SMZ yakiri kusajili meli 36 za mafuta kutoka Iran | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMZ yakiri kusajili meli 36 za mafuta kutoka Iran

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Aug 11, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi

  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imekiri kusajili meli 36 za mafuta kutoka nchini Iran kinyume na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN).

  Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, alisema hayo alipokuwa akifunga mkutano wa nane wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), mjini hapa.

  Balozi Seif alisema baada ya kuibuka taarifa za kusajiliwa kwa meli hizo serikali ilifanya uchuguzi na kubaini kuwa kampuni ya uwakala ya Philtex ilisajili meli 36 kwa niaba ya Zanzibar na kupeperusha bendera ya Tanzania.

  Alisema kampuni hiyo inafanya kazi yake nchini Dubai ikiwa na mkataba na Mamlaka ya Usafirishaji baharini Zanzibar (ZMA), kama wakala wake wa kusajili meli za kigeni.

  “Mheshimiwa Spika Serikali ilifuatilia suala hili kwa undani na imegundulika kuwa Mamlaka ya usafiri baharini (ZMA) kupitia kwa wakala wetu wa Dubai Philtex ilisajili meli 36 za Iran za mafuta na kutumia bendera ya Tanzania,” alisema Balozi Seif.

  Iran imewekewa vikwazo vya kiuchumi na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa vya kusafirisha mafuta na kuuza kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kushutumiwa kumiliki silaha za nyukilia na kusadia vikundi vya ugaidi duniani.

  “Baada ya kugundua ukweli kwamba meli hizo zinapeperusha bendera ya Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imo katika hatua za kuzifutia usajili meli hizo,” alisema Balozi Seif.

  Alisema Serikali pia imeamua kuifutia uwakala kampuni ya Philtex ya kufanya kazi ya kusajili meli kwa niaba ya Zanzibar baada ya kufanya makosa hayo.

  “Mheshimiwa Spika Serikali itafanya uchunguzi wa kina kujua ni vipi usajili huo ulifanyika.”alisema Makamu wa Pili wa Rais katika hotuba yake.

  Balozi Seif alisema kitendo hicho kimekwenda kinyume na azimio la Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na amri ya utekelezaji (Excutive Order) iliyotolewa Marekani na nchi Jumuiya ya Ulaya.

  Hata hivyo, alisema pamoja na tukio hilo uhusiano wa Iran na Zanzibar utaendelezwa kama kawaida kutokana na Zanzibar kuwa na historia kubwa na nchi hiyo.

  Balozi Seif hakusema serikali itawachukulia hatua gani watendaji wa ZMA Zanzibar ambao walitoa taarifa za uongo na serikali kuwasilisha katika chombo cha kutunga sheria.

  Julay 24, mwaka huu aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Hamad Masoud Hamad, aliwasilisha taarifa maalum ya serikali katika Baraza la Wawakilishi na kukanusha kuhusu Zanzibar kuhusishwa na kusajili meli za Iran nchini Dubai.

  Hamad alisema pamoja na Zanzibar kuwa na uwezo wa kisheria wa kusajili meli imekuwa ikifanya kazi ya kusajili meli kwa umakini na kutaka choyo cha biashara kuondolewa katika biashara hiyo.

  Alisema kwamba kimsingi Zanzibar kupitia wakala wake wa Dubai imesajili meli za mafuta 11 ambapo zote zinatoka katika nchi ya Cyprus na Malta.

  Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alithibitisha kupokea malalamiko kuhusu Zanzibar kukiuka Azimio la Umoja wa mataifa kwa kusajili meli za mafuta za Iran kupitia wakala wake wa nchini Dubai.

  Waziri Membe aliomba Marekani na Jumuiya ya Ulaya (EU) kufanya uchunguzi ili kupata ukweli wake baada ya Zanzibar kukanusha taarifa ya kusajili meli za Iran Dubai.

  Waziri Hamad alijiuzulu wadhifa wake Julai 23, mwaka huu kufuatia ajali ya meli ya Mv Skagit ambapo watu 136 walikufa maji, 146 kuokolewa na watu nane kutoweka tangu kutokea ajali hiyo Julai 18, mwaka huu.

  Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) limeahilishwa hadi Oktoba 10 baada ya kumaliza kujadili makadirio matumizi ya bajeti za serikali mwaka huu.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,135
  Trophy Points: 280
  Dah! Walikuwa wanaruka huku na kule kusema uongo kama hawahusiki!!! Sijui wamechukua mabilioni mangapi ili kuruhusu meli 36 za Iran kutumia bendera yetu!!!
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Umeona ee! Kwa nini Zenj isitangaze wazi kuwa imejitenga kwani vitendo ambavyo vinaingilia mamlaka ya serikali ya Muungano kujitwisha wenyewe ni kujitangazia uhuru.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,135
  Trophy Points: 280
  Yote haya yanasababishwa na DHAIFU, vinginevyo wasingekuwa na ubavu wa kujiamulia mambo kiholela ambayo yanaweza kuiingiza nchi matatani.

