Membe apinga kufutwa uchaguzi wote Zanzibar

Hongera membe kwa kuwafungua macho wana CCM.
Hili suala litakimaliza hiki chama cha kiharamia.
 
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar akisema dunia inashangaa, na akaitaka CCM na Serikali isiwaachie watu wawili tu kutafuta njia za kutatua mgogoro huo.

Membe anakuwa mwanasiasa wa kwanza mwandamizi kutoka chama tawala kuonyesha waziwazi kutoridhishwa na uamuzi wa kufuta uchaguzi huo wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani ambao ulifanyika sambamba na uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, wabunge na madiwani wa Bara na Visiwani.

“Kinachoishangaza dunia si kuahirisha uchaguzi, bali ni kufuta matokeo ya majimbo yote,” alisema mwanadiplomasia huyo katika mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili mapema wiki hii.

Uchaguzi wa viongozi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 sambamba na Uchaguzi Mkuu, ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28 kwa maelezo kuwa sheria na taratibu zilikiukwa na akaahidi kuitisha uchaguzi mwingine baada ya siku 90 zinazomalizika wiki ijayo.

Chama kikuu cha upinzani visiwani, CUF, ambacho kilimsimamisha Maalim Seif Sharif Hamad kugombea urais, kinapinga uamuzi huo kikisema si mwenyekiti wa tume wala ZEC wenye mamlaka ya kufuta matokeo na kutaka mshindi atangazwe ili chama hicho kwa kushirikiana na CCM vikutane kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Katika kujaribu kutatua mgogoro huo, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Maalim Seif wameshafanya vikao tisa Ikulu Zanzibar pamoja na marais wa zamani wa visiwa hivyo, Dk Amani Karume, Dk Salmin Amour na Ali Hassan Mwinyi, bila ya mafanikio na tayari katibu huyo mkuu wa CUF ameshatangaza kujitoa kwenye mazungumzo hayo.

Akizungumza kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani, Membe alisema inashangaza kuona uchaguzi ulifutwa kwenye majimbo yote, badala ya yale yaliyokuwa na matatizo.

“Kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi. “Watanzania waelewe, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake. Yaani majimbo yote hakuna hata moja lililofanya vizuri? Hapa ndipo tunapata kigugumizi. Sasa tunakwenda wapi, tunafanya kitu gani?

“Ilitakiwa kuwe na ubaguzi; majimbo mawili, matatu, manne, matano, haya hayajafanya vizuri ndiyo uchaguzi urudiwe. Kaubaguzi kale kangewekwa, hiyo ingefanana na sura ya dunia ya haki.”

Waziri huyo mstaafu aliyehudumu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka tisa, pia haridhishwi na jinsi mgogoro huo wa kisiasa unavyotafutiwa ufumbuzi kutokana na kuwahusisha zaidi Dk Shein na Maalim Seif.

“Kama kuna mwanasiasa anadhani tatizo la Zanzibar litamalizwa na sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee, anafanya makosa makubwa,” alisema Membe.

“Umoja wetu na Zanzibar ni umoja wa kusaidiana wakati wa raha na matatizo. Hili ni tatizo ambalo linaweza kuhatarisha si tu usalama wa Zanzibar, bali pia Muungano wetu. Hatuwezi kukaa tu na kuangalia.

“Chama chetu na Serikali yetu lazima vishiriki kwa vitendo na kauli kumaliza mgogoro wa Zanzibar na ikiwezekana wahamie huko. Hili tatizo ni kubwa.”

Membe alisema katika mgogoro huo, Watanzania wa Bara wana haki ya kujua kinachozungumzwa ili kushauri kwa lengo la kudumisha Muungano.

“Kuwaacha viongozi wawili tu wanakutana kila siku kwa muda wa mwezi mzima au miezi miwili na hujui kinachoendelea si sahihi. Huwezi kujua kinachoendelea,” alisema.

