Membe apinga kufutwa uchaguzi wote Zanzibar

Walizoea kuishi kwenye siasa hawana njia nyingine acha waisome lakini wakizidi kupiga kelele inabidi kuwatumbua maana nao ni majipu sasa.
kwa hiyo kila atakayeongea msichopenda kusikia anakuwa jipu kweli nyie ni wapumbavu. Hivi ni nani atakusifia wewe kwa kila kitu. Inaelekea hata jamaa akimtaka mkeo utaridhia tu.
 
Kila Kitu KINAJULIKANA Kuwa Anatumika Kwa MASLAHI Ya Mr. NIMESTAAFU Majuzi Tu Ili Kumdhoofisha Kabla Ya Msubi Kukabidhiwa Chama Rasmi. Mr. NIMESTAAFU Majuzi Tu Ana Hasira Na Chuki Ya Moyoni Hasa Baada Ya Mwanamume Wa KISUBI Kuipangua MIRADI Na MIRIJA Yake Mingi Na Ndiyo Maana Kama Upo Makini Mr. NIMESTAAFU Majuzi Tu Kila Kukicha ANAKONDA. Mbinu Inayotumika Ni Yeye Kujifanya Yupo KIMYA Kwa MSUBI Lakini Ramani Nzima Ya Vita Kamwachia Chinga Boy AMALIZE Huku Kampuni Hiyo Ya Tabata Relini Ikiingizwa Ktk Mpango MAALUM Kwa MASLAHI Ya Yule GABACHORI Mnafiki Ambaye CCM Yupo Na UKAWA Alikuwepo ( Lakini Hapo Hapo Mr. NIMESTAAFU Majuzi Tu Amesahau Kuwa MSUBI Ni MAFIA VILE VILE TENA ALIYETUKUKA Ambaye Anaweza Kukuingiza Choo Cha Kike Bila Kujua ). Ila Chinga Boy AMESAHAU Kuwa Ofisi Uliyokuwepo Ukitoka Tu Mambo Nayo HUBADILISHWA Mara Moja ( Especially IDARA NYETI ) Hivyo System Ya Sasa HAIJUI Na HATOKUJA KUIJUA Na Sana Sana Ni Vyema Tu ANGEKAA Kimya Na Mama Dorcas Wake Wale Pesa Za Mwanamume Wa Libya Huku WAKITUBU DHAMBI Ya WALIBYA Kufiwa Na Balozi Wao Hapa Tanzania Mwaka Jana. Kwa Mchana Huu Naomba Niishie Hapa Tu Japo Hatoacha Kukumbukwa Kuwa Na Yeye Alishawahi Kuwa Mmoja Wa MAAFISA WANAFIKI WALIOWAHI KUTOKEA Pale " Eagle Wing House " Oysterbay.
Naona uko mbali sana na system ila tatizo lako kujifanya mjuaji na kibaya zaidi kazi yako unaifanyia kwenye social media mbona muoga?
 
Hiki kimfumo cha chama chao kinawabana mpk wanashindwa kupumua,sasa wanapoachiwa ni sawa kipofu kufumbuliwa macho.
 
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar akisema dunia inashangaa, na akaitaka CCM na Serikali isiwaachie watu wawili tu kutafuta njia za kutatua mgogoro huo.

Membe anakuwa mwanasiasa wa kwanza mwandamizi kutoka chama tawala kuonyesha waziwazi kutoridhishwa na uamuzi wa kufuta uchaguzi huo wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani ambao ulifanyika sambamba na uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, wabunge na madiwani wa Bara na Visiwani.

“Kinachoishangaza dunia si kuahirisha uchaguzi, bali ni kufuta matokeo ya majimbo yote,” alisema mwanadiplomasia huyo katika mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili mapema wiki hii.

Uchaguzi wa viongozi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 sambamba na Uchaguzi Mkuu, ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28 kwa maelezo kuwa sheria na taratibu zilikiukwa na akaahidi kuitisha uchaguzi mwingine baada ya siku 90 zinazomalizika wiki ijayo.

