Mdude CHADEMA umejitakia mwenyewe

Mdude CHADEMA umejitakia mwenyewe

Unamaana gani tunaposema binti wa watu?. Kama mdude ni muuzaji na binti ni mnunuaji kwanini umwone binti hana kosa mpk kumwita eti binti wa watu!!!
Mbona kwenye kesi mahakamani hatujamwona huyo binti kama mnunuaji. Tuache ujinga.
Anayeshikwa na mzigo Wa wizi ndiye mwizi Huyo binti Wa nini hajakutwa na mzigo
 
Chikwuemeka,

Sio kweli kuwa huyo binti nfiye alimuwekea madawa mdude issue Ni hivi mdude alikuwa akifanya biashara ya madawa ya kulevya unamtumia pesa kwanza Halafu unaambiwa njoo uchukue mzigo binti wa watu akatuma pesa akaufuata mzigo kumbe polisi walikuwa wakimfuatilia mdude kwa muda mrefu akanaswa binti alikuwa Bado hajafika kuchukua mzigo akauuze Arusha
Una wadudu kichwani wewe...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mbunge wa ccm alikuwa anaikosoa serikali kama mdude cdm?
Kwa hiyo wakosoa serikali ni watakatifu hawawezi kuwa wezi,majambazi,wauza unga nk? Wazaa nje ya ndoa kama mbowe na Joyce mukya? Nk
 
Alikuwa anafanya Jambo la hatarii sanaa...! Alitakiwa awe nchi za nje huko wakati anafanya hayaa lakini duu kajichanganyaa mzeee...huruma sana atafungwa mpaka mzee baba amalize muda wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anayeshikwa na mzigo Wa wizi ndiye mwizi Huyo binti Wa nini hajakutwa na mzigo
Ukumbuke aliyepeleka mzigo wa wizi kajulikana japo utatumia nguvu yako ya dola kumkandamiza Ukweli umejulikana hata ukimfunga itajulikana umemuonea tu
 
Kwa hiyo wakosoa serikali ni watakatifu hawawezi kuwa wezi,majambazi,wauza unga nk? Wazaa nje ya ndoa kama mbowe na Joyce mukya? Nk
Spika alikula mapesa kibao India kwa kuwa anaisaidia serikali yako kuwanyanyasa chadema yeye ni mtakatifu, style yenu kwa mdude imewaumbua kinoma endelea kutumia style hiyo ipo siku yatakurudia na wewe.
 
Ukumbuke aliyepeleka mzigo wa wizi kajulikana japo utatumia nguvu yako ya dola kumkandamiza Ukweli umejulikana hata ukimfunga itajulikana umemuonea tu
Aliyejulikana ni aliyekutwa nao yeye Mdude ndie mahakanani akathibitishe kuwa haukuwa wake kazi anayo
 
Hakimu au jaji anayemfunga mtu kwa kosa ambalo si la kweli hubeba mzigo wa dhambi siku ya kiama atachomwa moto mkali usio na kikomo na wale waliomtuma kumfunga ipo siku mungu atawalipa malipo huwa hapa hapa Duniani
 
KAMANDA 'MDUDE' SIO SIRI UMEJITAKIA MWENYEWE

Hivi hukumuona mwezako Roma Mkatoliki, alivyokimbilia nchini Marekani baada ya kunusurika kuuawa alipotekwa na watu wasiojulikana?

Hivi hukuwaona wenzako akina Maria Sarungi, Ansbert Ngurumo, Evarist Chahali, Mange Kimambi na Kigogo 2014 wanavyoikosoa Serikali huku wakiwa nje ya Tanzania?

Hivi Mdude hakujifunza kwa Ben Saanane au hakujifunza pale alipotekwa kwa mara ya kwanza?

Hivi ulipata ujasiri gani kuanza kuikosoa Serikali ya CCM kila kukicha mtandaoni huku ukiwa unaishi hapahapa nchini? Kwani akina Kigogo, Ngurumo, Chahali na Mange Kimambi uliona ni wajinga walipoamua kukimbilia ughaibuni?

Ndio maana nasema kuwa, Mdude Nyagali Chadema umeyataka mwenyewe, ila shukuru tu kwamba utaendelea kuwa hai gerezani hata kwa muda wa miaka 10, kuliko kama ungetekwa tena na watu wasiojulikana.

