Meli ya MV Skagit yazama

Ngoja usikie. Kina JK watasema watahakikisha tukio hili halitokei tena! Wamesahau walishasema hivyo juzi tu!
 
meli hiyo imezama ikiwa na abiria 200.source ITV.

ITV wenyewe mbona hawajaipa kipaumbele kwa habari ya saa 10 maana wametoa heading isiyoeleweka na kuzungumza mambo ya watumia bahari kuwa waangalifu wawapo baharini hali ya hewa si nzuri
 
jamaa angu ananiambia idadi ya abiria ilizidi ile inayoruhusiwa kisheria.
 
Pole sana wote walipata mkasa huu ajali...
 
Taarifa zinachanganya sana, wengine wanasema ni jana na Watu wote 200 waliokuwemo inasemekana wameokolewa,

Huku wengine wakisema ni mida hii na imepinduka kabisa!

Hebu tunaomba mtujuze zaidi mwenye taarifa sahihi


Hakuna mwenye taarifa sahihi mkuu
 
It's so sad, kujua muda huu wewe uliotulia na glass ya juice ukitazama movie, mwenzako anatapatapa ndani ya Bahari ya Hindi akijaribu kujisaidia asisink ndani ya maji
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Wednesday, 18 July 2012 15:43[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
digg
Meli ya abiria MV. Karama ikiwa na watu 400 toka Dar es Salaam kwenda Zanzibar imezama leo karibu na Kisiwa cha Chumbe, source mwananchi[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
mpaka juzi makamu wa rais wa zenji alikuwa anachukua rambi rambi za ile ya nungwi lakini nilikuwa sioni hatua madhubuti zinachukuliwa...usikute hilo lijimeli halina hata maboya ya kutosha....
 
mara mv seagul mara mv karama....ni meli ipi hasa imezama?
 
Hali ya upepo hata hapa Dar leo inatisha na nadhani ndiyo kinaweza kuwa chanzo kikuu cha ajali
 
Safari hii lazima tumuondoe waziri hamna mjadala magamba kwisha habari yao
 
Hivi ni meli mbili zimezama? MV Seagull na MV Karama? Ama ni meli moja ina majina mawili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…