Meghan Markle: Walikataa kumfanya Mtoto wangu mwanamfalme (Prince) kisa mweusi kidogo

Okay nimekupata , VP kuhusu dada yake Samantha ? Mbona naye amemstumu Meghan ?
Samantha wana share baba. Mama ni tofauti, sasa kama Meghan haelewani na baba ataelewana vipi na dada yake huyo ?

Kitu kingine, hao watu wanazitumia hizi drama kama fursa yaani.

Huyo Samantha alikuwa anatumia jina la Samantha Grant, ila alivyoona tu Harry na Meghan wameanza ku-date akabadilisha jina ghafla , na kujiita Samantha Markle ili drama zianze.

Kaandika mpaka kitabu kumponda huyo Meghan kwamba yeye ni dada yake anamfahamu vizuri mwa zaidi ya miaka 20.
 
Hiyo familia ina ubaguzi sana. Kuanzia Diana walimbagua hadi akaamua kuzaa nje ya ndoa kwani mumewe alikuwa na danga lake na Diana hakupata pa kusemea.

Diana akaamua kwenda kula maisha hukoo wakamtilia shaka kuwa aweza zaa na ngozi nyeusi japo ya kiarabu walipohisi aweza kuwa mjamzito aongeze mtoto wa nje wakamwekea mtego wakammalizia mbali.

Yasemekana ndani ya kasri kuna mashankupe ya kizungu sijui ndo mawifi kina mama mkwe kazi yao ni kukukera tu kuwa hujui kuvaa hujui table manners hujui yaani hujui kila kitu.

Hao sasa ndo wamemgeukia huyu mwali. Ni kama mume wake anampenda sana hata kufikia kuhama nchi.

Hivyo ni visaa vya mastaa wa dunia, sie acha tupambane na maisha yetu.

Hii ni constitution na wana sheria zao katika ufalme, unapoingia kwao ni lazima ufuate sheria zao kama zilivyo
Masharti ni mengi sana na ni lazima afungwe mdomo mara anapoingia hapo
Bahati mbaya Meghan hakufikiria mbali wala kufuatilia habari zao kabla hajaingia kichwa kichwa
Kuhusu ubaguzi upo sana ila kuna wazee katika familia na washauri pia ambao ndio wanafanya kufuata sheria zao

Nakumbuka wakati Harry anamtambulisha Meghan kwa Malkia
Malkia alimchukua Meghan na kumtembeza katika Kasri la Buckingham na kumuonyesha picha moja ya bibi yake ambae alikuwa ni Malkia Charlotte na alikuwa Mweusi
Hapo Malkia alikuwa anamtoa wasiwasi Meghan na kumwambia kuwa hata mimi nina Vinasaba na black maana bibi yangu pia alikuwa mweusi

Yaani pamoja na kukimbia kwao ila yanayokuja ni magumu zaidi

Huyu hapa Queen Charlotte miaka hiyo
IMG_6066.jpg
 
Hiyo familia ina ubaguzi sana. Kuanzia Diana walimbagua hadi akaamua kuzaa nje ya ndoa kwani mumewe alikuwa na danga lake na Diana hakupata pa kusemea.

Diana akaamua kwenda kula maisha hukoo wakamtilia shaka kuwa aweza zaa na ngozi nyeusi japo ya kiarabu walipohisi aweza kuwa mjamzito aongeze mtoto wa nje wakamwekea mtego wakammalizia mbali.

Yasemekana ndani ya kasri kuna mashankupe ya kizungu sijui ndo mawifi kina mama mkwe kazi yao ni kukukera tu kuwa hujui kuvaa hujui table manners hujui yaani hujui kila kitu.

Hao sasa ndo wamemgeukia huyu mwali. Ni kama mume wake anampenda sana hata kufikia kuhama nchi.

Hivyo ni visaa vya mastaa wa dunia, sie acha tupambane na maisha yetu.
Nimependa tu ulivyomalizia maelezo yako hao ndio mastaa nilikerwa mno kuona watu wanajadili ishu ya mtoto sijui wa kajala na harmonize
 
Wewe hebu USINICHEKESHE...Kim Kardashian Ni Mweusi?... Angepata platform kuuubwa vile.marekani?..

Kim Kardashian Ana Asili ya Armenia..
Nikiangalia Sana keeping up.with the Kardashian...hadi namimi.nikawa Nawaza nipate hela..niongeze matitu...sijui Nichonge pua...


Upuuzi mtupu
Kama sio mweusi basi sio mzungu pia. Alafu unavyo sema angepata platform kubwa vile unamanisha nini?? Unataka kusema hakuna weusi wanao pata platform kubwa kumzidi kim na familia yke?
 
