Taarifa ya BLW Znz kuhusu Meli za Iran | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya BLW Znz kuhusu Meli za Iran

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Barubaru, Jul 8, 2012.

 1. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  [h=2]TAARIFA KWA BARAZA LA WAWAKILISHI JUU YA USAJILI WA MELI ZA NJE ULIOFANYWA NA SMZ KUPITIA MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI ZANZIBAR MARITIME AUTHORITY – ZMA[/h]Mhe. Spika,

  Tarehe 27/06/2012 Vyombo vya Habari hapa Tanzania (The Citizen) na nchi za nje (International news Agency – Bloomberg) viliandika makala kuhusu usajili wa meli 10 za mafuta (Tankers). Ilidaiwa katika makala hayo kuwa Meli hizo zilisajiliwa Zanzibar na zinapeperusha Bendera ya Tanzania na kwamba zinafanya biashara na Kampuni ya Serikali ya IRAN. Gazeti la “The Citizen la tarehe 27 Juni, 2012 lilikuwa na kichwa cha habari “Iran Tankers adopt TZ Flag to avoid embargo” (meli za mafuta za Iran zinatumia bendera ya Tz kukwepa vikwazo.

  TAARIFA YA ZMA

  Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar Maritime Authority – ZMA ni Mamlaka iliyoundwa kwa sheria No. 3 ya mwaka 2009 ambayo pamoja na kazi nyengine inasimamia utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari Zanzibar ya mwaka 2006 (Zanzibar Maritime Transport Act 2006).

  Sheria ya Zanzibar Maritime Transport Act 2006, kifungu no. 8 cha sheria hii, kinasomeka kama ifuatavyo:

  Section 8 (1). There shall be established the registers of Tanzania Zanzibar ships to be Known as:-
  (a). Tanzania Zanzibar International Register of Shipping for ocean going ships; and
  (b) Tanzania Zanzibar Register of Shipping for coastal Ships.
  (2). A ship shall be a Tanzania Zanzibar ship for the purpose of this Act if that ship is registered under this part.
  Katika kutekeleza jukumu la usajili wa meli kama ilivyoelekezwa katika kifungu 8(1)(a) hapo juu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za kimataifa. (Open Registry). Usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na mpaka sasa ZMA kupitia Wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, General cargo na meli za Abiria.

  Kama nilivyoeleza hapo awali, vyombo vya habari vimechapisha makala ya usajili wa meli 10 ambazo zinadaiwa ni meli za IRAN kulingana na makala zao hizo.

  SMZ inatoa taarifa rasmi juu ya meli za mafuta ilizosajiliwa wiki mbili zilizopita pamoja na majina ya meli, ukubwa wake, majina ya makampuni inayomiliki meli hizo na nchi zilizotoka kabla ya kupata usajili kwa ZMA, kama ifuatavyo:

  Jina la meli GRT (Ukubwa) Company name Ilikotoka

  1. Daisy 81479 Daisy Shipping Co. Ltd Malta
  2. Justice 164241 Justice Shipping Co. Ltd Cyprus
  3. Magnolia 81479 Magnolia Shipping Co. Ltd Malta
  4. Lantana 81479 Lantana Shipping Co. Ltd Malta
  5. Leadership 164241 Leadership Shipping Co. Ltd Cyprus
  6. Companion 164241 Companion Shipping Co. Ltd Malta
  7. Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd Malta
  8. Clove 81479 Clove shipping Co. Ltd Malta
  9. Courage 163660 Courage Shipping Co. ltd Cyprus
  10. Freedom 163660 Freedom shipping Co. Ltd Cyprus
  11. valor 160930 valor Shipping Co. Ltd. Cyprus

  Jumla ya GRT ni 1,388,368 tons

  Meli hizi ni 11 kama zinavyoonekana katika orodha hapo juu ni miongoni mwa meli nyingi zinazobadilisha usajili wao (De registration). Meli zilizosajiliwa na ZMA zinatoka nchini Cyprus na Malta. Sambamaba na meli hizi 11 zilizosajiliwa na ZMA, meli za mafuta nyengine 20 ambazo zinasemekana zilikuwa kwenye usajili wa nchi za Ulaya zimebadilisha usajili wao na kwenda usajili wa “TUVALU Islands”.

  ZMA ilimtaka Wakala wake Philtex Corporation kuwaita wenye meli hizi na kuwataka kujieleza kuhusu uhusuiano wao na Serikali ya au makampuni ya mafuta ya IRAN. Philtex ilikutana na Wamiliki hao siku ya Alkhamis tarehe 28/06/2012 katika afisi za Philtex Corporation na Wamiliki hao wameeleza kwamba hawana uhusianao na Serikali au mamlaka yoyote nchini Iran na wameamua kuja kusajili meli ZMA kwa ridhaa yao na kwa kufata matangazo ya usajili wetu wa nje (Open Registry).