   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka kipindi cha utawala wa Nyerere kilichompata Abdu Jumbe hadi kukaa kizuiani Mji Mwema Kigamboni, lakini leo hata ingelijensia imeshindwa kazi hadi habari zinatokea intelijensia ya nchi nyingine. Tutafika kwa mwendo huu?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,135
  Trophy Points: 280
  Acha yule Mzee aende zake. Kwenye Muungano alikuwa haruhusu madudu ya aina yoyote ile. RIP Mwalimu.

   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ndo shida ya kuwa na rais wa muungano dhaifu
   
 8. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu Candid Scope, intelligensia ya Tanzania kwa sasa inatumia Manpower yake yote kupambana na CHADEMA ndiyo maana hata wahamiaji haramu waingiapo nchini hugundulika tu pale maroli yanayowbeba yanapopata ajali tu. Unadhani kweli inaweza kuona Meli za Irani zinazopepea bendera ya Tanzani. Pia kwa upeo wa serikali ya DHAIFU Meli za Irani kupepea bendera ya Tanzania ilikuwa sifa kwa serikali ya ccm.
   
 9. m

  makundi4619 JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 486
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bwana wee Zenji ni wanafiki Muungano wanautaka kwa ajili ya manufaa yao tu. Hawana nia ya dhati kushirikiana na watu wa bara. Si mnaona? Kwa nini wasitumie bendera yao kama kweli ina nguvu. Tuache kuwabembeleza wawajibishwe ipasavyo.
   
 10. C

  Concrete JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Halafu tunadai nchi yetu ipo salama, inteligensia ya nchi yetu kazi yake ni umbeya tu,

  Wanausalama wetu wamegeuka kuwa mbwa wa watawala, wanasubiri maagizo kutoka kwa Nape, Chiligati, Mwigulu, Mukama ili watunge sababu za kuzuia harakati za kisiasa za upinzani.
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kazi ipo na serikali yenu ya ccm legelege
   
 12. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Tunahitaji serikali moja. Zanzibar tuwape mikoa 2 unguja na pemba. Hivi wizara ya mambo ya nje siyo ya Muungano? If not, tutakukuwa na mapungufu!
   
 13. J

  Jumaane Member

  #13
  Aug 11, 2012
  Joined: Jul 7, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyinyi mlitumia bendera yenu lini? Mnapotumia bendera ya Muungano kwenye biashara na mishemishe zenu (biashara zatwiga, dhahabu rada etc) mnaomba idhini/ruhusa kutoka wapi?. Kwa mantiki gani zanzibar ipaswe kupata idhini ya kutumia bendera ya Muungano toka Tanganyika? To hell with your MUUNGANO-UKOLONI.

  Kwa taarifa yenu hakuna UN resolution yoyote inayozuia biashara na taifa la Iran.
   
 14. B

  Bull JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazanzibari hongera kwa hili, mnajua jinsi ya kucheza na wamerikani sio sisi wa bara wazungu wakituangalia tunajinyea, win win stuation kwa sababu wao wamerikani wanaishi kinafiki
   
 15. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  Intelijensia ya nchi hii, ni kudhibiti chadema isifanye M4C katika vuguvugu la kuleta mageuzi ya nchi kuwa ya wananchi hasa wanyonge watawale rasilimali zao kwa haki na usawa ili kujiletea maendeleo chanya na yaliyosawia.Pia intelejensia ya nchi hii ni kudhibiti mwanahalisi na na madaktari wanaoipinga.hatuna usalama wa taifa.Kuna ombwe kubwa kwenye chombo hiki cha dola na kuhoji weledi wake.Hata hivyo pamoja na kufahamu , na hata kuzifutia meli hizo usajili, mbona makamu wa pili wa raisi yuko kimya kwenye ufisadi huu?au ndo sera ya ccm?walimu wakigoma mapema serikali kukimbilia mahakamani.je mbona hili haikimbilii kwenda mahakamani?
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Aug 11, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,799
  Likes Received: 5,082
  Trophy Points: 280
  1. "Baada ya kugundua ukweli kwamba meli hizo zinapeperusha bendera ya Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imo katika hatua za kuzifutia usajili meli hizo," alisema Balozi Seif.

  2. Alisema
  Serikali pia imeamua kuifutia uwakala kampuni ya Philtex ya kufanya kazi ya kusajili meli kwa niaba ya Zanzibar baada ya kufanya makosa hayo.
   
Loading...