Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchunguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchunguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 7, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  NA THOBIAS MWANAKATWE

  6th July 2012


  Sakata la meli za mafuta zinazodaiwa kuwa ni za Iran kupeperusha bendera ya Tanzania kwa lengo la kufanikisha biashara ya nishati hiyo limezidi kuikoroga serikali ambayo sasa imezipigia ‘magoti' nchi wanachama wa Baraza la Umoja wa Mataifa kusaidia kufanya uchunguzi ili kuthibitisha iwapo kuna ukweli kuwa meli hizo ni za Iran.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimelazimika kuomba msaada huo kwa sababu Tanzania ina uwezo mdogo wa kufanya uchunguzi na kuthibitisha suala hilo.

  Membe alisema iwapo uchunguzi huo utabaini kuwa kweli meli hizo ni za Iran, Serikali ya Mapinduzi ya Zanziar (SMZ) pamoja na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitachukua hatua ya kuzifutilia mbali meli hizo.

  "Hivyo tunahitaji ushirikiano kati ya serikali zetu mbili, serikali ya Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) kusaidia katika kuthibitisha taarifa hizi kwa sababu wao wana uzoefu mkubwa wa ‘verification' wa kukanusha ama kuthibitisha ya kuwa meli zinazopeperusha bendera ya Tanzania ni meli za Iran au la", alisema Membe.

  Alisema Serikali ya Tanzania itahakikisha inafanya utafiti wa kina na wa kuaminika kwa kushirikiana na nchi za Marekani na za Umoja wa Ulaya ili kupata ukweli wa meli hizo.

  Membe alisema zipo sababu tatu zinazosababisha kufanyika kwa utafiti huo ambapo moja ni kwamba wakala wa kampuni ya Philtex ya Dubai ambaye ameingia mkataba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amekataa kwamba meli hizo ni za Iran.

  Alisema sababu ya pili ni kwamba Julai 2 mwaka huu Wizara yake ilipomwita Balozi wa Iran kujadili utata wa meli hizo ili athibitishe au akanushe taarifa hizo alikataa.

  Membe alitaja sababu ya tatu ya kufanya uchunguzi huo kuwa ni kutokana na kwamba sheria ya kimataifa hasa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inayozikataza nchi wanachama kuruhusu Iran au meli zake kutumia jina la nchi kwenda katika maji ya kina kirefu kupakuwa na kupakia bidhaa zake ili kukwepa vikwazo walivyowekewa.

  "Vipo vikwazo vilivyowekwa na jumuiya ya kimataifa hasa Umoja wa Mataifa kulingana na azimio namba 1929 la mwana 2010 inayozikataza nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuruhusu Iran au meli zake kutumia jina la nchi kwenda katika maji ya kina kirefu kupakuwa na kupakia bidhaa zake ili kukwepa vikwazo alivyowekewa," alisema Membe.

  Membe aliwaomba Watanzania jambo hili lisizushe mtafaruku ndani ya nchi na kutetemesha Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar na kuwahakikishia kuwa litamalizwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

  Aliongeza kuwa lazima ifahamike Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hazitaki kupuuza taarifa ya kuwepo kwa meli hizo zinazopeperusha bendera ya Tanzania kwenye maji marefu na ndiyo maana zimeamua kufanya utafiti wa suala hilo.

  Mgogoro huu umezidi kupamba moto hapa nchini hasa baada ya Mbunge Marekani ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Howard Berman, kuweleza wazi kuwa kitendo cha kusajiliwa kwa meli za Iran na kupeperusha bendera ya Tanzania ni kuvunja vikwazo vya kiuchumi vya Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) dhidi ya Iran.

  Berman katika barua yake ya Juni 29, mwaka huu aliyomwandikia Rais Jakaya Kikwete alieleza masikitiko yake kwamba Tanzania imeruhusu Kampuni ya Taifa ya Meli za Iran (NITC) kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye walau meli sita na zinatarajiwa kufikia 10 na zimesajiliwa nchini.

  "Kwa kuruhusu meli hizo kuwa chini ya miliki ya NITC na kuendelea kusafirisha mafuta ghafi ya Iran, kitendo hiki kwa serikali yako kina madhara ya kuisaidia Serikali ya Iran kukwepa vikwazo vya Marekani na EU ili ipate mapato zaidi ya kugharimia mpango wake wa kutengeneza silaha za nyukilia na pia kusaidia ugaidi wa kimataifa," imesema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Rais Kikwete.

