BAVICHA kutoa Sadaka Maalum Kanisani ili kumuomba Mwenyezi Mungu atoe hukumu ya haki kwa wote waliohusika kuwabambikia kesi wanachadema

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,638
218,081
Baada ya kutembelea Magereza kadhaa za Kanda ya Nyasa na kujionea lundo la Wanachadema wanaozidi 100 waliolundikwa jela kwa uonevu kwa makosa ya Uongo ya mauaji , uhujumu uchumi, Madawa ya kulevya, ujambazi na Utakatishaji fedha, Ile Taasisi ya vijana inayoongoza Barani Africa kwa sasa inayoitwa Bavicha, pamoja na hatua kadhaa za kisheria inazochukua , pia leo imeamua kupeleka sadaka Madhabauni ili kumuomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atoe HUKUMU YA HAKI , kwa wote waliohusika kupanga njama za kutesa raia wasio na hatia kwa sababu za kisiasa kwa lengo la kuisaidia CCM .

Viongozi na wanachama wa Chadema wa kanda ya Nyasa wamebambikwa kesi za kijinga sana ambazo hata wabambikaji wenyewe wanapaswa kujishangaa , kwa Mfano Mdude Nyagali Mkulima duni wa Mahindi kutoka Mlowo Mbozi , pamoja na kushitakiwa kwa uongo kwa kukutwa na madawa ya kulevya , lakini pia anatuhumiwa kusafirisha madawa ya kulevya kutokea Pakistan na kuyasambaza Tanzania huku akiwa hajawahi hata kumiliki Passport !

Binafsi namuomba Mwenyezi Mungu ambaye sasa imethibitika kwamba ANAPOKEA MAOMBI YA WATANZANIA NA KUTOA MAJIBU KWA WAKATI TENA BILA KUCHELEWA Aingilie kati jambo hili ili iwe fundisho kwa wote wenye tabia ya kuwabambikia kesi wasio na hatia ili kuwakomoa kwa sababu za kisiasa .

Mungu ibariki Chadema .
 
Mi naona shortcut nzuri ni kwa waganga wa kienyeji kumshughulikia DPP haraka amfuate mwendazake, Ndugai na wengine
Naunga mkono hoja. Mimi nachangia vifaa vifuatavyo kwa utendaji :- Chungu kipya ambacho hakijapikia, mtama mwekundu kilo moja,ubani maiti kilo moja,ndimukisirani nusu kilo,chumvi ya mawe kilo moja, njiwa mweusi mwenyewe mayai tumboni,kitambaa cha sanda mita mbili, kisu chenye mpini wa ngozi ya kiboko. Vingine wataongezea walioguswa.
 
Naunga mkono hoja. Mimi nachangia vifaa vifuatavyo kwa utendaji :- Chungu kipya ambacho hakijapikia, mtama mwekundu kilo moja,ubani maiti kilo moja,ndimukisirani nusu kilo,chumvi ya mawe kilo moja, njiwa mweusi mwenyewe mayai tumboni,kitambaa cha sanda mita mbili, kisu chenye mpini wa ngozi ya kiboko. Vingine wataongezea walioguswa.
Tetetete
 
Inaonyesha chadema walivyowajinga na kukosa mvuto. Hivi huko jela wapo chadema tu? Eti wanadai wahalifu wote chadema jela wamebambikiwa makosa.😂😂
 
Back
Top Bottom