“Kuna mambo makubwa yanayoendelea, lakini hawataki tu kutuambia. Msije mkadanganyika kwamba wanakutana mle, wanakunywa chai, wanaondoka halafu mnasema hakuna kinachoendelea.”

Wakati ZEC imetangaza Machi 20 kuwa tarehe ya kurudia uchaguzi, CUF imekuwa imeshasema kuurudia si suluhisho na haitakubalika, badala yake ameitaka Tume kutangaza mshindi.

Membe, ambaye alikuwa mmoja wa makada 38 wa CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya kugombea urais lakini akaishia kwenye tano bora, alikuwa pia na maoni yake kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi.

“Lazima uangaliwe kwa mapana, tusiangalie kama turudie uchaguzi au tusirudie. Tusifikiri viongozi wa Zanzibar wakikutana wanaulizana swali hilo tu kwamba ‘turudie uchaguzi au tusirudie’. Hapana,” alisema Membe aliyeshiriki kutatua migogoro mbalimbali barani Afrika.

“Wenzako swali hilo ni dogo sana. Huenda wako kwenye swali kubwa. Wanaweza kuuliza swali kama ‘hivi tatizo la Zanzibar ni kitu hiki au kuna tatizo kubwa zaidi ya hapa’. Hivi mnaweza kukaa saa tatu au nne mkaulizana tu kwamba, ‘turudie, tusirudie, turudie tusirudie?’”

Waliohama CCM wananitia kichefuchefu

Membe pia alizungumzia kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM walioamua kutimkia upinzani wakati wa harakati za Uchaguzi Mkuu, akisema wanamchefua.

Akijibu swali lililotaka kujua anavyowazungumzia na kujisikia kuhusu watu hao, Membe alisema: “Nikionana nao najisikia kichefuchefu. Tena ukiwaona waambie, chama kichukue hatua kwa wasaliti.”

Alisema zipo taarifa za baadhi ya waliohama CCM kutaka kurejea, akashauri kisiwapokee tena.

“Nasikia wanataka kurudi, wasipokewe, hawa wasirudi,” alisema Membe ambaye alikuwa akichukuliwa kuwa mpinzani mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenye kinyang’anyiro cha urais ndani ya CCM.

Lowassa alihamia upinzani baada ya kuenguliwa na CCM na akapitishwa na Chadema kugombea urais.

Chanzo: Mwananchi
PESA a gadaff zmemuishia,muacheni aisome number
 
amezungumza ukweri..... maoni yake ni mazuri ila hayana msaada kwa sasa
 
Toka jana siamini mambo yanayo andikwa kuhusu membe kama kweli yametamkwa na Membe!
Watu wanatakiwa kujiuliza kama kweli haya yanasemwa na Membe .muda wote alikuwa wapi?
kweli kachelewa ilibidi atoe maoni yake mwanzo mwanzo angeeleweka ingawa aliyoyasema ni kweli tena kweli tupu.
 
Naona ameamua kujilipua baada ya kuona kuwa hakuna dalili za kupata cheo. Alitegemea pengine angeteuliwa kuwa mbunge then apate wizara. Kaona kimya. Sasa ameamua liwalo na liwe. Kweli CCM hawakukosea kumkata
ingawa hampendi alichosema lakini kasema kweli tena kweli kabisa.
 
Anchosema membe hakijaeleweka kashindwa kuwashauri wenzie ndani huko kaja kutuambia nini huku, hatudanganyiki
 
Membe is extremely shallow.
Hoja zake nyingi hazina ukweli, naona ana bifu na mzee Pombe. Mara ukubwa wa serikali, ukweli kama angeweza kuchambua angeona tofauti kati ya waziri mmoja na makatibu wa kuu 3 na Mawaziri 3 na makati wakuu 3, Kwake yeye ukubwa ni huo huo.
Membe ni replica ya Kikwete, inawezekana wana genetic resemblence kama wengine wanavyo dai humu
Acha kukariri bwana mdogo Membe ana HOJA unachotakiwa..
Kuuliza kwanini aseme sasa...
 
