Membe apinga kufutwa uchaguzi wote Zanzibar

Membe apinga kufutwa uchaguzi wote Zanzibar

Huyu Membe hafahamu kama Zanzibar ni nchi yenye mipaka yake, Rais wake, Bunge lake, mahakama zake na Jeshi lake!

Inawezekana hafahamu kama Zanzibar wana katiba yao!

Hafahamu kama wazanzibari wenyewe wakiongozwa na jopo la Marais wastaafu wa nchi ya Zanzibar wanaendelea na vikao!

Kwa hiyo anataka kutuambia kama yangefutwa baadhi ya majimbo asingeshangaa!

Hafahamu kama Maalim Seif alishinda Uchaguzi Mkuu wa 2010? Hakumsikia Mzee Hassan Nassor Moyo?

Ni nini kinamfanya ashangae kwa sasa kufutwa kwa matokeo yote?

Membe nadhani anasumbuliwa na weweseko la maisha nje ya siasa wakati umri bado unaruhusu. Tatizo aliaminishwa sana kama atakuwa mgombea Urais mpaka akaamua kuliachia Jimbo la Mtama.

Rais Magufuli ameamua kutomteua kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje. He's already casted aside and now, he's bitter!
Kati ya Membe na wewe nani anaijua Zanzibar vizuri au unajitia u much know, Membe ni ex Foreign affairs minister wakati wewe ni kapuku tu wa JF hata ujengaji wa hoja ni sifuri.
 
Kama mimi U-CCM umenijaa, wewe ndugu yangu umejaa U-nini?

Kitu gani kinakufanya udhani kwa sasa ndiyo dunia inatuona wa ajabu? Umejuaje kama dunia haikutuona wa ajabu kipindi cha nyuma?

Kwa hiyo walivyoiba kura mwaka 2010 kama unavyodai, dunia haikutuona wa ajabu?

Nimeuliza, huu ukweli anaosema Membe kwa nini ameanza kuusema baada ya mambo yake ya kisiasa kugonga mwamba.
Waswahili huangalia walipoangukia si walipojikwaa.
huyu jamaa ameona kile ambacho si sahihi na kusema, wewe unazungumzia kupitishwa na ccm kweli uko serious?
MCC imekata msaada wa Trillion 1 unaona kama umejificha watu hawakuoni kweli?
kweli kuna haja ya kuuliza kuhusu Nchi za Magharibi na Uchaguzi wa Zanzibar?
au ndiyo ulevi wa CCM
 
Kati ya Membe na wewe nani anaijua Zanzibar vizuri au unajitia u much know, Membe ni ex Foreign affairs minister wakati wewe ni kapuku tu wa JF hata ujengaji wa hoja ni sifuri.
Kwa hiyo?

Kama anaijua Zanzibar vizuri kimemshinda nini kwenda kutatua hayo anayodai ni matatizo. Mwambie aende akatatue hayo anayoyasema ni matatizo.

Matatizo ya Zanzibar ameanza kuyaongea baada ya kuisoma namba ya Rais Magufuli.

Hoja zako ziko wapi ambazo siyo sifuri?
 
Kwa hiyo?

Kama anaijua Zanzibar vizuri kimemshinda nini kwenda kutatua hayo anayodai ni matatizo. Mwambie aende akatatue hayo anayoyasema ni matatizo.

Matatizo ya Zanzibar ameanza kuyaongea baada ya kuisoma namba ya Rais Magufuli.

Hoja zako ziko wapi ambazo siyo sifuri?
Kutatua tatizo ni pamoja na kujua chanzo cha tatizo, Membe kaonyesha chanzo kuwa ni Jecha kufuta uchaguzi wote.
 
Kutatua tatizo ni pamoja na kujua chanzo cha tatizo, Membe kaonyesha chanzo kuwa ni Jecha kufuta uchaguzi wote.
Hakuna jipya alilolisema huyu Membe ambalo wananchi hawalifahamu. Watu wengi wanafahamu Zanzibar kuna mkwamo wa kisiasa.

Kwani huyo Jecha alijiwekwa mwenyewe kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi?

Vyama vya CCM na CUF vilikubaliana Jecha awe Mwenyekiti wa waliyokuwa wanaita Tume Huru ya Uchaguzi.

Mbaya zaidi, waliandika Katiba yao kwa haraka ili kuwakomoa Watanganyika lakini wakasahau kuweka political safety net ya kukabiliana na mikwamo ya kisiasa kama ilivyotokea kwa sasa.

Kikatiba, Rais Magufuli hana mamlaka ya kuingilia uchaguzi wa Zanzibar. Uchaguzi wa Zanzibar siyo suala la Muungano. Ulinzi wa ndani na nje ni suala la Muungano.
 
