Mei Mosi 2018: Rais Magufuli atapandisha Mishahara miradi mikubwa ya Serikali ikikamilika, Mwaka jana alinukuliwa Vibaya

Kuna neno maarufu sana lazima atalitamka: Haiwezekani....haiwezekani....haiwezekani....

Kila mtanzania mwenye akili timamu anaweza kutabiri (predict) hotuba ya mkuu. Ndo tutambue tuliingia chaka 2015. Rais wa nchi anayejitambua na anayejali wananchi wake kwenye matukio kama haya kila mtu angekuwa na hamu kusikia ataongea nini, na hakuna anayeweza kupredict kirahisi. Ila huyu wa kwetu mwepesi sana.

Utasikia, tumeibiwa vya kutosha.... Haiwezekani Iringa yenye mbuga ya Ruaha iwe tegemezi, Mimi ni Rais wanyonge....
 
IMG-20180501-WA0023.jpg
 
Kwa mara ya kwanza wafanyajkazi wa serikali ya umma tunaingia kwenye sherehe za mei mosi katika miaka mwiwli ya JPM. Ndugu wafanyakazi wenzanngu katika hili hatuwezi kujisaulisha tunaingia katika sherehe hizi ikiwa maelfu ya wafanyakazi wenzetu wamenyimwa hazi zao kwa kufukuzwa kazi kama mbwa koko, familia zilizokuwa zinasubiri mafao baada ya ya wazazi wao kuitumikia serikari kwa miongo kadhaa leo zinalia kwa sababu tu baba au mama amekutwa ntuhuma za cheti ambacho watoaji ni wao na wakaguzi ni wao wamefukuzwa kazi wengine wakiwa katika likizo ya kustaafu jaribu kuvaa kiatu cha familia hizi.
Ndugu zangu inatia uchungu sana leo hatuna speech za kuungana hakika mgeni rasmi amefanikiwa kutugawa, Nikikumbusha ule msimamo wa kufungua kesi ya kupinga kufukuza watumishi nitaonekana hamnazo lakini MUNGU yupo kuna wakati aliwaambia waisraili kaeni kimya na bwana ataenda kuwapigania AMENI,AMENI, AMENI. MH.mgeni rasmi chagua hivi leo utubu dhambi hii au unasubiri mapigo... maana hata wale watendaji uliyosema warudi kazini sitaki niwasemee sana lakini siasa mnazofanya mnazijua wenyewe na jaribuni kutambua kuwa mungu anaishi...
SOLIDALITY FOREVER...
 
Kwanini huwazi kupunguzwa kazi? Kwa awamu hii ukiwaza neema, waza na dhiki maana ni 50/50 yoyote inaweza kukukuta.
 
Tukutane hapa kwa updates zaidi.

Matarajio ya wafanyakazi.

1. Toka aingie madarakani hajawai kupandisha mishahara wafanyakazi.

2. Alipunguza 1% ya kodi iliyojificha na hajawai kuwa na impact kwa watumishi

3. Katika ukanda wa afrika mashariki na kusini mwa jangwa la sahara ndio mfanyakazi anakatwa kodi kubwa kuliko mtu yoyote.

4. Hajaajiri katika awamu yake kama ilivyokuwa kwa awamu zilizo pita. Na tukumbuke bajeti inayopitishwa bungeni hakuna kipengere cha ajira mpya na bajeti karibia zote zimepunguzw kwa 10-40%. Hivyo hakuna bajeti ya waajiriwa wapya.

6. Ajira za walimu ni changa la macho kwa sababu bajeti ya sasa imeongezwa kwa 5% tuuu, kwa lile la kusema serikali hii inaboresha elimu ni ndoto za mhana.
7. Bajeti kubwa kuliko zote ni usafiri yaani kuknunua ndege hata afya imekatwa kwa 20% sijajua hao wanaotakiwa kupanda ndege na treni sio watanzania au maana wagonjwa watapanda treni kwenda india kutibiwa? Au ndege zinafika india?
Poor dady huwaza mshahara utaongezwa lini,hua hawazi namna nyingine ya kujikwamua,poleni ma poor dady's
 
Mlioko uwanjani muambieni mkulu akumbuke kupunguza yale makato ya bodi ya mkopo elimu ya juu, yamekua mwiba.
 
Ntakuwa naangalia zangu series moja kali sana habari za hotuba za Jiwe hazieleweki sijui huwa anavuta
 
Back
Top Bottom