Membe kuwania urais 2015...

Membe kuwania urais 2015...

Asha rose mingiro hana uwezo hata nusu wa kuiongoza tz, Tanzania inahitaji watu wenye mukrari na force ya nguvu kwenye utendaji. Hata kama Lowasa hata kubalika, tunatakiwa mtu mwenye aina ya utendaji wa kilowasalowasa madarakani. hapo ndo tutafika. hivi wewe kwa akili yako umeona acha rose mingiro anaweza chochote, au kwasababu alipigiwa pande aende UN, hivi kila mtu aliyepata habati ya kwenda UN unafikiri ana uwezo wa kuwa rais?....unafikiri kama wangesema tuchague sisi watz kwa kura mtu wa kwenda UN asha angeenda? si bahati yake tu ilimdondokea.....hebu leta wazo lenye akili tafadhali, ondoa fikra za ajabuajabu hizi.

Lowasa anatakiwa kurudi, amejeruhiwa na akirudi lazima atahakikisha anasafisha jina na kuweka historia kuwa yeye si mtu mbaya, hiyo iko wazi. kama akiwa rais atajitahidi uwezo wake wote kufanya kitu cha maana ili ionekane kuwa yeye ndo alikuwa bora na safi kuliko wote. NA HAKUNA UBISHI KUWA KATIKA SELIKALI YOTE YA TZ, HAKUNA MCHAPAKAZI KAMA LOWASA...namfananisha na Kagame, akiwa kazini hataki kunegotiate ujinga, hataki utani ni kupiga kazi kwenda mbele. huu ndo ukweli wenyewe.

Mkuu, huwa nikiwaambia watu hivyo hawanielewi. Nina uhakika Lowasa akipewa rungu, nchi itabadilika? akiwa PM hajawahi kupewa riport za uongo kana JK ambaye ni Rais - kwa sababu watendaji wanajua akili yake si ya kivivu. Kama kosa alifanya, nina uhakika ameshajifunza na kujirekebisha. Huyu cheka cheka na bongo flava hatatupeleka popote zaidi ya shimoni tu.
Ikiwa atakuwa rais, kufikia 2015 inawezekana hata chai wengi wakashindwa kunywa kutokana na mfumko wa bei - watanzania wengi wanaweza wasimuda kununua sukari. to name the few.
 
Baada ya huyu mtu wenu, ni bora tukapata mtu asiye fungamana na chama cho chote cha siasa hasa ccm (better awe na dictatorship mind set) na siyo membe wala yeyote kutoka ccm
1-avunje na kuunda upya tume ya uchaguzi na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwa mwonekano wa kitaifa na si kisiasa, kabila wala dini
2-arekebishe au asimamie kuandikwa upya katiba
3-ikiwezekana hata mahakama iundwe upya na ipractice kuwa chombo huru
4-ikiwezekana hata vyama vya siasa vivunjwe na kuundwa upya

Labda tuwe na mgombea binafsi ndio hivi vitatekelezeka maana atayakwepa mengi
 
Baada ya huyu mtu wenu, ni bora tukapata mtu asiye fungamana na chama cho chote cha siasa hasa ccm (better awe na dictatorship mind set) na siyo membe wala yeyote kutoka ccm
1-avunje na kuunda upya tume ya uchaguzi na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwa mwonekano wa kitaifa na si kisiasa, kabila wala dini
2-arekebishe au asimamie kuandikwa upya katiba
3-ikiwezekana hata mahakama iundwe upya na ipractice kuwa chombo huru
4-ikiwezekana hata vyama vya siasa vivunjwe na kuundwa upya
Mnajiombea mabaya...Kumbuka dictator wengi wanataka kuambiwa kile wanachotaka kukisikia.Mmeona Kenya mama Kibaki alivyopiga watu vibao na Russia watu wanavyopotezwa.
Bora tubaki na huu uhuru wetu wakutoa hasira zetu hapa Jamboforums kuliko kukosa yote.
 
Hivi jamani Membe ana Digrii kweli? habari nilizo nazo ni kuwa hana.........mbali na hilo kichwa cha panzi!
 
Tunahitaji mabadiriko na haya mabadiriko sijui yataletwa na nani
Ndani ya CCM hakuna mtu mwenye sifa ya kuendelea kuwa Rais wa nchi hii basi wanalazimisha tu
 
Mnajiombea mabaya...Kumbuka dictactor wengi wanataka kuambiwa kile wanachotaka kukisikia.Mmeona Kenya mama Kibaki alivyopiga watu vibao na Russia watu wanavyopotezwa.
Bora tubaki na huu uhuru wetu wakutoa hasira zetu hapa Jamboforums kuliko kukosa yote.

Ukiwa raia mwema huwezi kupotezwa. Kwa waandishi wa habari wa TZ anatakiwa festi ledi kama mama kibaki. Wengi ni vibaraka na wameshanunuliwa na wanasiasa.
Bakora tu ndizo zinaweza kuwaamsha.
 