Chama kikuu cha upinzani visiwani, CUF, ambacho kilimsimamisha Maalim Seif Sharif Hamad kugombea urais, kinapinga uamuzi huo kikisema si mwenyekiti wa tume wala ZEC wenye mamlaka ya kufuta matokeo na kutaka mshindi atangazwe ili chama hicho kwa kushirikiana na CCM vikutane kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Katika kujaribu kutatua mgogoro huo, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Maalim Seif wameshafanya vikao tisa Ikulu Zanzibar pamoja na marais wa zamani wa visiwa hivyo, Dk Amani Karume, Dk Salmin Amour na Ali Hassan Mwinyi, bila ya mafanikio na tayari katibu huyo mkuu wa CUF ameshatangaza kujitoa kwenye mazungumzo hayo.

Akizungumza kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani, Membe alisema inashangaza kuona uchaguzi ulifutwa kwenye majimbo yote, badala ya yale yaliyokuwa na matatizo.

“Kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi. “Watanzania waelewe, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake. Yaani majimbo yote hakuna hata moja lililofanya vizuri? Hapa ndipo tunapata kigugumizi. Sasa tunakwenda wapi, tunafanya kitu gani?

“Ilitakiwa kuwe na ubaguzi; majimbo mawili, matatu, manne, matano, haya hayajafanya vizuri ndiyo uchaguzi urudiwe. Kaubaguzi kale kangewekwa, hiyo ingefanana na sura ya dunia ya haki.”

Waziri huyo mstaafu aliyehudumu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka tisa, pia haridhishwi na jinsi mgogoro huo wa kisiasa unavyotafutiwa ufumbuzi kutokana na kuwahusisha zaidi Dk Shein na Maalim Seif.

“Kama kuna mwanasiasa anadhani tatizo la Zanzibar litamalizwa na sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee, anafanya makosa makubwa,” alisema Membe.

“Umoja wetu na Zanzibar ni umoja wa kusaidiana wakati wa raha na matatizo. Hili ni tatizo ambalo linaweza kuhatarisha si tu usalama wa Zanzibar, bali pia Muungano wetu. Hatuwezi kukaa tu na kuangalia.

“Chama chetu na Serikali yetu lazima vishiriki kwa vitendo na kauli kumaliza mgogoro wa Zanzibar na ikiwezekana wahamie huko. Hili tatizo ni kubwa.”

Membe alisema katika mgogoro huo, Watanzania wa Bara wana haki ya kujua kinachozungumzwa ili kushauri kwa lengo la kudumisha Muungano.

“Kuwaacha viongozi wawili tu wanakutana kila siku kwa muda wa mwezi mzima au miezi miwili na hujui kinachoendelea si sahihi. Huwezi kujua kinachoendelea,” alisema.

“Kuna mambo makubwa yanayoendelea, lakini hawataki tu kutuambia. Msije mkadanganyika kwamba wanakutana mle, wanakunywa chai, wanaondoka halafu mnasema hakuna kinachoendelea.”

Wakati ZEC imetangaza Machi 20 kuwa tarehe ya kurudia uchaguzi, CUF imekuwa imeshasema kuurudia si suluhisho na haitakubalika, badala yake ameitaka Tume kutangaza mshindi.

Membe, ambaye alikuwa mmoja wa makada 38 wa CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya kugombea urais lakini akaishia kwenye tano bora, alikuwa pia na maoni yake kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi.

“Lazima uangaliwe kwa mapana, tusiangalie kama turudie uchaguzi au tusirudie. Tusifikiri viongozi wa Zanzibar wakikutana wanaulizana swali hilo tu kwamba ‘turudie uchaguzi au tusirudie’. Hapana,” alisema Membe aliyeshiriki kutatua migogoro mbalimbali barani Afrika.

“Wenzako swali hilo ni dogo sana. Huenda wako kwenye swali kubwa. Wanaweza kuuliza swali kama ‘hivi tatizo la Zanzibar ni kitu hiki au kuna tatizo kubwa zaidi ya hapa’. Hivi mnaweza kukaa saa tatu au nne mkaulizana tu kwamba, ‘turudie, tusirudie, turudie tusirudie?’”