  Pamoja na maelezo hayo, wamiliki hao wametangaza kwamba ikiwa ZMA haiko tayari kuendelea na usajili wa meli zao, wanaweza kufuta usajili wao na tayari wanafikiria kufanya mazungumzo na open Registry nyengine (PANAMA) lakini hawana nia ya kurudi walikotoka, yaani Cyprus na Malta.

  Kinyume na maelezo yaliyotolewa na vyombo vya habari juu ya uraia wa wamiliki wa meli hizi, Wamiliki wa meli hizi kama walivyojieleza katika usajili wa meli zao wana uraia wa British Vergin Islands na Sychelles.

  Kulingana na “United Nations Convention Law of the Sea”, Article 91, na za “Geneva convection of Registration” articles 6, 7 na 8, na kulingana na Zanzibar Maritime Transport Act of 2006, section 8, Zanzibar ikiwa ni nchi moja kati ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo haki ya kusajili meli yeyote kulingana na taratibu na Sheria za Zanzibar, na sheria za Kimataifa zinazoongoza usajili huo.

  Maelezo haya yanatolewa ili kutoa usahihi wa uvumi kuwa Zanzibar imesajili meli za IRAN ambazo zimewekewa vikwazo na Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya (European Union) juu ya usafirishaji na uuzaji wa mafuta kutoka Iran.

  Mhe. Spika, taarifa hizi za vyombo vya habari hazina madhumuni yeyote zaidi ya kuwavunja moyo wenye Makampuni ya meli wanaotaka kusajili meli zao kwetu.

  Hivyo basi Serikali inatamka wazi kwamba Usajili uliofanywa kwa meli hizi umefuata taratibu zote zilizowekwa kisheria na kwamba Serikali imekuwa ikifanya na itaendelea kufanya mazungumzo na wenye meli mbalimbali ili kuongeza idadi na ukubwa wa meli inazosajili nje ya nchi. Biashara hii ya ukubwa wa GRT 1,388,368 Tons katika kipindi cha wiki mbili na maombi mapya matano kwa meli zitakazokuwa na ukubwa wa zaidi ya GRT 500,000 imeshtua Makamuni mengine na hata nchi nyengine zisizoitakia mema Zanzibar katika juhudi zake za kukuza mapato na uchumi wake.

  Hata hivyo mamlaka itafata sheria zote zilizowekwa kitaifa na kimataifa katika biashara ya usafiri baharini na itahakikisha meli zinasajiliwa chini ya mamlaka hii zinafata taratibu ilizoweka.

  Mhe. Spika, kabla ya taarifa hizi za vyombo vya habari (The Citizen), Waziri wa Uchukuzi wa SMT Mhe. Harisson Mwakyembe) alipokuwa akijibu suala Bungeni hivi juzi hakuonyesha kurishika kwake katika usajili wa meli (Open Registry) inayofanywa na Zanzibar na kuahidi kufanya ziara ya kuja Zanzibar kuonana na Waziri anaehusika kuzungumzia suala hili. Taarifa za “The Citizen” zaweza kuwa ni muendelezo wa Mhe. Mwakyembe kutoridhika kwake katika usajili unaofanywa na Serikali kupitia uwakala wake huko Dubai.

  Mhe. Spika, Zanzibar haifungiki kusajili meli za nchi yeyote.
  Hili ni suala la kibiashara na kwamba kwa Serikali yetu ni njia moja ya kuongeza mapato yanayoendesha Serikali, alimradi tu usajili huo hauvunji sheria za Kimataifa.

  Mhe. Spika,

  Zanzibar ina uhusiano mkubwa na wa muda mrefu na nchi nyingi ikiwemo IRAN na hivi karibuni Zanzibar ilipata ugeni (Makamo wa Rais wa Iran) na viongozi wetu walifanya mazungumzo ya namna gani IRAN itaendelea kusaidia Zanzibar katika miradi ya Maendeleo. Zanzibar haingependa kuingizwa kwa visingizio vyovyote na kwa njama zozote katika migogoro isiyowahusu.

  Hivyo, kwa taarifa hii, Serikali inakanusha rasmi uvumi wa vyombo vya habari kuhusiana na suala hili kama taarifa hii ilivyofafanua hapo juu.

  Mhe. Spika, naomba kuwasilisha.

