Mdude Nyagali atimiza siku 244 gerezani

Mdude Nyagali atimiza siku 244 gerezani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
137,661
Reaction score
272,490
FB_IMG_1610308720895.jpg


Mfungwa wa kisiasa Kamanda Mdude Nyagali leo ametimiza siku 244 Jela ambako amewekwa kwa kesi isiyo na dhamana

Kwa mara ya kwanza alishitakiwa kwa makosa ya Uhujumu uchumi lakini baada ya kuthibitika kwamba Mhujumu uchumi huyo mpya mapato yake kwa mwezi hayafiki hata Tsh laki moja, akabadilishiwa mashitaka na kushitakiwa kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya , huku ushahidi ukionyesha kwamba hajawahi kuuza wala kumiliki hata Ugolo.

Nachukua nafasi hii kumuomba Mwenyezi Mungu ili aingilie kati na kuhakikisha haki inatendeka.
 
Kwani waliokuwa wana support waneshindwa kumsaidia?
 
Amekuwaje Mfungwa ilihali Hata Bado hajahukumiwa, Kamanda mbona ni waongo Sana nyinyi ili mpate huruma za Wananchi!!
Hawa bawacha wanamatatizo anataka wamwachie huku anakesi ya madawa isiyo na dhamana
 
Mimi nikajua utakuja na tamko la chama Namna ya kudeal na kesi yake ili awe huru na maisha yake kumbe upo kutafuta Huruma isiyokuwa na tija Wala mashiko katika kumuokoa Kamanda.

All in all poleni Sana wanafamilia wa Mdude Ila pia iwe fundisho wa wachumia siasa waliobaki..

Usimwamini Mwanasiasa.

Usimwamini Mwanasiasa.

Usimwamini Mwanasiasa.

Hatima yako itakuwa mbaya tu huku ukimuacha yeye akila milo kamil na familia yake.
 
Ajifunze kwa tundu na Lema, wenzako wamekimbia na mabeberu yao wakatukane wakiwa mbali yeye anajifanya hamnazo halafu yuko hapahapa.
 
Mdude is cool, angekuwa anaogopa jela angeshakimbia nchi siku nyingi.

Infact anafanya mazoezi jela ili kujiweka vizuri kiafya ya mwili na akili.
 
Chama kimesha msahau wale waliokuwa wanampa kichwa mitandaoni nao sasa kimya hakuna wa kumsaidia wote wako busy akitoka angalie hatma ya maisha yake na sio taifa manake kwa upande hui hakuna anayemjali kabisa
 
Mungu amjalie afya njema huko jela.
Mwisho wa ubaya ni aibu na laana kwa watawala.
 
Back
Top Bottom