Member mwenzetu hatunae

Member mwenzetu hatunae

Sina member anayenifahamu humu, siku nikitwaaliwa kwenda mbinguni kwa Mungu Baba sijui nani ataleta habari humu. Wengine wanabadili badili ID, wengine wana ID nyingi ni ngumu kuwajua kama nao watatwaliwa, hatutaweza kuleta habari zao humu
Nilipewa jukumu kwenye thread Fulani nimtafute Intelligent businessman

Hayupo what's up namba haipatikani
 
Kifo cha kijana ni simanzi ,kifo cha mzee ni shehereko, yote ya yote hakuna furaha katika kifo isipokuwa tumaini na shukrani kwa mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha.

Hivyo shukrani za dhati kwa mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha ya ndugu huyu, na uwepo wake katika jamii yetu pamoja na huduma yake katika jamii yetu .

Pole nyingi kwa familia , wakati mmoja tutakutana mahali pasipo kuwa na machozi, asubuhi ile ya milele inayotarajiwa na kila mtu.
 
Maisha ni mafupi sana,tupendane maana hakuna chenye thamani duniani zaidi ya uhai.

Uhai wa mtu haufananishwi na kitu chochote,hivyo hatuna sababu ya kuishi kwa kuumizana,kutesana.

Tumuombee member mwenzetu Mwenyezi Mungu ampokee.

MARANGU MOSHIView attachment 3675678
May your soul rest in heavenly place. See you in heaven #Praygod
 
Hakuna wakati kifo kilipokuwa jambo jepesi kwa mwanadamu. Hivyo tunawaombea wanafamilia na ndugu wa huyo mwenzetu, Mungu awajalie moyo mkuu wa kuweza kuyapokea magumu haya kwa moyo wa imani na matumaini.

Tunamwomba Mungu wa huruma na msamaha, ampokee katika makao yake ya milele. Raha ya Milele umpe Ee Bwana, Roho ya ndugu yetuhuyuipumzike kwa amani.
 
Back
Top Bottom