  Kadhalika, alisema inasikitisha kuona kwamba serikali ya Tanzania imekiuka makubaliano ya pamoja ya jamii ya kimataifa ambayo inafanya kazi kwa pamoja kutumia njia za amani zikihusisha vikwazo vya kiuchumi ili kubadili tabia ya Iran ya kuhatarisha amani duniani.

  "Kitendo cha kuruhusu meli za NITC kupeperusha bendera ya Tanzania inatia shaka hadhi ya Tanzania katika jamii ya kimataifa," inasema barua hiyo.

  Kwa maana hiyo, Berman alimuomba Rais Kikwete kufuta usajili wa meli hizo zinazopeperusha bendera ya Tanzania, kwani kwa mujibu wa uamuzi wa Rais wa Marekani, Barack Obama, wa 13608 ambao aliusani Mei mosi mwaka huu unajumuisha nchi zote na mashirika yote katika ukiukaji wa vikwazo dhidi ya Iran kama watakuwa wanaisaidia nchi hiyo kukwepa vikwazo hivyo."

  Kadhalika, mbunge huyo ameonya kwamba endapo Tanzania itaamua kuziacha meli hizo kuwa na usajili nchini na kuendelea kupeperusha bendera yake, basi wao katika Bunge la Marekani hawatakuwa na njia nyingine isipokuwa ni kutafakari kama bado mipango ya maendeleo baina ya Marekani na Tanzania kama bado inahitajika.

  Hata hivyo baada ya suala hili kuibuliwa na vyombo vya habari, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iliibuka na kutoa taarifa kuwa kwa kuzingatia sheria ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (Maritime Authority – ZMA) iliyoundwa kwa sheria No. 3 ya mwaka 2009 ambayo pamoja na kazi nyingine inasimamia utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari Zanzibar ya mwaka 2006 (Zanzibar Maritime Transport Act 2006).

  Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa SMZ, Hamad Masoud Hamad, aliwasilisha taarifa yake kwa Baraza la Wawakilishi Julai 2, mwaka huu akithibitisha kusajiliwa kwa meli 10 za Zanzibar ambazo zinapeperusha bendera ya Tanzania, lakini siyo za Iran ila zimetokea Malta na Syprus.

  Alisema SMZ imetiliana mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za kimataifa (Open Registry). Usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na mpaka sasa kupitia Wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, za mizigo ya jumla na meli za abiria.

  Alitaja meli hizo kuwa ni Daisy 81479 Daisy Shipping Co. Ltd Malta; Justice 164241 Justice Shipping Co. Ltd Cyprus; Magnolia 81479 Magnolia Shipping Co. Ltd Malta; Lantana 81479 Lantana Shipping Co. Ltd Malta; Leadership 164241 Leadership Shipping Co. Ltd Cyprus; Companion 164241 Companion Shipping Co. Ltd Malta; Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd Malta; Clove 81479 Clove shipping Co. Ltd Malta; Courage 163660 Courage Shipping Co. Ltd Cyprus; Freedom 163660 Freedom shipping Co. Ltd Cyprus na Valor 160930 valor Shipping Co. Ltd. Cyprus.

  Waziri huyo alisema walimtaka wakala wao Philtex Corporation kuwaita wenye meli hizo na kuwataka kujieleza kuhusu uhusuiano wao na Serikali ya au makampuni ya mafuta ya Iran na walisema kuwa hawana uhusiano na Serikali au mamlaka yoyote nchini Iran na wameamua kuja kusajili meli Zanzibar kwa ridhaa yao.

  Jana katika sehemu ya habari kuhusu meli hizi tulisema kuwa Waziri Hamad alisema Barazani kuwa meli hizo ni za Iran. Tunasikitika kwa upungufu wa aya hiyo katika habari yetu ya jana. Mhariri.


  CHANZO: NIPASHE


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Usajili wa Meli za Kimataifa ni kazi kweli kweli; Meli nyingi zina Usajili wa Cyprus; Liberia; Malta na ni za Nchi Mbalimbali

  Duniani, Sasa Inasemekana za Iran hivyo hivyo, itakuwa kazi kweli kuzi-pinpoint - labda huo Msaada wa UN utasaidia

  kabla ya Sanctions...
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kova Wapi kamanda msangi afanye uchunguzi teh teh teh
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  You guys dont seem to get the point.
  Wakubwa hawataki kuumbuana hadharani.
  Hapa naona kero ya muungano imejikikita.
  Kuna tetesi kuwa meli hizo zimesajiliwa Zanzibar ambao wamekana kufanya hivo kwa makusudi.

