Meli za Iran: Vigogo Zanzibar wahusishwa - mbinu za kudhoofisha Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meli za Iran: Vigogo Zanzibar wahusishwa - mbinu za kudhoofisha Muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 16, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mwandishi Wetu

  Toleo la 247
  11 Jul 2012  • Wana uhusiano na kampuni ya Philtex ya Dubai
  • Ni mbinu za kudhoofisha Muungano


  SAKATA la meli za Iran kusajiliwa na kisha kupeperusha bendera ya Tanzania kwa lengo la kukwepa vikwazo vya kimataifa vilivyoweka kupitia Umoja wa Mataifa (UN) limeingia katika sura mpya, taarifa za awali zikiwahusisha baadhi ya vigogo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.


  Vigogo hao wanadaiwa kuwa na uhusiano na kampuni ya Philtex ya jijini Dubai, inayodaiwa kusajili meli za mafuta za Iran ili kupeperusha bendera ya Tanzania kwa lengo la kukwepa vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa nchi ya Iran.

  Taarifa kutoka kwa baadhi ya maofisa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa zinabainisha kuwa baadhi ya viongozi wa serikali hiyo wamekuwa na maslahi katika masuala ya usajili wa meli hizo za kimataifa jijini Dubai.

  "Unajua kuna hali ya kuzidiana ujanja, awali huku Zanzibar walikataa SUMATRA (Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Maji na Nchi Kavu) kufanya shughuli zake na wakaunda Wakala wa Meli Zanzibar (ZMA) lakini wakala huyu akatoa zabuni ya kusajili meli kwa kampuni iliyoko Dubai (Philtex),"


  "Baadhi ya viongozi hapa Zanzibar hawakujua ujanja uliopangwa na wenzao, ujanja wa kuikataa SUMATRA Zanzibar na kuanzisha ZMA lakini pia ujanja wa kutoa zabuni kwa kampuni ya Philtex ya Dubai. Sasa hivi ndiyo wanashituka kwamba wapo wenzao wanaodaiwa kuhusishwa na kampuni hiyo," kilieleza chanzo chetu cha habari kutoka Serikali ya Zanzibar.


  Taarifa zaidi kutoka vyanzo vingine vya habari zinaeleza kuwa, licha ya Zanzibar kuanzisha wakala wake lakini ada za kimataifa za usajili wa meli zimekuwa zikilipwa na SUMATRA kwenda International Maritime Organisation (IMO) bila kuzingatia ukweli kwamba Zanzibar pia imekuwa ikisajili meli kwa kutoza ada, na kwa hiyo ilipaswa ama kuchangia malipo ya ada ya kimataifa kwa SUMATRA au kulipa moja kwa moja kupitia utaratibu ambao ungekubaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Tayari taarifa za Serikali ya Zanzibar zinathibitisha kwamba ZMA imesajili meli 399, ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, meli za mizigo ya jumla na zile za abiria.


  Lakini wakati usajili wa meli hizo za kimataifa visiwani humo ukiwa wa kasi kubwa kiasi hicho, taarifa za SUMATRA zinaonyesha kuwa mamlaka hiyo hadi sasa imesajili meli zisizozidi 100 tu tangu kuanzishwa kwake. Inaelezwa kuwa, sababu za meli chache kusajiliwa na SUMATRA ni kunatokana na udhibiti mkali.


  Kutokana na tofauti hizo za idadi ya meli zinazosajiliwa, baadhi ya viongozi waandamizi katika Serikali ya Muungano wanabainisha kuwa ni udhibiti huo ndio uliosababisha baadhi ya viongozi visiwani humo kuhakikisha SUMATRA inasimamisha shughuli zake Visiwani, nao kuanzisha ZMA.


  Gazeti la Lebanon la The Daily Star pia limefichua mbinu inayotumiwa na Iran kwa kuzipa meli zake nyingi za mafuta majina mapya ya Kiingereza kama inavyotuhumiwa kufanyika katika sakata la sasa linaloihusisha Tanzania.


  Mifano ya meli ambazo zimebadilishwa majina ni pamoja na Freedom ambayo awali
  ilifahamika kama Haraz, Truth (awali iliitwa Nesa), Blossom ambayo awali iliitwa Sima. Theluthi moja ya meli za Iran hivi sasa zimesajiliwa nchi nyingine na kati ya nchi hizo ni Tanzania pamoja na Tuvalu.


  Meli hizo zilizosajiliwa nchi nyingine mbali na kubadilishwa majina lakini pia zimepewa namba za usajili kama ifuatavyo Blossom (IMO 9357353), Camellia (IMO 9171462) naClove (IMO 9171450).


  Nyingine ni Companion (IMO 9357717), Courage (IMO 9357389), Daisy (IMO 9172038), Freedom (IMO 9357406), Justice (IMO 9357729), Lantana (IMO 9172040),Leadership (IMO 9356593), Magnolia (IMO 9172052) na Truth (IMO 9079107).

  Kwa mujibu wa tovuti ya Umoja wa Mataifa ni nchi za Brazil na Uturuki tu ndizo zimepinga kujihusisha katika usajili huo wa kinyemela wenye lengo la kukwepa vikwazo vya kimataifa.

  "Zanzibar waombe radhi na wafute open registration (usajili wa wazi wa meli), wameathiri sana taswira ya Tanzania," anasema kiongozi mwandamizi Serikali ya Muungano.


  Taarifa zaidi kutoka Zanzibar zinabainisha kuwa uamuzi unaochunguzwa sasa wa usajili wa meli hizo huenda ukawa umepata baraka za baadhi ya viongozi visiwani humo.


