Mdororo wa Uchumi: Landmark Hotels zabadilishwa kuwa hostel

Biashara yake ilikuzwa na tenda serikalini na wageni mbalimbali wa mikutano na makongamano, watu wa cash wengi walishindwa kumudu gharama za chakula na kulala pale , management nayo ikawa inafanya yake ...zikajengwa hotel nyingine nzuri za bei poa wateja wakaikimbia Landmark kama ilivyokimbiwa lunchtime
 
S H Amon kaaanza kuisoma namba T2015 JPM
Wenyewe CCM walikuwa wakiimba wataisoma namba, wakimaanisha wapinzani ndiyo watakayoisoma namba.

Sasa mambo yamekuwa vice versa, kwa kuwa huyo Mheshimiwa Amon Sauli, licha ya kuwa ndiye mmiliki wa chain za Hotel za Landmark zilizozagaa jijini Dar na kule kwao wilayani Rungwe, lakini pia kwa sasa ndiye Mbunge wa Jimbo la Rungwe.

Ambacho kimetokea ni kuwa Hoteli nyingi hususani za jijini Dar zilikuwa zinategemea kwa asilimia kubwa mapato yanayotokana na conferences kwa maana ya semina na warsha mbalimbali zinazofanyika kwenye mahoteli hayo.

Sasa baada ya kuingia JPM akapiga STOP hizo semina, warsha na mikutano ya idara mbalimbali za serikali kufanyika kwenye mahoteli na badala yake zifanywe kwenye Boardrooms za mahali pao pa kazi.

Hatua hiyo ya Magu imesababisha 'maafa' makubwa kama hayo tunayoyaona yaliyomkumba kada mkubwa wa CCM, Mheshimiwa Sauli Amon.

Kweli hivi sasa tunaisoma namba kwa mwendokasi na wanaoisoma namba zaidi ni wale wanaccm kindakindaki...........
 
sasa hapo si ndio mwake jamani, uzuri wa biashara ya hostel ni prepaid! Unavuta 160*4 kwa kila kichwa! Ukizidisha hio pesa mara 6 kama kila room ina deka 3 hela nzuri tu! Zidisha mara hoteli nzima uone hela ilivyo tamu na hata kodi atakayolipa itakuwa tofauti na ile ya hoteli! Jamaa nimemsifu sana, very strategic na flexible
Sio matatizo ni kubadili matumizi
 
hizo hostel hazitakosa wapangaji..

wanafunzi wa kigeni udsm wanateseka sana..

hasa wazungu wa exchange program wanateseka sana uchafu wa halls za udsm inawalazim wapange appartments ambazo bei ni kubwa kuliko hostel za landmark...

bado matajiri karibu wa nchi nzima mabinti zao na vijana wao wanasoma vyuo dar.. hawatashindwa kuwalipia watoto zao 160 kwa mwezi ili waishi mahari salama...

mtoto kasoma feza boys au feza girls anaenda udsm atashindwa vipi kuishi hostel landmark

wahitaji wa hiyo hostel wapo wengi sana na nina uhakika itajaaa haraka sana
Biashara ya kuishi room moja watu sita kwa 160,000 nani anataka sikuhizi?hata hiyo mabibo hostel haiko hivyo.
 
Pale LANDMARK kuna majengo mawili, naona jengo moja bado ni HOTEL na lingne NDIO inaandaliwa kuwa HOSTEL
 
Habari wakuu.
Nimepita maeneo ya Ubungo leo nikapita Landmarks Hotel nikakutana na bango la kubadilishwa kuwa hostel kuanzia September. Kwa hali hii sijui ni akina nani hawataisoma namba.

Nadhani kalenga sana soko la wanafunzi wa Udsm lakini sijajua gharama zake kama zitakuwa affordable, labda watu wa masters au foreigners.
ILE HOTELI ILIKAA MAHALA SIPO NA SIJUI WAKATI WANAANZA MRADI HUO WALIKUWA WANAWALENGA WATEJA WA AINA GANI. Kwa hostel italipa sana tu.
 