  Hivyo basi Membe is calling the bluff, na kuna mtu ataadhirika hapa.
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kumbe hatuna uwezo wa kuchunguza kashfa hii...!!
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  uwezo wetu ni wa kuchunguza ishu za msituni mabwepande
   
 7. R

  Recover Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawana uwezo aw kuficha..hawana hiyo akili..labda kwa msaada aw Irani
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Wanajikosha tu hawana uwezo kuchunguza wakati waziri wa Zbar amekiri wamezisajili?kunahitaji uchunguzi gani wa kimataifa hapo?au ndio diplomasia imetumika?
   
 9. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Itajulikana tu, na wala si kazi ngumu hiyo. Kama Membe angekuwa na akili ya ziada angenyamazia jambo hilo .. tunakwenda kuumbuka very soon!
   
 10. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Watasema ni njama za CHADEMA kuzipatia usajili meli za Iran bongo
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Aaah Wapi Wameweza kuchunguza MISIKITI? Wangeona UAMSHO Mapema then...
   
 12. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  kwani UAMSHO ina tatizo gani na nyinyi kama mkweli mnataka Tanganyika yenu muazishe somesing like, bila hivyo mpaka kiyama mtakuwa chini ya himaya ya Tanzania na vizazi vyenu havitajua asili yenu kama sisi tunajisifia uzanzibari wetu, aidha katika hili la meli mnapoteza muda tu na kama ilivyo sifa za watanganyika ni kuongea, basi mtaongea na mtaongea.

  Zanzibar imeshatoa tamko na lipo mpaka kwenye hansard za Baraza la Wawakilishi, mnataka kusema waziri kutoka Zanzibar kasema uwongo, hatuzifuti hizo meli, mkitaka itabidi mtulipe fidia kwa kukosa mapato, vikwanzo si vya UN ni vya USA na EU ndio maana China bado inanunua mafuta kutoka Iran, nyie watanganyika kazi yenu ngonjera basi sisi hazituyumbishi hizo, mara hii ngangari hatutokli kama tulivyotoka OIC, anayetujua sisi Nyerere na keshakufa nyie hamtujui sisi.
   
 13. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Wanachoweza wao kuchunguza ni Maandamano yenye kuleta fujo, migomo ya madaktari, hapo ndio umefikia mwisho wao wa kufikiri zaidi ya kutumia akili za ziada za masaburini kama Ikulu au Bunge linavyopisha Bajeti za Kipumbavu na za kihuni.

  Ikulu: Dhaifu, Jeuri, hawaambiliki, Waongo, Mafisadi, Wauza ardhi zetu na upumbavu mwingi wapo kwa ajili ya maslai yao
  Bunge: Limegeuzwa kuwa Kijiwe cha wahuni, wanapitisha bajeti za kipumbavu na zakijinga, imekuwa sehemu ya mipasho, kutete vyama vayo hasa Magamba. Wabunge wengi wpo kimaslai yao Hasa wa magamba na wengi wao ni waongo
  Polisi:Nafikiri wangeomba kupewa usajili ili liwe kama Chama cha siasa, Wengi wao ni wapumbavu na wajinga wengi wanaoliongoza jeshi letu, majeuri, majinga, maongo hayajui kufanyakazi wanachojua wao ni kula rushwa na kulinda mafisadi hasa wa Ikulu.

  Idara nyingine malizie
   
 14. m

  mob JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  sisi tuna madini ya uraniam ni vyema tukawaomba wenzetu watu wa jumuia ya iran kuja kutusaidia kuchimba ili tuweze kupata umeme wa uhakika kila wakati.si vizuri kuona watu wanasema hawa watu ni wabaya nasisi tukaingia mkumbo huo huo kusema ivyo ivyo. kuiona unasapoti kila kitu wewe una tabia ya uoga.
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Oh Nilikuwa natetea MSIKITI na sasa Unaniona Mbaya? UAMSHO haikuanzia MSIKITINI nilikuwa nampima huyo

  Mchangiaji; NA WELL KAMA ZANZIBAR HAIZIFUTI HIZO MELI SAWASAWA SANCTIONS ZIIMULIKE HUKO HUKO

  ZANZIBAR; FOR YOUR INFO SANCTIONS NI ZA USA WALIPELEKA UN; NDIO MAANA HATA INDIA SASA HIVI HAINUNUI

  MAFUTA TOKA IRAN, NA PIA EUROPE; HII NI SABABU YA KUWASAIDIA WANANCHI WA
  SYRIA MAJORITY NI SUNNI 74%

  WANATESWA, WANAUWAWA na WATAWALA KWA MUDA MREFU SANA ALAWITES 13% RELIGION YA ASSAD FAMILY,

  NDIO WANAOPENDELEWA NA WAIRAN; na WOTE NI WAISLAMU.