  Kwa mujibu wa taarifa hizo, inadaiwa kuwa viongozi hao waliruhusu usajili huo ama kutokana na uelewa mdogo wa masuala ya diplomasia ya kimataifa au ni kwa makusudi ikiwa ni sehemu ya mikakati ya viongozi hao (baadhi) kudhoofisha Muungano.


  Kwa mujibu wa tovuti ya Umoja wa Mataifa (UN), Azimio namba 1929 la Juni 9, 2010 ndilo lilikuwa chachu ya Iran kuwekewa vikwazo vya kiuchumi baada ya kuwapo mabishano ya muda mrefu kuhusu vinu vyake vya nyuklia. Azimio hilo liliweka baada ya Iran kushindwa kutimiza maazimio ya awali sita ya UN ambayo Tanzania iliyaunga mkono.


  Maazimio hayo ya awali ni pamoja na namba 1696 na 1737 yote ya mwaka 2006, namba 1747 la mwaka 2007 na mengine ni azimio namba 1803 na 1835 ya mwaka 2008. Azimio jingine ni namba 1887 la mwaka 2009. Ni kutokana na kutotii maazimio hayo, UN iliiwekea vikwazo Iran.


  Kutokana na mazingira hayo ya usajili wa meli hizo sasa Tanzania imetumbukia katika mgogoro mkubwa na Jumuiya ya Kimataifa unaotishia nchi kuwekewa vikwazo na UN kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kukiuka mikataba ya umoja huo ambayo Tanzania imeridhia.


  Meli zote hizo zimekwishakuthibitishwa na taarifa rasmi ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, iliyowasilishwa kwenye Baraza la Wawakilishi kupitia kwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano visiwani humo, Hamad Masoud Hamad, kuhusu sakata hilo la usajili wa meli za Iran.


  Nchi nyingine zinazotajwa kusajili meli za Iran zilizobadilishwa majina ni pamoja Tuvalu, meli moja na Malta, meli mbili.


  Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Mamlaka ya Usafiri Zanzibar (Zanzibar Maritime Authority - ZMA, iliundwa kwa sheria namba tatu ya mwaka 2009 ambapo pamoja na kazi nyingine, inasimamia utekelezaji wa sheria ya usafiri wa bahari Zanzibar ya mwaka 2006.


  Mwandishi wetu alizungumza na Mkurugenzi wa ZMA, Abdallah Hussein Kombo ambaye alirejea kauli yake iliyowahi kutolewa na Serikali ya Zanzibar kwamba kampuni yaPhiltex haijasajili meli za Iran.


  Hata hivyo, alisema kama kampuni ya Philtex ilitoa taarifa za uongo kwa ZMA basi uchunguzi unaofanyika kwa sasa utabaini na hatua zitachukuliwa.


  Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alikwishazungumzia suala hilo akitoa wito wa Marekani na Jumuiya ya Ulaya kushiriki katika uchunguzi na kama itabainika ni kweli, basi meli hizo zitafutiwa usajili wake.


  Kauli zenye mkanganyiko

  Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kwa nyakati tofauti imekwishawahi kutoa taarifa zinazoashiria kuiunga mkono Iran licha ya nchi hiyo kuwekewa vikwazo na UN.

  Taarifa hizo ni pamoja na ile iliyotolewa hivi karibuni kukanusha suala hilo la usajili wa meli za Iran, ukanushaji ambao kwa namna fulani ulitoa ujumbe wa kuiunga mkono Iran.


  Sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa hivi karibuni inasomeka; "Zanzibar ina uhusiano mkubwa na wa muda mrefu na nchi nyingi ikiwemo Iran,"

  "Hivi karibuni Zanzibar ilipata ugeni (Makamo wa Rais wa Iran) na viongozi wetu walifanya mazungumzo ya namna gani Iran itaendelea kusaidia Zanzibar katika miradi ya maendeleo."

  "Zanzibar haifungiki kusajili meli za nchi yoyote. Hili ni suala la kibiashara na kwamba ni njia mojawapo kwa serikali yetu kuongeza mapato ili kujiendesha, alimradi tu usajili huo hauvunji sheria za kimataifa,"

  "Zanzibar haingependa kuingizwa kwa visingizio vyovyote na kwa njama zozote katika migogoro isiyowahusu."


   
 2. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 867
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  "ielewe mitaa"-Fid Q
   
 3. m

  mkataba Senior Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pumba tupu.........
   
 4. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tatizo la wazenj ni msukumo wa jaziba kuliko akili.!!!!
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Naona meli zote zilizosajiliwa zina kibali cha IMO (mfano Blossom (IMO 9357353), Camellia (IMO 9171462) na Clove (IMO 9171450).Kwa hivyo kuna mambo hayaingii akilini.
  Kwanza, hii International Maritime Organization, uinternational wake uko wapi kufikia hadi ya kusajili meli bila ya kujua mwenye meli?

  Pili, kwa maelezo ya hapo juu, ni kuwa ili nchi iwee kusajili meli, lazima ilipe gharama, tuseme ZNZ imekuwa ikisajili kwa kutumia mgongo wa SUMATRA na bila ya kulipa pesa na kwa hivyo kuiingizia SUMATRA madeni?
   
 6. Isalia

  Isalia JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 950
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Hongera sana z'bar kwa kuikataa sumatra kufanya kazi z'bar kwani hilo lilitaka kuwa pandikizi jengine la kuchukua mapato ya zenji baada ya hayo yalokuwepo ZMA endeleeni na kazi zenu nzuri za kusajili meli kwa manufaa ya z'bar hiyo yote ni choyo tu kwa watanganyika kuona z'bar inanufaika
   
Loading...