Kwa mfano tuseme kweli kategwa kama alivyosema mababe wa twitter.
Hivi unawezaje kushitukia mchezo kama binti anatokea jimboni kwa mbunge wa CHADEMA, jimbo linalo dhaniwa hicho chama kina nguvu sana kuliko mahali popote duniani?
Mrembo anaigiza CHADEMA in blood, na anajitambulisha ni wa makabila yale ambayo CHADEMA iko damuni, huku akirusha mapicha au twitt kibao za kichadema?
Anakusifia kwa ujasriri wako wa ajabu kuongea lolote dhidi ya dola na mwenye kushika dola.
Anakupa pole na kukuonesha nia ya kukupunguzia machungu ya kutenguliwa nyonga ama 'center bolt' kama alivyo wahi kuiita mdudde mwenyewe. Kisha anakurushia muamla 1M na kitu tarehe hizi ngumu kiuchumi.
Ukimcheki mtoto mwenyewe pengine kwa mtazamo wako (sio wangu) mzuri balaa anakuahidi kuja kukutunuku tufaa(apple) lililomponza adamu.
Tuwe wakweli jamani hivi nani kati yetu angechomoka huo mtego hasa sisi wenye kipato cha kawaida kama mdude?
Tuache kumdhihaki mdude, tuache unafiki tuwe wakweli na tuseme kamanda imemkuta ajali kazini kama nzi kufia kwenye kidonda.
Zingatia elimu na umri wa Mdude kabla huja mhukumu au kumdharau kunasa kijinga hata kwa yale aliyokuwa anatuma mitandaoni bila tahadhari au kufanya yale yaliyo pelekea kuingia mikononi mwa vyombo vya sheria.