Meli za Iran-Karume anahusika ? (Raia Mwema) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meli za Iran-Karume anahusika ? (Raia Mwema)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by masopakyindi, Jul 18, 2012.

  1. masopakyindi

    masopakyindi JF-Expert Member

    #1
    Jul 18, 2012
    Joined: Jul 5, 2011
    Messages: 13,911
    Likes Received: 2,336
    Trophy Points: 280
    Raia Mwema la leo, Julai18-Julai24, 2012
    "Wakati uchunguzi wa kimataifa ungali ukiendelea,Raia Mwema imethibitisha kuwa Rais mstaafu aliyepata kuongoza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) na mmoja wa kigogo wa juu wa sasa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wanahusika.(Amani Abeid Karume?)

    Mtandao huo wa kiongozi huyo mstaafu ambaye anazo ndoto za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mwenzake ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa(Sheikh Hamad Sherrif?),wamefanya mpango huo na aliyepata kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM),ambaye pia amepata kuwa mbunge wa moja ya majimbo ya uchaguzi mkoani Tabora(Igunga-Rostam Aziz?).

    My Take:
    Niliwahi kumpongeza Membe humu jamvini kwa kazi nzuri ya kidiplomasia kuwaumbua hawa jamaa bila kudhuru serikali ya Tanzania kwa ujumla.
    Sasa mbivu na mbichi zitaanza kuonekana, Zanzibar ni Nchi bana , ebo!!
     
  2. Democracy999

    Democracy999 JF-Expert Member

    #2
    Jul 18, 2012
    Joined: May 26, 2012
    Messages: 947
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    Karume aliwahi kuogopa kuja Bara kwa kuhofia kikamatwa akiwa bado Governor wa Zanzibar, alisingizia ndege hairuki kwa matatizo ya hali ya hewa, kwa nini hakujiamini? Kaiba au kaharibu nini? Yeye ana nia ya kweli ya kuiondoa Zanzibar ili apate kuila bila kutizama huku na huko kwani mwizi kama yeye hamna.
     
  3. Bujibuji

    Bujibuji JF-Expert Member

    #3
    Jul 18, 2012
    Joined: Feb 4, 2009
    Messages: 35,307
    Likes Received: 22,111
    Trophy Points: 280
    Abdulrahman Kinana hausiki kweli?
     
  4. masopakyindi

    masopakyindi JF-Expert Member

    #4
    Jul 18, 2012
    Joined: Jul 5, 2011
    Messages: 13,911
    Likes Received: 2,336
    Trophy Points: 280
    Mkuu gemu hili ni la Wazenji na wa asili ya Irani
     
  5. Kunta Kinte

    Kunta Kinte JF-Expert Member

    #5
    Jul 18, 2012
    Joined: May 18, 2009
    Messages: 3,660
    Likes Received: 215
    Trophy Points: 160
    Mkuu una kitu cha ziada unajua/unataka kutwambia?
     
  6. J

    Jumaane Member

    #6
    Jul 18, 2012
    Joined: Jul 7, 2012
    Messages: 55
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    acha kupika majungu.
    Lete ushahidi

     
  7. Lole Gwakisa

    Lole Gwakisa JF-Expert Member

    #7
    Jul 18, 2012
    Joined: Nov 5, 2008
    Messages: 3,962
    Likes Received: 403
    Trophy Points: 180
    Hata maana ya neno majungu inaelekea imekupiga chenga.
    Hiyo quote uliyowekewa ya gazeti la Raia Mwema umelisoma au ndo unajifunza u-Great Thinker?
     
  8. J

    Jumaane Member

    #8
    Aug 11, 2012
    Joined: Jul 7, 2012
    Messages: 55
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Nimesoma hiyo makala mara 10. Majina yametajwa (humo kwenye red). Licha ya "evidence without any reasonable doubt" inayotarajiwa, haya doubtful one haipo - If you are a graduated great thinker. Unless the editor has safe-kept his nondos till the right moment comes at the court of law. But then to me, without evidence what has been quoted will remain speculations (majungu) and nothing more.
     
  9. MziziMkavu

    MziziMkavu JF-Expert Member

    #9
    Aug 12, 2012
    Joined: Feb 3, 2009
    Messages: 39,620
    Likes Received: 4,613
    Trophy Points: 280
    [​IMG]
    Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi


    Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imekiri kusajili meli 36 za mafuta kutoka nchini Iran kinyume na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN).

    Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, alisema hayo alipokuwa akifunga mkutano wa nane wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), mjini hapa.

    Balozi Seif alisema baada ya kuibuka taarifa za kusajiliwa kwa meli hizo serikali ilifanya uchuguzi na kubaini kuwa kampuni ya uwakala ya Philtex ilisajili meli 36 kwa niaba ya Zanzibar na kupeperusha bendera ya Tanzania.

