DALLAI LAMA
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 8,652
- 2,642
Hebu elezea hiyo equality uliyoionesha hapo? wanafanana nini? sura au? kuwa great thinker wewe acha kuandika kizembezembe ebooo! mnaboa sana humu watoto wa mayai ninyi
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema hajaoteshwa kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri Membe alisema harakati za kugombea urais siyo kitu kidogo cha kukurupuka, kwani unatakiwa kuwa na muono unaokujia kuwa mgombea.
Usikurupuke tu, lazima uwe na kitu kinakutuma kuomba kugombea Urais, lakini sasa ninachosikia ni kutoka kwa watu kuwa nataka kugombea kitu ambacho hakina ukweli, alisema Membe.
Membe alisema wakati alipotaka kugombea ubunge, alisikia sauti ikimtaka kugombea na akafanya hivyo, lakini kwa sasa bado sauti hiyo haijamjia.
Sauti kama hii ilinijia wakati nilipotaka kugombea ubunge nami nilifanya hivyo, lakini sasa bado sauti hiyo haijanijia, alisema Membe.
Aombe Mungu amsaidie hiyo sauti ismjie kamwe - sasa na hata milele. I hate this type statements kutoka kwa wanasiasa wetu!!! Wanatudanganya kuwa hawahitaji wakati tunashuhudia mikakati na vikumbo wanavyopigana kupitia vyama na hata serikalini!!! Mungu ibariki Tanzania.WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema hajaoteshwa kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri Membe alisema harakati za kugombea urais siyo kitu kidogo cha kukurupuka, kwani unatakiwa kuwa na muono unaokujia kuwa mgombea.
Usikurupuke tu, lazima uwe na kitu kinakutuma kuomba kugombea Urais, lakini sasa ninachosikia ni kutoka kwa watu kuwa nataka kugombea kitu ambacho hakina ukweli, alisema Membe.
Membe alisema wakati alipotaka kugombea ubunge, alisikia sauti ikimtaka kugombea na akafanya hivyo, lakini kwa sasa bado sauti hiyo haijamjia.
Sauti kama hii ilinijia wakati nilipotaka kugombea ubunge nami nilifanya hivyo, lakini sasa bado sauti hiyo haijanijia, alisema Membe.
Membe anauota urais kila siku na sidhani kama inapita nusu siku hajaukumbuka. Ni kama fisi anavyounyemelea mzoga. Lakini adui yake wa kwanza sio Kikwete kama ulivyosema. Adui yake ni mkubwa ni rekodi ya utendaji wake na mbinu anazotumia kuwania urais. Hakuna chochote katika rekodi yake ya kazi kinachoonyesha kuwa anaweza kuwa rais mzuri sembuse uwaziri alionao. Yeye na Kikwete kiutendaji wamefanana kama mayai. Na kadiri siku zinavyokwenda wapiga kura wanazidi kufunguka macho. Hivyo kwake itakuwa ngumu sana sana kupenya kwenye uchaguzi kwa sababu ya utendaji wake. Na mbaya zaidi anajaribu kutumia mbinu zile zile za kimbugwe alizotumia pacha wake (Kikwete) kuutafuta urais. Amekosea. Rais wa Tz 2015 atachaguliwa kwa kuangalia rekodi ya utendaji na si uswahili swahili kama aliotumia KikweteMembe anautaka urais na tayari ameishaanza mikakati miwili:
-Kujijenga kwa kuteua kamati ya mikakati inayoongozwa na Nyalandu
-Kuanza kubomoa na kuchafua wale anaoona ni kikwazo kwake. Adui na kikwazo chake kikubwa ni EL.
Mtu mwingine anayemwona ni tishio la kazi ni January Makamba. Juzi alipoteuliwa kuwa naibu wizara ya teknolojia, Membe alikunywa mzinga wa Whisky kwenye ndege akielekea London kwa kushangilia kuwa sasa January anampisha kwenye Sekretariat ya CCM maana alikuwa amechukua nafasi yake kwenye chama. January ana ndoto za kuwa Rais mwaka 2015 (msiniulize chanzo).
Lakini Membe anasahau kitu kimoja: Adui yake wa kwanza katika azma yake ya kuutaka urais ni JK. Huyu atamgeuka dakika za mwisho na atalia kilio cha mbwa koko. JK ana mtu wake, na huyo si Membe.
Anachopaswa kufanya Membe, ni kuunganisha nguvu zake bila kuchafua wengine. Kosa alilifanya JK na sasa linamgharimu.
Jambo moja nina uhakika kuhusu Membe na Urais.
Awali ya yote, wa kwanza kabisa kuzungumzia suala la Member na Urais ni gazeti Rai miaka kadhaa iliyopita pale alipomuumbua Hassy Kitine. Wakati huo Membe alikuwa ni Mbunge tu...enzi za Mkapa. Likewise, wengi wakati huo walikuwa hawamfahamu Membe.
Baada ya Kombora la Membe ambalo lilimwondoa Kitine kwenye nafasi ya Uwaziri, Rai ikafanya mahojiano na Membe na moja ya maswali ambayo ilimuuliza ni kama ana mpango wa kugombea Urais 2005. Membe akasema wazi kwamba hana mpango huo.
Baada ya kuingia JK, Membe alianza unaibu Waziri (if am not mistaken, mambo ya ndani au nishati). Later akateuliwa Waziri Mambo ya Nje! Kama ilivyo mazoea yetu, tunazani kila anayekuwa Mambo ya Nje, ni move towards Urais...hili lilitokana na Mkapa na JK kuwa Mambo ya Nje b4! Hapa sasa, ndipo Wabongo tukaendelea kuitilia nia suala la Membe na Urais. nakumbuka hata yeye mwenyewe aliwahi kujibu kwamba, hadi yeye, kuna Mawaziri 13 ambao walipitia nafasi hiyo, na only 2 ndio wamepata kuwa marais.
So, kama kweli Membe ana nia na Urais, basi nia hiyo ilijengwa na vyombo vya habari pamoja na wananchi. Katika hali ya kawaida, ikiwa watu wanakuzungumzia zungumzia kuhusu post fulani, basi huenda nawe ukajikuta unajihisi labda unastahili kwa nafasi hiyo!! Na as far as nae ni Mtanzania basi anastahili nafasi hiyo....Wapiga kura ndio watakaomua kama anafaa au hafai.
Binafsi, sijaona move yoyote ya Membe kutaka Urais sana sana ninachokiona ni hofu ya wanaotaka urais pamoja na wapambe wao. Hawa watu inaonesha dhahiri kwamba wanamuhofia Membe...!!!