Waliohama CCM wananitia kichefuchefu

Membe pia alizungumzia kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM walioamua kutimkia upinzani wakati wa harakati za Uchaguzi Mkuu, akisema wanamchefua.

Akijibu swali lililotaka kujua anavyowazungumzia na kujisikia kuhusu watu hao, Membe alisema: “Nikionana nao najisikia kichefuchefu. Tena ukiwaona waambie, chama kichukue hatua kwa wasaliti.”

Alisema zipo taarifa za baadhi ya waliohama CCM kutaka kurejea, akashauri kisiwapokee tena.

“Nasikia wanataka kurudi, wasipokewe, hawa wasirudi,” alisema Membe ambaye alikuwa akichukuliwa kuwa mpinzani mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenye kinyang’anyiro cha urais ndani ya CCM.

Lowassa alihamia upinzani baada ya kuenguliwa na CCM na akapitishwa na Chadema kugombea urais.

Chanzo: Mwananchi
tatito la hawa wanasiasa wetu ni MALAYA wa siasa kupindukia. Eti leo hii na membe anadai sio sawa akati yeye ni miongoni mwa wale waliosema ni sawa mwanzoni. Sasa sisi tuwaeleweje?
 
Ya ngoswe mwachie ngoswe kwani anajiona anaijua zanzibar kuliko wazanzibari wenyewe. Hebu apumzike asitake kupotosha watu. Simuungi mkono haya chembe
 
Naona ameamua kujilipua baada ya kuona kuwa hakuna dalili za kupata cheo. Alitegemea pengine angeteuliwa kuwa mbunge then apate wizara. Kaona kimya. Sasa ameamua liwalo na liwe. Kweli CCM hawakukosea kumkata
Kabla Dr MAGUFULI ajateua Mawaziri Membe alikua anatamba kuwa lazima awe Waziri wa mambo nje,hakuna MTU mahiri katika mahusiano ya nchi za nje kama yeye,hivyo lazima atateuliwa..JPM akamkata ndio amepaniki
 
Angetoa basi ushauri wake tangu uchaguzi ulipotangazwa kuwa utarudiwa.
Huenda alijua muafaka ungepatikana eidha wa kutangaza matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwaka jana, but cc wote hatujui kwann alinyamanza mda wote, tusubiri mda ukifika

Huyu amemiss ni headline ya magazine
 
Membeee tatizo lake ni UNDUMILA KUWILI... sasa kakosa kabisa nafasi yoyote ktk serikali ya Magufuli kaanza kuongea kwa KUONYESHA ANAJUA UKWELI... but akiwa ktk utawala ni B.WEGE kweli... hivi sasa anajionyesha mwenye busara ili watanzania wajue yuko makini, but UKIMPA UTAWALA HUYU, ANALEWA MADARAKA HANA ADABU KABISA..... muda wote asiseme hadi sasa hivi ALIKUWA WAPI.. wakati uchaguzi hadi umepangwa tar 20 March. kurudiwa... tena akae kimya.. kazi kumvuruga Magufuli tu... mm naomba Magufuli amwambie Membe..SHUT-UP... afunge domo lake kabisa..

Alishatoa maneno mabaya kweli kweli dunia ikashangaa....ETI U.S.A inatuonea wivu kuhusu CHINA... wakati anapewa taarifa ya uhakika Rais wa China alivyokuja Tz Meno ya Tembo tani kadhaa zilipakiwa na kuondoka nazo ktk ndege yake... alijibu bungeni Dodoma niliudhika sana kama mzalendo... basi tu, ana majibu mabovu sana ktk issues serious, eg Mauaji ya watanzania South Africa... alijibu kijinga jinga tu... watu wamekufa, akajibu kishenzi shenzi tu... yaani, mm ningekuwa Rais namchapa vibao vya nguvu vikali wazi wazi... damn..
 
