. Nitaelekea huko baada ya kupata ruhusa kazini ili tumwekee mdhamana

hawa mabwege wanaotanua huwa wananikera sana, wote tukikaa kwenye foleni huwa foleni inatembe haraka lakini hii mibwege inayotanua inasababisha sie tunaokaa foleni tuteseke sana.

KUTANUA barabarani ni ulimbukeni, ushamba, kutokustaarabika, uzuzu, ubinafsi, kuamini we ni bora kuliko mwenzako yaani ni kero,mngemwacha akae jela kidogo akitoka atakua kafundisha namna ya Kubehave, mngemwacha tu
 
Mkuu, kosa la kutanua faini yake ni 250,000 au 300,000 sina uhakika sana kati ya hizo mbili, au jela 2 weeks na faini juu.
Jamaa wakikufikisha mahakamani tu, unasomewa hukumu, sio mashtaka.............Waulizeni madereva wa daladala wanavyoteseka kwa hii sheria ya kishenzi.

Nguli, check na ndugu wa karibu au mshkaji wa karibu wamuwahi kabla ya kwenda mahakamani. Tafadhali.
Wana Jf ni vizuri tusiwe na double standards katika mambo ya sheria.
Mimi nakaa sehemu hizo na kati ya mambo yanayokera sana barabarani ni watanuaji!!
Kama mdau mmoja alivotoa, watanuaji wanafikiri baarabara wamejengewa wao, wanaovertake kushoto!! na kwa taarifa yenu HAIPITI siku nne bila kusikia mtoto,mzee,mama kagongwa na watanuaji na hawasimami!!
Namhurumia YOYO lakini ni vema akaelewa pilato yupo, mbaya zaidi anakimbia badala ya kuyamaliza mwenyewe barabarani.
What an irresponsibile character!!
 
kavunja sheria. vile vile ni mkorofi. angetakiwa apewe adhabu ya viboko kumi na faini. hatarudia tena.:shock:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom