SI KWELI Mechi ya Yanga dhidi ya Simba kupigwa Mei 10, 2025

SI KWELI Mechi ya Yanga dhidi ya Simba kupigwa Mei 10, 2025

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Screenshot 2025-04-23 162214.png

IMG_0784.JPG
IMG_0785.JPG
 
Tunachokijua
Machi 8, 2025 kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu ya NBC Tanzania ulipangwa mchezo dhidi ya Simba sports club na Dar es salaam Young Africans katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Klabu ya Simba usiku wa kuamkia Machi 8, walitoa taarifa kwa umma kuelekea mchezo huo kuwa hawatoshiriki katika mchezo huo, kutokana na walivyoviita vitendo visivyo vya kiungwana dhidi ya timu yao kwa kunyimwa haki ya kufanya mazoezi katika uwanja wa Benjamini Mkapa kinyume na kanuni.

Aidha bodi ya ligi ilitoa taarifa na kueleza kuwa mchezo huo umeahirishwa na itapangwa siku nyingine.

Madai

Kumekuwapo na barua zinayosambaa katima mitandao ya kijamii moja ikidaiwa kutolewa na klabu ya Simba, Yanga na nyingine ikidaiwa kuolewa na bodi ya ligi. Barua hizo zinaonesha kuwa mechi kati ya Yanga dhidi ya Simba (kariakoo derby) iliyohairishwa itachezwa tena Jumamosi, Mei 10, 2025 katika uwanja wa Amani Zanzibar. Tazama hapa

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. Ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa ya kuwa mechi ya Simba na Yanga itachezwa Mei 10, 2025 si ya kweli.

Ufuatiliaji umebaini kuwa barua inayoonekana kuwa ni ya Simba ikiwataka mashabiki wao kwenda kuishabikia timu hiyo siku ya mechi, haijachapishwa na ukurasa rasmi wa Simba na hivyo kuonekana kuwa ni ya kughushi.

Barua inayoonekana kutolewa na bodi ya ligi, haijachapishwa wala kutolewa na bodi ya ligi Tanzania (TPLB). Ufuatiliaji umebaini makosa kadhaa katika barua hiyo ikiwemo maneno yaliyotumika mathalani mwanzoni mwa barua wametumia maneno “kwa heshima na taadhima” ambalo si kawaida kutumika kwenye barua za bodi ya ligi. Aina ya mwandiko (font) iliyotumika pia haina mpangilio mzuri.

Barua inayooenaka kuwa ni ya Yanga nayo haijachapishwa na ukurasa rasmi wa klabu hiyo wala hawajatoa tamko lolote kuhusu kuchezwa mechi hiyo.

Aidha JamiiCheck imewasiliana na Afisa habari wa bodi ya ligi, Karim Boimanda ambaye amekunusha barua hiyo kutolewa na bodi ya ligi. Amesema;

"Hiyo taarifa haijatolewa na Bodi ya Ligi, itakuwa imetengenezwa, taarifa zetu rasmi zinatolewa kwenye pages rasmi zinazotambulika, kama haujaiona kwetu tambua siyo ya kwetu."
Back
Top Bottom