Meghan Markle: Walikataa kumfanya Mtoto wangu mwanamfalme (Prince) kisa mweusi kidogo

Pumba sana hao jamaa, kulisha wai kua na mtu mwenye asili ya Africa kwenye falme centuries ago, kwann wasifuate taratibu za wakati ule
Meghan, mke wa Prince Harry amefichua kuwa familia ya kifalme Uingereza iligoma kumkabidhi mwanaye haki za kuwa Mwanamfalme (Prince) kwa kile alichotaja kama hofu ya ngozi ya Kiafrika.

“Nikiwa hata bado sijamzaa mwanangu, tayari walikuwa wameanza kusema kwamba itifaki (protocol) hazitaruhusu aitwe Mwanamfalme.” Alisema Meghan kwenye mahojiano na Oprah.

Aidha Meghan pia amesema alinyimwa ulinzi alipotaka kutoka nje ya kasri mwenyewe. Waliongeza pia kwamba mwanawe, Archie, hangepewa ulinzi.

“Hawakuishia hapo lakini pia walidokeza kuwa ingekuwa vigumu kwao kumpa mwanangu ulinzi”

Meghan na mumewe Prince Harry walifanya wamuzi wa kuondoka kwenye kasri ya kifalme nchini Uingereza na kuishi maisha ya kawaida nje ya Uingereza.

 
Mbona huyo mtoto ni mweupe tu au wanataka awe mweupeje.

Hata enzi za utemi huku kwetu mtu wa kuja alikuwa hawezi kupewa utemi ulikuwa ni mwiko hivyo haya mambo ni ya kawaida tu ila sasa ninachoshindwa kuelewa huyo mtoto kwa kuwa ni wa Harry sasa tatizo liko wapi?
 
Back
Top Bottom