Membe aache unafiki alikuwa wapi mda wote huo au ni baada Jecha kutangaza tarehe ya uchaguzi?

Nadhani yeye ndio dunia inamshangaa kwa Kuficha hela za Misikiti za Gadaff na kumundia zengwe aliyekuwa balozi wa Libya hapa nchini.

Cc: funza
 
Acheni ujinga....mpiga kura yule yule hawezi kupiga kura halali ya mbunge halafu ya rais ikawa haram! Kufuta kila kitu ndio sahihi. Membe hana jipya na wala hakuna dunia iliyoshangaa!
 
Huwez sema uchaguz kila sehem ulikua na mazingira sawa hadi wa Udiwani???
 
Naona jamaa kaona opportunity (wanasisiem ambao hawamsupport JPM directly hawana kichwa) so kuamua kuwa kichwa. Malengo ni 2020.
 
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar akisema dunia inashangaa, na akaitaka CCM na Serikali isiwaachie watu wawili tu kutafuta njia za kutatua mgogoro huo.

Membe anakuwa mwanasiasa wa kwanza mwandamizi kutoka chama tawala kuonyesha waziwazi kutoridhishwa na uamuzi wa kufuta uchaguzi huo wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani ambao ulifanyika sambamba na uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, wabunge na madiwani wa Bara na Visiwani.

“Kinachoishangaza dunia si kuahirisha uchaguzi, bali ni kufuta matokeo ya majimbo yote,” alisema mwanadiplomasia huyo katika mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili mapema wiki hii.

Uchaguzi wa viongozi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 sambamba na Uchaguzi Mkuu, ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28 kwa maelezo kuwa sheria na taratibu zilikiukwa na akaahidi kuitisha uchaguzi mwingine baada ya siku 90 zinazomalizika wiki ijayo.

Chama kikuu cha upinzani visiwani, CUF, ambacho kilimsimamisha Maalim Seif Sharif Hamad kugombea urais, kinapinga uamuzi huo kikisema si mwenyekiti wa tume wala ZEC wenye mamlaka ya kufuta matokeo na kutaka mshindi atangazwe ili chama hicho kwa kushirikiana na CCM vikutane kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Katika kujaribu kutatua mgogoro huo, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Maalim Seif wameshafanya vikao tisa Ikulu Zanzibar pamoja na marais wa zamani wa visiwa hivyo, Dk Amani Karume, Dk Salmin Amour na Ali Hassan Mwinyi, bila ya mafanikio na tayari katibu huyo mkuu wa CUF ameshatangaza kujitoa kwenye mazungumzo hayo.

Akizungumza kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani, Membe alisema inashangaza kuona uchaguzi ulifutwa kwenye majimbo yote, badala ya yale yaliyokuwa na matatizo.

“Kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi. “Watanzania waelewe, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake. Yaani majimbo yote hakuna hata moja lililofanya vizuri? Hapa ndipo tunapata kigugumizi. Sasa tunakwenda wapi, tunafanya kitu gani?

“Ilitakiwa kuwe na ubaguzi; majimbo mawili, matatu, manne, matano, haya hayajafanya vizuri ndiyo uchaguzi urudiwe. Kaubaguzi kale kangewekwa, hiyo ingefanana na sura ya dunia ya haki.”

Waziri huyo mstaafu aliyehudumu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka tisa, pia haridhishwi na jinsi mgogoro huo wa kisiasa unavyotafutiwa ufumbuzi kutokana na kuwahusisha zaidi Dk Shein na Maalim Seif.

“Kama kuna mwanasiasa anadhani tatizo la Zanzibar litamalizwa na sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee, anafanya makosa makubwa,” alisema Membe.

“Umoja wetu na Zanzibar ni umoja wa kusaidiana wakati wa raha na matatizo. Hili ni tatizo ambalo linaweza kuhatarisha si tu usalama wa Zanzibar, bali pia Muungano wetu. Hatuwezi kukaa tu na kuangalia.

