Membe amkosoa Magufuli

Membe amkosoa Magufuli

Daah Membe bhna Siku ile mh. Rais aliposema safari zote za nje kwa watumishi wa Umma lazima ziwe na kibali kutoka kwa Rais au katibu mkuu kiongozi Membe alisema hiv nanukuu "Afadhali mh Rais ameliona la safari za nje kwani tulikuwa tunapishana angani utafikir nyumbani kuna vita" leo anaanza kuzitetea safari za nje tena mpaka za mstaafu.
Ninachokiona hapa ni kuwa kwa kuwa ameona mstaafu amepewa shavu la uchancellor UDSM na yeye anafikir Pombe ataanzisha ubalozi wa Uturuki ili apewe yeye kwani ameshagundua Rais kwa sasa hiv atateua wabunge.
 
Unaweza kuwa na Bifu na RAIS wa nchi!? Tena nchi unayoishi!? Tuwe makini msijisahau kwamba huyo jamaa huwa hajiulizi mara mbili. Membe angetulia tu huko alipo kwa sasa. Sidhani Kama ametumia busara kutoa hayo maneno dhidi ya RAIS.

Huyo jamaa amenishangaza sana.....kwani angeamua kumfuata JPM faragha ikulu na kumshauri, angepoteza kitu gani? Haya ndiyo yale yale ya Maximo alipokuwa anakosolewa hadharani na Mziray........alishangaa sana Tanzania, nakusema ilipaswa ashauriwe faragha maana milango ya kumwona yeye ilikuwa wazi!
 
Sasa nimeamini kuwa watakaomkwamisha Magufuli ni virusi ndani ya CCM...... Kwa hili nafikiri Membe katumwa na yule jamaa ili amchane Magufuli.

=====================
Katibu Mkuu Ikulu, Ombeni Sefue, tunaomba umjibu Membe kwa facts and figures. Kukaa kimya itaonyesha ni kweli na hii itashusha heshima ya Rais kuwa anafanya mambo bila kujua matokeo ya hatua anazochukua. Ombeni Sefue uwanja ni wako.
 
Ndio maana tulikuwa hatutaki Membe, kwa sababu mawazo yake hayana tofauti na Kikwete.

Ahamie UKAWA tu maana hamna namna nyingine sasa.
 
Acha wafu wazikane wenyewe
NADHANI HAJATUMWA NA MTU WALA NINI, ILA NI MAMBO TU YA KUAMUA BILA KUPEPESA MACHO NA KUSEMA YA MOYONI BAADA YA MAMBO KWENDA MRAMA, IA SJUI YTAMSHAWISHI jpm AU NDO ATAONGEZA MISIMAMO YAKE!!! MAANA NAYE NDO WALEWALE WASIOAMBILIKA HADI GARI LIKWAME TOPENI, JAPO HAWATASEMA LIMEKWAMA ILA WATATOA TU SABABU HATA KAMA NI ZA KITOTO.
 
Majipu unayajua wewe au unayaskia...Membe ana point hapo afu jamaa ni genius sana anajua anachokisimamia anaona jamaa anaenda mrama lazima aseme.Ni heri huyu bwana angekua rais kuliko huyu tulie nae sasa.
Mlitaka Membe awe Rais muicheke ujinga CCM?
Imekula kwenu.
 
Wao walikuwa na baraza kubwa mbona Bungeni waliaibika kilaleo na kulazimisha hoja?
Aliruhusu misururu ya watu kuongozana na Rais miaka kumi, jambo gani la kielelezo tulilofaidi zaidi ya picha za kung'aa za ulaya na hadithi?

Kwa mahusiano aliyojenga huko nje tumefaidi viwanda gani?

Alisaidia vipi nchi kujua utendaji na uhalali wa kampuni toka nje?

Zipo nchi zenye wizara chache ila watendaji wakutosha mfano Ghana, Algeria kwanini tujifunzie Namibia?

Ikileta upungufu tutashindwa kuongeza?

Sijaona hoja ya msingi na kama vitabu atavyotunga ataandika haya basi kila atayechukua alipwe ama abaki tunga hadithi.
 
Yaani niko hoi mkuu,sijui hesabu za membe alisomea wapi,haiingii akilini kuwa membe hajui faida za kupunguza mawaziri toka 60 hadi 34.tofauti ya mawaziri 26 haioni,haoni garama za kuwaweka ktk nyumba mawaziri 26!!!haoni ma VX V8 26 bei yake na gharama za kuyaweka barabarani.hivi anajifanya hamnazo au anawafanya watanzania wote mazuzu.

afadhali mungu ulituepusha na huu upupu ungetuwasha tena kwa miaka kumu.ahsante yesu,ahsante allah
 
Mie nashangazwa sana na huu mtazamo,huko mnataka akafanye nini ama mmetumwa?atakwenda wakati unaofaa,sasa kawaambieni waliowatuma haji sasa hivi ng'ooooo
 
Sasa nimeamini kuwa watakaomkwamisha Magufuli ni virusi ndani ya CCM...... Kwa hili nafikiri Membe katumwa na yule jamaa ili amchane Magufuli.