Ndio kusema Kuna baadhi ya wana CCM akili imeanza kuwarudi,au wanaongea kiunafiki maana kabla hawajatangaza kurudiwa uchaguzi walikuwa kimya,kama vile kulikuwa hakuna jambo lililokuwa linaendelea kule Zanzibar.
Ameshatumbuliwa
 
Membe is extremely shallow.
Hoja zake nyingi hazina ukweli, naona ana bifu na mzee Pombe. Mara ukubwa wa serikali, ukweli kama angeweza kuchambua angeona tofauti kati ya waziri mmoja na makatibu wa kuu 3 na Mawaziri 3 na makati wakuu 3, Kwake yeye ukubwa ni huo huo.
Membe ni replica ya Kikwete, inawezekana wana genetic resemblence kama wengine wanavyo dai humu
 


Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar akisema dunia inashangaa, na akaitaka CCM na Serikali isiwaachie watu wawili tu kutafuta njia za kutatua mgogoro huo.

Membe anakuwa mwanasiasa wa kwanza mwandamizi kutoka chama tawala kuonyesha waziwazi kutoridhishwa na uamuzi wa kufuta uchaguzi huo wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani ambao ulifanyika sambamba na uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, wabunge na madiwani wa Bara na Visiwani.

“Kinachoishangaza dunia si kuahirisha uchaguzi, bali ni kufuta matokeo ya majimbo yote,” alisema mwanadiplomasia huyo katika mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili mapema wiki hii.

Uchaguzi wa viongozi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 sambamba na Uchaguzi Mkuu, ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28 kwa maelezo kuwa sheria na taratibu zilikiukwa na akaahidi kuitisha uchaguzi mwingine baada ya siku 90 zinazomalizika wiki ijayo.

Chama kikuu cha upinzani visiwani, CUF, ambacho kilimsimamisha Maalim Seif Sharif Hamad kugombea urais, kinapinga uamuzi huo kikisema si mwenyekiti wa tume wala ZEC wenye mamlaka ya kufuta matokeo na kutaka mshindi atangazwe ili chama hicho kwa kushirikiana na CCM vikutane kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Katika kujaribu kutatua mgogoro huo, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Maalim Seif wameshafanya vikao tisa Ikulu Zanzibar pamoja na marais wa zamani wa visiwa hivyo, Dk Amani Karume, Dk Salmin Amour na Ali Hassan Mwinyi, bila ya mafanikio na tayari katibu huyo mkuu wa CUF ameshatangaza kujitoa kwenye mazungumzo hayo.

Akizungumza kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani, Membe alisema inashangaza kuona uchaguzi ulifutwa kwenye majimbo yote, badala ya yale yaliyokuwa na matatizo.

“Kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi. “Watanzania waelewe, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake. Yaani majimbo yote hakuna hata moja lililofanya vizuri? Hapa ndipo tunapata kigugumizi. Sasa tunakwenda wapi, tunafanya kitu gani?

“Ilitakiwa kuwe na ubaguzi; majimbo mawili, matatu, manne, matano, haya hayajafanya vizuri ndiyo uchaguzi urudiwe. Kaubaguzi kale kangewekwa, hiyo ingefanana na sura ya dunia ya haki.”

Waziri huyo mstaafu aliyehudumu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka tisa, pia haridhishwi na jinsi mgogoro huo wa kisiasa unavyotafutiwa ufumbuzi kutokana na kuwahusisha zaidi Dk Shein na Maalim Seif.

“Kama kuna mwanasiasa anadhani tatizo la Zanzibar litamalizwa na sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee, anafanya makosa makubwa,” alisema Membe.

“Umoja wetu na Zanzibar ni umoja wa kusaidiana wakati wa raha na matatizo. Hili ni tatizo ambalo linaweza kuhatarisha si tu usalama wa Zanzibar, bali pia Muungano wetu. Hatuwezi kukaa tu na kuangalia.

“Chama chetu na Serikali yetu lazima vishiriki kwa vitendo na kauli kumaliza mgogoro wa Zanzibar na ikiwezekana wahamie huko. Hili tatizo ni kubwa.”

Membe alisema katika mgogoro huo, Watanzania wa Bara wana haki ya kujua kinachozungumzwa ili kushauri kwa lengo la kudumisha Muungano.

“Kuwaacha viongozi wawili tu wanakutana kila siku kwa muda wa mwezi mzima au miezi miwili na hujui kinachoendelea si sahihi. Huwezi kujua kinachoendelea,” alisema.

“Kuna mambo makubwa yanayoendelea, lakini hawataki tu kutuambia. Msije mkadanganyika kwamba wanakutana mle, wanakunywa chai, wanaondoka halafu mnasema hakuna kinachoendelea.”

Wakati ZEC imetangaza Machi 20 kuwa tarehe ya kurudia uchaguzi, CUF imekuwa imeshasema kuurudia si suluhisho na haitakubalika, badala yake ameitaka Tume kutangaza mshindi.

Membe, ambaye alikuwa mmoja wa makada 38 wa CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya kugombea urais lakini akaishia kwenye tano bora, alikuwa pia na maoni yake kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi.

“Lazima uangaliwe kwa mapana, tusiangalie kama turudie uchaguzi au tusirudie. Tusifikiri viongozi wa Zanzibar wakikutana wanaulizana swali hilo tu kwamba ‘turudie uchaguzi au tusirudie’. Hapana,” alisema Membe aliyeshiriki kutatua migogoro mbalimbali barani Afrika.