“Chama chetu na Serikali yetu lazima vishiriki kwa vitendo na kauli kumaliza mgogoro wa Zanzibar na ikiwezekana wahamie huko. Hili tatizo ni kubwa.”

Membe alisema katika mgogoro huo, Watanzania wa Bara wana haki ya kujua kinachozungumzwa ili kushauri kwa lengo la kudumisha Muungano.

“Kuwaacha viongozi wawili tu wanakutana kila siku kwa muda wa mwezi mzima au miezi miwili na hujui kinachoendelea si sahihi. Huwezi kujua kinachoendelea,” alisema.

“Kuna mambo makubwa yanayoendelea, lakini hawataki tu kutuambia. Msije mkadanganyika kwamba wanakutana mle, wanakunywa chai, wanaondoka halafu mnasema hakuna kinachoendelea.”

Wakati ZEC imetangaza Machi 20 kuwa tarehe ya kurudia uchaguzi, CUF imekuwa imeshasema kuurudia si suluhisho na haitakubalika, badala yake ameitaka Tume kutangaza mshindi.

Membe, ambaye alikuwa mmoja wa makada 38 wa CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya kugombea urais lakini akaishia kwenye tano bora, alikuwa pia na maoni yake kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi.

“Lazima uangaliwe kwa mapana, tusiangalie kama turudie uchaguzi au tusirudie. Tusifikiri viongozi wa Zanzibar wakikutana wanaulizana swali hilo tu kwamba ‘turudie uchaguzi au tusirudie’. Hapana,” alisema Membe aliyeshiriki kutatua migogoro mbalimbali barani Afrika.

“Wenzako swali hilo ni dogo sana. Huenda wako kwenye swali kubwa. Wanaweza kuuliza swali kama ‘hivi tatizo la Zanzibar ni kitu hiki au kuna tatizo kubwa zaidi ya hapa’. Hivi mnaweza kukaa saa tatu au nne mkaulizana tu kwamba, ‘turudie, tusirudie, turudie tusirudie?’”

Waliohama CCM wananitia kichefuchefu

Membe pia alizungumzia kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM walioamua kutimkia upinzani wakati wa harakati za Uchaguzi Mkuu, akisema wanamchefua.

Akijibu swali lililotaka kujua anavyowazungumzia na kujisikia kuhusu watu hao, Membe alisema: “Nikionana nao najisikia kichefuchefu. Tena ukiwaona waambie, chama kichukue hatua kwa wasaliti.”

Alisema zipo taarifa za baadhi ya waliohama CCM kutaka kurejea, akashauri kisiwapokee tena.

“Nasikia wanataka kurudi, wasipokewe, hawa wasirudi,” alisema Membe ambaye alikuwa akichukuliwa kuwa mpinzani mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenye kinyang’anyiro cha urais ndani ya CCM.

Lowassa alihamia upinzani baada ya kuenguliwa na CCM na akapitishwa na Chadema kugombea urais.

Chanzo: Mwananchi
Lazima waufute wote kwasababu vile vituo ambavyo wamesema kumeibiwa kura na watu wamezidi(hadi hii leo wameshindwa kutaja vituo hivyo ni vipi) hata wakirejewa hivyo tu bado CCM watashindwa. Kwahiyo wakiifute wote watakuwa na uwezo wa kuiba kura, kuzuia wananchi wengi kupiga kura hasa wale wa CUF, kutopeleka balot paper chache katika majimbo ya CUF na kuleta watu kutoka huku bara
 
Tatizo sio eti kuna ukiukwaji,tatizo ni matokeo yanampa ushindi nani? Na uchaguzi ukirudiwa baadhi ya maeneo yaweza isibadili matokeo ya jumla na mshindi kubaki huyuhuyu tunayemjua...
Membe anajua vizuri hili sasa izikauli za kutuzuga aziache.
Kuhusu kichefuchefu "ale malimao" kisemo cha Gwajima. Mimi nilidhani kichefuchefu kingetokana na kurudiwa shughuli nzima badala ya baadhi ya maeneo yenyeshida.
 
Back
Top Bottom