Hivi jamani Membe ana Digrii kweli? habari nilizo nazo ni kuwa hana.........mbali na hilo kichwa cha panzi!
Membe ana MA aliipata Johns Hopkins University USA. Nilimwona kwa macho yangu wakati wa graduation. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Tanzania ya leo hii haihitaji mtu wa aina ya Membe!.i see him as too linient, na amekaa kisherehesherehe zaidi...Membe kauli zake kila siku ni za kitatanishi tu, na ana hali ya kupendelea baadhi ya nchi!....Tanzania hii by 2015 inahitaji rais ambaye ni 50%coctail ya udikteta na Busara!...Punda haendi, ila kwa mjeredi!

Kwa sifa hizi, ukilinganisha Lowassa na Membe, inaonekana Lowassa anafaa zaidi... lakini tunaweza kumfikiria na Wassira? - I mean sura yake ni ya kidikteta zaidi kuliko hawa
 
..kwangu mimi huu uchaguzi umekwisha na JK ndiyo Rais.

..matokeo haya yamenisikitisha sana, kwasababu naamini kabisa Slaa au Lipumba ni more capable kuliko JK.

..sasa CCM ina tabia ya "kujivua ngozi" ngozi kila inapofikia wakati wa kubadilisha mgombea Urais.

..kwa mtizamo wangu January Makamba, Magufuli, Membe na Migiro, wanapaswa kuangaliwa kwa umakini sana kuelekea mwaka 2015.

..wapinzani wajiandae jinsi ya kupambana na yeyote kati ya hao itakapofika 2015.
 
JokaKuu swala la January Makamba kuwa rais 2015 ondoa kabisa akili mwako kwa sababu kuu mbili CCM wana katiba ya siri isiyoandikwa mathalani rais wa sasa ni mwislamu ajaye ni lazima kuwa mkristo moja kwa moja J Makamba anakuwa nje ya mashindano pili atakuwa ni waziri junior jambo ambalo wakongwe hatakubali kabisa.

Magufuli haweze kwasababu hana mtandao kwenye chama yeye ni mchapa kazi tu kama Mizengo Pinda, kuhusu Membe ana maadui wengi akiwamo lowassa huyu kupita itakuwa kazi ukizingatia kuwa ni swahiba wa Kikwete na CCM wanataka kukoma kwa Kikwete Revolution by 2015 akilazimisha nchi itakwenda upinzani pia CCM wanataka rais ajaye atoke Bara na si Pwani kwani Tanzania imekuwa na marais wanne mmoja pekee Julus Nyerere ndiye aliyetoka bara wengine wote ni mwambao wa bahari ya hindi Ali Hassani Mwinyi, Benjamini Mkapa na Jkaya Kikwete kuuonezea Membe mwana pwani mwingine haitawezekana kabisa.

Urais 2015 uko wazi chunga sana Lowassa, Sumaye, Mwandosya na Rose Migiro
 
Heri mama Migiro at least nitampa kakura kangu ambako hakataniuma roho
 
Ata mwandosya nae anafaa kimtindo ingawa CCM ya leo haitaki watu ambao wanastand on what they say.
CCM ya leo wanataka watu wenye mzaa mzaaaaaaaaaaa
 
MAGHUFULI JOHN POMBE(PHD) / ASHA ROSE MIGIRO wanafaaa kuongoza nchi

 
Mama Tibaijuka mmemuweka wapi? Pinda je? Dr. Bilali???

Pinda tayari alishasema hii ndio mara yake ya mwisho. Wapiga kura wametoa message kali kwa hiyo CCM itajipanga 2015. Sidhani kama watamsimamisha mbabaishaji au mshikaji wa Kikwete. Lakini yote hayo pia yatategemea jinsi Kikwete atakavyoendesha nchi miaka 5 ijayo.
 
wakitaka CCM kushinda kirahisi wamweke Dr Harison George Mwakyembe, ila kama jadi yao CCM haitaki mtu mkweli au msomi mwenye msimamo
wenyewe na vuvuzelas, period
 
Sijaipenda thread hii mi nkijua baada ya 2010 mchakachuo, Dr.SLAA atawashika tena, siwezi fikiria mwingne kwa sasa. Kwa CCM yeyote watakaemtaka ila mwanamke haitawezekana kwa sasa, sori 4 this.

Siwachukii wamama ila kdogo upresidaa unataka kijeba, kutunisha misuli, kumbuka tangu mama Zakia meji aharibu pale benki kuu,watawala waliapa kutorudia kosa. Halafu kuhimili siku 71 za kampeni mwanamke hawezi sana sana kama bado anauona mwezi,sori 4this bt guess wote mu watu wazma.

Nasema na nina uhakika Tz ya leo mikononi mwa mwanamama bado sana!
 
Kiongozi yeyote wa CCM hawezi kuleta mabadiliko ya kuwasaidia watz..tusidanganyike, CCM machine is corrupt to the core kama kansa na hakuna tiba tena.
 
Back
Top Bottom