“Wenzako swali hilo ni dogo sana. Huenda wako kwenye swali kubwa. Wanaweza kuuliza swali kama ‘hivi tatizo la Zanzibar ni kitu hiki au kuna tatizo kubwa zaidi ya hapa’. Hivi mnaweza kukaa saa tatu au nne mkaulizana tu kwamba, ‘turudie, tusirudie, turudie tusirudie?’”

Waliohama CCM wananitia kichefuchefu

Membe pia alizungumzia kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM walioamua kutimkia upinzani wakati wa harakati za Uchaguzi Mkuu, akisema wanamchefua.

Akijibu swali lililotaka kujua anavyowazungumzia na kujisikia kuhusu watu hao, Membe alisema: “Nikionana nao najisikia kichefuchefu. Tena ukiwaona waambie, chama kichukue hatua kwa wasaliti.”

Alisema zipo taarifa za baadhi ya waliohama CCM kutaka kurejea, akashauri kisiwapokee tena.

“Nasikia wanataka kurudi, wasipokewe, hawa wasirudi,” alisema Membe ambaye alikuwa akichukuliwa kuwa mpinzani mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenye kinyang’anyiro cha urais ndani ya CCM.

Lowassa alihamia upinzani baada ya kuenguliwa na CCM na akapitishwa na Chadema kugombea urais.


Chanzo: Mwananchi
Huyo mzee sijui kaibukia wapi naona kaanza kuongea
 
Membe amejidhalilisha sana.
Anafikiri ukiwa waziri wa mambo ya Nje ni lazima usafir na kupishana angani kama kwenu " kunawaka moto"!!
Walipewa kuiendesha hii nchi , mambo ikawa madudu matupu.
Mbona hatujawahi kumsikia akimshauri Jakaya Kikwete?
 
Tatizo chama chako hakipendi kukosolewa namkumbuka sana Marehemu Horace Kolimba wakati akiwa katibu Mkuu wa CCM ,aliwakosoa akawaambia Chama kimepoteza Dira, kilichofatia hapo Mwenyezi Mungu ndio anajua, RIP kolimba.
 
Nadhani Memnbe yuko sahihi kuwa chanzo cha tatizo lililopo Zanzibar kwa sasa ni makosa yaliyo tokana na Jecha kufuta uchaguzi kwa hofu za kutokujiamini. Yawezekana pia nikutokana na hofu iliyomkumba wakati matokeo yanaendelea kuhesabiwa akaona bora afunike kombe mwana haramu apite. Kwa akili yake nyepesi iliyokumbwa na mashinikizo toka pande zote hakuona kwa haraka athari zinazoweza kutokana na kufutwa ka uchaguzu bila kufuata kanuni. Je kama fujo zingetokea na kusababisha maisha ya watu kupotea nani angelaumiwa kwa hilo? Ni Jecha au chama chake ambacho hakikutaka kushindwa uchaguzi Zanziba? Membe kama mwana diplomasia naamini anaijua Zanzibar vizuri sana, hivyo mawazo yake tuyheshimu jpo na sisi tunaweza tukawa tunaijua Zanzibar kidogo pia mawazo yetu yheshimiwe.
 
Mbona yeye ali support uhalifu unaofanywa na Nkurunzinza? Au anadhani hatufahamu? Nadhani hii ni mikakati ya kurudi kwenye ramani ya siasa TZ, maana alishapotea
Uko sahihi sana mkuu anatafuta kick huyu
 
Darasa la kutoka kwako? Labda ukawape wabunge wa ccm ambao kwa akili zao matope wanaweza kumchagua Martha Mlata kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na madini katika karne hii.
Nasisitiza wewe ni mzigo na sasa inaonyesha umeanza kutambua
Mpwa Mlata anasimamia gesi na mafuta?
 
Jecha ni janga, tume za zanzibar janga, kama sikosei mwaka 2000,zanzibar uchaguzi ulikuwa na matatizo kama haya, lakini haukufutwa uchaguzi wote bali walifuta majimbo yaliyokuwa na matatizo tu, iweje leo wafute uchaguzi wa majimbo yote? , pia kabla hajafuta uchaguzi kwa nini asiitishe kikao cha ZEC wakajadiliana kuhusu hali ya hewa? au hata angeita basi viongozi wa vyama vya upinzani wakajadili kabla hajafuta uchaguzi, tatizo la tume zetu sio huru, zinaongozwa kwa matakwa ya pande moja, hili ni tatizo. Sasa jecha atueleze kasoro zilizopelekea uchaguzi ukafutwa, pia aeleze kasoro hizo wamejiandaa vipi kukabiliana nazo? kuna hatihati ya matatizo yale yale kujirudia tena kwenye uchaguzi ujao, sasa tutakuwa tunafanya nini, haoni kuwa ni upotevu wa muda, pesa na usumbufu kwa wananchi? tunaimba maendeleo lakini kwa hali hii nchi yetu ni ngumu sana kufikia malengo yake, maendeleo lazima yaendane na strong institutions ambazo zitatoa maamuzi pasipo kuingiliwa na serikali au vyama.
 
Back
Top Bottom