Bai bai 'SUMU YA NYIGU'

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi akili uwa mnaiweka wapi?
Leo kwake kesho kwako haijalishi amefanya nini haijustify kumtengenezea kesi ambayo hapo mtu mnampandikizia madawa ya kulevya. Serikali haiwezi kuwa hivyo hiyo tulitegemea ifanyike kwa magenge.
Serikali inabidi iongozwe kwa haki si kuwapa watu kesi ambazo hawastahili
 
Ukiwa mwanaharakati unayepingana na serikali unatakiwa uoe haraka sana ili just in case something happen basi uwe umeacha japo katoto.

Ukiwa mwanaharakati unayepingana na serikali unatakiwa uachane kabisa na mademu wa mitandaoni au kufanya appointment na watu usiowajua, au uwafanyie thorough assessment kwanza kabla hujakutana nao.

Huyu jamaa kama kweli kashikwa kizembe hivyo atakiwa amewaangusha makamanda wenzie. Utakuwaje mwanaharakati mwenye njaa na papuchi?
Unforgetable

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani mdude alikuwa hajulikani alipo?

Sidhani kama polisi wanaweza kupoteza muda wote huo kumtafuta mdude

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyejulikana ni aliyekutwa nao yeye Mdude ndie mahakanani akathibitishe kuwa haukuwa wake kazi anayo
Kwa mahakama iliyo huru kama mahakama za kenya ama South Africa hapo kusingekuwa na kesi uchunguzi ungeibua Ukweli wote na mdude angeachiwa huru, lakini kwa mahakama yako binafsi tusitegemee haki kutendeka
 
Kufubgwa ni sehemu ya uanarakati na alikuwa anajua hilo. Kuna cku tutaheshimiana. Nyerere na Mandela walifungwa kwa uonevu kama huo badae wakawa wakubwa. Miaka 5 badae Jiwe hatakuwa na madaraka na ma RPC wanao mbambikia kesi watakuwa wamestaafu au wamepumuzika au kubadilishwa vitengo, hapo sas ndo the Hague ya Bongo itakapo washukia. Yule Raisi mfupi wa Zambia aliwatesa watangulizi wake alipotolewa madarakani Raisi Mwanawasa alimtolea kinga ya kutoshitakiwa kupitia bunge akasulubiwa vikali. Na Tz yanawezekana. Vijana wanaotizamiwa kuchomoza kwa Uraisi miak 5 badae ni kama akina January au Nape ambao wote ni majeruhi. Unategemea nini hata kama jiwe atakuwa mbabu, watamsulubu kwa kutaifisha mali zake na vidampa wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kufurushwa Dar na Makonda kumbe wakahamishia biashara yao Mbeya kwa Mdude?

Pole sana Mdude kwa kudanganywa uwe agent wa madawa ya kulevya

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
Mdude hakuwa agent hajui hata dawa zipoje, agent ni yule dada wa Arusha aliyetumwa kumpelekea nyumbani kwake wapate sababu ya kumfunga jela
 
Kufubgwa ni sehemu ya uanarakati na alikuwa anajua hilo. Kuna cku tutaheshimiana. Nyerere na Mandela walifungwa kwa uonevu kama huo badae wakawa wakubwa. Miaka 5 badae Jiwe hatakuwa na madaraka na ma RPC wanao mbambikia kesi watakuwa wamestaafu au wamepumuzika au kubadilishwa vitengo, hapo sas ndo the Hague ya Bongo itakapo washukia. Yule Raisi mfupi wa Zambia aliwatesa watangulizi wake alipotolewa madarakani Raisi Mwanawasa alimtolea kinga ya kutoshitakiwa kupitia bunge akasulubiwa vikali. Na Tz yanawezekana. Vijana wanaotizamiwa kuchomoza kwa Uraisi miak 5 badae ni kama akina January au Nape ambao wote ni majeruhi. Unategemea nini hata kama jiwe atakuwa mbabu, watamsulubu kwa kutaifisha mali zake na vidampa wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Watenda ubaya huzani kuwa watakaa huko madarakani miaka 50 huwa hawakumbuki kuwa ipo siku watastaafu na wale waliowatendea mabaya watakuwa juu
 
Nyie wajinga sana. Hivi yule Mbunge wa CCM mbona mlishangilia na hamkusema kesi ya kutunga??
Na hilo ndilo swali la msingi maana kwa yule mbunge sawa ila kwa chadema kabambikiwa siwaelewagi hawa WACHAGA
 
Back
Top Bottom