FJ kuna mtu ametuloga. Sasa hivi tunasahau hoja za leo na kuingia kwenye ramli zinazohusiana na miaka karibu sita ijayo. Kujadili kufaa au kutokufaa kwa Membe au mwanasiasa yeyote kwa sasa ni pre-mature na kwa maoni yangu hakuna tija yoyote maana hao tunaowaona leo siyo lazima wawepo ulingoni wakati huo na wala hawana hati miliki ya siasa za nchi hii. Kumbuka miaka sita ijayo population ya nchi hii itaongezeka by more than 5% na wapiga kura wa ngazi mbalimbali watabadilika kwa kiasi kikubwa na hata utashi wao na vipaumbele vyao vitabadilika. Hata hivyo, who said that Membe is interested in the presidency? He has not declared his intention or ambition. Mimi nadhani apimwe kwa nafasi yake badala ya kupaza sauti za watu ambao wamejazwa na hofu kuwa candidature yake (perceived) ita-scuttle bids za wanaoutaka kweli. Mimi nashauri tusiangukie kwenye mtego wa watu wanaoendesha opinion poll kupitia JF na kupima upepo wa kukubalika kwao kwa kuchochea mijadala isiyo na tija. Tujadili ya leo na vita ya karibu kwetu ambayo ni 2010 maana hatujui kama hata huyo Membe atatetea kiti chake cha ubunge, achilia mbali kuteuliwa tena kwenye uwaziri huo. Nionavyo mimi politics za 2015 zitatengenezwa 2012 kwenye chaguzi za chama chao CCM.