Meghan Markle: Walikataa kumfanya Mtoto wangu mwanamfalme (Prince) kisa mweusi kidogo

Wanawake.....wanawake......wanawake.....

Hawa viumbe hawa......basi ngoja tu niishie hapa.......
 
Huyu Meghan ni mtoto wa mjini sana kuliko Harry, hivyo tutegemee Harry kuendeshwa kama gari bovu.
Harry alikosea sana kuchagua mke!
Yaani binadamu sisiii...!! Hatimae mtu wa Ileje anamuelewa kiundani meghan kuliko Prince Harry.

Halafu eti wanasemagwa mawifi, ooh mawifi ndo wanaharibu ndoa, ooh mawifi wana gubu kwa mke wa kaka. Huku kuna Eleje one anamkosoa mke wa kaka ake.

Halafu eti kuna watu wanaona wazungu wana roho mbaya plus huo ubaguzi. Huyu mweusi wa Ileje mwenyewe anamkataa Meghan, unataka whites wafanye nini.

Kila mtu amind business zake. Kila mtu atii kiu ya moyo wake. Kila mtu atoe maoni na kukosoa juu ya mambo yake binafsi na mambo ya jumuiya tuu. Mimi leo nikipenda kumuoa Mwajuma nchokonole, kama nina akili timamu niachwe nimuoe tuu..

Meghan wa watu, wazungu wambague, weusi wamuone aliyataka, wengine wamuone mtoto wa mjini sana, hapo angekua mshamba mngemuita msukuma( am sorry folks, hata mimi ni msukuma).
 
Mke kamzidi umri kinoma, na alikuwa kaolewa akaachika, ata ingekuwa bongo mawifi awasingekubali kaka yake kufungiwa furushi kwenye gunia
Damu nzito kuliko maji. Kafuata mfano wa baba yake.
 
Kwenye maelezo yake amesema kuwa wakati anaanza mahusiano na mumewe hakuijia familia yake. Kuna muda alikutana na Queen Elizabeth akaambiwa piga goti akashangaa, akamuuliza jamaa yake huyu ni bibi yako na jamaa akamjibu huyo ni malkia. Kuanzia hapo akaanza kufundishwa jinsi ya kupiga goti mbele ya Queen Elizabeth.
Actress wa miaka kadhaa, mtu ambaye sio kwamba ametoka kijijini hajui current affairs na monarchies zinavyoishi ?

Hata kama hajui alikosa muda wa kufanya due dilligence, hata kama ukienda kuoa / kuolewa na familia ya wachawi unadhani utaenda kuwabadilisha au ni wewe na mwenzako kuishi maisha yenu na kuachana na ya kwao (hizi vuta nikuvute ndio zinaimarisha mahusiano ya familia zao) ?

Hana Busara huyu mtoto (Nadhani sio ulaya tu, hata bongo kuna msemo wa Don't Wash Your Dirty Laundry in Public)..... Yaani Aibu yako Aibu Yangu....
 
Nani aliyekataa?

Mbona hajatajwa?

Hicho kidemu kinapenda sana drama.

Si ajabu kimezusha ili kipate huruma tu.
Nasikia walinzi na wahudumu wanasema dada ana bad temper kichizi kiasi kwamba anagombana nao kila m'moja kwa wakati wake.

Na anapenda kucontrol mambo kupita maelezo na amemshika kichwa sana mume wake.

Me nadhani huyu binti angekuwa makini sana na namna anaishi na huyu kijana na familia yake. Asifurahie sana kuona huyu kijana anakaa mbali na ukoo wake. Wale ni familia yake no matter what, atake asitake ni vema akajenga nao mahusiano mazuri.

Sasa yeye analeta ligi za ajabu ajabu na ukoo wa mumewe hajui anamfanya huyu kijana kukosa amani sababu anakuwa mbali na familia yake na anachotaka ni mwanamke anaempenda awe na mahusiano mazuri na familia yake.