    Alisema kampuni hiyo inafanya kazi yake nchini Dubai ikiwa na mkataba na Mamlaka ya Usafirishaji baharini Zanzibar (ZMA), kama wakala wake wa kusajili meli za kigeni.

    “Mheshimiwa Spika Serikali ilifuatilia suala hili kwa undani na imegundulika kuwa Mamlaka ya usafiri baharini (ZMA) kupitia kwa wakala wetu wa Dubai Philtex ilisajili meli 36 za Iran za mafuta na kutumia bendera ya Tanzania,” alisema Balozi Seif.

    Iran imewekewa vikwazo vya kiuchumi na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa vya kusafirisha mafuta na kuuza kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kushutumiwa kumiliki silaha za nyukilia na kusadia vikundi vya ugaidi duniani.

    “Baada ya kugundua ukweli kwamba meli hizo zinapeperusha bendera ya Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imo katika hatua za kuzifutia usajili meli hizo,” alisema Balozi Seif.

    Alisema Serikali pia imeamua kuifutia uwakala kampuni ya Philtex ya kufanya kazi ya kusajili meli kwa niaba ya Zanzibar baada ya kufanya makosa hayo.

    “Mheshimiwa Spika Serikali itafanya uchunguzi wa kina kujua ni vipi usajili huo ulifanyika.”alisema Makamu wa Pili wa Rais katika hotuba yake.

    Balozi Seif alisema kitendo hicho kimekwenda kinyume na azimio la Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na amri ya utekelezaji (Excutive Order) iliyotolewa Marekani na nchi Jumuiya ya Ulaya.

    Hata hivyo, alisema pamoja na tukio hilo uhusiano wa Iran na Zanzibar utaendelezwa kama kawaida kutokana na Zanzibar kuwa na historia kubwa na nchi hiyo.

    Balozi Seif hakusema serikali itawachukulia hatua gani watendaji wa ZMA Zanzibar ambao walitoa taarifa za uongo na serikali kuwasilisha katika chombo cha kutunga sheria.

    Julay 24, mwaka huu aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Hamad Masoud Hamad, aliwasilisha taarifa maalum ya serikali katika Baraza la Wawakilishi na kukanusha kuhusu Zanzibar kuhusishwa na kusajili meli za Iran nchini Dubai.

    Hamad alisema pamoja na Zanzibar kuwa na uwezo wa kisheria wa kusajili meli imekuwa ikifanya kazi ya kusajili meli kwa umakini na kutaka choyo cha biashara kuondolewa katika biashara hiyo.

    Alisema kwamba kimsingi Zanzibar kupitia wakala wake wa Dubai imesajili meli za mafuta 11 ambapo zote zinatoka katika nchi ya Cyprus na Malta.

    Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alithibitisha kupokea malalamiko kuhusu Zanzibar kukiuka Azimio la Umoja wa mataifa kwa kusajili meli za mafuta za Iran kupitia wakala wake wa nchini Dubai.

    Waziri Membe aliomba Marekani na Jumuiya ya Ulaya (EU) kufanya uchunguzi ili kupata ukweli wake baada ya Zanzibar kukanusha taarifa ya kusajili meli za Iran Dubai.

    Waziri Hamad alijiuzulu wadhifa wake Julai 23, mwaka huu kufuatia ajali ya meli ya Mv Skagit ambapo watu 136 walikufa maji, 146 kuokolewa na watu nane kutoweka tangu kutokea ajali hiyo Julai 18, mwaka huu.

    Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) limeahilishwa hadi Oktoba 10 baada ya kumaliza kujadili makadirio matumizi ya bajeti za serikali mwaka huu.
    CHANZO: NIPASHE

     
  10. Lole Gwakisa

    Lole Gwakisa JF-Expert Member

    #10
    Aug 12, 2012
    Joined: Nov 5, 2008
    Messages: 3,962
    Likes Received: 403
    Trophy Points: 180
    Asante mkuu kwa quote.
    Kuna jamaa alikuwa anasema ati hii mada ni majungu, sasa mjue Zanzinar watu mnavyoswekwa kuwahudumia wajanja.
    Kwa Karume , shame on him!
     
  11. masopakyindi

    masopakyindi JF-Expert Member

    #11
    Aug 12, 2012
    Joined: Jul 5, 2011
    Messages: 13,911
    Likes Received: 2,336
    Trophy Points: 280
    Evidence yote iko magazetini, sema hutaki kuamini, na hapo ni tatizo lako.
    Mnachezewa shere bila kujijua na mwidhowe mnaingizwa mkenge,

    Sakata hili na mengi yanayayosikika magazetini yanamweka Karume katika genge la watu wasio waadilifu sana has ukichukulia kuwa alikuw kiongozi wa juu kabisa.
     
Loading...