Meghan Markle: Walikataa kumfanya Mtoto wangu mwanamfalme (Prince) kisa mweusi kidogo

Unadhani mtu mzima anatakiwa apangiwe nani wa kumpenda? Kama kulikuwa na protokali za kifalme kwanini alipoenda kumtambulisha hawakumzuia kwamba anakiuka taratibu za kifalme?
Huyu mama yake alikiuka taratibu zipi hadi wakaanza kumdhalilisha na kumnyanyasa?

Nimeitazama hii video ya Princess Diana, ni dhahiri alikua kwenye lindi la mawazo mengi yaliyosababishwa na unyanyasaji wa huko palace. Kitu hicho hicho anakipitia Meghan. Kuna kitu hakiko sawa huko kwa royal family
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ahsante sana Mkuu ni ushahidi tosha wa jinsi huu ufalme ulivyokuwa umejaa unyanyasaji na udhalilishaji wa kutisha.
Nimeitazama hii video ya Princess Diana, ni dhahiri alikua kwenye lindi la mawazo mengi yaliyosababishwa na unyanyasaji wa huko palace. Kitu hicho hicho anakipitia Meghan. Kuna kitu hakiko sawa huko kwa royal family
 
Mke kamzidi umri kinoma, na alikuwa kaolewa akaachika, ata ingekuwa bongo mawifi awasingekubali kaka yake kufungiwa furushi kwenye gunia
Kweli mkuu mkaliman
Unajua hata Malkia wa sasa Elizabeth asingekuwa malkia wa Uingereza ila baba yake mkubwa Edward Albert (baadaye alikuja kuwa Mfalme Edward VIII) alijiuzulu ufalme baada ya kutawala kwa siku 326 tu kuanzia tarehe 20 Januari mpaka tarehe 11 Disemba mwaka huohuo 1936 ili naye amuoe mwanamke wa Kimarekani Wallis Simpson ambaye alikuwa ameachika kwa mumewe wa kwanza na pia alikuwa kwenye mchakato wa kuachana na mumewe wa pili. Hivyo Mfalme Edward VIII akataka kuwa mume wa tatu. Ikabidi ajiuzulu ufalme.
Nafasi yake ikachukuliwa na mdogo wake Albert Frederick ambaye alipotawazwa kuwa Mfalme akachukua jina la Mfalme George VI. Mfalme George VI alifariki mwaka 1952 ndipo binti yake mkubwa Elizabeth akachukua Umalkia na anatawala mpaka leo hii.
 
Kashfa nzito imeikumba familia ya Kifalme ya Uingereza ambapo Meghan Markel, mke wa Mwanamfalme wa Uingereza (Prince Harry), amesema amekuwa akibaguliwa kutokana na rangi yake, hatua iliyomfanya kufikia wakati kutamani kujiua.

Akizungumza katika mahojiano na Oprah Winfrey, Bi. Markel amesema akiwa mjamzito kulikuwa na hofu kuhusu kwa kiasi gani mwanaye atakuwa mweusi, na hofu hiyo imechangia mtoto huyo kutopewa hadhi ya mwanamfalme.

Bi. Markel ambaye mama yake ni mweusi na baba yake ni mweupe amesema alikuwa na shauku kabla ya kuingia kwenye familia hiyo mwaka 2018, lakini alipoingia aliishia kuwa na mawazo ya kujidhuru/kujiua, baada ya kuomba msaada lakini hakupata.

Hata hivyo alikataa kueleza nani ndani ya Kasri la Kifalme alikuwa akizungumzia ubaguzi huo.

Wanandoa hao, Meghan na Prince Harry hawatekelezi majukumu yao katika familia ya kifalme na sasa wanaishi California nchini Marekani.
Katika kuchimbua mambo nimewahi soma mahala kuw Malkia mwenyewe anavinasaba vya black genes kutoka kizazi kimojawapo huko miaka ya nyuma sana, ila inafi chwa balaa isijulikane maana wao mtu mweusi ni laana kwao na mtu mweusi hujipendekeza kuoa mweupe akidhani ngekuwa.
 