  NI KAMA ILIVYOKUWA ZANZIBAR 1963, WANANCHI WAAFRIKA WALICHAGUA ASP LAKINI MTAWALA MWINGEREZA na

  MWARABU WAKAIPA CHAMA CHA KIARABU ambao WALIKUWA WACHACHE SANA KUITAWALA ZANZIBAR;

  WAAFRIKA WEUSI AMBAO NI MAJORITY... WAARABU na NDUGU ZAO WALIKIMBIA NAONA SASA HIVI WANARUDI

  KUIDAI ZANZIBAR.

  FYI

  Syria Sanctions Proposed By United States, European And Arab States
  Source: Huffington Post

  Kwahiyo Mtakuwa Against Oman, Kuwait, UAE, UK Nchi Ambazo Waarabu wa Zanzibar walikimbilia
   
 16. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ahsante mkuu kwa ufafanuzi mzuri!! Sasa hawa wenzetu wanataka mwarabu atawale, ndiyo yale yale enzi za utumwa.
   
 17. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Iran wenyewe wameshindwa kuimalizia mitambo yao ya kufua umeme ya nyuklia! Harafu unataka waje, si ndo kuzidi kujiongezea matatizo!
   
 18. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  na baado tutaysikia mengi katika hii naniii legelege, na haya ndo matokeo ya kuwa na serikali legelege, wajanja wanaCapitalize through ulegelege huo, aya jioni njema
   
 19. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Na kuzuia maandamano ya chadema kwa kisingizio cha interejensia.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nampongeza Membe kwa maelezo yake maana anajua kinachofanyika. Swala hapa ni kwamba Marekani hawataki kabisa nchi yoyote ishirikiane na Iran ktk kuhakikisha hawauzi Mafuta nje. Inajulikana wazi kwamba mashirika ya Meli ni ya watu binafsi wafanya biashara ambao hutafuta kazi ya usafirishaji ndani na nje ya nchi zao. Kwa hiyo swla hapa ni mbinu za kujaribu kuikomoa Iran na sii Tanzania wala shirika la meli kwa sababu Marekani inaweza kabisa kuelekeza malalamiko yake kwa shirika hilo. Tukikataa sisi wataenda kusajili nchi nyingine..

  Hapa Canada kuna mashrika mengi sana ya Marekani, China, Japan Uingereza na kadhalika, tena naweza kusema robo tatu ya mashirika makubwa Canada ni ya Kimarekani ikiwepo Barricks. Hivyo, kuilaumu Canada kwa sababu ya vitendo ama maamuzi ya Barricks wakati sisi wenyewe ndio tumeingia mkataba na Barricks sio Canada wala Marekani ni kukosa kuelewa usajili unafanyika vipi. Maadam Barricks wanafuata sheria zote za usajili Canada na wanalipa kodi, serikali ya Canada haitajali ni kiasi gani tunapewa iwe ruzuku au hatupewi kitu kabisa.. Ila watajali tu kama kuna ukiukaji wa sheria na haki za binadamu..

  Mbona Wayahudi (Jews) kote duniani hulipa kodi nchini kwao japokuwa ni raia wa nje na wanaishi na kufanya biashara nchi za nje?.. Sijasikia mtu hata mmoja akipinga Myahudi anayewekeza Tanzania, Canada au Marekani kujihusisha na ulipaji kodi kwa Israel wakati sisi tukifanya hivyo tu tunaambiwa Alqaeda na itachunguzwa hizo fedha zinakwenda Tz kufanya nini pengine hata kufungiwa accounts. Ifike mahala tuuthamini Uhuru wetu sisi wa tu huru na raia wa Tanzania, nchi huru yenye sovereign yake na tunafanya maamuzi kwa maslahi ya nchi yetu sio kuwaridhisha Marekani au EU. Kuna madai ya ukweli yapelekwe UN na maamuzi yafanyike kwa wanachama wote wa jumuiya hiyo.. Hivi kweli mkichukua nchi mtaweza kuongoza kwa maslahi ya Watanzania au tutakuwa vibaraka?
   
Loading...