Bernard Membe aitwa kwenye Kikao cha Kamati ndogo ya Udhibiti wa Nidhamu CCM

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
1580893895298.png

Kupitia Ukurasa wa Mtandao wa Kijamii wa Twitter, aliyekuwa Waziri wa zamani
wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amesema ameitwa Jijini Dodoma kwenye Kikao hicho cha CCM

Amesema amepata barua ya kuitwa hapo jana na ataudhuria bila kukosa au kuchelewa kikao hicho kitakachofanyika Februari 06 saa 3 asubuhi kwenye Jengo la White House

Mwaka Jana kulisambaa sauti zinaohusishwa kuwa ni za Membe na wengine waliowahi kuwa Viongozi wa CCM wakizungumzia kuhusu mpasuko ndani ya Chama na pia kusikika wakilaumu uongozi ulipo sasa

1.PNG


======
Dar es Salaam. Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe ameitwa kuhojiwa na kamati ya maadili ya CCM.

Mbali na Membe, wengine wanaotakiwa kuhojiwa na kamati hiyo ni makatibu wakuu wastaafu wa chama hicho tawala nchini Tanzania, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba.

Hata hivyo, makatibu wakuu hao wa zamani hawajathibitisha kama nao wameitwa kuhojiwa licha ya Desemba 2019 chama hicho kuwataja wote watatu kuwa watahojiwa na kamati hiyo.

Vigogo hao, waliokuwa mjadala hivi karibuni baada ya sauti za baadhi yao kusambaa mitandaoni wakizungumzia kupasuka kwa CCM.

Leo Jumanne Februari 4, 2020 katika wa mtandao wa kijamii wa Twitter uliotumwa na mtu mwenye jina kama la Membe umeeleza kuwa ameitwa kuhojiwa.

“Hatimaye jana jioni nimepokea barua ya kuitwa kwenye kikao cha kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu jijini Dodoma.”
“Kikao kitafanyika Februari 6, 2020 saa 3 asubuhi kwenye jengo la White House. Nitahudhuria bila kukosa na bila kuchelewa! Stay tuned,” amesema Mwanadiplomasia huyo.

Licha ya kutopatikana lakini Membe hutumia akaunti hiyo kueleza masuala mbalimbali, ikiwemo maendeleo ya kesi yake mahakama kuu.

Siku ilipotangazwa kuwa watatu hao watahojiwa, Halmashauri Kuu ya CCM ilieleza kuwasamehe na kuwaonya wabunge wa tatu, January Makamba (Bumbuli), William Ngeleja (Sengerema) na Nape Nnauye (Mtama) ambao kwa nyakati tofauti walimuomba msamaha mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Kuitwa kwao kuliibua upya sakata lililoonekana kutulia ndani ya CCM.

Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ali aliwahi kumlaumu Membe kutoonekana tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu. Dk Bashiru, akiwa mkoani Geita, alimtuhumu Membe hadharani kuwa anakwamisha mkakati wa urais 2020 wa Rais Magufuli, huku akimtaka afike ofisini kwake.

Lakini waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje alimjibu kuwa CCM ina utaratibu wake wa kuitana.

Siku hiyo ujumbe wa Twitter uliotumwa na mtu mwenye jina kama la Membe ulisema atakapokwenda ofisini kwa Dk Bashiru, mtu anay-emtuhumu kuandaa mkakati wa kumng’oa Rais Magufuli, naye awepo ili athibitishe tuhuma hizo.

Hivi karibuni ziliibuka sauti za viongozi mbalimbali, zikiwamo zinazosadikika kuwa ni za wabunge hao, zikizungumzia waraka ulioandikwa na Makamba na Kinana kuhusu uongozi wa CCM kutowalinda dhidi ya vitendo vya kudhalilishwa.

Makatibu hao wa zamani waliandika waraka huo kwa katibu wa Baraza la Ushauri wa Viongozi wa CCM, Pius Msekwa wakizungumzia mmoja wa wanaharakati ambaye amekuwa akiwachafua bila hatua kuchukuliwa.

Makamba na Kinana waliokuwa watendaji wakuu wa chama hicho tawala katika awamu ya nne, walitumia katiba ya CCM, toleo la 2017 ibara ya 122 kuwasilisha malalamiko yao ambayo yalizua mjadala ndani na nje ya chama hicho.

Msekwa aliwaandikia barua vigogo hao akijibu malalamiko yao waliyoyawasilisha kwake wakidai kudhalilishwa kwa mambo ya uzushi, uongo na mtu aliyejitambulisha kuwa mwanaharakati na mtetezi wa Serikali.

Soma: Ukumbi wa White House Dodoma: Membe, Makamba na Kinana kuhojiwa na Kamati ndogo ya Maadili ya CCM
 
Kwa jinsi unavyojiamini,ni wazi una hoja nzito za kujitetea, sema tu hawatasikiliza wala kuzingatia hoja zako bali wataingia kwenye kikao wakiwa tayari na maamuzi yao mifukoni.

Kwa mtazamo wangu, kikao hiki ni cha ushahidi tu ili ionekane umepewa haki ya kusikilizwa.
 
Kwa jinsi unavyojiamini,ni wazi una hoja nzito za kujitetea, sema tu hawatasikiliza wala kuzingatia hoja zako bali wataingia kwenye kikao wakiwa tayari na maamuzi yao mifukoni.

Kwa mtazamo wangu,kikao hiki ni cha ushahidi tu ili ionekane umepewa haki ya kusikilizwa.
Kikao hiki kitawapa hoja mpya Chadema na kuwasahaulisha yote yaliyopita ikiwemo barua ya Mbowe kwa mwenyekiti wa CCM!
 
Influenza,

barua kaandikiwa yeye, alafu yeye aanze kutangaza kwa umma kwani anaogopa nini kama anajiamini, mambo yake nayo yametuchosha, amalizane nao kisha kama anona kuna musada anataka kwa jamii ndo aandike, mbona anapotaka kufanya mambo yake ya kila siku haweki mtandaoni?

CCM aliingia mwenyewe na kuicha au kuivulimia ni wazo lake mwenyewe. Angetaka tujue angesema nimeitwa lakini sitaenda wachukue uamuzi wowote, ingekuwa na maana, atuache tupumue, bado tuna misiba mingi Arusha na JKT, tuna mawazo ya wapendwa wetu.
 
Kwa jinsi unavyojiamini,ni wazi una hoja nzito za kujitetea, sema tu hawatasikiliza wala kuzingatia hoja zako bali wataingia kwenye kikao wakiwa tayari na maamuzi yao mifukoni.

Kwa mtazamo wangu,kikao hiki ni cha ushahidi tu ili ionekane umepewa haki ya kusikilizwa.
Membe si wa kukumbushwa kuhusu maamuzi onevu ndani ya CCM. Yeye mwenyewe alishawahi kuwa wehemu yq waratibu wakuu wa mipango miovu ya chama kea watanzania. Kwahiyo acha naye aionje na kufurahia kazi ya mikono yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom