Membe apinga kufutwa uchaguzi wote Zanzibar

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970


Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar akisema dunia inashangaa, na akaitaka CCM na Serikali isiwaachie watu wawili tu kutafuta njia za kutatua mgogoro huo.

Membe anakuwa mwanasiasa wa kwanza mwandamizi kutoka chama tawala kuonyesha waziwazi kutoridhishwa na uamuzi wa kufuta uchaguzi huo wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani ambao ulifanyika sambamba na uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, wabunge na madiwani wa Bara na Visiwani.

“Kinachoishangaza dunia si kuahirisha uchaguzi, bali ni kufuta matokeo ya majimbo yote,” alisema mwanadiplomasia huyo katika mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili mapema wiki hii.

Uchaguzi wa viongozi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 sambamba na Uchaguzi Mkuu, ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28 kwa maelezo kuwa sheria na taratibu zilikiukwa na akaahidi kuitisha uchaguzi mwingine baada ya siku 90 zinazomalizika wiki ijayo.

Chama kikuu cha upinzani visiwani, CUF, ambacho kilimsimamisha Maalim Seif Sharif Hamad kugombea urais, kinapinga uamuzi huo kikisema si mwenyekiti wa tume wala ZEC wenye mamlaka ya kufuta matokeo na kutaka mshindi atangazwe ili chama hicho kwa kushirikiana na CCM vikutane kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Katika kujaribu kutatua mgogoro huo, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Maalim Seif wameshafanya vikao tisa Ikulu Zanzibar pamoja na marais wa zamani wa visiwa hivyo, Dk Amani Karume, Dk Salmin Amour na Ali Hassan Mwinyi, bila ya mafanikio na tayari katibu huyo mkuu wa CUF ameshatangaza kujitoa kwenye mazungumzo hayo.

Akizungumza kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani, Membe alisema inashangaza kuona uchaguzi ulifutwa kwenye majimbo yote, badala ya yale yaliyokuwa na matatizo.

“Kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi. “Watanzania waelewe, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake. Yaani majimbo yote hakuna hata moja lililofanya vizuri? Hapa ndipo tunapata kigugumizi. Sasa tunakwenda wapi, tunafanya kitu gani?

“Ilitakiwa kuwe na ubaguzi; majimbo mawili, matatu, manne, matano, haya hayajafanya vizuri ndiyo uchaguzi urudiwe. Kaubaguzi kale kangewekwa, hiyo ingefanana na sura ya dunia ya haki.”

Waziri huyo mstaafu aliyehudumu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka tisa, pia haridhishwi na jinsi mgogoro huo wa kisiasa unavyotafutiwa ufumbuzi kutokana na kuwahusisha zaidi Dk Shein na Maalim Seif.

“Kama kuna mwanasiasa anadhani tatizo la Zanzibar litamalizwa na sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee, anafanya makosa makubwa,” alisema Membe.

“Umoja wetu na Zanzibar ni umoja wa kusaidiana wakati wa raha na matatizo. Hili ni tatizo ambalo linaweza kuhatarisha si tu usalama wa Zanzibar, bali pia Muungano wetu. Hatuwezi kukaa tu na kuangalia.

“Chama chetu na Serikali yetu lazima vishiriki kwa vitendo na kauli kumaliza mgogoro wa Zanzibar na ikiwezekana wahamie huko. Hili tatizo ni kubwa.”

Membe alisema katika mgogoro huo, Watanzania wa Bara wana haki ya kujua kinachozungumzwa ili kushauri kwa lengo la kudumisha Muungano.

“Kuwaacha viongozi wawili tu wanakutana kila siku kwa muda wa mwezi mzima au miezi miwili na hujui kinachoendelea si sahihi. Huwezi kujua kinachoendelea,” alisema.

“Kuna mambo makubwa yanayoendelea, lakini hawataki tu kutuambia. Msije mkadanganyika kwamba wanakutana mle, wanakunywa chai, wanaondoka halafu mnasema hakuna kinachoendelea.”

Wakati ZEC imetangaza Machi 20 kuwa tarehe ya kurudia uchaguzi, CUF imekuwa imeshasema kuurudia si suluhisho na haitakubalika, badala yake ameitaka Tume kutangaza mshindi.

Membe, ambaye alikuwa mmoja wa makada 38 wa CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya kugombea urais lakini akaishia kwenye tano bora, alikuwa pia na maoni yake kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi.

“Lazima uangaliwe kwa mapana, tusiangalie kama turudie uchaguzi au tusirudie. Tusifikiri viongozi wa Zanzibar wakikutana wanaulizana swali hilo tu kwamba ‘turudie uchaguzi au tusirudie’. Hapana,” alisema Membe aliyeshiriki kutatua migogoro mbalimbali barani Afrika.

“Wenzako swali hilo ni dogo sana. Huenda wako kwenye swali kubwa. Wanaweza kuuliza swali kama ‘hivi tatizo la Zanzibar ni kitu hiki au kuna tatizo kubwa zaidi ya hapa’. Hivi mnaweza kukaa saa tatu au nne mkaulizana tu kwamba, ‘turudie, tusirudie, turudie tusirudie?’”

Waliohama CCM wananitia kichefuchefu

Membe pia alizungumzia kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM walioamua kutimkia upinzani wakati wa harakati za Uchaguzi Mkuu, akisema wanamchefua.

Akijibu swali lililotaka kujua anavyowazungumzia na kujisikia kuhusu watu hao, Membe alisema: “Nikionana nao najisikia kichefuchefu. Tena ukiwaona waambie, chama kichukue hatua kwa wasaliti.”