Sasa yeye anamfitisha kijana wa watu na ukoo wake..... Stupid kabisa.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Latest &current issue (udaku wa mbele). ...lakini haitapata wachangiaji wengi humu tofauti na mada za udaku wa ndani

Ongelea Diamond, Ravnav & likes
Kuna watu wanaifuatilia hii familia humu hutaamini....uzi huwa unajongea mdogo mdogo lakini utafika mbali
 
Akili yake ipoje?
Kavurugwa yule mzee. Kwanza yuko depressed sana, amezeeka akiwa hana hela. Anatangaganga tu.

Hakai hata Marekani, anazurula huko Mexico. Wakati Meghan anaolewa, alikuwa anapewa pesa na media za UK anafanya nazo interview, anamponda mwanaye.

Meghan alivyoona imekuwa too much akamwandikia barua. Cha kushangaza hiyo barua akawauzia tena hizo media.

Yaani yule mzee hajieweli kabisa wala hamtakii mema mwanaye.
 
sio wabaguzi ndugu yangu, hivi wewe unaona sawa mhindi/mzungu siku moja aje agombee urais wa nchi yetu?!? ndiyo maana katiba ina mashariti katika hili. Princes diana alipoanzisha uhusiano wa Dody akapata ujauzito wa mwarabu ilikuwa khashfa kwa royal family, halafu ujue ni anglican mwanzo mwisho leo waje wawe na mjukuu anaitwa farouk al habash omar!!! wewe haiwezekani hiyo, hata sisi tuwe na presidaa anaitwa chadrikhan amitabachan, haa hiyo haipo. sio ubaguzi but there is certain values hatuwezi kuziachia kirahisi hivyo potelea mbali uitwe majina mabovu kama ya mbaguzi au kaburu

Usiogope kumjibu....mwambie hata huku ubaguzi upo + ukatili....ulishawahi kuona polisi au jeshi likawa na mwarabu, mhindi au mzungu? Football players, Au hata ofisi za serikali!!! Kwahiyo ubaguzi upo tena wa 6G kuliko hata hizo nchi.

Binafsi, jamii nayoiona inaongoza kwa ubaguzi duniani ni "wahindi" japo wako baadhi yao wana roho nzuri.
 
Wadada weusi wa Kimarekani ni moto. Sema Harry ni kipenzi cha bibi ama sivyo muda utaongea.
 
Kashfa nzito imeikumba familia ya Kifalme ya Uingereza ambapo Meghan Markel, mke wa Mwanamfalme wa Uingereza (Prince Harry), amesema amekuwa akibaguliwa kutokana na rangi yake, hatua iliyomfanya kufikia wakati kutamani kujiua.

Akizungumza katika mahojiano na Oprah Winfrey, Bi. Markel amesema akiwa mjamzito kulikuwa na hofu kuhusu kwa kiasi gani mwanaye atakuwa mweusi, na hofu hiyo imechangia mtoto huyo kutopewa hadhi ya mwanamfalme.

Bi. Markel ambaye mama yake ni mweusi na baba yake ni mweupe amesema alikuwa na shauku kabla ya kuingia kwenye familia hiyo mwaka 2018, lakini alipoingia aliishia kuwa na mawazo ya kujidhuru/kujiua, baada ya kuomba msaada lakini hakupata.

Hata hivyo alikataa kueleza nani ndani ya Kasri la Kifalme alikuwa akizungumzia ubaguzi huo.

Wanandoa hao, Meghan na Prince Harry hawatekelezi majukumu yao katika familia ya kifalme na sasa wanaishi California nchini Marekani.
Dada kuwa mwangalifu na taarifa zako, usikosee majina ya wahusika! Ni Markle!
 
Naskia CBS wamelipa bill 16.38 kumfanyia interview huyo mwamba , nafkr wazungu wabaki kuwa wazungu na Sisi wengine tuendelee kuwa wachuuzi na wanyonge
Hiyo interview imevunja record. Noma sana
 
Kamanda Harry


1615291240242.png
 
Back
Top Bottom