1. Sadifa yuko wapi ili amjibu Membe?

2. Kama Zanzibar ni nchi likuwaje wale mashehe wazenji waliotuhumiwa kufanya makosa kwao Zanzibar wakaletwa kuhifadhiwa Tanganyika?
 
Sio kila mkosoaji ni mpinzani Membe anaitakia mema serikali ya magufuli,mchukue Ushauri wake ni viwavi mwenzenu Huyo wa lumumba.
huyu ndugu yake mkwere hana lolote baada ya jina lake kugoma kutoka mfukoni kwa mkwere na kurudi nalo msoga,tangu awali nilimuona hafai na ni adui mkubwa wa maendeleo ya watanzania maana anapenda starehe kama sungura,alishindwa kumshauri kaka yake eti leo anakuja na vistory vya kipuuzi.yeye atulie atumbuliwe zile hela za libya hazimuachi pema,na zile za manji zilizokamatwa dodoma.anatia kichefuchefu huyu panya buku
 
Naona ameamua kujilipua baada ya kuona kuwa hakuna dalili za kupata cheo. Alitegemea pengine angeteuliwa kuwa mbunge then apate wizara. Kaona kimya. Sasa ameamua liwalo na liwe. Kweli CCM hawakukosea kumkata

Lakini aliyosema si ni kweli tupu?
 
Ni kweli huyu bwana kaamua kujilipua baada ya kuona JPM hajamwona kabisa kwenye wadhifa wowote labda ukuu wa mikoa baadaye.
Ninaonavyo mimi kuna dalili za CCCCMMM b kuibuka hapa.

Anataka kutafuta support ya wale ambao kwa sababu fulani fulani hawampend JPM.
Hapa nina maana zaidi mafisadi na matajiri ambao walikuwa wanajineemesha kila siku.Na watamsumbua sana huyu bwana. Cha msing JPM akaze uzi na wakimtema atabebwa na vyama vingine na kuwa mgombea wao baada ya hii ngwe.

Sidhani ni sahihi kwa mtu kama yeye kama hakubaliani na raisi akatumie vyombo vya habari kutoa ya moyoni.Vikao vya chama viko wapi?
M/Kiti bado yupo na ninasikia ni swahiba wake. Kwanini asitumie chama kuongea na ikishindikana atumie media????

Hapo kimenuka
 
Membe kuwa mkweli unalo jambo. Siku chache za zilizopita ulilianzisha la kusafiri nje ya nchi. Ulipoona hukusomeka umezua la Uchaguzi wa Zanzibar. Mhe kila Rais ana style yake ya kutawala. Hii ni style ya Magufuli mwache atatue mgogoro wa Zanzibar kwa namna yake na atawale kwa utaratibu wake mradi havunji sheria.
Suburi 2020 ugombee upate hiyo nafasi halafu utuoneshe mbinu zako. Kwa sasa kuwa mpole vinginevyo vuka mpaka ili ukisimamie vizuri hicho unachotaka kukisema. Kwa sasa huwezi unachokisema sicho unachokiishi maana huwezi kutoboa mtumbwi unaosafiria
 
Membe kwa sasa sio heavy weight katika chama cha CCM wala serikali.Bora ajinyamazie kimya ale mafao yake,lakini akiendeleza kelele za mfa maji yatampeleka kweli.
kwani akiongea mtamfanya nini? Hayo mafao anayokula Si ni haki yake!? Au analipwa na ccm?
 
Membe anaanza kujifanya Baba Mdogo wa Taifa
 
Kuna mwana zuoni mmoja alishawahi kusema. Ukiona Taifa watu wake wanakubaliana kwa kila jambo basi taifa hilo ni la watu wapumbavu. Tanzania si wapumbavu. Membe is right
 
Back
Top Bottom