=====================

JPM ni binadamu, anaweza akafanya makosa, kumkosoa siyo dhambi ni mojawapo ya kumsaidia.... tuache mawazo ya kijinga kudhani ni kosa kukosoa.. nina hakika JPM yupo tayari kukosolewa anapokosea...nyerere aliifikisha nchi hii pabaya kiuchumi na kielimu kwasababu hakupenda kabisa kukosolewa hata alipofanya makosa, ilifka mahali watendaji wake na wananchi walikuwa wakimwitikia katika kila jambo kuiridhisha nafsi yake tu, lakini ukweli ukabaki palepale..ndiyo maana leo tunaulizana maswali ambayo hakuna aliye na majibu nayo…
 
Tatizo linakuja hapo kwenye kuacha kila mtu aongee anachotaka ndio tutakapokuwa nchi ya wajinga Kama ulivyoiweka.
Nchi yoyote huwa Inaongozwa na SHERIA NA KANUNI. Otherwise itakuwa Chaos.
Kuna kitu kinaitwa "First Amendment Rights" nafikiri umeshaisikia hiyo kitu!!! Freedom of speech inaangukia humo, lakini bado kuna sheria ambazo zinaipa mipaka hiyo freedom of speech na ukiitumia vibaya inaweza kukuletea matatizo ya kisheria.

Kuna tofauti ya KUSEMA na KUSEMA UKWELI. Watu wengi huwa wanasema tuu bila hata kufanya utafiti kidogo na kujua ukweli wa Jambo husika. Mimi nafikiri kistaarabu kabisa na unyenyekevu wa hali ya juu naomba nipingane na wewe katika hoja yako. Ahsante.
Looh, na hii kali. First Amendment Rights?? Unajua unacho andika au ni ulimbukeni wa uelewa. Katiba ya Marekani unaihusisha na habari hii? Basi at least nenda Google ujue First Amendment Rights ni kitu gani.
 
JPM ni binadamu, anaweza akafanya makosa, kumkosoa siyo dhambi ni mojawapo ya kumsaidia.... tuache mawazo ya kijinga kudhani ni kosa kukosoa.. nina hakika JPM yupo tayari kukosolewa anapokosea...nyerere aliifikisha nchi hii pabaya kiuchumi na kielimu kwasababu hakupenda kabisa kukosolewa hata alipofanya makosa, ilifka mahali watendaji wake na wananchi walikuwa wakimwitikia katika kila jambo kuiridhisha nafsi yake tu, lakini ukweli ukabaki palepale..ndiyo maana leo tunaulizana maswali ambayo hakuna aliye na majibu nayo…

Lakini pia hao wanaokosoa si lazima sana kuwakubali kuwa wako sahaihi 100% wakati mwingine wanakosoa kwakuwa wanaona wamekosa mbinu ya kuzuia madudu yao yasijulikane huko ughaibuni, kwa maana kwamba wanatafuta mwanya safari za ughaibuni ziruhusiwe ili wawatume watu wao wakasawazishe mambo kabla ya hali haijawa mbaya
 
ben membe kumkosoa mh rais ni mtizamo wake, asilaumiwe, ni maoni yake, na maoni yanaweza kuwa sahihi au siyo sahihi...katoa mchango wake mh rais ataufanyia kazi
 
Lakini pia hao wanaokosoa si lazima sana kuwakubali kuwa wako sahaihi 100% wakati mwingine wanakosoa kwakuwa wanaona wamekosa mbinu ya kuzuia madudu yao yasijulikane huko ughaibuni, kwa maana kwamba wanatafuta mwanya safari za ughaibuni ziruhusiwe ili wawatume watu wao wakasawazishe mambo kabla ya hali haijawa mbaya

ni kweli kabisa mkuu, hayo ni maoni yao tu si lazima yawe sahihi..
 
Mkuu kweli hizi nikejeli baada ya kunyanganywa tonge mdomoni kwahyo huyo mb angepewa Nafac vipaumbele vyake vingekuwa nn ili aonyeshe utofauti nahaliyepita mwache jpm afanye kile anacho amini kwan ajaomba msaada kuwa ameshindwa na bado mda ni mfupi lkn matokeo yake warau yameonekana kuliko nyie mliokaa miaka kumi mkashidwa kutangaza nchi vzr licha ya watalii kujua mlima Kilimanjaro unapatika kenye na mengine mengi
 
I
Sasa nimeamini kuwa watakaomkwamisha Magufuli ni virusi ndani ya CCM...... Kwa hili nafikiri Membe katumwa na yule jamaa ili amchane Magufuli.

=====================
Anasema "If you isolate yourself you will be isolated (ukijitenga, utatengwa).”
Pure NOSENSE. Ni kama kwenda kushiriki kwenye vikao vya harusi kutoa pledge za michango usiyo kuwa na uwezo nayo. Masikini anajitambua kwa nafasi yake.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali iliyopita, Bernard Membe ameungana na waziri mwenzake wa zamani, Dk Makongoro Mahanga kukosoa sera ya kubana matumizi ya Rais John Magufuli ya kudhibiti safari za nje na kuteua baraza dogo la mawaziri.

Kama ilivyokuwa kwa Dk Mahanga, waziri huyo aliyedumu kwa miaka tisa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje amesema kiuhalisia, Rais hajapunguza idadi ya wizara kama alivyosema bali amepunguza “idadi ya mifuko”, huku akisisitiza kuwa mkuu huyo wa nchi atalazimika kutoka nje “atake asitake”
 
hawa mawaziro wa zamani wakiona media zimewasahau wanamponda magufuli ili
watokee kurasa za mbele za magazeti
 
lazima akosoe maana haamini kama kanyimwa hata uwaziri
 
hii ngonjera inasaidia nini Taifa.hatuna muda wa ku discuss haya mauozo. Magufuli wewe piga kazi tu! muda wa kupiga siasa umekwisha tupo nyuma ya muda. we cannot waste time for bla-blas
 
Back
Top Bottom