Ikaria
Member
- Jul 17, 2019
- 74
- 205
Kituo cha habari CBS kilimlipa Oprah Winfrey takriban dola za Marekani Milioni 8 ili kupewa leseni ya mahojiano yake na mtoto wa Mfalme Harry na mkewe Meghan.
Mahojiano hayo yalifanikishwa na kampuni ya Harpo Production inayomilikiwa na Oprah
Mahojiano hayo ya takriban masaa mawili yalipeperushwa Marekani usiku wa jana na kuoneshwa kwenye vyombo vya habari vya Uingereza Jumatatu ya tarehe 8 usiku kwa ushirikiano na CBS.
Ni mahojiano yaliyovutia hisia mseto kote ulimwenguni baada ya Meghan kufichua uchungu aliopitia ndani ya kasri ya kifalme Uingereza kutokana na kuwa yeye ni mwanamke Mwafrika.
Meghan anasema hata kabla ya kumzaa mtoto wake Archie, tayari alikuwa ameambiwa kwamba itifaki (protocol) hazingeruhusu Archie kupewa hadhi ya Mwanamfalme kwa sababu sio mzungu kamili.
Aliendelea kusema alitamani hata kujitoa uhai kwani alikuwa ameanza kujiona hafai kabisa.
“Kuna muda niliwaza hata ni bora nife kutokana na jinsi walivyokuwa wakinibagua” alisema Meghan huku machozi yakimtoka.
Kwa upande wake Harry pia alisema alikuwa akipata maswali mengi ya kibaguzi kutoka kwa familia yake jambo ambalo lilimshtua sana.
“Niliulizwa natarajia mwanangu atakuwa mweusi kiasi gani” amesema Harry.
Ni baada ya kushindwa kuvumilia masaibu haya ambapo sasa waliamua kuondoka kwenye Kasri Uingereza kwenda kuishi Marekani maisha ya kawaida.
Aidha pia Harry amesema familia yake iliacha kumsaidia kifedha na kwamba hata baba yake aligoma kupokea simu zake.