Lazima hali itakuwa mbaya.....hakuna wateja ndio maana mmiliki ameona bora iwe hostel mpangaji anakaa zaidi ya miezi 6. Sasa hivi business ya hotel (pamoja na utalii) imeshuka sana. Hela imeshuka thamani, uchumi wa mtu mmoja mmoja nao unadidimia......nchi ikikurupuka kwenye sera zake za kiuchumi na kisiasa mambo ndiyo anavyokuwa.
Dah... Kama ulikuwa unaishi kwa kupiga lazima iisome
 
Ana mahoteli na biashara nyingi tofauti tofauti ndani na nje ya nchi.Mmiliki wake ni S.H.AMON kubadilisha biashara kwake ni kitu cha kawaida.Anaitendea haki pesa yake.Yuko huru kuibadilisha hata kutoka hostel na kuwa nyumba ya kupaki magari.Ni jengo lake aweza litumia kwa biashara yoyote apendavyo.
Huu utetezi una walakini! mbona yamekutoka mengi? pamoja na maelezo yoote ukweli unabaki palepale kuwa ni kwa sababu biashara imedoda kwa maana haikujengwa kwa lengo hilo, na asipoangalia atabadili sana matumizi ya hayo majengo
 
Jamaa amesikia kilio cha wanaudsm. Asante mbunge wa Rungwe
Hali za wanafunzi na ustaarabu wao unaujua? kaangalie mabibo hostel, mwaka 2002 kulikuwa na kila kitu kuanzia majiko, friji kila angle mule kwa aliyetaka kutumia, makochi ya kupumzika, kuoga kwa shower n.k nenda sahizi kaangalie yamebaki magofu, hapa kaamua kula hasara maana hakuna waharibifu km wanafunzi na hii sio kwa kupenda kwake bali kalazimishwa kuisoma namba, usimshukuru maana mwenzio anaumia roho
 
Habari wakuu.
Nimepita maeneo ya Ubungo leo nikapita Landmarks Hotel nikakutana na bango la kubadilishwa kuwa hostel kuanzia September. Kwa hali hii sijui ni akina nani hawataisoma namba.

Nadhani kalenga sana soko la wanafunzi wa Udsm lakini sijajua gharama zake kama zitakuwa affordable, labda watu wa masters au foreigners.
Huyu bwana SH Amon ana matatizo.
Hizo Hotels alitakiwa KODISHE mtu wa kuziendesha, yeye ana ng'ang'ania kuziendesha mwenyewe wakati hana training wala experience ya kuendesha hoteli.
Kweli ana uwezo kuzijenga, lakini kujenga na kuendesha hoteli vitu viwili tofauti.
Hospitality Industry ni kitu ingine kabisa.
Hoteli zake hazina wateja kabisa hata ile ya kule White Sands ni tupu, nimeenda pale kua chakula cha joni nikajikuta iko mwenyewe, nikasepa.
Ashauriwe aingie mkataba na kampuni maarufu kuziendesha.
 
Lazima hali itakuwa mbaya.....hakuna wateja ndio maana mmiliki ameona bora iwe hostel mpangaji anakaa zaidi ya miezi 6. Sasa hivi business ya hotel (pamoja na utalii) imeshuka sana. Hela imeshuka thamani, uchumi wa mtu mmoja mmoja nao unadidimia......nchi ikikurupuka kwenye sera zake za kiuchumi na kisiasa mambo ndiyo anavyokuwa.
Lipa kodi kwa maendeleo ya Taifa
 
Naona hali ya uchumi inazidi kuwa mbaya mitaani. Ukiona dalili kama hizi ni wazi hali imebana ile mbaya...

Wachumi ebu tusaidieni jamani!... Things are not right

1468432252479.jpg
1468432262038.jpg
 
sasa hapo si ndio mwake jamani, uzuri wa biashara ya hostel ni prepaid! Unavuta 160*4 kwa kila kichwa! Ukizidisha hio pesa mara 6 kama kila room ina deka 3 hela nzuri tu! Zidisha mara hoteli nzima uone hela ilivyo tamu na hata kodi atakayolipa itakuwa tofauti na ile ya hoteli! Jamaa nimemsifu sana, very strategic na
flexible
Kwatarifa yako KWA HERUFI KUBWA HAKUNA BIASHARA KICHAAA KAMA HIYO SIJUWI KAMA ULISHA WAHI ATA KUWAUZIA MAHINDI YA KUCHOMA WANAFUNZI !?
ATAJUTA MUNGU ATUPE UHAI BIASHARA HAIFANYWI KWA STORY !!!
SIMJUWI ILA NINAUZOEFU WA MIAKA KWENYE HIYO KITU ATA UTUMIE SATELLITE HUWEZI FANYA BIASHARA NA WANAFUNZI LABDA NA CHUO!!!!! TENA KWA MIKATABA ILIYOP TYT!!
 
Back
Top Bottom