Meli ya MV Skagit yazama

Meli ya MV Skagit yazama

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Posts
4,192
Reaction score
678
inasemekana MV seagul ikitokea Dar kuelekea zanzibar imezama. kila tupato habari tutazidi kuhabarishana

Update:
Ilikua na abiria 200 na juhudi za uokoaji zinaendelea na tayari baadhi ya watu wameokolewa wakiwa hai na wengine bado wanaelea wakiwa na maboya. Taarifa za vifo bado hazijathibitishwa japo ukweli ni kwamba vifo vipo. Meli hiyo imewahi kuripotiwa kuwa mbovu mara kadhaa.
seagull4.jpg
 
Hata mimi nimeona hiyo facebook, nkajua utani!! Ilikua na uwezo wa kubeba watu wangapi??
 
je kuna watu waliopoteza maisha? ilikuwa na abiria wangapi?
 
Mkuu kwa nini unasema hii ni breaking news wakati huna taarifa kamili???? Subiri ukishakuwa na taarifa kamili ndo uanzishe uzi.
 
KUMBE MELI YENYEWE ILIKUA MBOVU MBOVU TOKEA ZAMANI.... Soma hiyo iliyotokea tarehe 12/05/2012:

Mv. Seagull yazima moto ikiwa safarini kuelekea Pemba


Written by Mrfroasty (Ufundi) // 13/05/2012 // Habari // 5 Comments

Salma Said,
ABIRIA waliokuwa katika meli ya Mv. Seagul jana walikuwa katika wakati mgumu baada ya meli hiyo kuzima moto wakati ikitokea Pemba kuelekea Unguja. Hali hiyo iliozusha tafrani na kukumbushia ajali kubwa ya Mv. Spice Islander iliyotokea Septemba mwaka jana na kuuwa zaidi ya watu 200 ilitokea majira ya saa 7:00 mchana eneo la Nungwi.

Juhudi za kuwapata Nahonda wa meli hiyo na viongozi wa shirika la meli la zanzibar hazikuweza kuzaa matunda lakini baadhi ya aribira waliowasiliana na mwananchi walithibitisha hali hiyo kutokea.

Abiria mmoja aliyejitambulisha Nassor Masoud alisema walianza safari yao saa 4:00 asubuhi kutoka badanri ya Mkoani lakini meli ilipokaribia eneo la Nungwi ikaanza kwenda katiak mwendo usio wa kawaida na kupiteza muelekea na kisha kuzima kabisa mashine.

"Kwa kweli tulikuwa katika hali ngumu huku upepo ukivuma na abiria wengi tukiwa na wasiwasi huku wafanyakazi wa meli hiyo wakihangaika kutengeneza meli lakini khofu kubwa ilikuwa kwa akina mama na watoto ambao walikuwa wakipiga kelele" alisema Masoud.

Meneja wa meli hiyo, Said Abdulrahman alipohojiwa alisema kuwa juhudi za kurekebisha tatizo ndani ya njini lilifanikiwa na meli ikawa inaendelea na safari zake.
Awali abiria walisema kuwa katika hekaheka na upepo mkali meli ilipoteza muelekeo na kuelekea upande wa Tanga, kabla ya mafundi kufanikiwa kutengeneza.
Safari ya meli hiyo ilianza baada ya matengenezo yalichukua muda wa zaidi ya masaa mawili majini na kutarajiwa kufika bandari ya zanzibar ambapo ilitarajiwa ifike saa 10 jioni.

Hadi tunakwenda mitamboni meli hiyo haijafika zanzibar. Na hakuna taarifa zozote kutoka mamlaka zinazohusika kuhusiana na suala hilo licha ya wananchi kuwasiliana moja kwa moja na mamlaka hizo. wakizungumza na gazeti hili wananchi mbali mbali wamesema bado serikali haijapata funzo kutokana na vifo vilivyotokea katika ajali mbaya iloiyotokea mwaka jana ambapo mamia ya watu walipoteza maisha.

wamesema ni jambo la kushangaza kwa serikali iliyo makini kushindwa kutafuta usafiri wa uhakika na badala yake kuwaacha wananchi wake wakitumia usafiri usio na uhakika jambo ambalo wananchi wengi wanasafiria boti hizo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupanda ndege.

"Ingekuwa tuna ndege basi tungekuwa tunasafiri kwa ndege maana usafiri wa baharini imeshakuwa ni kifo sasa lakini kwa kuwa sisi ni masikini hatuna budi kucheza bahati nasimu na maisha yetu kwa sababu ndio usafiri wa watu wanyonge tutafanya nini? alihoji Haji Hamadi Mkaazi wa Mwembetanga Unguja.

Hii ni mara ya nne katiak kipindi cha wiki moja kutokea misukosuko kama hiyo inayohusu meli hiyo hiyo ya Seagul na Sea Express ambapo wananchi wamekuwa na khofu ya usafiri wa Unguja na Pemba kutokana na meli nyingi zinzofanya safari za visiwa hivyo kutokuwa na uhakika wa usalama majini.
 
yeah imesikika ivo muda sio mrefu watu wakinena ivo...stil we r looking for the proof...stay tuned!
 
Sikiliza radio one...ajali ni maeneo ya kisiwa cha chumbe ilikuwa na abiria 200
 
Meli iliyobeba abilia zaidi ya 200 inasadikiwa kuzama Chumbe huko visiwani. Source ITV breaking news
 
La Hawla Wala Quwata Ila Billahi LaAliyu La Adhyim.
 
Nasikia walioverload! Abiria zaidi ya mia tatu wakati uwezo ni abiria mia mbili!
 
Kuna habari juu ya hii meli kuzua kizazaa mara nyingi huko nyuma labda wanafanya references ktk hizo
 
Poleni sana wasafiri, hope you will survive kwa uwezo wa mwenyezi mungu!!
 
meli hiyo imezama ikiwa na abiria 200.source ITV.
 
Back
Top Bottom