Alisema zipo taarifa za baadhi ya waliohama CCM kutaka kurejea, akashauri kisiwapokee tena.

“Nasikia wanataka kurudi, wasipokewe, hawa wasirudi,” alisema Membe ambaye alikuwa akichukuliwa kuwa mpinzani mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenye kinyang’anyiro cha urais ndani ya CCM.

Lowassa alihamia upinzani baada ya kuenguliwa na CCM na akapitishwa na Chadema kugombea urais.


Chanzo: Mwananchi
 

Attachments

  • Mwananchi.png
    Mwananchi.png
    79.1 KB · Views: 120
Though sijaliona hilo gazeti lakini mara chache chache huyu jamaa ana vi point
 
Huyu Membe hafahamu kama Zanzibar ni nchi yenye mipaka yake, Rais wake, Bunge lake, mahakama zake na Jeshi lake!

Inawezekana hafahamu kama Zanzibar wana katiba yao!

Hafahamu kama wazanzibari wenyewe wakiongozwa na jopo la Marais wastaafu wa nchi ya Zanzibar wameamua kujifungia kwenye chumba na wanaendelea na vikao!

Kwa hiyo anataka kutuambia kama yangefutwa baadhi ya majimbo asingeshangaa!

Hafahamu kama Maalim Seif alishinda Uchaguzi Mkuu wa 2010? Hakumsikia Mzee Hassan Nassor Moyo?

Ni nini kinamfanya ashangae kwa sasa kufutwa kwa matokeo yote?

Membe nadhani anasumbuliwa na weweseko la maisha nje ya siasa wakati umri bado unaruhusu. Tatizo aliaminishwa sana kama atakuwa mgombea Urais mpaka akaamua kuliachia Jimbo la Mtama.

Rais Magufuli ameamua kutomteua kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje. He's already casted aside and now, he's bitter!

Maalim Seif alitamaka haya

Tuesday, August 5, 2008 ·
“Sasa, mimi hapa natamka kwa mdomo mpana. Natamka asikie Pinda huko aliko, kwamba Zanzibar ilikuwa ni nchi, Zanzibar imekuwa ni nchi, Zanzibar ni nchi mpaka sasa hivi na Zanzibar itaendelea kuwa nchi mpaka yaumul-qiyama. Hapa mimi nimesimama kwenye jukwaa lililo kwenye ardhi ya nchi ya Zanzibar. Sasa kama kuna watu wanaona baya kwa hilo, kama wana uhasidi kwa hilo, watafisidika wao. Zanzibar itakuwepo milele na milele. Walikuwepo maadui wengi tu wa Zanzibar, lakini leo wako wapi? Wamepita. Na kila mbaya wa Zanzibar atakwenda na maji”
Hotuba ya tarehe 16 Julai, 2008 ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, kujibu kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwamba Zanzibar si Nchi.
Maelezo zaidi yako hapa;
na hapa,
 
Membe ametoa mawazo yake kama mtu binafsi na kusema kweli huo ndio ukweli.Tatizo lenu watu wa CCM mnatanguliza maslahi ya tumbo na ya chama mbele na hii itakuja kutugharimu sana.
Mbona yeye ali support uhalifu unaofanywa na Nkurunzinza? Au anadhani hatufahamu? Nadhani hii ni mikakati ya kurudi kwenye ramani ya siasa TZ, maana alishapotea
 
Huyu Membe hafahamu kama Zanzibar ni nchi yenye mipaka yake, Rais wake, Bunge lake, mahakama zake na Jeshi lake!

Inawezekana hafahamu kama Zanzibar wana katiba yao!

Hafahamu kama wazanzibari wenyewe wakiongozwa na jopo la Marais wastaafu wa nchi ya Zanzibar wanaendelea na vikao!


Maelezo zaidi yako hapa;
Zanzibar haina jeshi lake mkuu naomba tukuweke sawa jeshi n moja tu jwtz je niambie zanzibar wana jeshi lake lipi
 
Zanzibar haina jeshi lake mkuu naomba tukuweke sawa jeshi n moja tu jwtz je niambie zanzibar wana jeshi lake lipi
Kwa maelezo zaidi, Pitia hii thread;
AMIRI JESHI MKUU WA VIKOSI VYA SMZ ZANZIBAR AWATUNUKU VYEO MAAFISA WA JESHI HILO ZANZIBAR.

Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi.Dkt Ali Mohammed Shein amewavalisha vyeo maafisa wa KMKM,katika sherehe za ufungaji wa mafunzo maalum ya maafisa 97 (special Duty)mkupuo wa saba (7) katika kambi ya KMKm Kibweni wilaya ya magharibi unguja leo.
 
KAMA MUNASEMA TUNA KILA KITU CHETU ZNZ
TUNA KATIBA YETU NA SHERIA ZETU

KWANINI MUMEWACHUKUA MASHEHE WETU WA UAMSHO
KAMA HAYAWAHUSU WAACHIENI HARAKA MASHEHE WETU MUFANYA UJANJA UJANJA TU

MBONA MUMEWAKAMATA TENA HAMUWATENDEI HAKI

SASA MUMEWASHIKA KWA SHERIA GANI NA YA ZNZ SIO YENU
 
Ndio kusema Kuna baadhi ya wana CCM akili imeanza kuwarudi,au wanaongea kiunafiki maana kabla hawajatangaza kurudiwa uchaguzi walikuwa kimya,kama vile kulikuwa hakuna jambo lililokuwa linaendelea kule Zanzibar.
Hamna akili huko CCM zaidi ya unafiki
 
Back
Top Bottom