Kwanini uchangue kufanya Mambo kinyume na taratibu alafu...ukipatwa na changamoto....uje ulalamike

Huyu Harry kwanini Alioa mwanamke kutoka USA...Tena mwenye weusi ndani yake.....hakujua kadhia ziwakutazo watu weusi ulaya?....

Hakujua Royal family inataka Aoe mwanamke wa Aina gani?..

Hivi kukaa kote kwenye Ufamle hajui protokali za ufalme?

Mapenzi ni upofu ndugu yangu wee
 
Binadamu tuna kerana sana haya mambo hata huku bongo yapo sana tu.

Kuna jamii hapa bongo zinadai haziwezi kuoana na makabila mengine sababu ya tamaduni na mila zao.

Wengine ukiwa mweusi huna maana kwao.

Binadamu ni kiumbe mbaguzi tu kwa ujumla.
 
Unadhani mtu mzima anatakiwa apangiwe nani wa kumpenda? Kama kulikuwa na protokali za kifalme kwanini alipoenda kumtambulisha hawakumzuia kwamba anakiuka taratibu za kifalme?
Huyu mama yake alikiuka taratibu zipi hadi wakaanza kumdhalilisha na kumnyanyasa?


Kwanini uchangue kufanya Mambo kinyume na taratibu alafu...ukipatwa na changamoto....uje ulalamike


Huyu Harry kwanini Alioa mwanamke kutoka USA...Tena mwenye weusi ndani yake.....hakujua kadhia ziwakutazo watu weusi ulaya?....

Hakujua Royal family inataka Aoe mwanamke wa Aina gani?..

Hivi kukaa kote kwenye Ufamle hajui protokali za ufalme?
 
Meghan, mke wa Prince Harry amefichua kuwa familia ya kifalme Uingereza iligoma kumkabidhi mwanaye haki za kuwa Mwanamfalme (Prince) kwa kile alichotaja kama hofu ya ngozi ya kiafrika.

“Nikiwa hata bado sijamzaa mwanangu, tayari walikuwa wameanza kusema kwamba itifaki (protocol) hazitaruhusu aitwe Mwanamfalme.” Alisema Meghan kwenye mahojiano na Oprah

Aidha Meghan pia amesema alinyimwa ulinzi alipotaka kutoka nje ya kasri mwenyewe. Waliongeza pia kwamba mwanawe, Archie, hangepewa ulinzi.

“Hawakuishia hapo lakini pia walidokeza kuwa ingekuwa vigumu kwao kumpa mwanangu ulinzi”

Meghan na mumewe Prince Harry walifanya wamuzi wa kuondoka kwenye kasri ya kifalme nchini Uingereza na kuishi maisha ya kawaida nje ya Uingereza.

View attachment 1720119
Ngozi nyeupe balaa,huyu dada mwanzoni nilijua ni mzungu kwa wazazi wote wawili.Mama yake ni mweusi,baba mzungu,Richa ya kuonekana kama "mzungu"lakini kale ka damu keusi kutoka kwa mama yake,kanaleta balaa.

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri kuna mambo ya siri sana ktk hii familia (huenda ushirikina au matambiko ) kwenye familia hii ya kifalme, ambazo viapo vyake ni vikali sana. Nafikiri hivyo sababu mbona wamempa mturuki Boris Johnson uwaziri mkuu?

Princess Diana kabla hajafa alipanga ku expose mambo yao ya ushirikina. Alikua anasema it’s a devilish family. Sema walimuwahi kabla hajatoa hizo siri zao, ila hii familia ni kiboko kwenye mambo meusi
 
Yaani binadamu sisiii...!! Hatimae mtu wa Ileje anamuelewa kiundani meghan kuliko Prince Harry.

Halafu eti wanasemagwa mawifi, ooh mawifi ndo wanaharibu ndoa, ooh mawifi wana gubu kwa mke wa kaka. Huku kuna Eleje one anamkosoa mke wa kaka ake.

Halafu eti kuna watu wanaona wazungu wana roho mbaya plus huo ubaguzi. Huyu mweusi wa Ileje mwenyewe anamkataa Meghan, unataka whites wafanye nini.

Kila mtu amind business zake. Kila mtu atii kiu ya moyo wake. Kila mtu atoe maoni na kukosoa juu ya mambo yake binafsi na mambo ya jumuiya tuu. Mimi leo nikipenda kumuoa Mwajuma nchokonole, kama nina akili timamu niachwe nimuoe tuu..

Meghan wa watu, wazungu wambague. Weusi wamuone aliyataka, wengine wanuone mtoto wa mjini sana, hapo angekua mshamba mngemuita msukuma( am sorry folks, hata mimi ni msukuma).
Wapumbavu kama wewe hawakosekani katika jamii!
 
Back
Top Bottom