MgonjwaUkimwi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2006
- 1,336
- 875
Hivi Membe anavyotuambia kwamba aligombea ubunge baada ya kusikia minongonezo hizo ni kauli za kutoa kiongozi mkubwa serikalini kama yeye? Tanzania bana ni zaidi ya uijuavyo. Hizo whisper ultras anazosema Membe kama zinamsaidia yeye hilo ni juu yake na maluweluwe yake yanayoendelea kichwani mwake. Lakini aliita waandishi wa habari bila aibu akasema hivo, dah. Anyway ni mwanaccm na hicho ndo chama kinachoongoza serikali. Mungu tunusuru hata kabla ya 2015.
Duh, kumbe wala hujui kwanini aliita waandishi wa habari na bado unanguvu ya ku draw conclusion ya kwanini aliita waandishi! Unanikumbusha mtoto wa rafiki yangu moja, siku moja rafiki yangu akamwambia mtoto wake "vaa vizuri na ingia kwenye gari", mtoto akasema "sawa baba". Akaenda kuvaa vizuri na kurudi nakuingia kwenye gari, wakiwa wanatoka getini mtoto akamuuliza babake "hivi baba tunakwenda wapi?" Babake akasema "eboh! sasa wewe ulifikiaje hatua ya kuvaa, kuingia kwenye gari na kufunga mkanda bila kujuwa unakwenda wapi?"