Kweli mkuu mkaliman
Unajua hata Malkia wa sasa Elizabeth asingekuwa malkia wa Uingereza ila baba yake mkubwa Edward Albert (baadaye alikuja kuwa Mfalme Edward VIII) alijiuzulu ufalme baada ya kutawala kwa siku 326 tu kuanzia tarehe 20 Januari mpaka tarehe 11 Disemba mwaka huohuo 1936 ili naye amuoe mwanamke wa Kimarekani Wallis Simpson ambaye alikuwa ameachika kwa mumewe wa kwanza na pia alikuwa kwenye mchakato wa kuachana na mumewe wa pili. Hivyo Mfalme Edward VIII akataka kuwa mume wa tatu. Ikabidi ajiuzulu ufalme.
Nafasi yake ikachukuliwa na mdogo wake Albert Frederick ambaye alipotawazwa kuwa Mfalme akachukua jina la Mfalme George VI. Mfalme George VI alifariki mwaka 1952 ndipo binti yake mkubwa Elizabeth akachukua Umalkia na anatawala mpaka leo hii.
Duh, story hii naiwekea lamination
 
Hahaaaa mkuu yule ni Prince Philip ana sura ile ya kikoloni kabisa. Hata Prince Charles nae ana sura chachu sijui wasingekua royal family wangekuaje 😂😂
Mkuu nasikia waingeleza ndio ugly people in Europe sijui ukweli wake ukoje huko ualaya, ila hapa bongo sijawahi ona mzungu wa uingereza mzuri kwa wale niliokutana nao, tofauti na wazingu wa maëka akinaa lady gaga,madona pamoja na waitaliano, wako moto kasoro makalio nk.
 
Wanawake wanaoongoza kwa makalio ulaya nadhani ni wa Scandinavian kantrez. Unaweza kutana na mzungu kafungasha zigo la haja! Cha ajabu sasa wanaume wa kule hawawapendi wao wanapenda vimbaombao.
 
Cha msingi Prince Harry ameamua kufanya maamuzi ya kiume kwa kujitoa kwenye jumba la wabaguzi kwa ajili ya mke wake.

Huku tanzania jamaa bila aibu linamuambia mchumba wake wa muda mrefu waachane kwasababu familia inataka aoe mchaga mwenzake/msukuma mwenzake. Pambaf.
Mkuu unawafahamu wa mama wa kibantu wewe! unataka nongwa ya milele.
Binafsi nipo kwenye huo mtihani, mother hampend mke nilieoa huko moro, tena aliniambia makavu kabisa na nimemuhidi mambo yakikaa sawa nikaoe mke wa pili mmanyema anaemtaka yeye,
Mkuu ukiwa kichwa ngumu hutoboi maisha.
Kuna muha wa kwetu alimpenda binti wa kichaga,aliposhirikisha wazazi wakamtolea nje wakamwambie bora akaoe mtusi kgm kuliko mchaga akawakatalia.Jamaa tulipoteana sijui iiliishiaje ile kesi.
Wazazi wa kiafrika wanashida sana, japo siku hizi wanakutana na "NO"!!
 
Harry ni mtoto wa prince Charles ambaye ni. MUME WA MALKIA.
ndo maana kama wanawatenga tenga hivi.
Angekuwa anatokana na malkia mwenyewe isingekuwa hivi.
Imebidi tu nicheke...prince charles ni mume wa malkia?

Anyway, Harry ni mtoto wa Prince Charles na late Princess Diana, huyo malkia elizabeth anamzaa huyo prince charles angalau now umepata kapicha picha mkuu eti?...
 
Wanawake wanaoongoza kwa makalio ulaya nadhani ni wa Scandinavian kantrez. Unaweza kutana na mzungu kafungasha zigo la haja! Cha ajabu sasa wanaume wa kule hawawapendi wao wanapenda vimbaombao.
Mkuu yale macho meupe unafikiri yanaona sawa na sisi? Huko Scandinavia naweza oa mke hao vimbau mbau siwaelewi kabisa wala hawanivutii hata awe na sura kama malaika labda itokee nimeenda kwao na ni wao tu huna option, maana mwili ukihitaji huwa hakuna kulemba ataejileta mbele ndio unapita nae.
 
Wazungu walishasema akifa Malkia hawatoruhusu mtu kusimikwa. Wamechoka kodi zao kutumika kulipa watu ambao hawana manufaa yoyote!
Hizo ni story tu watu wanatunga "rumors"

Ila kiukweli British people wanaiheshimu sana royal family na wanajivunia sana kuwa nayo

Na kamwe Monarch system haitakaa iondoke England

Kama tu Scotland ilishindikana kujitoa Great Britain unadhani system itaondoka?

Kiufup imeota mzee hio system
 
Nani aliyekataa?

Mbona hajatajwa?

Hicho kidemu kinapenda sana drama.

Si ajabu kimezusha ili kipate huruma tu.

Nakubaliana Na wewe haswa
Mengine anabadili apate huruma kwa watu
Mme wake wa kwanza ni ushuhuda tosha
IMG_6041.jpg
 
Back
Top Bottom