Meli za Iran: Membe 1: Rostam na Karume combine 0

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,172
Katika sakata la usajili wa meli za Iran inaelekea Membe amfunga goli la kiufundi kwa kuwacharaza Rosta na mshirika wake Karume goli moja bila.

Membe aliagiza shoti la mbali kwa kutaka uchunguzi wa kimataifa kutoka Marekani na Uingereza na akaupata.
Jamaa wakawekwa kati na ikagundulika kuwa SMZ haikuwa na picha kamili ya gemu lilivyochezwa na akina Rostam and co.

Membe katamba Bungeni majuzi kuwa meli 39 za kutoka Iran zitafutiwa usajili, meli 28 ni za mizigo na 11 za mafuta.Hii yote imefanyika bila kumyooshea kidole mtu lakini watuhumiwa wanafahamika kutokana na maandishi ya magazeti nchini.

Kampuni inayosemekana ina mkono wa Rostam, Filtex ya Dubai, iliyopewa tenda ya kusajili meli , imefutiwa uwakala wake na SMZ.

Si wengi walioona ufundi wa kidiplomasia uliomo katika sakata hili.
 
Cjaelewa ? Au?

Hii picha wachache sana wameelewa gemu la chess,lilivyochezwa.
Lingechezwa vibaya tu leo ungesikia maandamano ya uamsho huko visiwani, jipu la hizi meli limetumbuliwa na watu inaelekea walitiwa ganzi!
 
Nchi hii kuna filamu nyingi sana; filamu nyingi ni za hatari. Sijui kama ushindi utapatikana hivi karibuni!
 
Nchi hii kuna filamu nyingi sana; filamu nyingi ni za hatari. Sijui kama ushindi utapatikana hivi karibuni!
Mimi naona ni kutokana na kulegeza na kupanua uwigo wa kisiasa, mtu inabidi acheze kwa uangalifu sana hata kama ni serikali yenyewe.
 
Wamarekani/waingereza huwezi kuwapa majibu ya kipuuzi/kisiasa kama yanavyotolewa na watawala wa kitanzania wakakuelewa. Ni afadhali serikali ya Tanzania ingeungama kosa lao na kuomba msamaha wa dhati ya moyo kwamba hawatarudia tena kosa lao kuliko kufikiri kwamba wanaweza kupiga chenga. Angalia sasa magharibu hawatuamini tena hata kidogo na sasa wamebuni namna, na wapo bega na mh dada Joyce wa Malawi. Siasa za kafu, sisiem na chadema ndizo tunazotaka kuzitumia kuwafanyia magharibi propaganda? Hebu tuache hizo.
.
 
Back
Top Bottom