  Hamad Masoud Hamad
  WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
   
 2. H

  Hute JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,045
  Likes Received: 3,917
  Trophy Points: 280
  hawa midebwedo waongelea puani, dawa yao ni kujitenga nao tu, ili waendelee na zenji yao, hapo ndipo watakapoona kumbe walikuwa wanaponea kwenye muungano....kwanza wanatuchafulia hata jina, kwano wao ndo vinara wa ugaidi tz....
   
 3. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Imedadavuliwa vizuri na inaeleweka, naombeni kuuliza je? Hii taarifa Kwenye gazeti la Citzen,na ile BARUA toka congress Kama sikosei kipi kilitangulia? Je Wamarekani siku hizi wanafanyia "kazi" habari za magazeti ya kibongo.
  Anyway Mbona kila kitu kiko wazi kutokana na maelezo ya Huyo waziri! Sasa hizi tuhuma za wamarekani kwa watanzania zinatokea wapi? Au mishemishe za MASLAHI binafsi zimeanza? I'm confused a bit nipeni mwanga.

   
 4. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,802
  Likes Received: 2,576
  Trophy Points: 280
  Home keeping youth have ever homely wits.
   
 5. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 280
  Zanzibar do what you want na sio sisi wa BARA tunataka mfanye...As long as you dont break international laws...Kusajiri MELI za IRAN hakuna kosa lolote kwani MAREKANI na ULAYA wamewawekea makampuni ya nchi zao kutofanya biashara ya mafuta na IRAN na kuondoa insurance kwenye MELI za ULAYA kwenda IRAN...So lazima mfahamu TANZANIA,ZANZBAR kufanya biashara na IRAN hakuna kosa kwani we all benefit na sio kutegemea misaada ya US/EU...Huo ugomvi wa US na IRAN hauwezi kutufanya sisi tu side na US by the way vikwazo sio vya UMOJA WA MATAIFA ila ni vya US/EU sasa kwanini watutishie kisa wanatupa misaada? Hakuna aja ya kuogapa eti tutawekewa vikwazo ata km wakiweka sio vikwazo vya UN bali ni vya nchi moja na huo ndo utakua mwanzo wa kupata akili na ndo chachu ya kujitegemea na sio kufikiria misaada ambayo inadharirisha utu wetu na isitoshe imekuepo tokea uhuru na still bado tupo maskini...nini tunaweza kufanya incase tumewekewa vikwazo na sisi ndo mwanzo wa kuwafukuza ktk mariasili zetu mf dhahabu,gas,mafuta urine nadhani apo watapata picha kua uhuru wa nchi moja hauwezi kuingiliwa na ka sanetor kamoja ka US
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,311
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Hamad wewe Hamad unatamba tu na usiyoyajua subiri watakavyokugeuka na kuombwa kujiuzulu baada ya tishio la kupigwa na vikwazo vya uchumi!!tulia tu utayakana maneno yako hayo!!yangu macho na masikio
   
 7. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kama tanganyika wakijitenga na znz basi znz itakuwa sehemu ya ugaidi duniani.
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Aaaahhhh hii ni ya zamani mkuu ila si MBAYA tukaicheki tena maana hata meli zilizotajwa sizo zilizoripotiwa
   
 9. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kwani inshu kabisa ikoje mkuu?
   
 10. A

  Albimany JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45

  Labda nikweli uyasemayo ila na zanzibar kutapungua ujambazi, ukimwi na umalaya!
   
 11. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa wazanzibar hawana focus. wamepania kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na yote yanautata katika mtazamo wa kidunia. UAMSHO inamwelekeo wa kigaidigaidi hivi na watu duniani wanawaangalia!hizi meli nazo mmh zina utata wake.kuna baadhi ya viongozi wanajitafutia shida duniani!ntie hata vikwazo wazungu hawata viweka watakuja mchana kweupeee watawakamata hao wanao wadanganya eti ZANZIBAR NI NCHI HURU haihitaji kuchaguliwa marafiki sawa lakini kufanya biashara na IRANI ni kujipalia mkaa wa moto angalieni mnakoekea siyo kuzuri,
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Zanzibar soon kitageuka kituo maarufu cha magaidi kama wakiamua **** huhu na kule. Pesa ina madhara yake.
   
 13. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  umenichekesha sana.,...wewe mbara sio?? umeamua kujifanya mbara ili uongeze ***** humu?? Can you stand stand on you own withouth them and Tanganyika?? Probably mnataka kuwaua wananchi wenu kwa kwashiokor...
   
 14. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Na huku bara pia tutaepuka ushoga....bora uvunjike kabisa....
   
 15. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  kumekucha!
   
 16. K

  KengeWaKijani Senior Member

  #16
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi cjaelewa kabisa.
   
Loading...